Akaunti za wanaharakati Tanzania zafunguliwa baada ya miezi nane
Mwanae Idris Deby amechukua usukani wa Chad baada ya kifo cha baba yake huku waasi wakiapa kuimarisha. mashambulizi ya pamoja.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Akaunti za benki za mtandaoni zafunguliwa Tanzania baada ya kufungwa kwa miezi minane

Chanzo cha picha, THRD
Akaunti za benki za mtandaoni zafunguliwa Tanzania baada ya kufungwa kwa miezi minane. Taarifa ya kufunguliwa kwa akaunti hiyo imetolewa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
‘’Kufunguliwa kwa akaunti hizo kumetokana na maelekezo kutoka kwa mamlaka za serikali zilizoagiza kufungwa ili uchunguzi wa tuhuma ufanyike na kisha kutoa maelekezo (Notisi kwa Benki) kuwa zifunguliwe’’, imesema taarifa ya THRDC.
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa Kufungwa kwa akaunti hizo tangu Agosti 2020 hadi sasa kulisababisha Mtandao kushindwa kutekeleza sehemu kubwa ya majukumu yake kwenye miradi ya utetezi wa haki za binadamu kama ilivyokuwa imeainishwa kwenye mipango yake ya 2020.
Bodi ya Wakurugenzi wa Mtandao imewashukuru, wahisani, taasisi mbalimbali na wanachama wa Mtandao walioshiriki kwa namna mbalimbali kuhakikisha kuwa Mtandao unaendelea kutekeleza majukumu yake na pia mamlaka mbalimbali za Serikali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa namna zilivyoshirikiana na Mtandao ili kuhakikisha kuwa suluhu ya tatizo hili inapatikana.
Imemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan ''kwa uongozi wake unaojali na kuzingatia haki za binadamu na utawala bora''.
Kulingana na taarifa yake Mtandao wa THRADC unaahidi kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na kwa kushirikiana na wadau na viongozi mbalimbali, mamlaka za serikali, na wadau wengine ili kuahakikisha kuwa utetezi wa haki za binadamu unafanyika kwa ufanisi na weledi mkubwa hapa nchini.
Waliochanjwa chanjo ya corona wazawadiwa msokoto wa bangi bure New York

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakazi wa New York jijini Marekani ambao wamekuwa wakichanjwa chanjo ya Covid-19 waliweza kupata zawadi ambayo haikutarajiwa siku ya Jumanne: Msokoto wa bangi.
Wanaharakati wanaosherehekea kuidhinishwa rasmi kwa bangi katika jimbo la New York walimpatia msokoto wa bangi wa bure mtu yeyote mjini Manhattan aliyethibitisha kuwa alipokea walau dozi moja ya chanjo moja ya corona.

"Hii ni mara ya kwanza tunaweza kuketi pamoja na kuwapatia kisheria watu bangi," alisema Michael O'Malley, mmoja wa waandalizi wa ‘’utoaji wa bangi’’ katika Union Square.
"Tunaunga mkono juhusi za shirikisho za utoaji wa chanjo. Na pia tunajaribu kuhamasisha wahalalishe kisheria matumizi ya mmea wa bangi katika nchi nzima ," aliliambia shirika la habari la AFP.
Watu wenye silaha wawateka nyarawanafunzi ‘’wengi’’ Nigeria

Chanzo cha picha, GREENFIELD UNIVERSITY
Watu wenye silaha wameteka nyara wanafunzi kadhaa kutoka katika chuo kikuu kilichopo katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria.
Msemaji wa polisi katika jimbo hilo, Muhammad Jalige, amethibitisha utekaji nyara huo kwa BBC, akisema wanafunzi‘’wengi ‘’ wametekwa kutoka katika mabweni yao.
Lakini amesema shughuli ya kuhesabu wanafunzi bado inaendelaili kubaini idadi kamili ya wanafunzi waliotekwa. Waliotekwa ni wanafunzi wa kike na wakiume, aliongeza.
Watu wliokuwa wamebeba silaha walivamia Chuo Kikuu cha Greenfield kilichopo viungani mwa mki wa Kaduna Jumanne na kufyatua risasi.
Utekaji nyara kwa ajili ya kikombozi unaofanywa na watu wenye silaha umekuwa ukiongezeka katika miezi ya hivi karibuni nchini Nigeria, huku zaidi ya wanafunzi 800 wakiripotiwa kutekwa nyara mwezi wa Disemba.
Wengi wao wamekuwa wakiachiliwa baada ya mashauriano na watekajilakini wanafunzi 29 waliotekwa mwezi uliopita kutoka katika chuo kilichopo katika eneo la msitu bado wanashikiliwa
Waalimu pia wamekuwa wakilengwa na mashambulio.
Wagonjwa wa corona wafariki baada ya kuvuja kwa oksijeni India

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, India imeanza mpango wa kuisafirisha wa haraka wa Oxygen Express kusafirisha gesi ya oksijeni katika majimbo yanayoihitaji Takriban wagonjwa 22 Covid wamefariki katika hospitali nchini India baada ya mfumo wa oksijeni kutoboka.
Tukio hilo limetoka Jumatano wakati mfumo wa oksijeni ulipokuwa ukijaza tanki la kuhifadhia katika hospitali Zakir Hussain katika jiji la Nashik.
Haijawa wazi ni kwa vipi tukio hilo lilivyotokea na ni kwanini lilivuruga mfumo wa usambazaji wa hewa hiyo kwa wagonjwa.
Lakini maafisa walisema hapakuwa na oksijeni kwenye mashine za kusaidia kupumua kwa takriban dakika 30, na hivyo kusababisha vifo vya wagonjwa.
"Tutataka kuchunguza suala hili na kuchua hatua," Kamishna wa manispaa ya jiji Kailash Jadhav alisema.
Hospitali kote nchini India zinahangaika kuendelea kuwapatia wagonjwa oksijeni huku wanaoihitaji wakiendelea kuongezeka.
Tazama jinsi helikopta ndogo ya kwanza ya Nasa ilivyotua katika sayari ya Mars
Maelezo ya video, Jinsi helikopta ndogo ya Nasa ilivyotua katika sayari ya Mars Kwa mara ya kwanza Shirika la safari za anga za mbali la Marekani NASA limeweza kupeleka helikopta ndogo nje ya sayari dunia na kuweza kuiwezesha kupaa kwenye sayari ya Mars. Tukio hilo lililorekodiwa tarehe 19 Aprili limekua ni la kihistoria na kutoa matumaini ya safari nyingine zaidi.
Rais wa Ufaransa amuomboleza ‘rafiki jasiri’

Chanzo cha picha, AFP
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa rambirambi zake kwa hayati rais wa Chad Idris Deby, akimtaja kama ‘’rafiki jasiri ‘’ na ‘’mwanajeshi bora’’,Shirika la habari Reuters limenukuu ofisi ya rais huyo ikisema.
Bw Macron pia alisema kuwa Chad inahitaji kipindi cha mpito cha utulivu na amani, kulingana na ripoti ya shirika la habari la AFP.
Vyombo vya habari nchini Chad vinatoa ripoti tofauti juu ya 'ufyatuaji risasi'' katika kasri la rais

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mahamat Idriss Déby Itno alitangazwa kama mkuu wa baraza la mpito la kijeshi akimrithi baba yake Vyombo vya habari vya Chad vinatoa taarifa zinazokinzana kuhusu madai ya tukio la ufyatuaji risasi katika kasri la rais lililopo katika mji mkuu N’Djamena kuhusiana na kile kinachotajwa kama mzozo ndani ya familia yaDéby family kuhusu uteuzi waMahamat Idriss Déby Itno kumrithi baba yake.
Msururu wa jumbe za Twitter kutoka katika wavuti wa kibinafsi wa habari wa Tchatinfos unanukuu vyanzo adhaa visivyojulikana vikikanusha tukio la ufyatuaji wa risasi.
‘’Rais wa baraza la kijeshi la mpito yuko hai na mwenye afya. Hapakuwa na ufyatuaji wowoye wa risasi katika kasri na hakuna malalamiko kutoka kwa kaka yake [Mahamat] Zakaria," wavuti wa Tchadifos ulisema
Hatahivyo, Toubou Media ulinukuu vyanzo vya habari ambavyo vilidai kwamba Mahamat alijeruhiwa katika tukio la ufyatuaji risasi lililosababishwa na "tofauti ndani ya familia".
Hayati Déby alikuwa na familia kubwa kutokana na kuoa mara kadhaa, na ana idadi ya watoto isiyojulikana.
Wakati huo huo wavuti wa habari unaounga mkono serikali Alwihda Info uliripoti kuwa milio ya bunduki ilisikika katika mkoa wa Ati, lililopo kilomita 378 (au maili 234 ) mashariki mwa mji mkuu N'Djamena, baada ya wafungwa kujaribu kutoroka gerezani. Wavuti huo uliongeza kuwa “hali ya utulivu imerejeshwa” baada ya kupelekwa kwa wanajeshi zaidi katika mkoa huo.
Mwanae Idris Deby achukua uongozi wa nchi baada ya kifo cha baba yake

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Mahamat Kaka akiwa pamoja na wanajeshi wengine walipokuwa wakitangaza kifo cha baba yake Idris Deby Mwanae Idris Deby amechukua usukani wa Chad huku waasi wakiapa kuimarisha mashambulizi ya pamoja.
Kifo cha ghafla cha Rais wa Chad Idriss Deby kimemfanya mwanae , Luteni Mahamat Idris Deby Itno (al maaruafu General Kaka), kuwa uongozi wa taifa hilo la Afrika ya kati, kwa kipindi cha mpito cha mwaka mmoja kabla kufanya uchaguzi.
Waasi wanatishia kufanya upya mashambulizi dhidi ya mji mkuu N’Djamena.
Mahamat, mwenye umri wa miaka 37, jana alitangaza Baraza la Mpito la wanajeshi la wanachama 15 (TMC) linaloundwa na majenerali ambao wataiawala Chad kwa miezi 18 ijayo.
Baraza la mawaziri na Bunge lilivunjwa na amri ya kitaifa ya kutotoka nje imewekwa.Waasi kutoka chama cha Front for Change and Concord in Chad (FACT) wameripotiwa kuanza tena harakati zao kuelekea N'Djamena, baada ya kifo cha Deby.
Deby, ambaye aliongoza Chad kwa miongo mitatu, alifariki saa kadhaa baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Aprili 11 na karibu 80% ya kura.
Katika taarifa iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii jana usiku, FACT ilisema: "Vikosi vya upinzaji viko katika milango ya N'Djamena.
''Tuko hapa kupiga kengele, sio za chuki au mgawanyiko, bali kupiga kengele za amani na matumaini mapya. Na zitakapolia, hakutakuwa na mikono tena nchini Chad kupiga ngoma za vita. " ilisema taarifa hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta amewasili mjini Kinshasakatika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ziara ya siku tatu kwa mwaliko wa Felix Tshisekedi.
Uhuru amepokelewa na Rais Tshisekedi na kupewa mapokezi ya taifa na gwaride la heshima.
Katikia uwanja wa ndege Rais Kenyatta alipokelewa na Rais Tshisekedi ambaye aliambatana na maafisa wa serikali ya Congo ikiwa ni pamoja na Waziri wa mambo ya nje Christophe Lutundula na Gavana wa jiji la Kinshasa Gentiny Ngobila Mbala.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Rais Kenyatta na mwenyeji wake leo wataongoza ujumbe wao katuika mazungumzo ya ushirikiano baina ya Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo na kusaini makubaliano mbali mbali ya ushirikiano baina ya nchi hizo.
Hujambo na karibu kwa matangazo haya mubashara tarehe 21.04.2021
