Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Rais Deby alikuwa anafanya nini vitani?
Mwaka jana Rais Deby aliongoza vikosi vyake vitani 'kuwaangamiza wanamgambo 1,000 wa Boko Haram'
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Je, Rais Deby alikuwa anafanya nini mstari wa mbele?
Japo baadhi ya watu wanasema ni jambo lilisilo la kawaida kwa Rais kuwa mstari wa mbele vitani, mwandishi wa BBC Beverly Ochieng anaripoti kuwa Rais Idriss Déby alikuwa mwanajeshi wa cheo cha juu cha field marshal na ilikuwa ni jambo la kawaida kwake kuwa mstari wa mbele na wanajeshi wake.
Takribani mwaka mmoja uliopita, Déby aliongoza operesheni ya kijeshi akiwa mstari wa mbele na inaripotiwa wanamgambo 1,000 wa Boko Haram waliuawa katika mapambano hayo.
Alipokea mafunzo ya kijeshi nchini Ufaransa na kufuzu kama rubani wa ndege vita.
Déby alikuwa afisa wa jeshi wa cheo cha juu aliporatibu mapinduzi yaliyomng'oa madarakani rais Hissène Habré mwaka 1990. Toka hapo Deby akachukua hatamu za uongozi mpaka umauti ulipomkuta, akiwa vitani.
- Idriss Deby: Rais wa Chad auawa na waasi mstari wa mbele
Sudan Kusini yaharibu chanjo 60,000 Corona
Sudan Kusini imeharibu chanjo za virusi vya corona aina ya AstraZenica ikisema kuwasili nchini humo zikiwa karibu muda wake unakwisha.
Chanjo hizo zilikuwa zimetolewa kama msaada kutoka kwa kampuni ya Afrika ya mawasiliano MTN na Muungano wa Afrikamwishoni mwa mwezi uliopita.
Hatahivyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Muungano wa Afrika CDC director John Nkegasong anasema walikuwa na muda wa kutosha kutumia chanjo hizo kabla hazijapitwa na wakati.
Sudan Kusini kwa sasa ni nchi ya pili baada ya Malawi kutangaza kuwa inawenda kuharibu chanjo.
Hii inakuja wakati wakati nchi nyingine za Afrika zikahangaika kupata chanjo za kutosha.
Sudan Kusini Salva Kiir alipokea chanjo ya corona wiki iliyopita.
Déby alikuwa amewaahidi raia wa Chad amani, kabla ya kifo chake
Rais Idriss Déby, mtu muhimu katika mapambano dhidi ya wapiganaji wa Jihadi katika kanda ya Sahel Afrika Magharibi alikuwa ameahidi kuleta Amani kama sehemu ya kampeni zake za kuchaguliwa tena.
Mkurugenzi wake wa kampeni alisema alikuwa akiwatembelea wanajeshi wanaopigana na waasi kaskazini mwa mji mkuu Jumatatu kwahiyo aliamua kujiondoa katika sherehe za ushindi wake.
Kampeni yake ya Mbele kwa ajili ya mabadiliko na Concord nchini Chadilianza katika siku ya uchaguzi kwa kushambulia kituo cha mpaka wan chi hiyo na Libya.
Upiga kura wa mapema mwezi huu ulikuwa wa ushindani mkubwa na wagombea wa upiunzani walilazimika kujiondoa kwenye uchaguzi wakisema wanashambuliwa na vikosiu vya taifa.
Rais Déby amekuwa akikosolewa kwa ukiukaji wa haki za binadamu lakini amekuwa akionekana kama mshirika muhimu wa usalama na nchi kama Ufaransa na nchi nyingine katika kanda hiyo kama katika mapambano dhidi ya Boko Haram na makundi mengineyenye uhusiano al-Qaeda ana Islamic State.
La muhimu pia majirani wa Chad, Libya, Sudan na Jamuhuri ya Afrika ya kati ambao wamekabiliwa na ukosefu wa usalama katika miaka ya hivi karibuni.
Unaweza pia kusoma:
Marekani iliikabidhi Zanzibar vifaa ya kukabiliana Covid -19
Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ilikabidhi vifaa vya UVIKO-19 kwa Wizara ya Afya ya Zanzibar.
Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani kwenye mtandao wake Twitter inasema Mradi wa USAID wa Mnyororo wa Ugavi wa Afya Duniani hivi karibuni ulinunua vifaa vya upumuaji na usafi wa mazingira vyenye thamani ya Dola za Marekani $400,000.
Vifaa hivyo viliwasilishwa mwezi uliopita Bandari ya Zanzibar na kusambazwa kwenye vituo vya umma vya kutolea huduma za afya kupitia bohari kuu ya madawa.
‘’Shehena hiyo inajumuisha vifaa vya kupumulia kama vile vipimo vya mwenendo wa damu, mirija ya kupimia puani kwa watoto na watu wazima, barakoa; na vifaa vya usafi wa mazingira kama vile dawa za mkoba za kunyunyizia, na mifuko ya kuwekea taka hatarishi’’, inasema taarifa hiyo.
Akizungumzia kuhusu utoaji wa vifaa tiba, Dk Abdullah S. Ali, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto, Zanzibar alisema “Tunaamini katika uhusiano wa ushirikiano ambao unatoa huduma bora za afya kwa watu wote. Shehena ya vifaa tiba vilivyopokelewa vitaziba mapengo yaliyopo katika kupunguza hofu inayohusishwa na tishio la UVIKO- 19 kwa suala la vifo, maradhi na kulazwa hospitalini. ”
Taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa:’’ Katika miezi ya hivi karibuni, anuwai mpya ya virusi vya korona imesababisha wimbi lingine kali zaidi la maambukizi ulimwenguni, pamoja na bara la Afrika. Imekuwa wazi kuwa virusi viko Tanzania pia.
Serikali ya Marekani imejitolea kufanya kazi bega kwa bega na washirika wote katika sekta ya afya ya Tanzania ili kupunguza athari za UVIKO-19. Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, Marekani imetoa Dola za Marekani milioni 16.4 kupunguza UVIKO-19 nchini Tanzania’’.
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt.Donald J. Wright alisema “Chanjo zimesaidia kutokomeza baadhi ya magonjwa mabaya zaidi duniani, na hakuna shaka kuwa kampeni ya chanjo kwa wote ya UVIKO-19 itaokoa maisha.”
Balozi Wright aliendelea, “Mbali na kutekeleza tahadhari za msingi za kuzuia kuenea kwa UVIKO-19, ni muhimu kukusanya na kuripoti habari kuhusu upimaji na visa. Kufanya hivyo kunafanya serikali kujua ikiwa hatua za kukabiliana zina matokeo yanayokusudiwa. Kwa kushirikisha taarifa hii kunawahakikishia raia kwamba serikali zao zinapambana kulinda afya zao na maisha yao.”, imesema taarifa hiyo.
Polisi wa Tanzania wathibitisha kumkamata na kumuachilia Kajala na mwanawe Paula
Muigizaji nyota nchini Tanzania Kajala na mwanawe Paula walikamatwa kwa saa kadhaa na kufanyiwa mahojiano na maafisa wa polisi kabla ya kuachiliwa kwa dhamana kwa madai ya kusambaza picha za utupu zinazodaiwa kutoka kwa nyota wa muziki nchini Tanzania Harmonize.
Taarifa hiyo imethibitishwa na afisa mkuu wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Lazaro Mambosasa aliyesema kwamba mama na mwanawe walikamatwa na kuachiliwa baada ya kuwasili nchini humo kutoka Dubai.
Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, ripoti za kukamatwa kwao zilianza kusambaa mtandaoni hapo jana na hii leo Mambosasa alithibitisha kwamba walikamatwa usiku wa kuamkia jana na kuhojiwa na polisi lakini wakaachiliwa kwa dhamana saa kadhaa baadaye.
Kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Dar es Salaam alisema kwamba mashtaka dhidi yao ni ya kusambaza picha za utupu za Harmonize mtandaoni na kwamba msanii huyo ndiye mlalamishi.
‘’Ni kweli kwamba tulimkamata Kajala na mwanawe Paula na kuwahoji kwa saa kadhaa baada ya Harmonise kuwasili katika kituo cha polisi ,lakini tumewaachilia kwa dhamana’’, alisema Mambosasa.
Alinukuliwa na The Citizen Tanzania akisema kwamba wawili hao wataendelea kuripoti katika kituo hicho cha polisi hadi pale uchunguzi utakapokamilika na kuwasilishwa mahakamani kwa kuwa kesi kama hizo huchukua muda mrefu kuchunguza.
Wakati huohuo kamanda Mambosasa amesema kwamba Rayvanny, Babalevo na Juma Lokole pia wametuhumiwa na Harmoniza kwa kusambaza picha za utupu na tayari wamehojiwa na maafisa wa polisi na uchunguzi unaendelea.
Siku tano zilizopita, Harmonize kupitia mtandao wake wa instagram alisema kwamba atawawasilisha mahakamani malalamishi yake na kuomba kulipwa fidia na wale wanaomchafulia jina lake mtandaoni kupitia kusambaza picha zake za utupu.
Polisi wamuokoa mtoto aliyefungwa kwa miaka 10
Polisi nchini nigeria wamemuokoa msichana ambaye alifungiwa ndani ya chumba na wazazi wake kwa miaka 10 katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano.
Polisi imesema kuwa msichana huyo alitoroshwa Jumatatu baada kupewa taarifa na mama yake mwenye umri wa miaka 35, amekamatwa huku baba yake akiwa ametoroka.
Polisi imesema kuwa msichana huyo amekuwa ndani tangu alipokuwa na umri wa miaka mitano, katika mazingira machafu na bila kulishwa vyema chakula, imeripoti idhaa ya lugha ya Pidgin ya BBC.
Msichana huyo mwenye umri wa miaka 15 sasa anapewa matibabu katika hospitali ya Murtala Mohammed.
Mwaka jana, kulikuwa na visa vya polisi kuwaokoa watu waliofungwa na namna hiyo hadi miaka mine kote nchini Nigeria.
Urusi yampeleka hospitalini mkosoaji mkuu wa utwala wa Putin
Kiongozi wa upinzaji wa Urusi Alexei Navalny amehamishiwa hospitali ya gereza, ambapo mamlaka inasema hali yake ni "ya kuridhisha".
Amekuwa kwenye mgomo wa kususia kula kwa siku 20, akilalamika juu ya matibabu duni. Sasa yuko Vladimir, jiji la umbali wa kilomita 180 (maili 112) mashariki mwa Moscow.
Huduma ya gereza ,FSIN inasema anachunguzwa na daktari kila siku na amekubali kuchukua vitamini.
Navalny aliwekewa sumu ya kulemaza neva mnamo Agosti iliyopita na alinusurika kifo kwa tundu la sindano .
Baada ya kuhamishiwa hadi kitengo cha wagonjwa mahututi huko Berlin, wataalamu wa sumu walisema sumu hiyo ilikuwa ya kiwango cha silaha ya Urusi, Novichok.
Serikali za Magharibi zililaumu serikali ya Urusi kwa shambulio hilo, na Navalny alimlaumu Rais Vladimir Putin moja kwa moja. Kremlin ilikana kuhusika kwa njia yoyote na ilipinga matokeo hayo kuhusu sumu aliyowekewa Novichok.
Mapato ya mrembo mwenye ushawishi yazuiwa YouTube baada ya kuwatumia jumbe za ngono wavulana
Mtandao wa kijamii wa YouTube umetangaza kuwa umezuia kwa muda mapato ya fedha ya mrembo mwenye ushawishi baada ya kutuma jumbe za ngono kwa wavulana wawili
Mapema mwezi huu, mrembo huyo mwanaume kwa jina James Charles alikiri kutuma jumbe za wazi za ngono kwa wavulana wawili wenye umri wa miaka 16.
YouTube imeithibitishia BBC kwamba Charles mwenye umri wa miaka 21 ameondolewa kwa muda katika mpango wa ushirika na mtandao huo.
Mpango huo unawaruhusu watumiaji wa YouTube (YouTubers) kutumia maudhui yao kwa ajili kupata fedha.
.
Hawakusema hata hivyo ni kwa muda gani hataweza kutumia mtandao huo kwa kipato cha pesa.
Msemaji wa YouTube amesema kampuni hiyo inatekeleza sera yake ya uwajibikaji, ambayo inasema: "kama tukiona kwamba mienendo na tabia ya mbunifu wa maudhui ya jukwaa yanawadhuru watumiaji, jamii, waajiriwa, au bayo anuwai, tunaweza kuhitaji kuchukua hatua kuilinda jamii ."
Wahitimu wa shule za sekondari walala nje kutokana sheria ya 'Lockdown' Kenya
Wanafunzi waliomaliza kidato cha nne wamelala katika bustani ya umma ,Uhuru Park jijini Nairobi baada ya kushindwa kupata usafiri wa kwenda nyumbani kwa sababu ya zuio la usafiri linalotekelezwa sasa katika kauti tano nchini Kenya .
Hii ni baada ya kushindwa kuendelea na safari yao ya kuelekea nyumbani baada ya muda wa amri ya kutotoka nje kuwapata wakiwa bado hawajaondoka mjini humo kuelekea makwao walipomaliza kuufanya mtihani wao wa mwisho .
Rais Uhuru Kenyatta alitangaza amri ya kukaa nyumbani katika kaunti 5 ukiwemo mji wa Nairobi ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Amri hiyo inatekelezwa ikiambatana na amri ya kutotoka nje usiku kuanzia saa mbili usiku hadi saa kumi alfajiri.
Vituo vya habari nchini humo vimekua vikitoa taarifa kuhusu namna wanafunzi hao walivyohangaika kupata usafiri na jinsi amri ya kutotoka nje ilivyoathiri usafiri na shughuli mbalimbali mjini Naiirobi .
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 20.04.2021