Waliochoma chanjo ya corona tu ndio wataruhusiwa kuhiji Mecca mwaka huu
Mamlaka ya nchini Saudi Arabia imesema watu waliopata chanjo ya corona tu ndio wataruhusiwa kuhiji Mecca mwaka huu.
Moja kwa moja
Esther Namuhisa
Mama mjamzito ashinda medali ya dhahabu ya mchezo wa Taikondo
Mwanariadha wa Nigeria wa mchezo wa taikondo ameshinda medali ya dhahabu katika kiwango cha taifa huku akiwa na ujauzito wa miezi nane.
Aminat Idrees alikuwa katika kipengele cha wanawake na wanaume, akiwa na mchezaji mwenzake ambaye ni mwanaume Arowora Roqeeb, katika michezo ya kitaifa iliyofanyika jimbo la Edo.
Idrees na Roqeeb walikuwa wanawakilisha Lagos katika michuano hiyo.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Ukinizingua...Tunazinguana – Rais Samia Suluhu Hassan
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yusuf Juma
- Nafasi, BBC Swahili

Rais wa Tanzania Samia Suluhu amewapa watendaji wake tasiwra ya jinsi atakavyokabiliana na wale wambao hawatafanya kazi alizowapa kwa njia inayotakiwa. Wakati akiwaapisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa taasisi za serikali aliyowateua mwishoni mwa wiki rais Samia alionekana kutoa ishara ya jinsi atavyowakabili watendaji wazembe
“Wewe ni kijana mimi ni mama ,ukinizingua tutazinguana,” alimuambia mkurugenzi mkuu wa Wakala wa Meli Tanzania (Tasac), Kaimu Mkeyenge muda mfupi baada ya hafla hiyo ya kula kiapo .
Katika maelezo yake rais Samia amesema amemteua Mkeyenge kushika nafasi hiyo ili asafishe madudu yaliyopo kwenye taasisi hiyo.
“Ulikuwa ndani ya Tasac unayajua madudu yaliyopo. Jambo lililoniudhi zaidi kwa mwaka mmoja mmefanya vikao 23 vya bodi na imetumiwa karibu Sh 600 milioni, ukiangalia kilichozungumzwa na tija ya vikao hivyo hakuna.”
“Nataka ukafanye kazi na sio kwenda kupandisha mabega kwa wenzio uliowaacha, kama kuna makundi ukayaondoe, tunataka Tasac izalishe. Nasisitiza kafanye kazi ukinizingua tutazinguana,” amesema.
Rais Samia pia amempa miezi sita mkurugenzi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Erick Hamis kuhakikisha mambo yanakwenda kama inavyostahili.
Virusi vya corona: Maharusi wakesha uwanja wa mpira siku yao ya harusi

Chanzo cha picha, Rwanda TV
Picha na video za bibi na bwana harusi wakiwa pamoja na familia zao zimepigwa wakiwa wamekesha katika uwanja wa mpira katika siku ya harusi yao kwa kukiuka masharti dhidi ya kujikinga na corona. Jambo ambalo limesababisha raia wengi wa Rwanda kukosoa kitendo hicho.
Polisi katika mji mkuu wa Kigali nchini Rwanda walisitisha harusi tatu katika sikukuu za pasaka kwa kosa la kukiuka masharti yaliyowekwa dhidi ya corona ya kukataza sherehe na kuwa na kikomo cha watu 20 pekee cha wageni wa kwenye harusi.
"Bibi harusi kukesha kwenye uwanja wa mpira usiku wote wa siku ya harusi yake ni kumbukumbu mbaya sana na haiwezi kusahaulika katika maisha yangu", bibi harusi asema.
“Ni maumivu yasiyoelezeka na kudhalilisha watu kiasi hiki hakuwezi kutufanya kuiogopa corona au kufuata masharti yaliyowekwa ” – aliiambia BBC.
Msemaji wa polisi ameviambia vyombo vya habari kuwa kuna watu wengine zaidi wanafanya sherehe na kukiuka masharti yaliyowekwa dhidi ya corona na polisi hawataruhusu haya yaendelee.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Baadhi ya watu wamekosoa tukio hilo katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa wamevuka mipaka na hakuna sheria inayosema watu inabidi wazuiliwe usiku mzima , wengine walisifia hatua hiyo dhidi Covid ili kuhakiksha wanakuwa salama.
Clarisse Karasira, mwanamuziki kutoka Rwanda ameandika katika kurasa yake kuwa umekosa utu na kuongeza kuwa ni jambo linaloleta machungu kwa wapenzi hao waliokuwa wameoana.
Rwanda imesifiwa kimataifa kwa jinsi inavyokabiliana na janga la virusi vya corona lakini wanaharakati wameikosoa kwa kukiuka haki za binadamu katika hatua wanazozichukua kuhakikisha jitihada hizo zinafanikiwa.
Rwanda imerikodi zaidi ya watu 22,000 waliopata virusi vya corona na vifo 311 vilivyosababishwa na virusi hivyo.
Lupita atembelea Serengeti kwa mara ya kwanza

Chanzo cha picha, Lupita-Twitter
Nyota wa Hollywood kutoka nchini Kenya Lupita Nyong'o ametembelea kwa mara ya kwanza mbuga ya wanyama ya Tanzania ya Serengeti, Aprili 5, 2021,.
Mwanamitindo huyo muigizaji alipiga picha na kuiweka kwenye mitandao yake ya kijamii na kuandika serengeti.
Picha hiyo aliyojipiga mwenyewe yaani selfie inaonesha mazingira ya mbuga hiyo na kukiwa na tembo nyuma yake.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Miezi michache iliyopita, kulitokea gumzo la kwanini Lupita hakupewa ubalozi wa utalii nchini Kenya na kupewa mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell.
Lakini waziri wa Utalii nchini Kenya Najib Balala alitetea uamuzi wa kumtaja mwanamitindo wa Uingereza Naomi Campbell kuwa balozi wa utalii kimataifa kwa nchi hiyo.
Wakati wa hafla ya umma, Bwana Balala alisema anajua Wakenya wengi wameuliza kwanini muigizaji wa Hollywood Lupita Nyong'o hakuchaguliwa katika nafasi hiyo.
Waziri akajibu kwamba wamekuwa wakimtafuta Bi. Nyong'o lakini hajapatikana kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Muigizaji huyo wa Kenya ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya Oscar alipendekezwa na Wakenya katika mitandao ya kijamii kuwa mtu sahihi wa kushikilia nafasi ya balozi wa utalii kimataifa kuwakilisha Kenya.
Bwana Balala alisema Bi. Campbell amechukua nafasi hiyo kwa maslahi ya umma na kwamba serikali inafanyia kazi namna ya kutumia ushawishi wake kutangaza utalii, kulingana na vyombo vya habari vya nchini Kenya.
- Lupita Nyong'o adai kunyanyaswa kijinsia na Weinstein
- Lupita Nyong'o alikosoa jarida kwa kuhariri picha yake
Kwa nini Jay Z ameghadhabisha Waislamu Lamu, Kenya?
Mwanamuziki maarufu wa mziki wa Hip Hop wa Marekani Jay Z asababisha hasira miongoni mwa baadhi wa wenyeji wa kaunti ya Lamu baada ya kuonekana amevaa fulana yenye picha ya msikiti wa eneo hilo.
Wenyeji na wawakilishi wa msikiti wa Riyadha ambacho pia ni kituo kinachotoa mafunzo ya dini ya Kiislamu, wameghadhabishwa na mbunifu mmoja nchini Kenya aliyemtengenezea fulana hiyo kwa madai kwamba anatumia vibaya picha ya msikiti wa Lamu.
Hayo yamejiri baada ya Jay Z ambaye pia ni mfayabishara kuonekana akitoka kwenye eneo moja la burudani huko California akiwa amevaa fulana hiyo.
Hata hivyo, usimamizi wa msikiti wa Riyadha umeelekeza hasira zake kwa mbunifu wa fulana hiyo, Zeddie Lukoye, ambaye kampuni yake imekuwa ikielimisha watu kote duniani juu ya historia, asili na taarifa za habari.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
UN yahofia wakimbizi wa Msumbiji wanaolazimishwa kurudi kwao na Tanzania

Chanzo cha picha, EPA
Umoja wa Mataifa umetoa tahadhari kuhusu ripoti ya Tanzania kuwalazimisha mamia ya wakimbizi wa Msumbiji waliokimbia wanamgambo wa kijihadi mwezi uliopita kurejea kwao.
Maelfu ya watu wamekimbilia msituni wakati wanamgambo wa kiislamu walipoanza kushambulia kaskazini mashariki mwa mji wa Palma mwezi Machi tarehe 24, ambapo wanamgambo hao wanaripotiwa walikuwa wakiwachinja wananchi.
Kuna wengine ambao wamekwama msituni wakiwa na changamoto ya upatikanaji wa chakula na maji, baadhi walikimbilia kusini na wengine kaskazini katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika Wakimbizi (UNHCR) limesema limepokea ripoti kuwa wakimbizi wa Msumbiji wapatao 600 waliokimbilia Tanzania wametakiwa kurejea kwao.
"UNHCR ina wasiwasi juu ya familia zilizozuiwa makazi au kulazimishwa kurudi kwao na Tanzania," taarifa imeeleza.
Serikali ya Tanzania haijatoa tamko lolote kuhusu taarifa hiyo, AFP imeeleza.
Kumekuwa na ghasia nchini Msumbiji katika mji wenye utajiri wa gesi, Cabo Delgado tangu mwaka 2017.
Shambulio la mwezi Marchi lililotokea Palma limelazimisha watu wapatao 10,000 kukimbia makazi yao, kwa mujibu wa UNHCR.
Watu kadhaa wameuawa , wakiwemo raia wawili wa kigeni ingawa hakuna taarifa rasmi kuhusu idadi ya vifo vilivyotokea.
Wasiwasi wa usalama baada ya shambulio hilo umefanya kampuni kubwa ya kifaransa ya mafuta Total kuondoa katika eneo hilo ambalo walikuwa wamewekeza mabilioni ya fedha katika mradi wa gesi huko Afungi peninsula,kilomita chache kutoka Palma.
UN pia imelazimika kusitisha operesheni zake za ndege kutoka Afungi, lna kusababisha maelfu ya watu kuwa na sintofahamu.
Taasisi ya majanga nchini Msumbiji imesema Jumatatu kuwa watu wapata 30,000 wanahitaji kupatiwa misaada ya kibinadamu.
Wafanyakazi wa mashirika ya msaada na wamishionari kwa sasa wanawasaidia mamia ya wakimbizi waliokimbia makazi yao katika mji wa Pemba.
Wengi wa wakimbizi wanasaidiwa na ndugu na marafiki, UNHCR imesema.
Mapigano hayo yamesababisha watu zaidi ya 2,600 kuuawa, nusu yake wakiwa raia na watu wapatao 700,000 kukimbia makazi yao.
Unaweza kusoma pia:
- Wanamgambo wa Kiislamu 'wawavamia wafanyakazi waliokuwa wakitoroka hotelini'
- Wanamgambo na 'laana' ya utajiri wa gesi na madini ya rubi Msumbiji
- Kwanini wanajeshi wa Marekani wamo nchini humo?.
Rais Samia akiapisha Makatibu Wakuu na Wakuu wa taasisi za serikali


Maelezo ya picha, Alan Kijazi Katibu mkuu wa Mali Asili na utalii 
Maelezo ya picha, Makatibu wakuu na wakuu wa taasisi 


Chanzo cha picha, BB
Rais Samia ataka uhuru wa vyombo vya habari uheshimiwe

Chanzo cha picha, IKULU-Tanzania
Rais wa Tanzania Bi.Samia Suluhu Hassan amesema ni muhimu kusimamia vyombo vya habari vya ndani.
Rais Samia amesema "nasikia kuna vyombo vya habari vilivyofungiwa fungiwa na TV za mikono, vifungulieni na vifuate sheria na muongozo wa serikali".
Aliongeza kusisitiza kuwa ;"Tusiwape mdomo wa kusema kuwa tunaminya uhuru wa vyombo habari."
Aidha Rais Samia amesema wahakikishe kuwa kila atakayepewa ruhusa ya kuendesha chombo cha habari anafuata sheria za serikali na kanuni ziwe wazi kuwa kosa ili adhabu yake ilingane na adhabu inayotolewa.
"Tusifungie tu kibabe, wafungulieni lakini hakikisha wanafuata miongozo ya serikali".
- Rais wa Tanzania kuunda kamati ya wataalamu kumshauri
Sudan yatangaza hali ya tahadhari baada ya watu 40 kuuawa Darfur

Chanzo cha picha, AFP
Sudan imetangaza hali ya dharura Magharibi mwa Darfur kufuatia mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yaliyosababisha watu 40 kufariki na maelfu kukimbia makazi yao.
Jumatatu, Umoja wa mataifa umesema watu wapatao 40 waliuawa na zaidi ya watu 50 walijeruhiwa katika ghasia zilizotokea siku ya Jumamosi kati ya makundi ya kiarabu na wasio katika makundi ya jamii ya kiarabu katika mji wa El Geneina.
Milio ya risasi ilisikika katika maeneo ya jirani ya Hay Al Jabal na Al Jamarik siku ya Jumatatu mchana, Umoja wa mataifa umesema.
Hali ya usalama bado inatia hofu katika mji huo kwa kuwa kila upande unachochea wanajeshi wake, aliongeza.
Operesheni mbalimbali za msaada zimesitishwa mpaka hali irejee kuwa nzuri.
Mji huu ambao umekuwa eneo la kupokea misaada na zaidi ya watu 700,000 wameathirika na mgogoro huo, kwa mujibu wa UN.
Mwezi Januari, mgogoro kati ya jamii ya Massalit na jamii ya kiarabu umesababisha vifo vya watu wapatao 129 na watu zaidi ya 108,000 kukimbia makazi yao na kupelekea kuishi katika shule na maeneo ya afya.
Uganda kumpatia ardhi mwanamuziki mashuhuri Marekani, Akon
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Isack Mumena
- Nafasi, BBC Swahili Kampala

Chanzo cha picha, Twitter-Museveni
Waziri wa ardhi nchini Uganda Dkt.Chris Barayamunsi amewaambia wandishi wa habari pamoja na msanii huyo kuwa serikali inapatia aridhi ya ekari ya mraba mmoja katika eneo lolote ambalo mwanamuziki huyo atalitaka nchini humo.
Mwanamuziki mashuhuri na mzaliwa Senegal, Akon aliwasili nchini Uganda mwishoni mwa juma akiambatana na mkewe Rozina Negusei, ambapo wanaenda kuwekeza Dolla milioni $12 nchini Uganda katika tasnia mitindo.
Msanii huyo alikutana na Rais Museveni nyumbani kwake Rwakitura baada ya Museveni kumutumia Elikoputa ya jeshi la UPDF mwishoni mwa juma.
Kwenye mkutano na wandishi habari hapo jana, Akon ameahidi kuwekeza nchini Uganda katika sekita ya utalii, nishati na miundo mbinu chini ya kampuni yake ya Akon Lighting Afrika.
Pia ameahidi kutangaza jina la Uganda kimataifa, amesema jumuiya za kimataifa zinazungumza mabaya tu kwa Uganda yaliyofanywa katika utawala wa aliyekuwa rais wa zamani wa Uganda Idd Amin.
Msanii huyo amechaguwa Uganda kuwa makao makuu ya mradi wake wa kuboresha miji barani Afrika yaani Acon City Projects mataifa mengine katika mradi huo ni Senegal anakozaliwa,Ghana na Ethiopia.
- Akon afanya ziara nchini Uganda
Waliochoma chanjo ya corona tu ndio wataruhusiwa kuhiji Mecca mwaka huu

Mamlaka za nchini Saudi Arabia zimesema watu waliopata chanjo ya corona peke yake ndio wataruhusiwa kufanya ibada ya Hija mwaka huu huko Mecca.
Wizara ya Hija na Umrah imetoa taarifa kuwa watu waliopata chanjo pekee ndio watakuwa na vigezo vya kujihi mwaka huu katika mji mtakatifu wa Mecca.
"Watu ambao tayari wamepata chanjo dozi mbili za COVID-19, na wale ambao wamepata chanjo dozi moja ya corona siku 14 kabla ya Hija au mtu ambaye ametoka kupona corona", wizara imesema.
Wizara hiyo imesema pia kuwa itazingatia taratibu zote za kujikinga dhidi ya maambukizi ya corona.
Haijawekwa wazi kama sera hiyo itaendelea mpaka wakati wa Hija kuu baadae mwaka huu.
Saudi Arabia imeripoti kuwa na maambukizi ya virusi vya corona zaidi vya zaidi ya watu 393,000 na zaidi ya vifo 6,700 vinavyotokana na virusi hivyo.
Wizara ya afya ya taifa hilo imesema watu zaidi ya milioni tano wamepata chanjo dhidi ya corona, katika taifa lenye watu zaidi ya milioni 34.
Mwezi uliopita mfalme Salman alimbadilisha waziri wa Hija , alafu mwezi mmoja baadae ilifanyika Hija ndogo katika mfumo mpya wa kihistoria kutokana na changamoto ya virusi vya corona.
Mwaka jana, waislamu 10,000 ambao ni wakazi wa Saudi Arabia ndio waliruhusiwa katika Hija takatifu mwaka jana,ingawa mara zote huwa ni watu milioni 2.5 kutoka duniani kote na ndio walishiriki mwaka 2019.
Habari...karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili leo 06/04/2021.
