Marais waahidi kushirikiana na Rais Samia Suluhu Hassan

Marais waliohudhuria shughuli za kuaga mwili wa hayati rais Magufuli wasema wako tayari kushirikiana na Rais Samia Suluhu

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu, Dinah Gahamanyi and Lizzy Masinga

  1. Museveni aomboleza kwa kusaini kitabu ubalozi wa Tanzania nchini Uganda

    Rais Yoweri Museveni akiwa na mkewe mama Janet Museveni

    Chanzo cha picha, MUSEVENI/TWITTER

    Rais Yoweri Museveni akiwa na mkewe mama Janet Museveni wameongoza raia wa Uganda katika maombolezo ya aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati Dk.John Pombe Magufuli kwa kusaini kitabu cha maombolezo kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo mtaa wa Kagera mjini Kampala.

    Uganda na Tanzania wamekuwa na ushirikiano mkubwa na ushirikiano wao umeongezeka zaidi tangu alipoingia madarakani Rais Yoweri Museveni mwaka 1986, ndiyo sababu Rais Museveni alitangaza bendera kupeperushwa nusu mlingoti hadi siku ya mazishi siku ya Ijumaa nyumbani kwao wilayani Chato mkoa wa Geita.

    Rais Museveni katika hotuba yake fupi amefahamisha kwamba siku ya leo Hayati Magufuli na yeye Rais Museveni pamoja na kampuni ya Total walipanga kusaini rasmi mkataba wa kuanza ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima Uganda hadi bandari ya Tanga.

    Pia amekumbusha katika barua aliyomuandikia hayati Magufuli alimfahamisha kwamba sherehe ya leo ingekuwa sherehe ya mara mbili ya sherehe ya siku jeshi la Tanzania JWTZ lilipoingia wilayani Mbarara nchini Uganda magharibi kuondoa utawala wa Idd Amin.

    Katika ubalozi wa Tanzania raia wa Tanzania wakiongozwa na Balozi wa Tanzania Dk.Mlima walifanya ibada ya kumuombea Hayati Dk.John Pombe Magufuli.

  2. Kifo cha Magufuli:Marais mbalimbali wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa hayati Magufuli

    Marais na wawakilishi kutoka nchi mbalimbali walipokuwa wakitoa heshima zao za mwisho kumuaga aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Dkt. John Pombe Magufuli kwenye shughuli ya kuaga iliyofanyika leo tarehe 22 Machi, 2021 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

    m

    Chanzo cha picha, MAELEZO

    N

    Chanzo cha picha, MAELEZO

    M

    Chanzo cha picha, MAELEZO

    M

    Chanzo cha picha, MAELEZO

    M

    Chanzo cha picha, MAELEZO

  3. Rais Kenyatta asifiwa kwa kusitisha kwa muda hotuba yake kwa ajili ya adhana

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiaga mwili wa Hayati Magufuli

    Chanzo cha picha, Habari Maelezo Tanzania

    Maelezo ya picha, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akiaga mwili wa Hayati Magufuli

    Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesimamisha hotuba yake kwa zaidi ya dakika moja kupisha wito wa swala (adhana) ya adhuhuri wakati akitoa salamu za pole kwa Watanzania katika shughuli ya kumuaga aliyekuwa Rais wa taifa hilo, John Magufuli.

    Wakati akianza kutoa salamu zake katika uwanja wa Uhuru jijini Dodoma adhana ilisikika kutoka katika msikiti uliopo karibu na uwanja huo na kumfanya Rais Kenyatta kusitisha kwa muda kutoa hotuba yake na adhana ilipomalizika aliendelea na maelfu ya watu waliopo uwanjani hapo walimpigia makofi.

    Katika hotuba yake Kenyatta amemwomba Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuendeleza falsafa ya Hapa Kazi Tu aliyoiacha Magufuli kwa kuwa inawafanya Watanzania kuwa na moyo wa ushujaa na kusonga mbele.

    Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya nchi ya Kenya, na Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa mwenyekiti wake Kenyatta amesema wanaomboleza kumpoteza John Magufuli, rais aliyeheshimika si tu Tanzania bali Afrika Mashariki, Afrika nzima na dunia yote.

    ''Kwa muda wa miaka michache ameonesha sisi kama Waafrika tuko na uwezo wa kujitoa katika utegemezi wa watu na nchi za nje na tuna uwezo kama Waafrika kusimamia uchumi wetu na kuhakikisha kuwa wananchi wetu wametendewa haki.'' ameeleza Rais Kenyatta.

    Amemtaka Rais Samia kujipa moyo wa ushujaa bila kuteteleka na kuwa Kenya itakuwa pamoja naye wakati wote. "Katika maandiko ya Biblia Mungu alimwambia Joshua kuwa ‘uwe hodari na moyo wa ushujaa na usiogope kokote uendako Mungu yu pamoja nawe’," amesema Uhuru.

    Amesema enzi za uhai wa Magufuli walizungumza kuhusu maendeleo na usalama wa nchi hizo mbili.

    Rais Kenyatta amezungumzia maamuzi aliyokuwa akiyafanya Magufuli kuhusu miradi mikubwa aliyoitekeleza Magufuli bila kutegemea mataifa ama watu wa nje.

  4. Samia Suluhu: Nilipata ugumu kutangaza kifo cha hayati John Magufuli Rais wa Tanzania

    sAMIA

    Rais Samia Suluhu Hassan amesema alipata wakati mgumu sana kutangaza kifo cha mtangulizi wake John Magufuli kilichotokea Machi 17, 2021 katika hospitali ya Mzena mkoani Dar es Salaam na kuwataka Watanzania kuamini kuwa kwa sasa yeye ndiye yupo katika usukani wa kuiendesha nchi.

    Akizungumza leo wakati wa shughuli ya kitaifa ya kuaga mwili wa kiongozi huyo katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, Rais Samia amesema siku hiyo kuwa ngumu na leo ilikuwa siku ya pili kwa ugumu kwake anapotoa hotuba mbele ya jeneza lenye mwili wa mtangulizi wake.

    "Nilipotakiwa kutangaza msiba wa Rais wangu nilipata wakati mgumu, nilijiuliza kama vile namkosea kiongozi wangu, lakini nikaambiwa mimi ndiyo natakiwa kufanya hivyo," amesema Rais Samia.

    Hata hivyo Rais Samia amesisitiza kuwa mtangulizi wake amemuachia mema yatakayokumbukwa wakati huu na vizazi vijavyo ikiwemo utendaji kazi wake ambao aliona muda wa saa 24 kwake haukuwa ukimtosha.

    Bi.Samia amewataka Watanzania wenye mashaka watambue aliyesimama uwanjani hapo ni Rais licha ya kuwa yeye ni mwanamke. Amesema yuko imara kutokana na namna alivyolelewa na mtangulizi wake huyo kwa hiyo haoni kama kuna mahali watu wanaweza kuwa na hofu naye.

  5. Felix Tshisekedi: 'Magufuli mtetezi wa kiuchumi Afrika'

    Rais wa DRC, Felix Tshisekedi

    Chanzo cha picha, Habari Maelezo Tanzania

    Rais wa DRC Felix Tshisekedi na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika amesema DRC na Umoja wa Afrika kwa pamoja wamesikitishwa na kifo cha 'mwanamapinduzi' Dkt John Magufuli.

    ''Msiba huu si tu unagusa Watanzania pekee, bali kifo chake kimegusa bara zima la Afrika...bara la Afrika linajikuta yatima.. alilenga kuboresha maisha ya wananchi wake, pia aliyekuwa akitetea, kuendeleza uchumi kwenye bara letu la Afrika.

    ''Tutabaki na kumbukumbu ya Hayati Magufuli ya mtu mpiganaji, mzalendo si tu kwa maslahi ya Tanzania, bali pia kwa Umoja wa Afrika''.Alisema Rais Tshsekedi.

    Felix Tshsekedi amesema Hayati Magufuli alikuwa mtetezi mkuu wa uhuru wa kitamaduni na kiuchumi wa bara la Afrika, aliyekuwa akilenga kutimiza ndoto ya waasisi wa mataifa ya Afrika uliolenga kuleta umoja ndani ya bara hilo.

  6. Uhuru Kenyatta: 'Nimepoteza rafiki'

    Rais Uhuru Kenyatta akisaini kitabu cha wageni

    Chanzo cha picha, Habari Maelezo Tanzania

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa amempoteza rafiki.

    Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya nchi ya Kenya, na Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa mwenyekiti wake Kenyatta amesema wanaomboleza kumpoteza John Magufuli, rais aliyeheshimika si tu Tanzania bali Afrika Mashariki, Afrika nzima na dunia yote.

    ''Kwa muda wa miaka michache ameonesha sisi kama Waafrika tuko na uwezo wa kujitoa katika utegemezi wa watu na nchi za nje na tuna uwezo kama Waafrika kusimamia uchumi wetu na kuhakikisha kuwa wananchi wetu wametendewa haki.'' ameeleza Rais Kenyatta.

  7. Kwa picha: Wakazi wa Dodoma walivyoupokea msafara ulioubeba mwili wa Magufuli

    Watanzania
    Maelezo ya picha, Baadhi ya akinamama walivalia kanga maalumu zilizotengenezwa kwa ajili ya kumuenzi Bw Magufuli
    Watanzania
    Maelezo ya picha, Baadhi wa Wakazi hawa wa Dodoma walilazimika kupanda juu ya lundo la mbao ili walau kupata picha ya msafara wa magari ulioubeba mwili wa aliyekuwa rais wao
    Watanzania
    Maelezo ya picha, Baadhi walibeba kanga zilizotengenezwa rasmi kwa ajli ya kumuaga Dkt John Pombe Magufuli kuonyesha hisia zao na jinsi watakavyomkumbuka rais huyo wa awamu ya tano
    Watanzania
    Maelezo ya picha, Maelfu walijipaga kando ya barabara na mitaa ya jiji la Dodoma kupokea msafara wa magari yaliyoubeba mwili wa aliyekuwa rais wao
  8. Mwili wa Hayati Magufuli wawasili uwanja wa Jamhuri

    Mwili wa Hayati Magufuli umewasili kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma tayari kuagwa.

    TZ
  9. ‘Magufuli aliongoza maombi kabla ya kukata roho’

    Magufuli

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Hayati Dkt John Pombe Magufuli alikuwa na uhusiano wa karibu na viongozi wa dini nchini Tanzania

    Aliyekuwa rais wa Tanzania Hayati Dkt John Pombe Magufuli aliongoza sala na madaktari pamoja na wahudumu wake hospitalini kabla ya kuaga dunia , kulingana na msemaji wa familia , Ngusa Samike, limeripoti gazeti la Citizen.

    Msemaji wa familia amesema hayati Magufuli alipata sakramenti ya 'mpako wa wagonjwa' pamoja na dua akiwa pamoja na Askofu Mkuu wa zamani wa jimbo la Dar es salaam, Kadinali Polycarp Pengo, Padre wa Kanisa la St. Peter's Alister Makubi, na Sheikh Mkuu wa Tanzania , Abubakar Zubeir.

    Magufuli alifahamika kuwa na mahusiano ya karibu na viongozi wa kidini nchini Tanzania.

  10. Waziri Mkuu Majaliwa: 'Tumebadili utaratibu wa kuaga'

    Mwili wa Hayati Rais Magufuli ukiagwa Dodoma

    Serikali ya Tanzania imebadilisha utaratibu wa kuaga mwili wa aliyekuwa rais wa Tanzania, John Magufuli.

    Hayo yameelezwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza katika viwanja vya Bunge Makao Makuu ya serikali ya nchi hiyo, Dodoma.

    ‘’Kutokana na uzoefu tuliopata Dar es Salaam kwa siku mbili,watu ni wengi mno ratiba tumeibadilisha kidogo baada ya kuona matamanio ni makubwa

    ‘’Kuanzia jana, utaratibu wa kumuaga tumeubadilisha ili kila mmoja aweze angalau kuona jeneza kwa kufika pale kupata sala na baadae badala ya kwenda kuaga kwa kumwangalia tutakachokifanya ni kuzungusha mwili angalau mara mbili tatu uwanjani, halafu baadae tutapita kwenye mitaa maarufu ili watu wapate nafasi.Alisema Majaliwa.

    ‘’Tumeshuhudia watoto wadogo wa umri wa kati mpaka wazee, tukiruhusu kila mmoja kwenda pale (viwanjani) hatutamudu kwa sababu familia imetutaka mwili huu ulale siku ya tarehe 26’’. Alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

  11. Kwa picha: Mawaziri na wabunge wa Tanzania wamlilia Magufuli Dodoma

    dom
    dom
    Wabunge
    Wabunge
    Wabunge
    Wabunge
    b
  12. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa awasili Tanzania

    Rais Cyril Ramaphosa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amewasili nchini Tanzania, ataungana na Watanzania katika shughuli ya kitaifa ya kumuaga Hayati John Magufuli katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  13. Kamanda Mambosasa azungumzia waliojeruhiwa wakimuaga Magufuli

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa

    Chanzo cha picha, Mwananchi

    Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema baadhi ya wananchi walioshiriki shughuli ya kumuaga Rais John Magufuli wamejeruhiwa baada ya kukanyagwa na wenzao.

    Mambosasa ameielezea Mwananchi Digital kuhusu taarifa za kuwepo kwa watu waliojeruhiwa na kukimbizwa hospitali katika shughuli hiyo iliyofanyika Uwanja wa Uhuru na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya watu.

    Kutokana na wingi huo, shughuli ya kuaga ilisitishwa saa 9 alasiri na mwili wa kiongozi huyo ukiwa katika gari maalum ulizungushwa mara tano uwanjani hapo ili maelfu ya wananchi wapate fursa ya kuaga baada ya kuomba kutokana na kuelezwa kuwa wote hawataweza kupita mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa Magufuli.

    Raia wakiwa wamepanda kwenye uzio ulio kwenye lango kuu la kuingilia uwanjani

    Katika maelezo yake Mambosasa amesema hana idadi kamili ya watu waliojeruhiwa katika shughuli hiyo lakini ni wengi.

    “Binafsi sina idadi lakini ni watu wengi ambao walikanyagana na kukosa hewa. Walikuwa wanaanguka na kubebwa,” amesema Mambosasa.

    Msongamano ulikuwa mkubwa wa watu waliofika kuaga mwili wa hayati Rais John Magufuli huku wengine wakiwa nje wakisubiri kuingia na wengine kukosa uvumilivu licha ya tangazo kutolewa kuwa wote watafanikiwa kutoa heshima kwa kiongozi wao.

  14. Rais Tschisekedi alivyowasili Dar es salaam kwa ajili ya shughuli za kumuaga Magufuli

    Tschisekedi

    Chanzo cha picha, @foxtimecongo/Twitter

    Rais wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo Felix Tshisekedi amewasili Jumapili usiku jijini Dar es Salaam nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli ya ibada ya kumuaga Hayati John Pombe Magufuli.’

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  15. Mwili wa rais wa awamu ya tano wa Tanzania ulivyopokelewa Dodoma

    Umati

    Chanzo cha picha, Msemaji Mkuu wa serikali/Twitter

    Maelfu ya wananchi walijitokeza usiku wa kuamkia leo katika mji mkuu wa Tanzania Dodoma kuupokea mwili wa aliyekuwa rais wao Dkt John Pombe Magufuli aliyefariki tarehe 17.03.2021.

    Shuguli ya kuuaga mwili wa hayati Magufuli inatarajiwa kufanyika tarehe 22.03.2021, ambapo marais wa nchi 10 na viongozi wengine wanatarajiwa kuhudhuria shughuli hiyo.

    Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, ametuma ujumbe wa Twitter ulioonesha jinsi wakazi wa Dodoma walivyoupokea mwili wa Dkt John Pombe Magufuli:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  16. Shughuli ya kuuaga mwili wa hayati John Pombe Magufuli yaanza Dodoma

    Ibada ya kuuombea mwili wa Magufuli yaanza Dodoma
    Maelezo ya picha, Ibada ya kuuombea mwili wa Magufuli yaanza Dodoma

    Shughuli Maalum ya kuuaga mwili wa hayati Rais John Pombe Magufuli imeanza mkoani Dodoma ambapo Wabunge watapata fursa ya kuuaga mwili wa kiongozi huyo.

    Baada ya hapo shughuli ya kitaifa itafanyika katika Uwanja wa Jamhuri ambapo viongozi wa ndani na nje ya nchi watashiriki, pamoja na wananchi wa kawaida.

  17. Rais Emmerson Mnangagwa na Felix Tshisekedi wawasili Tanzania kumuaga Magufuli

    Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na mwenzake wa DR Congo Felix Tshisekedi tayari wamewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa hayati Magufuli hii leo jijini Dodoma.

    Mnangagwa na Tshisekedi ni miongoni mwa marais 10 wanaotarajiwa kuhudhuria shughuli za kuuaga mwili wa hayati John Pombe Magufuli katika Uwanja wa Jamhuri, uliopo mji mkuu wa Tanzania Dodoma.

    Marais wengine ni kutoka Kenya, Zambia, Morocco, Namibia, Malawi ,Botswana , Afrika Kusini na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

    Kwa upande wa waliotuma wawakilishi ni Waziri Mkuu wa Rwanda, waziri wa mambo ya nje wa Angola, Makamu wa Rais wa Burundi pamoja na wawakilishi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Muungano wa Mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, Mabalozi na kutoka Umoja wa Mataifa

  18. Natumai hamjambo. Ni siku nyengine tena ambapo tunawapatia habari Mubashara kuhusu Kifo cha hayati John Magufuli