Kenya ‘haiwezi kukabidhi bandari’ kwa China kama njia ya kulipa deni
Kenya yakanusha taarifa kuwa ipo katika hatari ya kupoteza bandari yake kubwa kwa China ikiwa itashindwa kulipa deni lake.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi, Esther Namuhisa and Asha Juma
Mwalimu mkuu Afrika Kusini 'amemlazimisha mtoto kutafuta simu kwenye shimo la choo'

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwalimu mkuu wa shule moja nchini Afrika Kusini amesimamishwa kazi kwa madai ya kumlazimisha mwanafunzi kijana wa miaka 11 kutafuta simu kwenye shimo la choo.
Inadaiwa kwamba mwalimu huyo alimshukisha mwanafunzi huyo kwenye shimo la choo kwa kutumia kamba akimuahidi randi 200 sawa na dola 14 za Marekani.
Bibi ya kijana huyo amesema mjukuu wake anaogopa kwenda shuleni kwasababu wanafunzi wengine wanamdhihaki.
Bodi ya elimu ya eneo imezungumza na gazeti la TimesLive na kusema tukio hilo ni "aibu".
Vyoo vya mashimo nchini Afrika Kuusini ambapo mwaka jana vilikadiriwa kuwa sudusi au moja ya sita ya shule zote bado vinatumika licha ya kwamba ni hatari.
Afisa wa juu wa elimu eneo la Mashariki la Cape, Fundile Gade, amewaambia wananahabari kuwa tukio hilo lilikuwa "zaidi ya aibu" na atamtembelea mwanafunzi huyo nyumbani kwao kuomba msamaha.
Mwalimu mkuu anayedaiwa kutekeleza hayo katika shule ya Luthuthu Junior sasa hivi anachunguzwa na idara ya Cape ya Mashariki na hatua stahiki zitachukuliwa.
Inasemekana kuwa pia alihamasisha watoto wengine kusaidia kutafuta simu hiyo ambayo inadaiwa ilianguka kwa bahati mbaya katika choo cha walimu mwanzoni mwa Machi.
Vyombo vya habari vya eneo vimesema tukio hilo lilijulikana baada ya shirika lisilo la serikali ambalo linafanyakazi ya kuhamsisha umuhimu wa kwenda shuleni kusikia kuhusu kisa hicho.
Petros Majola, kutoka shirika la jamii la Khula aliweka video mtandaoni ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha kuwa utafutaji wa simu hiyo uliendelea kwa saa moja.
Baada ya baadhi ya wanafunzi kutumia ndoo kupunguza kinyesi ndani ya shimo hilo la choo, Bwana Majola amenukuliwa akisema kwamba kijana huyo alishukishwa kwa kamba hadi "magoti yake yakawa yameingia ndani ya kinyesi".
"Alitumia mikono yake kutafuta simu hiyo huku kinyesi kikimfikia juu ya mikono yake na kiwiko cha mkono."
Kulingana na taarifa za News24, baada ya simu hiyo kukosekana, mwalimu mkuu alimpa mtoto huyo randi 50 kwa juhudi zake.
Bibi yake kijana huyo amesema kuwa mjuu wake aliona aibu sana kurejea shuleni baada ya kitendo hicho.
'Nilibaini mume wangu anatengeneza picha za ngono'

Chanzo cha picha, Stop it Now
Mume wake ambaye amekuwa naye kwa miaka 25 alikamatwa karibu miaka 5 iliopita kwa kutengeneza picha chafu za watoto.
"Sikujua alichokuwa anafanya hadi siku moja, polisi walipovamia nyumba yetu ghafla saa za asubuhi nikiwa kwenye chumba changu nikijayarisha kwenda kazini," alisema.
Kenya ‘haiwezi kukabidhi bandari’ kwa China kama njia ya kulipa deni

Chanzo cha picha, bbc
Waziri wa Afya nchini Kenya Ukur Yatani amekanusha taarifa kuwa nchi hiyo iko katika hatari ya kupoteza bandari yake kubwa kwa China ikiwa itashindwa kulipa deni lake kwa nchi hiyo, ambalo pesa zake zimetumika kwa ujenzi wa reli mpya.
Reli hiyo yenye umbali wa kilomita 472 inagharimu karibu mara tatu zaidi ya viwango vya kimataifa na mara nne ya makadirio halisi.
Magazeti ya eneo yameripoti Jumatatu kuwa China ambayo ndio iliyokopesha deni hilo, inaweza kuchukua udhibiti wa bandari ya Mombasa ikiwa Kenya itashindwa kulipa mkopo wake wa dola bilioni 3.2.

Lakini katika taarifa, waziri wa fedha amesema "Hakuna hatari ya China au nchi nyingine yoyote ile kuchukua bandari".
Alisema deni la ujenzi wa reli haliwezi "kulipwa kwa njia nyingine yoyote ile ya kuleta kipato au kupitia shirika jingine bila idhini ya bunge".
"Serikali ya Kenya haiwezi na haijawahi kuahidi mali ya serikali kama dhamana ya deni kwasababu hatua kama hiyo… inakiuka makubaliano ya sasa ya mkopo yaliyofikiwa," Bwana Yatani amesema.
Mwanamfalme Philip: Duke wa Edinburgh atoka hospitalini baada ya mwezi

Chanzo cha picha, PA Media
Duke wa Edinburgh inasemekana kwamba sasa hali yake ya afya imeimarika baada ya kuondoka hospitali kufuatia upasuaji wa moyo uliofanikiwa.
Mwanamfalme Philip, 99, alilazwa katika hospitali ya King Edward VII Februari 16 baada ya kuhisi vibaya.
Duke amerejea katika Kasri la Windsor baada ya kulala hospitali kwa siku 28, na ndio muda mrefu zaidi kuwa hospitalini.
Katika taarifa iliyotolewa Jumanne, Makazi ya Kifalme yalisema, Duke ametolewa hospitali "baada ya kupata matibabu ya ugonjwa wa kuambukiza na mchakato uliofanikiwa wa tatizo jingine la afya".
"Mwanamfalme angependa kuwashukuru wahudumu wote wa afya waliomtunza…na kila mmoja ambaye amekuwa akituma risala zake za rambi rambi," taarifa hiyo imesema.
Mwanamfalme Philip na Malkia, 94, wamekuwa wakisalia ndani England katika Kasri la Windsor wakiwa na kundi dogo la wafanyakazi.
Wanandoa hao ambao wameoana kwa miaka 73, walipata chanjo yao ya kwanza ya corona mnamo mwezi Januari.
Soma zaidi:
- Mwanamfalme Philip alazwa hospitalini 'kama tahadhari'
Chama Cha upinzani Cha ACT- Wazalendo yaitaka serikali kueleze hali ya afya ya Magufuli

Chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania kimeitaka serikali kuvunja ukimya na kueleza umma juu ya afya ya Rais wa nchi hiyo John Pombe Magufuli.
“Afya ya rais sio jambo linalopaswa kuwa la siri, yeye ni kiongozi wa taifa, tumekua na viongozi waliougua huko nyuma , marehemu Mzee Mkapa alipougua na kukaa muda mrefu nchini Uswizi wananchi walijulishwa” inasema taarifa hiyo.
Hata hivyo taarifa hiyo imeendelea kusema kuwa majibu yaliyotolewa na viongozi mbalimbali wa serikali hayajitoshelezi.
Rais magufuli hajaonekana hadharani tangu Februari 27.
Waziri mkuu Kasim majaliwa mwishoni wa wiki iliyopita alisema kuwa rais Magufuli anaendelea na majukumu yake kama kawaida.
Tayari watu wanne wamekamatwa kwa kusambaza taarifa za kuumwa kwa Magufuli katika mitandao ya kijamii.
Facebook kuilipa News Corp kwa kushirikisha habari zake Australia

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Shirika la Habari la Rupert Murdoch kulipwa Facebook huko Australia Facebook imekubali kulilipa shirika la habari la News Corp linalomilikiwa na Rupert Murdoch nchini Australia kwa kutumia taarifa zake.
Mkataba huo umefikiwa wiki kadhaa baada ya Australia kupitisha sheria tata inayolenga kuzishurutisha kampuni za teknolojia kulipia maudhui ya habari.
News Corp haijasema thamani ya mkataba huo wa miaka mitatu nchini Australia. Mwezi uliopita , ilifikia mkataba na kampuni ya Google.
Himaya ya Bw.Murdoch ya uwasilishaji habari ilianza na uchapishaji wa magazeti nchini Australia. Mkataba huo unajumuisha maudhui yote ya habari kutoka News Corp nchini humo – ambao unakadiriwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
News Corp inashikilia karibu asilimia 70 ya usambazaji wa magazeti nchini Australia ikiwa na machapisho yake katika magazeti ya The Daily Telegraph na The Herald Sun miongoni mwa zingine. Pia inamiliki tovutu ya news.com.au.
Mnyama Simba dimbani kimya kimya kuwavaa El Merreikh

Vinara wa kundi A, wawakilishi pekee wa ukanda wa Afrika mashariki katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Africa Simba almaarufu kam wekundu wa Msimbazi , leo hii itashuka katika dimba la Mkapa Jijini Dar Es Salaam kuwakabili El Merreikh kutoka Sudan.
Mchezo huu utacheza saa kumi jioni kwa saa za Afrika mashariki, Simba wanaongoza kundi A wakiwa na alama 7, baada ya michezo mitatu.
Simba kama watapa ushindi leo au kutoka sare watakuwa wamejikita zaidi kileleni mwa kundi na kujihakikishia zaidi nafasi ya kucheza hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika
Michezo mingine itakayopigwa leo ni As Vita Club ya Jamhuri ya Kidemocracya Congo watakuwa wenyeji wa Al Ahly kutoka Misri.
Al Hilal vs Cr Belouizdad
Atletico Petroleos vs Kaizer Chiefs
Horoya Ac vs Wyadad Ac
Mamelodi Sundowns vs Tp Mezembe
Teungueth vs Mc Alger
Zamalek Sc vs Es Tunis.
Kenya yahofia ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona

Chanzo cha picha, AFP
Kenya imeripoti ongezeko la viwango vya maambukizi ya virusi vya Corona hadi asilimia 16 baada ya watu 731 kupatikana na ugonjwa huo siku ya Jumatatu.
Takwimu kutoka Wizara ya Afya nchini humo, zinaonyesha kwamba watu 109 walikuwa katika kitengo cha wagonjwa mahututi huku 23 wakisaidiwa kupumua kutumia mashine.
Kupitia taarifa Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema watu 4,513 ndio walipimwa virusi hivyo katika saa 24 zilizopita. Idadi ya waliombukizwa virusi hivyo nchini Kenya sasa ni 113,967 kutoka sampuli 1,373,839 zilizopimwa hadi sasa.
''Kwa bahati mbaya watu watano wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo na kufikisha 1,918 jumla ya watu walioaga dunia kutokana na ugonjwa huo'', alisema Bw. Kagwe.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wizara hiyo imesema kufikia Jumamosi iliyopita wahudumu wa afya 9,144 walikuwa wamepewa chanjo ya Corona katika kaunti 40 tangu kuanzishwa kwa kampeini ya kutoa chanjo, Machi tarehe 5.
Serikali inalenga kuwachanja takribani Wakenya milioni 1.25 kufikia mwisho wa mwezi Juni katika awamu yake ya kwanza ya kutoa chanjo hiyo.
Nairobi inaongoza kwa idadi ya watu waliochanjwa 2,020 ikifuatwa na Kaunti ya Uasin Gishu ambayo imewachanja watu 1,304 kisha Kisumu ni ya tatu kwa kuwachanja watu 764.
- Virusi vya Corona: Ukweli kuhusu hali ya mtu baada ya kupata chanjo ya Covid-19
- Virusi vya corona: Endeleeni kutumia chanjo ya AstraZeneca, yasema WHO
'Rwanda haitasitisha kutoa chanjo ya AstraZeneca'
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili

Serikali Rwanda imesema haitasitisha mpango wa kutoa chanjo ya AstraZeneca.
Afisa mkuu wa mamlaka ya afya Dkt Sabin Nsabimana amewaambia waandishi wa habari mjini Kigali kwamba chanjo ya Astrazeneca haina madhara.
Tangu wiki mbili zilizopita Rwanda imeishatoa chanjo kwa watu wapatao 257,000 ambapo zaidi ya theluthi mbili walipewa chanjo ya AstraZeneca na wengine chanjo ya Pfizer.
Rwanda inatarajia kupata dozi za chanjo ya corona 1,098,960, aina ya AstraZeneca/Oxford na Pfizer-BioNTech, zitatolewa kwa awamu ya kwanza na wa pili wa mwaka 2021.
Uganda na Nigeria zimeondoa wasiwasi juu usalama wa chanjo ya Oxford-AstraZeneca wakati mataifa mbalimbali ya Ulaya pamoja na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimesitisha matumizi ya chanjo hiyo wakihofia dozi hiyo kusababishia watu damu kuganda.
Serikali ya Nigeria imewahakikishia wananchi wake kuwa wamejaribu chanjo hiyo na ni salama kuitumia.
Nigeria imepokea dozi milioni 3.94 ya chanjo ya corona ya Oxford-AstraZeneca mapema mwezi Machi na kuanza kutoa kwa makundi ya watu ambao wamewapa kipaumbele.
Nchini Uganda, Katibu katika Wizara ya afya Dkt Diana Atwine, amesema taifa lake halitasitisha matumizi ya chanjo ya AstraZeneca kwa kuwa hakuna taarifa waliyopokea kuhusu chanjo hiyo kumdhuru mtu mpaka sasa.
Wakati mkuu wa mpango wa kinga nchini Uganda-UNEPI Dkt. Alfred Driwale, amerpotiwa akisema chanjo ni salama na watu watu wasisikilize taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii.
- Kwanini chanjo ya AstraZeneca inakataliwa na nchi mbalimbali?
- Endeleeni kutumia chanjo ya AstraZeneca, yasema WHO
Wanamgambo wa Kiislamu 'wawakata vichwa watoto' Msumbiji

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la kimataifa linasema watoto wadogo wa hadi miaka 11 wanauawa kwa kuchinjwa na wanamgambo wa Kiislamu katika mkoa wa Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji.
Mwanamke mmoja ameliambia shirika la Save the Children kwamba alishuhudia mtoto wake aliyekua na umri wa miaka 12 akiuawa karibu na mahali alipokuwa amejificha na watoto wake wengine.
"Baada ya mwanangu kuuawa, tulibaini hni hatari kuendelea kuishi katika kijiji chetu,"alisema.
"Tulikimbili anyumbani kwa baba yangu katika kijiji kingine, lakini baada ya siku chache mashambulio yakaanza tena huko pia ."
Zaidi ya watu 2,500 wameuawa na wengine 700,000 wametoroka makwao katika mkoa wa Cabo Delgado ulio na utajiri mkubwa wa gesi na mafuta tangu mashambulio ya wanamgambo yalipoanza mwaka 2017.
Baadhi ya watu wamefariki wakijaribu kutoroka eneo hilo baada ya boti waliyokuwa wakisafiri kuzama.
- Video ya kuogofya iliyochukuliwa Kaskazini mwa Msumbiji
- Msumbiji: Je, Cabo Delgado ni kituo cha wapiganaji wa Islamic State?
Mwezi Novemba, chombo cha habari cha kitaifa kiliripoti kwamba zaidi ya watu 50waliuawa kwa kuchinjwa katika uwanja wa mpira wa miguu huko Cabo Delgado.
Na mwezi April mwaka jana, makumi ya watu walichinjwa na wengine kuuawa kwa kupigwa risasi katika kijiji kimoja.

Makundi ya kutetea haki yanasema vikosi vya serikali vimekuwa vikitekeleza ukiiukwaji wa binadamu, ikiwa ni pamoja na kukamtwa kiholepa, ukatili na mauaji wakati wa oparesheni dhidi ya wanamgambo wa kijihadi.
Serikali ya Msumbiji imeomba jamii ya kimataifa kuisaidia kukabiliana namashambulio ya wanamgambo.
Habari...Karibu katika matangazo ya moja kwa moja ya ukurasa wa BBC Swahili leo ikiwa Machi 16, 2021.
