Wasafiri wa Tanzania, Afrika Kusini na Nigeria wazuiwa kuingia Oman kwa muda
Nchi zingine zilizopigwa marufuku ni Ethiopia, Sudan, Guinea, Ghana, Sierra Leone, Lebanon na Brazil
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Tazama jinsi Jumba hili lilivyohamishwa kutoka eneo moja hadi jingine
Maelezo ya video, Jumba kubwa lahamishwa kutoka eneo moja hadi jingine San Fransisco Wakaazi wa San Fransisco walijipata wakitazama uhamisho wa jumbe kubwa la Victorian House lenye miaka 139 katika barabara za mji huo. Eneo la jumba hilo litajengwa jumba jingine lenye ghorofa nane. Uhamisho huo uligharimu $200,000 .
Mwili wa balozi wa Italia waagwa DRC
Gavana wa Kivu Kaskazini Carly Nzanzu na mshauri mkuu wa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameongoza maafisa wengine kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa balozi wa Italia nchini DRC, Luca Attanasio na mlinzi wake.
Mwili wa marehemu unasafirishwa leo nchini Italia kutoka uwanja wa ndege wa Goma mashariki mwa DRC.

Chanzo cha picha, Presse Présidentielle DRC
Maelezo ya picha, Gavana wa Kivu Kaskazini Carly Nzanzu kasivita akiongoza shughuli ya kuaga mwili wa balozi Luca Viongozi wa DRC na maafisa wa Italia wakishauriana kabla ya kuuaga mwili wa balozi wa Italia ambao unasafirishwa nyumbani leo.

Chanzo cha picha, Presse Présidentielle DRC
Maelezo ya picha, Viongozi wa DRC na maafisa wa Italia wakishauriana Bw Luca Attanasio na mlinzi wake waliuawa baada ya msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa kushambuiliwa siku ya Jumatatu mashariki mwa nchi hiyo.

Chanzo cha picha, Presse Présidentielle DRC
Maelezo ya picha, Ndege itakayosafirisha mwili wa balozi wa Italia kutoka DRC Kenya kuandaa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya katiba

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta(Kulia) na Kiongozi wa upinzani Raila Odinga Kenya inatarajiwa kuandaa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho ya katiba baada ya mswada wa Building Bridges Initiative (BBI) kuidhinishwa katika mabunge 24 kwa mujibu wa katiba.
Mabunge ya majimbo 10 zaidi yanajadili mswada huo kwa sasa na huenda idadi ya majimbo yanayounga mkono mchakato huo yakaongezeka.
Japo mswada wa BBI utahitajika kuidhinishwa na Bunge la Kitaifa na Bunge la Seneti kura ya maamuzi itafanyika hata mabunge hayo yasipouunga mkono.
Baadaye maspika wa mabunge hayo mawili watamfahamisha rais kuhusu uamuzi wao.
Maelezo zaidi:
- Namna ripoti ya BBI itakavyobadili mfumo wa utawala Kenya
- Je ripoti ya BBI itasaidia kutatua matatizo ya Wakenya?
Walinda amani wa UN Tigray 'wakataa kurudi nyumbani'

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Walinda usalama 169 wa Ethiopia katika Umoja wa Mataifa walikuwa wabadilishwe Walinda usalama 15 wa Ethiopia nchini Sudan Kusini, kutoka eneo la Tigray, wamekataa kurudi Ethiopia siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari la AFP inayomnukuu msemaji wa Umoja wa Mataifa Stéphane Dujarric.
Kikosi cha maafisa 169 wa Ethiopia kilikuwa kiondoke nchini Sudan Kusini.
"Tunajaribu kutafuta maelezo, lakini nafahamishw akwamba karibu maafi 15 wa kikosi cha Ethiopia walikata kupanda ndege katika uwanja wa ndege wa Juba... wameomba kusalia huko," Bw. Dujarric alinukuliwa kusema katika mazungumzo na wanahabari.
Mzozo ulizuka katika jimbo la Tigray mapema mwezi in Novemba mwka 2020 baada ya wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF) kuvamia kabi ya majeshi ya muungano katika eneo hilo baada kufuatia tofauti kati yao na serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed.
Maelfu ya watu waliripotiwa kuawa na wengine karibu milioni mbili kufurushwa makwao.
Soma zaidi:
- Mzozo wa Tigray: Jukumu la Eritrea katika mzozo wa Ethiopia
- ‘Sababu za mjomba wangu kuwa mkimbizi nchini Sudan'
Waasi DRC wajitenga na mauaji ya mwanadiplomasia wa Italia

Chanzo cha picha, Reuters
Kundi la waasi la wa Rwanda (FDLR), limekanusha kuhusika na mauaji ya siku ya Jumatatu ya balozi wa Italia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Luca Attanasio, 43, alifariki hospitalini kutokana na majeraha aliopata baada ya msafara wa magari ya Umoja wa mataifa kushambuliwa karibu na mji wa Goma mashariki mwa nchi hiyo.
Afisa wa kijeshi alikuwa katika msafara huo pia aliuawa.
Wizara ya mambo ya ndani ya DR Congo imelaumu kundi la waasi la FDLR kuhusika na mashambulio hayo.
Lakini msemaji wa kundi hilo amekanusha madai hayo.
“Zaidi ya makundi 100 yaliyojihami yanahudumu eneo hili, hatujui kwa nini wanatuhusisha na mauaji hayo. Hatukuhusika kwa njia yoyote na mashambulio hayo,” Cure Ngoma aliambia BBC.
Pia unaweza kusoma:
- Makundi ya waasi bado yanahatarisha maisha ya watu wa mashariki mwa Jamuhuri ya Congo
- Je, wakati umewadia kwa DRC kuzungumza na waasi?
Chanjo ya Ebola yawasili Guinea

Chanzo cha picha, WHO
Ndege maalum iliyobeba shehena ya chanjo ya Ebola imewasili nchini Guinea usiku wa Jumatatu.
Dhoruba ya vumbi iliyokumba eneo la Sahara siku ya Jumapili ililazimisha ndege hiyo kuelekezwa Senegal, hali iliyochelewesha kutolewa kwa chanjo kwa siku moja.
Shughuli ya kutoa chanjo itaanza kufanyika katika mji mkuu wa Guinea, Conakry, hivi leo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Dozi 11,000 ya chanjo hiyo zitapelekwa mji wa Nzérékoré kusini mashariki mwa nchi hiyo.
Watu watano wamefariki hivi karibuni kutokana na Ebola.
Huu ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huo hatari Afrika Magharibi tangu mwaka 2016.
Maelezo zaidi:
- Utaratibu wa kulala na maiti kueneza maambukizi ya ebola DRC
Mtandao wa spotify kuzinduliwa Afrika Mashariki

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Simu ya rununu ya Spotify Mtandao wa Spotify unatarajiwa kuzindua huduma zake katika masoko 85 mapya katika hatua ambayo itaipatia watu zaidi ya bilioni.
Tangazo hilo lilitolewa kupitia hafla iliyooneshwa mubashara kupitia mtandao ikiwajumuisha na Justin Bieber, Prince Harry na Meghan Markle.
Spotify pia imetangaza huduma mpya ya usajili wa ubora wa juu wa sauti na soko jipya la matangazo ya podcast.
Baadhi ya masoko mapya ya mtandao huo yako katika nchi zinazoendelea barani Asia, Afrika, Pacific na Caribbean.
“Masoko haya kwa pamoja yanawakilisha zaidi ya watu bilioni moja, nusu yao tayari wanatumia intaneti,” msemaji wa Spotify Alex Norstrom, alisema.
“Maeneo mengine tunayopeleka huduma zetu kama Bangladesh, Pakistan na Nigeria yana ukuaji wa haraka wa intaneti duniani,” aliongeza kusema.
Upanuzi wa awali wa mtandao huo nchini India, Urusi na Mashariki ya Kati tayari imewavutia mamilioni ya wafuatiliaji.
Pia unaweza kutazama:
- Spotify yamtaja Bad Bunny mwanamziki maarufu zaidi duniani
Maambukizi ya Corona yako 'juu kuliko ilivyodhaniwa' Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Watafiti wanasema watu milioni nne huenda wameambukizwa mjini Lagos Matokeo ya uatafiti nchini Nigeria unaashiria kiwango vya maambukizi ya ugonjwa wa Covid -19 nchini humo iko juu zaidi kuliko ilivyoripotiwa awali.
Matokeo ya utafiti huo umebaini kuwa mtu mmoja kati ya kila watu watano ameambukizwa virusi vya corona katika majimbo ya Lagos, Enugu na Nasarawa.
Mji wa Lagos ambao ndio mkubwa zaidi nchini humo, huenda watu milioni nne wameambukizwa ugonjwa huo ijapokuwa, idadi rasmi ya waliombukizwa kwa sasa ni watu 54,000.
Utafiti huo ulifanywa mwezi Septemba na Oktoba mwaka jana na Kitio cha kuzuia na kudhibiti magonjwa nchini Nigeria (NCDC) kw aushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Kimatibabu
Mkuu wa NCDC amesema matokeo ya utafiti huo umefanya juhudi za kutafuta chanjo Nigeria "kuwa muhimu zaidi".
Zaidi ya watu 1,800 wamefariki nchini humo kutokana na ugonjwa Covid-19.
Maelezo zaidi:
- Tunachojua kuhusu aina mpya ya virusi vya corona
- Maswali 4 ambayo hayajajibiwa kuhusu chanjo ya corona
Ofisi ya Rais DRC yajiunga na uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamepelekwa katika eneo lililoshambuliwa Maafisa kutoka ofisi ya rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanatarajiwa kupelekwa mjini Goma kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya balozi wa Italia nchini humo.
Maafisa hao wataondoka leo kuelekea Goma na watakuwa wakiwasilisha ripoti kwa za mara kwa mara kwa rais.
"Mjumbe wa rais wa DRC atazuru [Italia] Jumanne ya leo Februari 23 kuwasilisha barua ya kibinafsi kwa rais wa baraza la Italia," Kulingana na ripoti kutoka kwa idara ya Idara ya habari ya rais.
Katika ujumbe uliyochapishwa katika mtandao wa Twitter, Rais Félix Tshisekedi alisema alisikitishwana taarifa za kufuatia kuuawa kwa mwanadiplomasia wa Italia, Luca Attanasio.
Alilaani shambulio la kigaidi lililolenga msafara wa magari ya Umoja wa Mataifa.
Balozi Luca Attanasio alikuwa ameabiri gari la Shirika la Chakula Dunia (WFP).
Rais amezitaka asasi husika kutoa maelezo kuhusiana shambulio hilo haraka iwezekanavyo ili waliyohusika wachukuliwe hatua za kisheria.
Maelezo zaidi:
- Balozi wa Italia auawa DRC
Tanzania, Afrika Kusini na Nigeria zawekewa marufuku ya muda ya usafiri Oman

Wasafiri wanaoingia Oman kutoka nchi 10 wamepigwa marufuku ya kuingia nchini humo.
Nchi zilizopigwa marufuku ni Tanzania Afrika Kusini, Lebanon, Sudan, Brazil, Nigeria, Guinea, Ghana, Sierra Leone, na Ethiopia.
Marufuku hiyo itaanza kutekelezwa usiku wa Alhamisi wiki hii na itadumu kwa siku 15.
Hatua hiyo imetokana na maamuzi yaliyotolewa na kamati ya udhitibi wa Corona nchini humo.
Kamati hiyo imesema uamuzi huo ni wa kupambana na maambukizi ya Corona.
Marufuku hiyo pia inawahusisha watu watakaopita katika nchi hizo ndani ya siku 14 kabla ya kuingia Oman.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Oman, mkutano wa kamati hiyo uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Oman Hammoud bin Faisal Al Busaid.
Kamati hiyo imewataka wananchi wa Oman kutosafiri nje ya nchi ili kuzuia maambukizi na ikibidi kusafiri basi kuwe na sababu maalum.
Maelezo zaidi:
Hujambo na karibu katika matangazo mubashara Jumanne 23.02.2021
