Uchaguzi Uganda 2021: Vyombo vya usalama vyaanza doria baada ya kura kupigwa Uganda
Raia wa Uganda hii leo wanashiriki katika shughuli ya kihistoria ya kumchagua rais na wawakilishi wa bunge lao
Moja kwa moja
Abdalla Seif Dzungu and Dinah Gahamanyi
Matokeo ya uchaguzi Uganda 2021:Kura zikihesabiwa katika vituo mbalimbali
Kura zinaendelea kuhesabiwa katika vituo mbalimbali huku maafisa wa usalama wakiwa katika mitaa mbalimbali kuhakikisha wanazuia wananchi kubaki kwa madai ya kulinda kura zao.
Mwandishi wa BBC Munira Hussein ametuandalia picha zifuatazo;
Matokeo ya Uchaguzi Uganda 2021: Vyombo vya usalama vyaanza doria
Chanzo cha picha, Reuters
Zoezi la kuhesabu kura limeanza katika baadhi ya vituo vya kupigia kura nchini Uganda.
Idadi ya askari ilianza kuonekana kuongezeka saa moja kabla ya vituo vya kupigia kura kufungwa saa kumi jioni.
Malori yakiwa yamewabeba wanajeshi wakizunguka mjini huku polisi na vikundi vya usalama vikiwa vinafanya doria.
Katika baadhi ya maeneo, watu bado wanapiga kura kwa kuwa taratibu za uchaguzi zinaruhusu watu wote waliokuwa wamepanga foleni kabla ya muda wa vituo vya upigaji kura kufungwa kupiga kura.
Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35 anawania tena kuchaguliwa kwa muhula wa sita.
Rais Museveni mwenye umri wa miaka 76-anakabiliana na wapinzani 10 huku mpinzani wake mkuu akiwa mwanamuziki aliyeamua kuwa mwanasiasa Bobi Wine, mwenye umri wa miaka 38.
Uchaguzi Uganda 2021: Museveni apiga kura muda mfupi kabla ya vituo kufungwa
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, 76, amepiga kura ikiwa zimesalia chini ya dakika 15 kabla ya vituo vya kupiga kura kufungwa.
Vituo vya kupiga kura vimefungwa saa kumi jioni ingawa watu waliokuwa kwenye foleni wanaruhusiwa bado kupiga kura.
Rais Museveni, amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, na sasa anawania muhula wa sita.
Mpinzani wake mkuu akiwa Bobi Wine,38, mwanamuziki aliyeamua kuwa mwanasiasa.
Rais amepiga kura katika mji wa Rushere Magharibi mwa nchini Uganda.
Uchaguzi Uganda 2021: Mashine za uhakiki wa wapiga kura zashindwa kufanya kazi
Maelezo ya picha, Vituo vya kupigia kura vilifunguliwa saa moja asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki
Mashine za
uhakiki wa wapiga kura nchini Uganda zimeshindwa kufanya kazi katika baadhi ya vituo
vya kupigia kura ambavyo BBC ilivitembelea.
Msemaji
wa Tume ya uchaguzi, Paul Bukenya, amesema kuwa walipokea taarifa kwamba baadhi
ya vifaa hivyo havifanyi kazi.
Vifaa
hivyo vya kieletroniki hutumiwa kunasa na kuhakiki taarifa za wapiga kura kabla
ya kutolewa kwa karatasi za kupiga kura.
Foleni ndefu ilionekana katika
vituo vya kupigia kura ambavyo BBC ilivitembelea BBC, japo kulikuwa na ucheleweshaji wa vifaa vya
kupigia kura katika baadhi ya vituo.
Upigaji
kura ulipangwa kuanza saa moja asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki ingawa kwa baadhi maeneo ulichelewa.
Magufuli asema 'Maalim Seif amefanya maamuzi ya kishujaa'
Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli amempongeza mwanasiasa wa upinzani Maalim Seif Shariff kwa kukubali kujiunga na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) visiwani Zanzibar.
Rais Magufuli amesema kuwa uamuzi huo wa Maalim Seif ulikuwa ni wa busara na ulioangalia maslahi ya Zanzibar.
"Uliacha maslahi yako binafsi, ukafanya uamuzi mkubwa na wa busara kwa maslahi ya Wazanzibari," ameeleza Magufuli na kuongeza: "Kuna ndoa zilivunjika, hasa Pemba kutokana na uchaguzi kwa kuwa mwanamke kapigia kura CCM na mume ACT, lakini baada ya maamuzi ya Maalim Seif wanandoa hao wakarudiana."
Chanzo cha picha, Ikulu-Tanzania
Maalim Seif, kutoka chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo alipinga matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar mwezi Oktoba 2020 ambapo alipata 19.78% ya kura za urais huku mpinzani wake Hussein Mwinyi akipata ushindi wa 76.27% na kuapishwa kuwa rais.
Hata hivyo, mwezi Disemba ACT ikatangaza kukubali kuingia katika serikali ya Zanzibar kama katiba ya visiwa hivyo inavyoelekeza na kupendekeza jina la Maalim Seif kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais. Maamuzi hayo yalipokelewa kwa hisia mseto huku baadhi ya wanaharakati wakikikosoa chama hicho kwa 'kuwasaliti wananchi'.
Rais Mwinyi na Maalim Seif wapo nyumbani kwa rais Magufuli wilayani Chato kwa ziara ya siku mbili.
Chuck Norris akana kushiriki ghasia katika jengo la Capitol Hill
Chanzo cha picha, Chuck Norris/ Twitter
‘Sio mimi!’,
Chuck Norris akana kuwa katika ghasia za Capitol Hill.
Msanii wa filamu Chuck Norris amelazimika kukanusha kutoshiriki katika
vurugu zilizotokea wiki iliyopita katika jengo la bunge la seneti la Marekani-
Capitol Hill, baada ya picha ya mtu aliyefanana na yeye kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya maandamano hayo, picha hiyo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii ya wafuasi
wa Rais Donald Trump, ambao walimshirikisha picha
ya mtu huyo Chuck Norris ambaye sasa ana umri wa miaka 80.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Picha ya mwanaume huyo ambaye anafanana na Chuck Noris , ilisababisha mkanganyiko, huku wengi mtandaoni wakiamini nyota huyo wa filamu kweli alikuwa miongoni mwa watu waliosababisha vurugu katika Capitol Hill.
Norris alipata umaarufu baada ya kuonekana katika filamu ya Bruce Lee ya Way of the Dragon na kuwa mchezaji filamu za stalwart ikiwa ni pamoja na Delta Force.
Uchaguzi Uganda 2021: Sanduku la kura laibiwa
Msemaji wa Tume ya uchaguzi nchini Uganda amesema Sanduku la kura lililokuwa na kura ndani yake limeibiwa katika eneo la Rushenyi wilayani Ntungano Mashariki mwa nchini humo.
Bw Paul Bukenya amesema tukio la wizi huo limeripotiwa kwa kitengo cha Tume ya uchaguzi cha malalamishi na kwamba polisi wanamtafuta mtu aliyeliiba.
Bw Bukenya amesema kuwa watu wa eneo hilo wataweza kupiga kura yao licha ya kuibiwa kwa sanduku, lakini tukio kama hilo ni la bahati mbaya kwasababu linavuruga mchakato.
"Tunalishughulia suala hili na tutawafahamisha mambo yatakavyokuwa", amesema Bw Bukenya.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Mchungaji wa Kenya ahukumiwa miaka 140 baada ya kuwabaka binti zake wawili
Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama nchini
Kenya imemfunga kifungo cha miaka 140 jela mchungaji aliyewabaka wasichana wake wawili wa
miaka 14 na miaka 16 na kuwapatia mimba.
Akitoa hukumu hiyo hakimu mkazi wa Baricho Anthony Mwicigi, alimuhukumu Mchungaji John Gichira
kifungo cha miaka 70 kwa kila msichana . Mahakama iliamua kuwa hukumu hizo zitatekelezwa moja baada ya nyingine na hivyo mchungaji huyo ataishi jela miaka 140.
Mchungaji huyo kutoka kaunti ya Kirinyaga
kati kati mwa Kenya, mwenye umri wa
miaka 51 alikiri kuwabaka watoto wake tarehe 5 Januari na kuwekwa jela tangu
tarehe 7 Januari. Alimlaumu shetani kwa ubakaji huo watoto wake na akawaomba
msamaha watoto wake na mahakama.
Hakimu mkazi Anthony Mwicigi alisema kuwa mchungaji huyo alipataikana na
hatia kwa kukiri mwenyewe kuwabaka
watoto wake na akaagiza hukumu dhidi yake itolewe tarehe 14 Januari.
Mchungaji huyo anayefahamika kwa jina la Gichina
alikamatwa mahala alipokuwa amejificha baada ya polisi kuanzisha harakati za
kumsaka.
Msichana mmoja tayari ana mtoto wa miezi 7 na
mwingine ana mtoto wa miezi 5.
Wanajeshi wa Msumbiji wawaokoa raia waliotekwa na Islamic State
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Zaidi ya watu zaidi ya 400,000 wameyakimbia mashambulio ya wapiganaji wa kiislamu
Wanawake 15 na watoto sita waliokuwa wametekwa na wanamgambo wa
Islamic State katika jimbo lenye utajiri wa mafuta la Cabo Delgado nchini
Msumbiji wameokolewa na jeshi.
Wengi
wao walikuwa wametekwa kutoka katika kisiwa cha Matemo wiki iliyopita, kulingana na mkuu wa polisi Bernardino Rafael.
Mapigano
ya hivi karibuni yanaonesha kua vikosi vya usalama vilifahamu ni wapi walipokuwa
wanamgambo hao, kwa hiyo kwa usaidizi wa helikopta waliweza kuwazingira na
kuwatenganisha na watekaji wao, alisema.
Watarejeshwa tena Matemo, eneo ambalo limezongwa na mashambulizi tangu mwezi Oktoba.
Lakini mkuu wa polisi amesema kuwa kisiwa
hicho ni salama kwa sasa.
Wanamgambo wa IS, wanaofahamika na wakazi kama al-Shabab,
au vijana , wamefanya mashambulio kadhaa katika vijiji na miji katika eneo hilo
kwa zaidi ya miaka mitatu.
Chanzo cha picha, AFP
Hivi karibuni zaidi
waliahidi kulitii kundi la IS , na wanafahamika kwa mashambulio ya ukatili,
ambayo huwa ni pamoja na kuwakata vichwa wanavijiji na kuchoma moto nyumba.
Mara nyingi huwateka
wanawake na watoto ambao hutumiwa kama watumwa wa ngono na kusafirisha bidhaa
walizoiba kufuatia mashambulio.
Mwishoni mwa juma,
Waziri wa ulinzi wa Marekani alisema kuwa Anthony Tata, naibu waziri wa mashauri
ya kigeni anayehusika na masuala ya sera alitembelea Msumbiji Ijumaa na kufanya
mazungumzo na mawaziri juu ya umuhimu wa mpango wa kimkakati wa kuleta utulivu
katika jimbo la Cabo Delgado.
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Wanamgambo wa Islamic State wanafahamika kwa kukata vichwa na kuchoma nyumba za wanavijiji
Taarifa
kutoka ubalozi wa Marekani inasema kuwa Marekani itatoa msaada wa kibinadamu na
kiuchumi wa dola milioni 42 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika jimbo hilo
lililopo kaskazini mwa nchi.
Juhudi hizi na nyinginezo, kwa mujibu wa balozi Dennis
Hearne, ni sehemu ya msaada wa kila mwaka wa dola milioni 500 ambao Marekani
hutoa kwa Msumbiji.
Uchaguzi Uganda 2021: Bobi Wine athibitishwa kupiga kura Uganda
Maelezo ya picha, Bobi Wine alipiga kura katika kituo cha Freedom Square
Mgombea mkuu wa upinzani nchini Uganda Bobi amethibitishwa kupiga kura yake mapema leo .
Bobi Wine anawania urais nchini Uganda kwa mara ya kwanza huku akidaiwa kutoa upinzani mkali kwa rais aliyepo madarakani Yoweri Museveni.
Yupo katika kinyanganyiro hicho kwa ahadi ya kuvutia uwekezaji na kuwapatia ajira vijana iwapo atachaguliwa.
Uchaguzi wa Uganda 2021: Siku ya uchaguzi kwa picha
Waandishi wa BBC waliopo nchini Uganda wametembelea maeneo mbali mbali kushuhudia shughuli ya upigaji kura iliyoanza saa moja kamili kwa saa za Afrika Mshariki.
Hizi ni baadhi ya picha kuhusu uchaguzi wa Uganda na hali kwa ujumla ilivyo katika mji mkuu Kampala.
Maelezo ya picha, Milolongo mirefu ya wapiga kura imeshuhudiwa katika vituo mbali mbali vya kupigia kura
Maelezo ya picha, Wapiga kura wakisubiri kupiga kura
Maelezo ya picha, Maandalizi ya kuanza kwa shughuli ya kupiga kura katika moja ya vitongoji vya mji mkuu Kampala
Maelezo ya picha, Hali ilionekana kuwa tulivu katika barabara nyingi za mji wa Kampala ambazo kwa kawaida huwa na shughuli nyingi
Wanaowatumia walemavu kujipatia kipato wafikishwa mahakamani Tanzania
Maelezo ya picha, Mtu amevalishwa pingu
Watu 15 akiwemo mfanyabiashara, Sadikiely Meta (71) wamefikishwa
katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka 41 yakiwemo ya
kufanya biashara haramu ya kusafirisha binadamu kinyume cha sheria, kukwepa
kodi na kuisababishia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) hasara ya Sh31 milioni.
Kulingana na
mtandao wa mwnanchi nchini Tanzania , Meta na wenzake wanadaiwa kusafirisha
wenye ulemavu 37, wakiwemo watoto wadogo wenye umri wa miaka saba na 11 kutoka
mikoa ya Tabora, Shinyanga na kuwaleta Dar es Salaam na kisha kuwataka waombe
fedha mitaani ili wao wajiingizie kipato.
Kulingana na
mtandao huo washtakiwa hao walisomewa mashtaka na wakili wa Serikali
mwandamizi, Mkunde Mshanga akisaidiana na Wankyo Simon mbele ya hakimu mkazi
mkuu, Kassian Matembele.
Uchaguzi wa Uganda 2021: Waganda wakosa huduma za intaneti mkesha wa uchaguzi
Mamlaka nchini Uganda ilikatiza hudama za intaneti saa
kadhaa kabla ya uchaguzi wa urais unaokumbwa na ushindani mkali kati ya nyota
wa muziki na mmoja viongozi wa muda mrefu wa Afrika waliohudumu miaka mingi
madarakani.
Kundi la ufuatiliaji wa masuala ya Itaneti NetBlocks liliandika
kwenye Twitter yake kwamba nchi hiyo ilizima mitandao yote ya intaneti
Jumatano saa moja usiku majira ya Afrika Mashariki.
Hatua hiyo ilifuatia agizo la serikali kufungia mitandao
yote ya kijamii na programu tumishi za kutuma ujumbe.
Rais Yoweri Museveni alisema alifikia uamuzi huo kwa sababu
Facebook ilifunga akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.
Mgombea wa urais,mwanamuziki aliyegeuka Bobi Wine aliandika
katika Twitter yake kwamba huduma za intaneti zimekatizwa kama sehemu ya njama
ya kuiba kura.
"Watu wa Uganda wako imara na hakuna jambo lolote
litakatiza azma yao ya kikomesha utawala wa kiimla," aliongeza.
Shughuli za upigaji kura ilianza saa moja asubuhi ya leo
Alhamisi, japo matokeo hayatarajiwi kutolewa kabla ya Jumamosi.
Kampeni za uchaguzi zilikumbwa na ghasia ambazo zilisababisha
vifo vya makumi ya watu.
Bw. Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani
kwa miaka 35.
Uchaguzi Uganda 2021: Milolongo mirefu yashuhudiwa kwenye vituo vya kupigia kura
Milolongo mirefu imeshuhudiwa katika vituo vya kupigia kura katika mji mkuu
Kampala, na maeneo menginge ya nchi
Serikali
imeamuru kufungwa kwa mitandao yote ya
kijamii.
Shughuli
ya kupiga kura ilipangwa kuanza saa moja asubuhi na kukamilika saa kumi jioni kwa
saa za Uganda, ingawa Tume ya uchaguzi nchini humo ilisema kuwa wapigakura wote
waliojisajiri ambao watakuwa bado katika mstari wa kupiga kura wakati shughuli
hiyo itakapofungwa, wataruhusiwa kupiga kura yao.
Mgombea
wa urais wa upinzani Bobi Wine anatarajiwa
kupiga kura yake katika kituo kilichopo viungani mwa mji mkuu Kampala.
Rais
Yoweri Museveni atapiga kura yake kijijini kwao magharibi mwa Uganda.
Baadhi ya wanadiploamsia wameelezea wasi wasi wao juu ya mchakato wa uchaguzi, wakielezea kukamatwa kwa wapinzani wakati wa kampeni zilizogubikwa na gasia.
Pia wamezungumzia dhidi ya mashambulio dhidi ya uhuru wa kujieleza, baada ya serikali kuwaambia watoaji wa huduma za intaneti kukata huduma zao.
Yanga yaifunga Simba kutwaa Kombe la Mapinduzi
Chanzo cha picha, Young Africans SC
Maelezo ya picha, Washindi wa Kombe la mapinduzi nchini Tanzania Young Africans
Klabu ya Yanga imenyanyua Kombe la Mapinduzi baada ya kuwafunga watani wao wa jadi klabu ya Simba kwa mikwaju ya penati 4-3.
Miamba hiyo ya soka nchini Tanzania ilimaliza dakika 90 za mchezo bila upande wowote kuliona lango la mwenzie katika dimba la Amaan visiwani Zanzibar.
Matokeo ya mchezo huo yaliamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Simba ilipoteza mikwaju miwili na Yanga ikapoteza mkwaju mmoja.
Fainali hiyo iliyopigwa jana usiku ilikuwa ni ya pili kwa Yanga na ubingwa huo ni wa pili kwao.
Simba imecheza fainali nane na kunyakua kombe hilo mara tatu.
Kombe la Mapinduzi hufanyika kila mwaka mwezi Januari kuadhimisha Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12, 1964.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa Instagram ujumbe
Uchaguzi wa Uganda 2021: Vifaa vya uchaguzi vyachelewa kufika katika baadhi ya vituo vya kupigia kura
Waandishi wa habari
walioko Uganda wanaripoti kuwa vifaa vya kupigia kura vimechelewa kufikishwa
katika baadhi ya maeneo ya kupigia kura.
Wale waliotweet kutoka vituo mbali mbali vya kipigia kura
wamesema kuwa vifaa vilikuwa bado havijafikishwa katika vituo vya kupigia kura
saa moja asubuhi, muda ambao upigaji kura ulitakiwa kuanza.
Serikali imeamuru kufungwa kwa mitandao
ya kijamii.
Ufuatao ni baadhi ya ujumbe wa Twitter
uliotumwa na waandishi wa habari kuhusu kuchelewa kwa shughuli ya kupiga kura.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Waziri wa zamani wa Masuala ya kigeni Ethiopia auawa na Jeshi
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Mesfin
Jeshi la Ethiopia limetangaza kwamba
limemuua waziri wa zamani wa mambo ya nje Seyoum Mesfin, mmoja wa wanachama
waanzilishi wa chama Tigray People’s Liberation Front (TPLF).
Bw.Seyum, ambaye alihudumu kama waziri wa
mambo ya nje wa kutoka mwaka 1991 hadi 2010, aliuawa pamoja na wanachama
wengine wa ngazi ya juu TPLF kaskazini mwa jimbo la Tigray, wanajeshi walisema.
Serikali ilikuwa imetoa waranti ya
kukamatwa kwake- pamoja na viongozi wengine wa ngazi ya juu katika chama hicho
– kufuatia oparesheni ya kijeshi ya mwezi Novemba eneo la Tigray. Zawadi ya
birr milioni 10 sawa na ($254,000; £187,000) iliahidiwa kutolewa kwa wale
watakaotoa taarifa zitakazosidia kukamatwa kwao.
Jeshi linasema kwamba liliwaomba
wajisalimishe lakini wakakata kufanya hivyo. Makumi ya wancahama wengine wa
TPLF waliuawa na wengine kukamatwa katika oparesheni ya hivi punde, iliongeza
kusema.
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed aliamuru
oparesheni ya kijeshi dhidi ya jimbo la Tigray mnamo Novemba 4 na kuiondoa
madarakani chama tawala, baada ya vikosi vyake kuvamia kambi ya majeshi ya
serikali.
Uchaguzi Uganda 2021: Museveni akabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa Bobi Wine
Maelezo ya picha, Museveni na Bobi Wine
Mwanamuziki nyota wa pop aliye na umri wa mika 38- anachuana kisiasa na mmoja wa viongozi wa Afrika aliyehudumu muda mrefu madarakani katika uchaguzi wa Uganda unaokabiliwa na ushindani mkali
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.
Kampeni zilikumbwa na vurugu ambazo zilisababisha vifo vya watu kadha.
Serikali imeagiza kufungwa kwa mitandao yote ya kijamii.
Rais Museveni anasema hii ni kwa sababu Facebook ilipiga marufuku akaunti kadhaa zinazounga mkono chama tawala.
Sera ya polisi nchini Uganda inasema maafisa watapanda juu ya majengo marefu mjini Kampala siku ya uchaguzi, baaada ya magari yaliyo na silaha kuanza kuzunguka katika mitaa ya jiji hilo.
Vituo vya kupiga kura vinafunguliwa saa moja kwa saa za Afrika Mashariki (04:00 GMT), lakini matokeo ya uchaguzi hayatarajiwi kutangazwa kabla ya Jumamosi.
Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Kampeni zilikuwa zimepigwa marufuku katika mji mkuu wa Kampala na katika baadhi ya wilaya.
Upinzani unasema hatua hiyo ilichukuliwa kwasababu ya umaarufu wake lakini serikali inasema ilifikia uamuzi huo ili kudhibiti msambao wa ugonjwa wa Covid-19.
Uchaguzi Uganda 2021: Raia wa Uganda washiriki katika shughuli ya kihistoria leo
Maelezo ya picha, Raia wapiga kura Uganda
Raia wa Uganda hii leo wanapiga kura kumchagua rais na wawakilishi wapya wa bunge .
Akizungumza siku ya Jumatano mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo jaji Simon Byabakama aliserma kwamba wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni tisa huku wenzao wa jiniai ya kike wakiwa zaidi ya milioni tisa.
Katika uchaguzi huo rais Yoweri Museveni ambaye anatetea wadhfa wake anakabilia na upinzani mkali kutoka kwa mwanamuziki wa zamani maarufu Bobi Wine.
Bobi Wine ni mgombea ambaye amevutia idadai kubwa ya vijana nchini humo.
Rais Museveni anagombea muhula wa sita baada ya kuwa madarakani kwa miaka 35.
Hatahhivyo rais Museveni anajivunia utawala wake wa muda mrefu ambapo amefanya baadhi ya maenedeleo.
Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, anasema kuwa anawakilisha kizazi kipya cha vijana wa nchini humo, huku Yoweri Museveni, 76, akisema kuwa anasimamia ustawi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Natumai hujambo. Karibu katika matangazo yetu hii leo moja kwa moja kutoka Uganda