Rais Museveni atetea kufunga mitandao ya kijamii kabla ya uchaguzi

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameilaumu mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuwa na kiburi na upendeleo.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Mpaka hapa tumefikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, shukrani na tukutane tena hapo kesho

  2. Aina ya virusi vya corona vya Afrika Kusini vyaripotiwa Taiwan

    Aina ya virusi vya corona ya Afrika Kusini inadhaniwa kusambaa kwa kasi zaidi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Aina ya virusi vya corona ya Afrika Kusini inadhaniwa kusambaa kwa kasi zaidi

    Waziri wa afya wa Taiwan Chen Shih-chung amesema kuwa kisiwa cha Thailand kimethibitisha wagonjwa wa kwanza waliopata aina ya virusi vya corona vya Afrika Kusini.

    Watu hao walikuwa wamesafiri katika nchi jirani ya Eswatini, iliyokuwa ikiitwa zamani kama Swaziland, inayopakana na Afrika Kusini.

    Kuanzia Alhamisi, yeyote anayesafiri kwenda Eswatini katika kipindi cha siku 14 atalazimika kwenda karantini katika majengo ya serikali.

  3. Waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati wafanya mashambulio karibu na mji mkuu

    Majeshi ya serikali  (pichani)

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Majeshi ya serikali (pichani) yamekuwa yakipambana na muungano wa waasi kwa miezi kadhaa

    Umoja wa Mataifa na serikaliktika Jamuhuri ya Afrika ya kati (CAR) wanasema waasi wamefanya mashambulio mashambulio mawili karibu na mji mkuu, Bangui.

    Taarifa kutoka nchini humo zinasema shambulio moja lililenga kituo cha ukaguzi kinachodhibitiwa na wanajeshi wa serikali na mamluki wa Urusi.

    Mawaziri wanasema kuwa washambuliaji walirudishwa nyuma, lakini msemaji wa Umoja wa Mataifaameelezea mapigano kama yanayoendea.

    Ubalozi wa Marekani unasema kuwa umepokea taarifa za makabiliano katika mji wa Bungui na katika eneo la Bimbo kuelekea magharibi mwake

    Vikosi vya waasi, vilivyopinga kuchaguliwa tena kwa Faustin-Archange Touadéra na vilimuunga mkono rais wa zamani François Bozizé,wamekuwa wakisonga mbele kuelekea katika mji mkuu.

  4. Uchaguzi Uganda 2021:Tume ya uchaguzi yatangaza kumalizika kwa kampeni

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Jaji Simon Byakama

    Chanzo cha picha, bbc

    Maelezo ya picha, Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Jaji Simon Byabakama

    Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, Jaji Simon Byabakama ametangaza kuwa kuanzia leo mtu yeyote hatakiwi kufanya kampeni za namna yeyote ile.

    Aidha amesema uchaguzi utafanyika kesho Januari 14,2021 siku ya Alhamis, huku kukiwa na jumla ya wapiga kura wa kiume ni zaidi ya milioni nane na wanawake wakiwa zaidi ya milioni tisa.

    Amesisitiza pia kuwa waandishi wa habari hawataruhusiwa kuingia kwenye chumba cha kupitia kura.

  5. Kwa picha: Watetezi wa haki za binadamu nchini Kenya wakamatwa nje ya ubalozi wa Uganda

    Watetezi wa haki za binadamu wanne wa Kenya wamekamatwa nje ya ubalozi wa Uganda jijini Nairobi asubuhi muda mfupi kabla ya kuwasilisha taarifa yao kwa vyombo vya habari kuhusiana na ukatili wa polisi dhidi ya upinzani nchini Uganda.

    Wanaharakati hao ambao kwa sasa wanashikiliwa kwa ajili ya kuhojiwa na polisi ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Haki Afrika, Hussein Khalid pamoja na mwandishi wa habari Yassah Musa.

    Wanaharakati
    Maelezo ya picha, Mtetezi wa haki za binadamu na Mkurugenzi wa Haki Afrika -Hussein Khalid akiwa amelala chini mbele ya polisi
    Mwanaharakati
    Mwnaharakati
    Polisi
    Maandamano
    Maandamano
  6. Marekani yalalamika baada ya Uganda kuwanyima idhini wakaguzi wake wa uchaguzi

    Balozi wa Marekani nchini Uganda ameeleza kusikitishwa na hatua ya serikali ya kukataa kuwapatia wasimamizi wao idhini ya kusimamia uchaguzi.

    Balozi Natalie Brown amesema kuwa zaidi ya asilimia 75 ya maombi ya idhini za ujumbe wa wakaguzi wa Marekani yalikataliwa.

    Ni watu 15 pekee ndio waliopewa idhini hiyo, lakini ubalozi huo unasema idadi hii haitoshi kufuatilia uchaguzi.

    Bi Brown ameongeza kuwa Tume ya uchaguzi haikutoa maelezo yoyote juu ya ni kwanini maombi yao yalikataliwa, ingawa ubalozi huo uliwasilisha nyaraka zote zinazohitajika.

    Kupitia ujumbe wa Twitter Balozi Natalie E. Brown alisema kuwa anasikitika kutangaza uamuzi wa Marekani wa kutosimamia uchaguzi wa Uganda baada ya asilimia 75 ya maombi ya idhini ya kusimamia uchaguzi kukataliwa:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mwaka 2016, Marekani ilikuwa na wakaguzi wa uchaguzi zaidi ya 80 kote nchini Uganda.

    Jumuiya ya Afrika Mashariki na Muungano wa (IGAD), ndio waliothibitisha kupata idhini ya kufuatilia uchaguzi mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii.

  7. Kasisi ‘anayepinga vita dhidi ya madawa ya kulevya’ ashitakiwa kwa fitna

    Father Flavie Villanueva ni mkosoaji mkubwa wa "vita dhidi ya madawa ya kulevya"
    Maelezo ya picha, Father Flavie Villanueva ni mkosoaji mkubwa wa "vita dhidi ya madawa ya kulevya"

    Kasisi wa kikatoliki nchini Ufilipino anatarajiwa kufikishwa mahakamani akishitakiwa kwa makosa ya " kuhamasisha umma kuuasi utawala " kuhusiana na madai ya njama ya kumpindua madarakani rais Rodrigo Duterte.

    Padre huyo, Flavie Villanueva ni mkosoaji mkubwa wa "vita dhidi ya madawa ya kulevya", vya rais Duterte ambayo alivianzishwa Julai Julai 2016.

    Tangu mapambano dhidi ya biashara ya mihadarati yaanzishwe nchini Ufilipino, maelfu ya watu wameuliwa na polisi.

    Padre Flavie Villanueva ameshutumiwa pamoja na watu wengine 10 kwa kuwa miongoni mwa watu walioandaa misururu ya video zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ambazo serikali ilisema ziliichafua sifa ya rais Duterte.

  8. Chama cha 'wanaume wachoyo' chaanzishwa Nigeria

    Taarifa kuhusu chama cha wanaume wachoyo cha Nigeria- Stingy Men Association of Nigeria (Smen), imeenea kwenye mtandao wa kijamii waTwitter nchini Nigeria huku wanaume maarufu wa Nigeria wakishirikisha umma kadi za uanachama wao wa kikundi hicho.

    Ujumbe wa Twitter wa mzalishaji wa muziki Don Jazzy wa kadi yake ya uanachama ulishirikishwa tena na wafuasi wake mara 11,000.

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Nyota wa muziki wa Afrobeats Bw Eazi pia alituma kati yake ya uanachama katika chama cha wanaume wachoyokupitia mtandao wa Twitter:

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

    Akaunti rasmi ya chama cha wanaume wachoyo kwenye mtandao wa Twitter ilionekana kwenye mtandao huo kwa mara ya kwanza Jumatatu:

    Ruka X ujumbe, 3
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 3

    Wanaotuma jumbe za Twitter wamekuwa wakitania kuwa watabuni wimbo wao maalumu, makao makuu na kiapo.

    Haijawa wazi ni vipi taarifa ya chama cha wanaume wachoyo iliyoshirikishwa zaidi kwenye Twitter ilivyoanza nchini Nigeria. Wazo hilo tayari limesambaa katika mataifa mengine ya Afrika.

    Mwezi Disemba taarifa ya gazeti la Uganda la Daily Monitor iliainisha pendekezo la kikundi hicho nchini Uganda.

    Katika taarifa hiyo iliyoandikwa na , Ian Ortega aliandika: "Katiba hii iliandikwa katika mwaka wa janga la corona itaelezea maana ya hatua kali ."

    Sehemu ya"katiba yake " iliwalengamarafiki wa kike wanaowaomba wapenzi wako wa kiume pesa.

    "Kila binti wa Eva ambaye anaomba pesa atachukuliwa kama muhamiaji haramu na kuepukwa; ‘hafai kuwa mke ,’" aliandika.

    Aliendelea kusema kuwa “mjumbe hapaswi kuhisi aibu yoyote katika kukataa ombi lolote la pesa linalowasilishwa kwake.”

    Hii ni pamoja na maombi ya pesa za usafiri au salio la simu.

  9. Museveni atetea sababu za kufunga mitandao ya kijamii kabla ya uchaguzi

    Museveni

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni amethibitisha kuagiza mitandao kadhaa ya kijamii nchini humo kufungiwa.

    Katika hotuba yake iliyooneshwa mubashara katika televisheni usiku wa Jumanne saa tatu kabla ya muda wa mwisho wa kufanya kampeni, Rais Museveni aliyekuwa amevalia koti la kijeshi alisema ameagiza kufungwa kwa mtandao wa kijamii wa Facebook kwa kuwa na kiburi na kupendelea upande mmoja.

    Alisema ikiwa Facebook itatumiwa nchini Uganda, lazima itumiwe kwa usawa na kila mtu anayetaka kufanya hivyo. Bw. Museveni pia alisema hatakubali mtu yeyote kucheza na nchi yake ama kuamua ni nani mzuri au mbaya.

    Hatua ya Rais inakuja siku moja baada ya Facebook kuthibitisha kwamba imezifungia akaunti zinazohusishwa na serikali ikidai kuwa zinatumiwa kushawishi mijadala ya umma katika kinyang'anyiro kikali cha uchaguzi, ambapo rais aliye madarakani na mpinzani wake mkuu, Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine wanatafuta ushindi wa kura za vijana.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Watumiaji wa mitandao ya kijamii ya Facebook na WhatsApp, Instagram na Snapchat walianza kulalamikia kukatizwa kwa huduma hizo mapema siku ya Jumanne.

    Twitter imejibu hatua hiyo ikisema kuzingiwa kwa huduma za intaneti ni hatari na inakiuka haki za kimsingi za binadamu na kanuni ya uhuru wa mawasiliano.

    Wakati huo huo Marekani imelaani uamuzi wa serikali kufunga mitandao ya kijamii, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akitoa wito wa kuheshimiwa haki za binadamu.

  10. Karibu katika matangazo mubashara Jumatano 13.01.2021