Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Magufuli, Nyusi wazungumzia maendeleo, usalama
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewasili nchini Tanzania leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Magufuli, Nyusi wajadiliana kuhusu maendeleo, usalama
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yusuph Mazimu
- Nafasi, BBC Swahili
Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi yuko nchini Tanzania kwa ziara yake ya siku mbili, ambapo leo amekutana na mwenyeji wake Rais John Pombe Magufuli na Kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo maendeleo na Usalama. Kabla ya mazungumzo na Mwenyeji wake, Rais Nyusi aliweka jiwe la msingi, kwenye hospitali ya rufaa ya kanda ya Chato, itakayohudumia wagonjwa zaidi ya milioni 14 kutoka Tanzania na nchi jirani kama Kenya na Uganda.
Moja ya maeneo ambayo nchi hizo zinajaribu kuzungumza ni kuhusu kuboresha uchumi kupitia biashara baina ya nchi hizo mbili.
'Biashara ya sasa hivi kati ya Tanzania na Msumbiji imeongezeka na kufikia bilioni 93.6, kuna makampuni ya Msumbiji yanafanya kazi hapa, na kuna makampuni ya Tanzania yanafanya kazi msumbiji', alisema Magufuli
Wadadisi wengi wa siasa za Afrika, wanasema ziara ya Nyusi nchini Tanzania, pamoja na mambo mengine, suala la usalama ni jambo litakalochukua nafsi zaidi.
'Tumeongelea kuhusu mambo ya Covid 19, namna gani tukabaliana nayo na pia kuangalia mambo ya usalama', alisema Nyusi.
Rais Nyusi ambaye amesoma elimu yake ya msingi nchini Tanzania,hakuweka wazi ni mambo gani ya usalama ambayo wamejadiliana, ni jambo lililo wazi kuwa mpaka wa nchi hizo umekumbwa na matukio ya kigaidi toka mwaka 2017.
Serikali ya Tanzania mwaka jana ilituma vikosi vyake vya jeshi ili kujihami na tishio hilo la ugaidi.
Wanamgambo wa Kiisilamu wenye mafungamano na kundi la IS wanaendesha shughuli za kigaidi kaskazini mwa Msumbiji kwenye jimbo la Cabo Delgado na mara kadhaa wamevuka mpaka na kushambulia vijiji vya Tanzania.
Mwezi Oktoba mwaka jana magaidi hao walifanya shambulio katika Kijiji cha mpakani cha Kitaya mkoani Mtwara. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa Tanzania IGP Simon Sirro magaidi zaidi ya 300 walivuka mpaka na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji.
Sirro alithibitisha kuwa baadhi ya washukiwa wa ugaidi waliokamatwa walikuwa ni raia wa Tanzania.
Rais Museveni atoa video ya densi ya Jerusalema
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa video ya kibonzo chake akicheza densi ya wimbo uliovuma wa Jerusalema.
Densi ya Jerusalema ilikuwa ni densi iliyovuma na kuchezwa kote duniani mwaka jana, kupitia kampeni ya mtandao iliyojulikana kama #Jerusalemachallenge baada ya kutolewa kwa wimbo wa Jerusalema na mwanamuziki wa Afrika Kusini Master KG.
Rais Museveni amesema kuwa ametoa video hiyo baada ya kushawishiwa na wafuasi wake vijana.
Waganda watapiga kura Alhamisi wiki hii kuwachagua wabunge na rais.
Bw Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 35, anawania muhula wa sita. Jumla ya wagombea 11 wanawania kiti cha urais akiwemo mwanamke mmoja.
Michael B. Jordan na Lori Harvey watangaza uhusiano wa kimapenzi
Baada ya miezi kadhaa ya tetesi , sasa mchezaji filamu maarufu wa Marekani Michael B. Jordan amethibitisha kuwa na mahusiano na Lori Harvey.
Wawili hao wamezungumzia kuhusu mapenzi yao, kupitia kurasa zao rasmi za Instagram siku ya Jumapili, huku wakishirikisha umma picha za mapenzi yao katika ukurasa huo wa Instagram.
Jordan, ambaye amekuwa msiri kuhusu maisha yake ya mapenzi, alikuwa wa kwanza kushirikisha umma picha yao kwenye Instagram.
Michael B. Jordan alitangazwa kama mwanaume mwenye muonekano mzuri zaidi duniani mwaka 2020.
Mchezaji filamu Michael Jordan B. mwenye umri wa miaka 33 alionekana katika picha moja ya snap na Harvey, kabla ya kuonesha akimbusu. Alimshirikisha Harvey picha hizo, pamoja na mpiga picha Leo Volcy.
Harvey – ambaye aliasiliwa na Steve Harvey baada ya kumuoa mama yake 2007 Marjorie Bridges – alishirikisha umma picha hizo akiwa na Michael Jordan B. dakika chache tu baadae.
Lori ni mwanamitindo na amekuwa akionesha mitindo ya Dolce and Gabbana, katika wiki za mitindo za Paris na Milan.
Watu maarufu akiwemo mcheza filamu Gabrielle Union na mwanamuziki wa rap Teyana Taylor, walituma jumbe zao kuonesha upendo wao kwa wapenzi wao.
Mwanafunzi wa Kenya akiri kuiua familia yake
Mwanafunzi wa chuo kikuu nchini Kenya amekiri kwa polisi na kutoa taarifa zaidi juu ya namna alivyopanga na kuwauwa watu watano wa familia yake, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.
Simon Warunge, mwenye umri wa miaka 22, ameripotiwa kuwaambia polisi kwamba alitumia chuma kumgonga mama yake, kaka yake, baba yake na binamu yake kabla ya kuwadunga visu na kuwauwa.
Mwanafunzi huyo aliwaambia polisi kuwa wazazi wake walikuwa wafuasi wa shetani na makatili, limeripoti gazeti la the Star.
Alisema kuwa walimchukia na kumsema wakati hayupo, imeripoti televisheni ya Citizen.
Madada zake wawili ambao walikuwa wamerejea shuleni walinusurika na shambulio hilo.
Mama yake alikuwa ni muuguzi wa kisaikolojia nchini Kenya, na baba yake alikuwa muuguzi nchini Marekani na alikuwa amewasili nchini Kenya kwa ajili ya sherehe za Krismasi kabla ya mauaji hayo.
Wachunguzi wamefungua uchunguzi upya kuhusiana na mauaji mengine ambayo yalitokea katika ndugu wengine wa familia hiyo.
Polisi pia wamemkamata mpenzi wa kike wa mshukiwa. Wawili hao wamefikishwa mahakani Jumatatu:
Aliko Dangote apoteza mamilioni ya pesa ndani ya siku moja
Mwenyekiti wa kampuni ya Dangote, Alhaji Aliko Dangote, amepoteza kiasi cha dola milioni 900 katika hisa nchini Nigeria, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bloomberg.
Kwa mujibu wa jarida la Bloomberg, ambalo huripoti kuhusu watu 500 tajiri zaidi duniani, mapato ya Dangote yalishuka kwa kiwango cha dola bilioni 18.4 siku ya Alhamisi hadi dola bilioni 17.5 siku ya Ijumaa ,akishuka kutoka mtu wa 106 hadi hadi mtu wa 106 katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani , kulingana na gazeti la Punch.
Mwezi Disemba mwaka jana, utajiri wa Dangote ulikuwa na jumla ya thamani ya dola bilioni 17.8 kutoka dola bilioni 15.5 zilizoripotiwa awali.
Dangote alipata mapato ya ziada ya dola milioni 600 katika wiki ya kwanza ya mwezi wa Januari 2021, lakini kapoteza pesa yote hiyo Ijumaa iliyopita.
Hata hivyo Dangote bado ndiye mtu tajiri zaidi barani Afrika na mtu mweusi tajiri zaidi duniani.
Tajiri akabiliwa na kesi ya machimbo ya madini nchini Guinea
Mfanyabiashara, raia wa Israeli anashitakiwa mjini Geneva Jumatatu kwa mashitaka ya ufisadi unaohusiana na haki za uchimbaji wa madini ya chuma nchini Guinea.
Beny Steinmetz, ambaye tayari alikwisha hukumiwa kifungo cha miaka mitano jela na mahakama ya Romania kwa madai ya utakatishaji wa fedha bila kuwepo mahakamani, ingawa atafika mahakamani mwenyewe mjini Geneva.
Amekuwa akikana madai yote ya ufisadi dhidi yake.
Waendesha mashitaka wa Uswiss walisema alilipa hongo ya mamilioni ya dola , baadhi kupitia akaunti za benki za Uswiss , ili kupata haki ya kuchimba madini ya chuma ya Guinea katika machimbo ambayo hayajawahi kuchimbwa duniani.
Hongo hizo – kwa maafisa wa umma wa Guinea –zilidaiwa kulipwa kwa usaidizi wa mjane wa rais wa zamani wa Guinea Mamadou Toure, Lansana Conte.
Amekuwa akielezewa kama shahidi nyota wa uendesha mashitaka- lakini huenda asiwepo mahakamani.
Kwa sasa Bi Lansana Conte anaishi nchini Marekani.
Beny Steinmetz atafika mahakamani na anatarajiwa kukanusha tuhuma zote. Iwapo atapatikana na hatia anakabiliwa na kifungo cha miaka 10 jela.
Filipe Nyusi: Rais wa Msumbiji awasili Tanzania kwa ziara ya siku mbili
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi amewasili nchini Tanzania leo kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.
Nyusi ametua wilayani Chato, Mkoani Geita Kaskazini mwa Tanzania na kupokewa na mwenyeji wake rais John Magufuli.
Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania Prof Palamagamba Kabudi ameielezea ziara hiyo kuwa ya kindugu ambayo itaangazia masuala ya kidiplomasia na biashara. Waziri huyo ameeleza kuwa ziara hiyo ilipangwa kufanyika mwaka jana lakini ikashindikana kutokana na uchaguzi wa Tanzania.
Japo Waziri Kabudi hakutanabahisha mbele ya wanahabari jana Jumapili iwapo suala la usalama katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji litakuwa sehemu ya majadiliano, bila shaka viongozi hao watajadili suala hilo.
Serikali ya Tanzania mwaka jana ilituma vikosi vyake vya jeshi ili kujihami na tishio hilo la ugaidi.
Wanamgambo wa Kiisilamu wenye mafungamano na kundi la IS wanaendesha shughuli za kigaidi kaskazini mwa Msumbiji kwenye jimbo la Cabo Delgado na mara kadhaa wamevuka mpaka na kushambulia vijiji vya Tanzania.
Mwezi Oktoba mwaka jana magaidi hao walifanya shambulio katika Kijiji cha mpakani cha Kitaya mkoani Mtwara. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi wa Tanzania IGP Simon Sirro magaidi zaidi ya 300 walivuka mpaka na kufanya uhalifu ikiwemo mauaji.
Sirro alithibitisha kuwa baadhi ya washukiwa wa ugaidi waliokamatwa walikuwa ni raia wa Tanzania.
Rais wa Zambia amfuta kazi waziri wa afya
Rais wa Zambia, Edgar Lungu amemfukuza kazi waziri wa afya nchini humo Bw. Chitalu Chilufya, ambaye alikamatwa mwezi Juni kwa madai ya ufisadi lakini aliachiliwa baadae.
Bw Chilufya alishitakiwa makosa manne ya kumiliki mali ambazo alishukiwa kuzipata kwa njia ya uhalifu. Aliachiliwa huru kutokana na ukosefu wa ushahidi dhidi yake na kurejea kazini.
Jumapili Rais Lungu hakutoa sababu za kumfuta kazi, lakini akasema kuwa uamuzi huo unatekelzwa mara moja.
Mwandishi wa BBC Kennedy Gondwe ameripoti kuwa wizara ya afya imekuwa ikigubikwa na madai ya ufisadi, ambapo madai ya hivi karibuni yalihusisha usambazaji wa mipira ya kondomu yenye kasoro ya thamini ya dola milioni 17 (£12m) pamoja na glovu zinazotumika katika shughuli ya upasuaji.
Kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema amesema kuwa "kumfuta kazi Dkt Chitalu Chilufya haitoshi na ni hatua ndogo sana iliyochelewa kuchukuliwa''
Walinzi sita wauawa katika mbuga ya kitaifa ya Virunga DR Congo
Walinzi sita wameuawa baada ya kushambuliwa katika mbuga ya kitaifa ya Virunga mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Maafisa wameelekezea kidole cha lawama kundi la waasi linalojulikana kama Mai-Mai, ambalo ni miongoni mwa makundi kadhaa ya waasi yanayohudumu katika eneo hilo.
Katika taarifa yake mbuga hiyo imesema uchunguzi wa awali unaashiria kuwa walinzi hao walivamiwa ghafla na hawakuwa na muda wa kujilinda na shambulio hilo lililotokea asubuhi Jumapili.
Ilisema mlinzi aliyejeruhiwa vibaya anapokea matibabu.
Mjumbe wa serikali ya mtaa Alphonse Kambale aliliambia shirika la habari la AFP kuwa wanamgambo wawili wa Mai-Mai pia wameuawa.
Walinzi hao walivamiwa walipokuwa wakifanya doria za kawaida ndani ya mbuga hiyo, kwa mujibu wa msemaji aliyezungumza na BBC.
Wafanyakazi katika mbuga hiyo ambayo huwahifadhi sokwe wa milimani wanaokabiliwa na tishio la kuangamia, wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara.
Mwezi Aprili mwaka jana walinzi 13 waliuawa na waasi baada ya kushambuliwa ghafla.
Uchaguzi Uganda 2021: Facebook yaeleza ni kwanini ilifunga akaunti za maafisa wa Uganda
Kampuni ya Facebook imeeleza sababu ya kufunga makumi kadhaa ya akaunti za mtandao huo za wafuasi wa chama tawala cha Uganda cha National Resistance Movement (NRM).
Kmapuni hiyo kubwa ya Teknolojia imezishutumu akaunti hizo kwa kutaka kuendesha mjadala wa umma kabla ya uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Alhamisi.
"Mwezi huu, tuliondoa mtandao wa akaunti na kurasa nchini Uganda ambazo zinahusika katika uratibu wa tabia ya kutokuwa na uhalisiaili kulenga mjadala wa umma kabla ya uchaguzi ," Mkuu wa mawasiliano wa Facebook kusini mwa jangwa la Sahara, Kezia Anim-Addo, aliliambia shirika la habari la AFP.
Hii inakuja baada ya wamiliki wa akaunti 50 za Facebook zinazounga mkono chama tawala nchini Uganda cha National Resistance Movement [NRM] kulalamikia kufutwa kwa akaunti zao au kushindwa kuchapisha jumbe zao kupitia mtandao huo wa kijamii.
“Aibu kwa mamlaka za kigeni ambazo zinadai zinaweza kupandikiza uongozi wanaoweza kuutumia kwa kuzuia utendaji wa akaunti za mtandao za wafuasi wa NRM . Hautamtoa RaisYoweri Kaguta Museveni,” alisema afisa wa habari wa rais Don Wanyama.
Mwanaboligi maarufu nchini Uganda Ashburg Kato alidai kuwa kampuni kubwa ya teknolojia yenye makao yake makuu California ilifuta akaunti zao kufuatia maombi ya chama tawala cha upinzani nchini Uganda cha National Unity Platform (NUP) cha mgombea Robert Kygulanyi al maarufu Bobi Wine na ''washirika '' wake
“Facebook yenyewe ilifuta akaunti zetu kutokana na ombi la washirika wa Bobi Wine''Kato alitweet.
Alitoa wito kwa rais achukue hatua dhidi ya Facebook.
Hujambo na karibu katika matangazo mubashara Jumatatu 11.01.2021