Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Vyama vya upinzani Uganda waungana kuwa na kituo kimoja cha 'kuhesabia' kura

Vyama vya upinzani nchini Uganda wameungana kuwa na kituo chao kimoja cha kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu.

Moja kwa moja

Abdalla Seif Dzungu

  1. Uchaguzi Uganda 2021:Vyama vya upinzani Uganda wameungana kuwa na kituo kimoja cha 'kuhesabia' kura

      • Author, Isack Mumena
      • Nafasi, BBC Swahili Kampala

    Jukwaa linalojulikana kama UID litahusisha matumizi ya teknolojia na nyenzo zingine kuhakikisha kuwa takwimu za matokeo ya uchaguzi kutoka sehemu mbalimbali nchini Uganda yanahakikiwa ipasavyo.

    Hii ina maana kuwa wawakilishi wa vyama vyote vya kisiasa kwenye kituo watashirikiana katika kutoa taarifa kuhusu hali ilivyo kuanzia mwanzo hadi mwisho hasa wakifuatilia vitendo ya ukiukaji wa haki za binadamu.

    Mwanasiasa mkongwe Paul Semwogerere aliyewahi kuwania kiti cha urais mwaka 1996 dhidi ya rais ndiye mratibu wa jukwaa hilo.

    Daktari Kizza Besigye ambaye amewahi kugombea kiti cha urais mara nne na kushindwa na rais Museveni amekanukuliwa kwamba ijapokuwa upinzani ulishindwa kuungana kuwa na mgombea mmoja, muungano huu ni muhimu sana kuweza kukabiliana na jaribio lolote la wizi wa kura.

    Vyama vya upinzani nchini Uganda wameungana kuwa na kituo chao kimoja cha kuhesabu kura katika uchaguzi mkuu, vyama hivyo ni NUP, FDC, JEEMA,DP,ANT na mgombea wa kiti cha urais wa kujitegemea Jeneri Henery Tumukunde na Dk.Kiiza Besigye wa serikali ya wananchi.

    Mwenyeti wa chama cha Jeema anaelezea kwani wameamuwa kuwa na kituo chao kwasababu tayari chama tawala cha NRM kimetangaza kuwa watakuwa na kituo chao tofauti na tume ya uchaguzi lakini wenye kutangaza matokeo ni tume ya uchaguzi.

  2. Waziri wa fedha wa Marekani azuru Sudan kwa mazungumzo

    Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin yuko nchini Sudan kwa mazungumzo kuhusu uchumi, kufuatia hatua ya mwaka jana ya kuindoa Khartoum katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi.

    Serikali ya Sudan imesema Bw. Mnuchin atajadili utatuzi wa madeni na misaada ya Marekani siku zijazo ya thamani ya zaidi ya dola bilioni moja sawa na (£970m).

    Uchumi wa Sudan umezorota kufuatia mfumko wa bei wa hali ya juu na uhaba wa sarafu.

    Marekani iliiondoa Sudan kutoka kwa orodha ya ugaidi mwezi Decemba baada ya Khartoum kufufua uhusiano wake na Israel.

  3. 'Wimbi la pili la corona barani Afrika ni baya zaidi'

    Wimbi la pili la corona linalokumba Afrika ni “kali zaidi” kuliko la kwanza, kwa mujibu wa John Nkengasong wa Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika (CDC),

    Aliambia BBC kwamba bara hilo kwa sasa linaripoti maabukizi mapya ya karibu 30,000 kila siku ikilinganishwa na 18,000 katikati ya mwezi Julai.

    Takwimu za shirika hilo la afya zinaonesha kwamba Afrika kufikia sasa imethibitisha kuwa watu karibu milioni 3 wameambukizwa virusi vya corona, na vifo 68,755.

    Nchi kama Rwanda, Namibia, Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zimeweka vikwazo vipya vya kuzuiz kuenea kwa virusi.

    Dkt Nkengasong alisema kuvaa barakoa ndio njia pekee ya kuzuia kuenea kwa virusi na kutoa wito kwa serikali kupunguza bei ya bidhaa hiyo.

    Aliongeza kusema:

    ‘’Unapotembea katika nchi tofauti barani Afrika inasikitisha kuona watu wengi hawavai barakoa mara kwa mara ama hawavai kabisa,na pia hawazingatii umati kati ya mtu moja na mwingine. Hii ni hatari, wimbi la pili ni kali sana."

  4. Dr Dre alazwa hospitalini akiuguza tatizo la ubongo

    Mwanamuziki wa mtindo wa Rap na mtayarishaji wa muziki Dr Dre, mmoja wa wanamuziki maarufu, aliiyefanikiwa zaidi na mwenye ushawishi mkubwa katika muziki nchini Marekani anapokea matibabu katika hospitali baada ya kupatikana na tatizo la ubongo.

    Msanii huyo mwenye umri wa miaka 55 alisafirishwa hadi katika hospitali ya Cedarsmjini Los Angelssiku ya Jumatatu, kulingana na mtandao wa TMZ.

    Katika chapisho la Instagram , aliserma : Naendelea vyemana matibabu ya kiwango cha juu .

    ‘’Anapumzika akiwa katika hali shwari baada ya kupata matibabu hayona atarudi nyumbani hivi karibuni’’.

    ‘’Nawapongeza maafisa wote wwq wmatibabu katika hospitali ya Cedar’’ .

    Mapenzi tele!!

  5. Rais Museveni amemteua mwanajeshi kusimamia usalama wakati wa uchaguzi Uganda

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda amemteua meja generali Kayanja Muhanga kuwa mratibu wa masuala ya usalama nchini Uganda .

    Naibu msemaji wa jeshi luteni kanali Deo Akiiki ameambia BBC kwamba meja jenerali Muhanga atakuwa mratibu wa operesheni za vitengo vyote vya usalama.

    ‘Ni kweli kwamba Brigedia Kayanja Muhanga amepewa nafasi ya kuratibu vikundi vyote vya usalama kwa madhumuni ya kuunganisha shughuli ya usalama wa pamoja hususan katika mji wa Kampala na nchi yote’ .

    "Hiyo ina maana kwamba atakuwa kiunganishi kati ya kikosi cha polisi , jeshi na idara ya ujasusi , alithibitisha luteni huyo.

    Rais Yoweri Museveni ameweka shinikizo katika polisi wa mji wa Kampala ambao karibia utawaliwe na ghasia pamoja na wahalifu ambao walikuwa wamewaonya polisi kutofika katika maeneo fulani.

    Tangu uzinduzi wa kamera za CCTV , kituo kinachohusika na jeshi pamoja na maafisa wa polisi kilibuniwa katika kituo cha polisi cha Kampala.

    Kulingana na gazeti la the Monitor, kunapotokea tisho lolote Meja jenerali Samuel Kawagga, kamanda wa polisi wanaosimamia wanajeshi kanali Keith Katungi na kamanda wa polisi katika mji wa Kampala Moses Kafeero, hukutana katika kituo hicho cha kati ili kutafuta mbinu ya kuangazia tatizo lililopo

  6. Je ndoa ya Kanye west na Kim kardashian ipo mashakani?

    Mlimbwende wa Marekani Kim Kardashian na mume wake msanii Kanye West wamekuwa wakipata ushauri wa ndoa yao,lakini mtandao wa TMZ nchini humo umegundua kwamba kwa suala la wawili hao kutengana limekuwepo kwa muda mrefu lakini hawajakata tamaa.

    Vyanzo kadhaa vilivyo na habari zinazowahusu wawili hao vimeambia mtandao huo nchini Marekani , kwamba ndoa hiyo ilikuwa katika matatizo makubwakatika nusu ya mwisho wa mwaka 2020.

    Habari zinasema kwamba Kim alikuwa tayarikuomba talakakatika tukio moja lakini kwasababu Kanye alikuwa anakumbwa na tatizo la kiakili akaona kwamba sio vyema kuchukua hatua hiyo wakati ambapo hali ya mume wake sio nzuri.

    Wamekuwa wakiishi kandokando kwa miezi kadhaahuku Kanye West akitumikia wakati wake mwingikatika eneo la Wyomingnaye Kim Kardashian akiwa katika eneo la Calabasas na watoto.

    Wote wamekuwa katika harakati za kazi zao na hawakuangazia kufanya uamuzi wowote wa mwisho.

  7. Natumai Hamjambo