Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Rais Museveni amteua tena mwanae kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi

Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni amiri jeshi mkuu amefanya mabadiliko katika jeshi la Uganda (UPDF)na kumrejesha mwanae Lt.Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais yaani Special Force Command(SFC)

Moja kwa moja

Ambia Hirsi and Dinah Gahamanyi

  1. Rais Museveni amteua tena mwanae kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi

      • Author, Isack Mumena
      • Nafasi, BBC Swahili Kampala

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye pia ni amiri jeshi mkuu amefanya mabadiliko katika jeshi la Uganda (UPDF)na kumrejesha mwanae Lt.Jenerali Muhoozi Kainerugaba kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais yaani Special Force Command(SFC)

    Mabadiliko hayo yamefanyika wakati wanasisa wa upinzani wakilaumu jeshi la polisi kwa kuwasumbua katika kampeni zao za uchaguzi zinazoendelea nchini.

    Aliyekuwa naibu wa mkuu wa jeshi la polisi IGP Meja Jenerali Sabiiti Muzeyi na nafasi hiyo imechukuliwa na Gen Paul Lokech aliyekuwa katika uangalizi maalum wa masuala ya Sudani kusini, ikiwa Sabiiti Muzeyi amerudishwa makao makuu ya jeshi kusubiri kupewa nafasi nyingine.

    Naibu wa msemaji wa jeshi la UPD Luteni Kanali Deo Akiiki amedhibitisha uteuzi huo alipozungumuza na BBC kwa njia ya simu.

    Jenerali Mhoozi amerudishwa kwenye cheo ambacho aliwahi kukitumikia kabla ya kubadilishwa kuwa mshauri wa rais Museveni katika masuala ya ulinzi.Na kitengo hicho ndicho kina husika na kumulinda rais wa Uganda.

    Mabadiliko haya yamefanyika wakati zikiendelea kampeni za uchaguzi mkuu wa rais ambapo wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakituhumu jeshi la polisi kuwatatiza kwenye kampeni zao,lakini Msemaji wa jeshi amesema ni mabadiliko ya kawaida tu.

    Katika uteuzi huo rais Museveni amemubakiza mkuu wa jeshi la polisi IGP Okoth Ochola kuhifadhi wadhifa wake.

  2. Shule zafungwa Nigeria baada ya watoto kutekwa

    Majimbo manne nchini Nigeria wametoa amri ya shule kufungwa baada ya wanafunzi zaidi ya 100,kutekwa katika jimbo la Katsina.

    Shule hizo zimefungwa katika jimbo la Kano, Kaduna, Zamfara na jimbo la Jigawa.

    Umoja wa walimu nchini Nigeria wametishia kufanya mgomo kupinga kutishiwa kiusalama katika nchi yao.

    Chama hicho kinasema wanafunzi na walimu ndio wamelengwa zaidi na hao watekaji na wapiganaji.

    Wiki iliyopita mamia ya wanafunzi walitekwa katika shule moja ya sekondali ya serikali inayofundisha masomo ya sayansi katika jimbo la Kankara.

    Wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram walikiri kufanya shambulio hilo.

    Serikali shirikishi bado hawajaeleza wamefikia wapi katika uokoaji ili wanafunzi 333 wamepotea mpaka sasa.

  3. Seven ateuliwa kuwa kiongozi wa Sony Music Afrika Mashariki

    Kampuni ya burudani barani Afrika Sony Music imemchagua Christine Mosha, anayejulikana kama “Seven,” kusimamia masoko na maendeleo ya wasanii katika ukanda wa Afrika Mashariki.

    Seven atatengeneza utaratibu katika kampuni hiyo kukuza vipaji vya wasanii kimataifa akianzia Tanzania. Yeye atakuwa anafanya kazi moja kwa moja na Sean Watson, Mkurugenzi wa Sony Music Africa.

    “Seven amekuwa katika tasnia ya muziki kwa miaka 15 akiwa meneja wa wanamuziki maarufu kama Ali Kiba,Lady Jaydee, Ray C, TID, Rose Muhando na Ommy Dimpoz.

    Mwaka 2017,Seven alianzisha kampuni yake mwenyewe ya kurekodi inayojulikana kama Rockstar Africa,ambako aliweza kuwa na matokeo chanya kibiashara kwa wanamuziki anaowasimamia.

    Mnamo mwaka 2006, Seven alikuwa mtangazaji wa radio katika kampuni ya Clouds Media Group, kabla ya kuhamia MTV.

  4. DRC kuweka kafyu ya kitaifa kudhibiti wimbi la pili la corona

      • Author, Mbelechi Msochi
      • Nafasi, BBC Swahili Kinshasa

    Mamlaka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza kuweka kafyu ya kitaifa kuanzia Disemba 18 kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

    Kwa mujibu wa taasisi ya kukabiliana na janga la covid 19, hatua hio yamechukuliwa kulingana na ongezeko la kushangaza la visa vipya vyamaambukizi Jana, kumeriptiwa kesi mia tatu arbaini na nane ya visa vipya vya maambukizi, iapo sikuzilizo ijapita takwimu za kesi za maambukizi zilikuwa chini sana.

    Kuanzia Disemba 18, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wataanza likizo licha ya kuwa walipaswa kufunga tarehe 24.

    Baada ya saa saa tatu usiku hakuna mtu atakayeruhisiwa kutoka nje na polisi wataanza kushika doria. Maandamani na tamasha za muziki zimepigwa marufuku.

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imekuwa miongoni mwa nchi zinazokabiliana na wimbi la pili la maambukizi ya corona kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani,WHO.

  5. Wabakaji Pakistan kuhasiwa kwa kemikali

    Rais wa Pakistan amesaini sheria mpya itakayotoa adhabu kali dhidi ya wahusika wa ubakaji.

    Kulingana na sheria hiyo serikali itaweka sajili ya watu wanaopatikana na makosa ya ubakaji, kulinda utambulisho wa waathiriwa na matumizi ya kemikali kuwahasi baadhi ya wabakaji.

  6. Wawili wafariki katika mkanyagano wa zawadi za Krismasi

    Polisi katika jimbo la Rivers nchini Nigeria wamethibitisha vifo vya watu wawili waliouawa katika mkanyagano wa hafla iliyoandaliwa na shirika lisilokuwa la kiserikali kugawanya zawadi za krismasi.

    Vyombo vya habari katika eneo hilo vinaripoti kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka kwasababu watu wengi wamelazwa hospitali

    Mkanyagano huo ulitokea siku ya Jumanne katika eneo la Rumuodara katika mji wa bandari wa Port Harcourt.

    Waliyoshuhudia tukio hilo wanasema watu hao walikuwa wanang'ang'ana kufika katika ofisi za shirika hilo mkanyagano ulipotokea.

    Msemaji wa polisi katika jimbo hilo Nnamdi Omoni amenukuliwa kusema kwamba "uchunguzi umeanzishwa kubaini kilichotokea na watakaopatikana na makosa kuchukuliwa hatua za kisheria".

  7. Kenya kufungua ubalozi katika jimbo linalotaka kujitenga na Somalia

    Kenya itafungua ubalozi mdogo katika jimbo la Somaliland kufikia mwisho wa mwezi wa Machi wakati Somaliland nayo ikipanga kupandisha hadhi ofisi yake ya Kenya kuwa ubalozi mdogo.

    Tangazo hilo la pamoja limetolea na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Somaliland Muse Bihi Abdi mwisho wa ziara yake nchini humo.

    Viongozi hao wawili pia walikubaliana ndege ya Shirika la ndege la Kenya Airways kufanya safari ya moja kwa moja kutoka mji mkuu wa Nairobi, Kenya hadi mji wa Hargeisa ambao ni mji mkuu wa Somaliland kabla ya mwisho wa mwezi Machi.

    Hatua hiyo inaonekana kuikera Somalia, ambayo imetangaza kukatiza uhusiano wake wa kidiplomasia na Kenya.

    Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka 1991, lakini juhudi zake za kutaka kutambuliwa kimataifa kama taifa huru hazifanikiwa huku Somalia ikisisitiza kuwa bado ni sehemu ya eneo lake.

    Somalia imewaita nyumbani wanadiplomasia wake kutoka Kenya na kuwapatia muda wa siku saba wanadiplomasia wa Kenya kuondoka nchini humo.

    Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna amesema kamati ilikuwa imebuniwa kutatua mzozo kati ya nchi hizo, kwani zina uhusiano wa muda mrefu ambao unastahili kulindwa.

  8. 'Zaidi ya watoto milioni 2' wakosa msaada Tigray

    Umoja wa Mataifa umesema kuwa zaidi ya watoto milioni mbili katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia wamekatiziwa misaada ya kibinadamu huku ghasia zikiendelea.

    Licha ya makubaliano ya yaliyofikiwa na serikali ya Ethiopia, mashirika ya kutoa misaada yanalalamikia kuzuiliwa kuingia Tigray ambako vikosi vya serikali vimekuwa vikikabiliana na wapiganaji wa Tigray Liberation Front kuanzia mapema mwezi Novemba.

    Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa, Unicef, linahofia kadri linavyochelewa kuwafikia watoto wanaohitaji msaada wa dharura hivyo kusababisha hali yao kuzorota.

    Mapema mwezi huu wanajeshi waliwamiminia risasi wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Tigray.

    Serikali imesema wafanyakazi wa UN hawakuwa na idhini ya kusafiri katika eneo hilo na kuwalaumu kwa kupuuza vizuizi vya barabarani.

  9. Uganda yataka YouTube kufunga vituo vinavyohusishwa na Bobi Wine

    Mamlaka ya mawasiliano nchini Uganda imeandikia Google, jukwaa la kushirikisha video, kuomba ifunge vituo 14 vya YouTube vinavyodaiwa kuhusishwa na ghasia za mwezi uliopita ambazo zilisababisha zaidi ya watu 50 kufariki.

    Ghasia zilizuka katika mji mkuu wa Kampala na miji mingine mikuu kufuatia kukamatwa kwa mgombea wa urais wa upinzani ambaye ni mwanamuziki Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kwa kukiuka masharti ya kudhibiti ugonjwa corona.

    Baadhi ya vituo vya YouTube vinavyohusishwa na Bobi Wine ndivyo vinalengwa, lakini mkuu wa masuala ya sheria wa Tume ya Mawasiliano ya Uganda ameambia kituo cha televisheni cha Bloomberg kwamba ni "bahati mbaya" tu.

    Katika barua yake kwa Google,Tume hiyo ilisema vituo hivyo vilitumiwa kuchochea vurugu na vinatangaza maudhui yanayokiuka sheria, Gazeti la Daily Monitor linaripoti.

    Raia wa Uganda wanajianda kushiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge Januari 14. Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa zaidi ya miongo mitatu, inawania kuchaguliwa tena.

  10. Karibu katika matangazo mubashara Jumatano 16.12.2020