Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

China yaipongeza Tanzania kwa mapambano dhidi ya virusi vya Corona

Rais wa China Xi-Jiping amempongeza rais John Magufuli wa Tanzania kwa namna Tanzania inavyokabiliana na ugonjwa wa corona.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi and Dinah Gahamanyi

  1. Mpaka hapo tumefikia mwisho wa matangazo ya moja kwa moja ya BBC swahili, Shukrani na tukutane tena kesho.

  2. China yaipongeza Tanzania kwa mapambano dhidi ya virusi vya Corona

    Rais wa China Xi-Jiping amempongeza rais John Magufuli wa Tanzania kwa namna Tanzania inavyokabiliana na ugonjwa wa corona.

    Rais Xi-Jiping ameeleza hayo katika mazungumzo yake ya simu na rais Magufuli yaliyochukua saa moja.

    Xi-Jiping alimuelezea pia jinsi China inavyoendelea kukabiliana na janga hilo la corona.

    Takwimu rasmi za mwisho za Tanzania zilitangazwa 29 Aprili na Waziri Mkuu ambapo wagonjwa walikuwa 480, na waliokuwa wamefariki kutokana na ugonjwa huo walikuwa 21.

    Zanzibar baadaye ilitangaza ongezeko la wagonjwa mara moja, mnamo tarehe 7 mwezi Mei walipotangaza wagonjwa 29 wapya.

  3. Uchaguzi Uganda 2021:Bobi Wine kuitikia wito wa Tume ya Uchaguzi

    Mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha NUP nchini Uganda, Robert Kyagulanyi hatimaye amefika kwenye tume ya uchaguzi kama alivyoitwa na mwenyekiti wa tume Jaji Simon Byabakama.

    Kyagulanyi aliyevalia suti nyeupe aliongozana na viongozi wengine wa chama na wanasheria wake walipokelewa na mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi na kufanya mkutano wa faragha bila kuwaruhusu wandishi habari ndani

    Baada ya mkutano huo Bobi Wine alifahamisha mkutano wa wandishi habari kwamba Tume ya uchaguzi inamutuhumu kwa kuhatarisha maisha ya wananchi kwa kusambaza virusi vya corona kutokana na mikusanyiko mikubwa ya watu katika kampeni zake.

    Kyagulanyi na yeye ametowa malalamiko yake kukatazwa na vyombo vya habari baadhi ya sehemu kufanya mikutano na hata kumuzia kupata Hoteli ya kulala baadhi ya sehemu baada ya kampeni zake.

    Leo Bobi Wine hakufanya mikutano ya kampeni kufatana na kuchelewa katika mkutano huo lakini anatarajiwa kuendelea na kampeni zake magharibi mwa Uganda hapo kesho.

  4. DRC kujenga jengo maalum kumuenzi Patrice Lumumba

    Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itajenga jengo maalum la kumbukumbu kwa ajili ya shujaa wa uhuru Patrice Lumumba, rais Félix Tshisekedi alisema Jumatatu.

    Rais Tshisekedi alisema pia kuwa Ubelgiji itarudisha mabaki ya waziri mkuu huyo wa zamani ,ingawa hakutoa maelezo zaidi kufafanua suala hilo.

    Jengo hilo maalum litajengwa kabla taifa hilo halijaadhimisha kumbukumbu ya miaka 61 ya uhuru mnamo Juni mwaka 2021.

    "Wakati wa maadhimisho ya miaka 61 ya uhuru wetu, taifa litaonesha shukrani zake za dhati kwa Patrice Emery Lumumba, ambaye ni miongoni mwa mashujaa wa kukumbukwa katika taifa hili kutokana na kujitoa kwake," rais Tshisekedi alisema.

    Patrice Lumbumba aliuawa mnamo Januari 1961. Mwili wake haukupatikana na jino lake moja liliaminika kuwa lilihifadhiwa Brussels na mtu aliyehusika katika mauaji yake.

    Mahakama nchini Ubelgiji , mwezi Septemba ilisema Binti yake Lumumba anapaswa kupewa jino hilo.

  5. Uchaguzi Uganda 2021:Museveni auliza 'hata nikiondoka nani ataweza kuliongoza taifa hili'

    Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema kuwa bado hajaona mtu mwenye uwezo wa kuiongoza Uganda kwa sasa, hivyo ataendelea kuwa madarakani.

    Museveni mwenye umri wa miaka 76, ameliongoza taifa la Uganda kwa zaidi ya miongo mitatu.

    Akizungumza na viongozi wa chama chake cha National Resistance Movement (NRM) hapo jana, amesema kwamba wapinzani wake hawana vigezo vya kuliongoza taifa la Uganda.

    "Ninakasirika sana ninaposikia watu wakiniambia niondoke madarakani,”Museveni alinukuliwa na vyombo vya habari nchini humo.

    Na kuongeza;“ Wapiga kura ndio wanaoamua, hata nikiondoka nani ataweza kuliongoza taifa hili, nitaondoka tu iwapo kuna mtu wa maana nitakayeona naweza kumuachia Uganda".

    Rais Museveni amekaa madarakani tangu mwaka 1986, aliingia madarakani kwa njia ya mapigano ya msituni.

    Katika uchaguzi mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika Januari 14 mwakani una wagombea 11 wa nafasi ya Urais, 10 kati yao wakitaka kuchukua nafasi ya Yoweri Museveni wa chama tawala cha NRM anayetaka kutetea nafasi yake kwa muhula wa sita.

  6. Muigizaji mkongwe Tanzania maarufu kama 'Jengua' afariki dunia

    Msanii mkongwe wa filamu nchini Tanzania Mohammed Fungafunga maarufu kama Mzee Jengua, amefariki dunia asubuhi ya leo huko Mkuranga mkoani Pwani.

    Taarifa katika vyombo vya habari nchini humo vinasema, Mzee Jengua alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi.

    Enzi za uhai wake marehemu ameigiza kwenye filamu ya Babu hatari, Handsome wa kijiji, Kidedea, Fitina na nyingine.

    Wadau wa filamu, wamuomboleza mzee Jengua kwenye mitandao ya kijamii.

  7. Waziri wa Malawi aamuru Nabii Bushiri na mkewe warudishwe Afrika Kusini

    Waziri wa usalama nchini Malawi , Richard Banda, amesaini nyaraka kwa ajili ya mchungaji tajiri na maarufu Shepherd na mke wake, Mary kurejeshwa Afrika Kusini, vimeripoti vyanzo vya habari vya Malawi.

  8. Wasanii wa Nigeria Omah Lay na Tems waendelea kuzuiliwa Uganda

    Ubalozi Nigeria nchini Uganda unajitahidi kuwasaidia wasanii Omah lay na Tems waliyokamatwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki siku ya Jumapili.

    Lakini mamlaka nchini Uganda zinasisitiza sheria lazima ifuatwe, Abike Dabiri, Mwenyekiti wa raia wa Nigeria wanaoishi nje ya nchi (NIDCOM )amesema.

    Waziri wa Mambo ya nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama pia amesema anafuatila suala hilo kwa usirikiano na NIDCOM na mawakili wao, aliongeza kusema.

    Vyombo vya habari vinasema polisi nchini Uganda waliwakamata Omah lay na Tems kwa kukiuka masharti yaliyowekwa na mamlaka nchini humo kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.

    Stanley Omah Didia maarufu Omah Lay, Temilade Openyi maarufu kama Tems na Muyiwa Awoniyi walifikishwa mahakamani siku ya Jumatatu Disemba 14 na kushtakiwa kwa kosa la "vitendo vya kueneza magonjw aya kuambukiza".

    Raia wanne wa Uganda pia walishtakiwa pamoja na wasanii hao wa Nigeria, polisi wamethibitisha.

  9. Boko Haram 'yadai kuwateka wanafunzi wa Nigeria'

    Kundi la kigaidi la Boko Haram limesema lilihusika na utekaji nyara mamia ya wavulana wa shule katika jimbo la kaskazini –magharibi la Katsina State, likigusia jinsi lilivyoendelea kutekeleza mashambulio hatari katika wiki za hivi karibuni, Tovuti ya kibinafsi ya Daily Nigerian limeripoti.

    Mamia ya wavulana wa shule ya upili ya serikali, Kankara katika jimbo la Katsina hawajulikani kufuatia shambulio hilo la Ijuma usiku wiki iliyopita.

    Kwa mujibu wa Daily Nigerian, kiongozi wa Boko Haram, Abubakar Shekau, alisema hayo katika ujumbe wa dakika nne uliyorekodiwa na kundi lililotekeleza shambulio hilo "kwa sababu elimu ya magharibu inaenda kinyume na mafundisho ya Kiislamu".

    "Kilichofanyika Katsina hi hatua ya kunadi Uslamuna kupingaelimu inayoenda kinyume na mafundisho Kiislamu kwani elimu ya magharibi hairuhusiwi na Allah na Mtume wake mtakatifu," tovuti hiyo ilimnukuu Shekau akisema.

    Tovuto hiyo aidha ilisema Shekau hakutoa maelezo kuhusu shambulio hilo, idadi ya wanafunzi waliotekwa au kuthibitisha ripoti kuhusu majadiliano na serikali.

  10. Kenya 'yaagiza dozi milioni 24 ya corona'

    Kenya imeagiza dozi milioni 24 ya chanjo ya Covid-19, Gazeti la The Star limeripoti, likiwanukuu maafisa wa wizara ya afya.

    Serikali ya Kenya itatumia shilingi bilioni 10 sawa na($89m; £66m) kununua chanjo hiyo, gazeti hilo linaripoti.

    Wizara iliwasilisha ombi lake kwa Mpango wa Ushirikiano wa Chanjo Duniani (Gavi) wiki iliyopita, kwa mujibu wa ripoti.

    Hii itawafikia asilimia ya 20 ya idadi ya watu nchini humo.

    Benki ya Dunia inakadiria kuwa Kenya wa sasa ina zaidi ya watu milioni 52.

    Haijabainika ni chanjo ipi iliyoagizwa na nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

    Kati kati ya mwaka huu Gavi ilisema kila dozi ya Covid-19 itagharimu $3.

    Waliorodheshwa kupewa chanjo ni wahudumu wa afya, wazee na wale waliyo na changamoto zingine za kiafya

    Gavi imetia saini mkataba na makampuni karibu tisa ya utengenezaji chanjo.

    Maelezo Zaidi:

  11. Kenya yaunda kamati ya maridhiano na Somalia baada ya uhusiano wao kudorora

    Serikali ya Kenya imeunda kamati maalum yakutatua mzozo baina yake na Somalia baada ya mahusiano ya nchi hizo mbili kudorora .

    Hatua hii ya Kenya imekuwa baada ya serikali ya Somalia kutangaza leo kuwa imesitisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya.

    Nchi hiyo imewaita nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Nairobi na kuwapatia wanadiplomasia wa Kenya muda wa siku saba kuondoka nchini humo.

    Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Habari Osman Abukar Dubbe katika chombo cha habari cha kitaifa.

    "Serikali ya Somali, kulingana uhuru wake iliyohakikishiwa na sheria ya kimataifa, inatekeleza wajibu kwa mujibu wa katiba ili kulinda utaifa, umoja na ustawi wa nchi imeamua kukatiza uhusiano wake wa kidiplomasia na serikali ya Kenya," alisema.

    Hatua hiyo inakuja baada ya Somalia kuwasilisha barua ya malalamiko dhidi ya Kenya kwa Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Viongozi wa nchi wanachama wa muungano wa maendeleo Afrika Mashariki na pembe ya Afrika (IGAD).

    Hivi karibuni Somalia iliituhumu Kenya kwa kuingilia masuala yao ndani.

  12. Karibu katika matangazo haya mubashara leo Jumanne 15.12.2020