Rais Tshisekedi atangaza kuunda serikali mpya

DRC Felix Tshikedi ametangaza tena nia yake ya kuunda serkali mpya, baada ya kuona serikali ya pamoja aliyoiunda na rais mstaafu Joseph Kabila kushindwa kufanya kazi.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi and Dinah Gahamanyi

  1. Mpaka hapa tumefikia mwisho wa matangazo yetu mubashara, shukrani.

  2. Rais Tshisekedi atangaza kuunda serikali mpya

    nn

    Katika hotuba yake mbele ya wanaseta na wanabunge, rais wa DRC Felix Tshikedi ametangaza tena nia yake ya kuunda serkali mpya, baada ya kuona serikali ya pamoja aliyoiunda na rais mstaafu Joseph Kabila kushindwa kufanya kazi.

    Tshekedi aliamua kuvunja ushirikiano na timu ya rais mstaafu, na sasa anasubiri kuteua mtu ambaye ataweza kujadili na vyama mbalimbali vya kisiasa ili aunde serikali hiyo ambayo ana matumaini ya kwamba mafanikio yake yatatumikia kwa faida ya raia wa DRC.

    Disemba mwaka 2019 ndani ya bunge hili lilitangaza ya kwamba mwaka 2020 utakuwa mwaka wa kazi , juhudi zote zilipaswa kufanyika ili kutimiza maendeleo ya nchi.

    "Mbele ya raia nilihaidi kufanya mabadiriko nikakubali kutumikia na mtagulizi wangu kupitia muungano ili pamoja tuinue nchi sisi wote kama raia wa nchi hii nzuri , lakini ukweli ni kwamba, lichaya juhudi zangu, nilijitolea, nilikubali hadi kufedheheshwa lakini haikuwezesha muungano huu kuendelea,"rais Tshekedi ameeleza.

    Aliongeza kusema; "Kulingana na hali hio ambayo ilikuwa inazuia uongozi wangu ilibidi tu nijibu".

    Rais wa nchi hiyo amehaidi kuunda shule ya vita kwa ajili ya maafisa wa jeshi la taifa , huku rais akijaribu kuungwa mkono na jeshi la taifa ambalo kwa sasa linasusiwa kushindwa vita dhidi ya waasi huko mashariki mwa Kongo, Rais amehaidi pia kurejesha mwaka ujao mabaki ya Patrice Lumumba Papa wa uhuru wa taifa ambaye mabaki ya mwili yake yako Ubegiji.

  3. Rais Magufuli atuma salamu za rambirambi baada ya ajali kuuwa watu 14

    L

    Chanzo cha picha, IKULU

    Rais John Magufuli ametuma salamu za pole kwa familia za watu 14 waliofariki & watu watatu wamejeruhiwa katika ajali iliyotolea usiku wa kuamkia leo ikihusisha gari dogo aina ya Hiace na lori la mizigo.

    Ajali hiyo ilitoa katika eneo la Mkiwa wilayani Manyoni, katika barabara kuu ya kutoka Singida kuelekea Dodoma.

    "Nawapa pole wafiwa wote , Mwenyezi Mungu awatie nguvu ,uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu, nawaombea marehemu wapumzike mahali pema peponi na majeruhiwote wapate kupona haraka,"alisema Magufuli

    Aidha ametoa rai kwa kwa vyombo vya usalama barabarani kuongeza jitihada za kuthibiti ajali haswa katika kipindi hiki cha kufunga mwaka ambako kumekuwa kukitokea ajali nyingi za barabarani na watumiaji wote kuwa makini na kujiepusha kuvunja sheria na taratibu za barabarani.

  4. Rais Algeria aongea kwenye TV baada ya kupata Covid

    Raia wa Algeria wengi wameonekana katika mitandao ya kijamii, wakimpokea rais wao Abdelamdjid Tebboune ,baada ya kuonekana kwenye video kwa mara ya kwanza baada ya kuugua corona na kutibiwa huko Ujerumani.

    Rais Tebboune anaonekana kutotengamaa kiafya bado ingawa amehaidi kurejea nchini baada ya wiki kadhaa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Bwana Tebboune alionekana kwa umma tangu oktoba 15 akiwa na waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Jean-Yves le Drian.

  5. Baadhi ya maeneo ya dunia kushuhudia kupatwa kwa jua.

    Tukio la kupatwa kwa jua, huufanya mchana kuwa usiku kwa dakika chake

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Tukio la kupatwa kwa jua, huufanya mchana kuwa usiku kwa dakika chake

    Leo Jumatatu Disemba 14, baadhi ya maeneo ya dunia yanatarajia kushuhudia tukio la kupatwa kwa jua.

    Maeneo kadhaa ya Amerika Kusini yatashuhudia sehemu ndogo tu ya kupatwa kwa jua , maeneo mengine ya dunia, lakini tukio hilo kamili litashuhudiwa katika nchi za Chile na Argentina.

    Kwa dakika 24, mwezi mpya utapita kwenye uso wa jua na kulifunika kabisa kwa zaidi ya dakika mbili, anasema mtaalamu wa masuala ya anga Tania de Sales Marques, kutoka taasisi ya Royal Greenwich Observatory mjini London, Uingereza.

    Tukio hili la mwezi hufanya mchana kuwa usiku kwa dakika chache.

    Wale watakaobahatika kuona tukio hili watatakiwa kuchukua tahadhari, kwa mfano kutumia vifaa kama vile miwani maalumu ili kuepuka kuharibika kwa macho yao.

    Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu kupatwa kwa jua:

    • Jua lapatwa Afrika
    • Kupatwa kwa jua Marekani
  6. Ureno kuisaidia Msumbiji kukabiliana na wanamgambo

    Hundreds of thousands have been displaced by the insurgency

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maelfu ya watu wametoroka makwao

    Ureno imejitolea kuisaidia Msumbiji kupanga mkakati na kuiwezesha jeshi la nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wanaotishia usalama katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado wenye utajiri wa gesi.

    Mwezi uliyopita wanamgambo waligeuza uwanja wa michezo kuwa "kichinjio", ambako walikata watu vichwa na miili, kwa mujibu wa ripoti.

    Waziri wa Ulinzi wa Ureno, Joao Gomes Cravinho, amesema kundi la wanajeshi wa nchi hiyo kuanzia mwezi ujao litaanza kufanya kazi na wenzao wa Msumbiji.

    Wikendi iliyopita Bw Gomes Cravinho alikamilisha ziara ya kikazi ya siku tatu katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

    Alisema, Ureno ambayo itakuwa rais wa Muungano wa Ulaya kuanzia mwaka 2021, itaunga mkono ombi la Msumbiji la kupewa msaada ambalo tayari limewasilishwa Brussels.

    Ghasia katika mkoa wa Cabo Delgado umesababisha mzozo wa kibinadamu, huku zaidi ya watu 2,000 kuuawa na wengine 560,000 kufurushwa makwao.

    Maelezo zaidi:

  7. Marekani yaiondoa Sudan katika orodha ya wafadhili wa ugaidi

    Shambulio la kigaidi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Marekani imeiondoa rasmi Sudana katika orodha ya wafadhili waugaidi, kwa mujibu wa ubalozi wake mjini Khartoum.

    "Muda wa ilani ya siku 45 iliyowasilishwa kwa bunge la Congress umepita na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ametia saini ya kuiondoa Sudan katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi kuanzia leo (Desemba 14), ambayo itachapishwa katika sajili ya serikali," Ubalozi wa Marekani umeandika katika mtandao wa kijamii wa Facebook.

    Rais wa Marekani Donald Trump mnamo mwezi Oktoba alisema kwamba Sudan itaondolewa katika orodha hiyo baada ya kulipa fidia ya $335m kwa waathiriwa na familia ya shambulio la bomu la al-Qaeda mwaka 1998 dhidi ya ubalozi wa Marekani Afrika.

    Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok alijibu kwa kusema fedha hizo zimetumwa.

    Sudan iliorodheshwa mwaka1993 wakati kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden alipoishi nchini humo kama mgeni wa serikali. Nchini zingine zilizojumuishwa katika orodha ya kufadhili ugaidi ni Iran, Korea Kaskazini na Syria.

  8. Mamia ya wanafunzi watoweka baada ya shule kushambuliwa Nigeria

    Wazazi wakisubiri taarifa kuhusu watoto wao

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wazazi wamekusanyika katika shule hiyo kujulia hali ya watoto wao

    Mamia ya wavulana hawajulikani waliko baada ya watu waliyojihami kwa silaha kuwateka kutoka shule moja ya bweni kaskazini mwa Nigeria usiku wa Ijumaa.

    Wazazi waliojawa na wasiwasi wamekusanyika katika shule hiyo kusubira taarifa kuhusu watoto wao huku vikosi vya usalama vikiendelea kuwatafuta katika msitu ulioko viungani mwa mji wa Kankara

    Karibu wanafunzi 800 wanasomea shule hiyo ya bweni ya wavulana pekee.

    Makundi yaliyojihami mara kwa mara yanawateka watu na kisha kudai kikombozi katika eneo la kaskazini -magharibi mwa Nigeria. Kufikia sasa watu hao hawajatoa masharti yoyote.

    Awali msemaji wa Rais wa Nigeria, Garba Shehu, amesema anaamini ni watoto 10 waliotekwa na kwamba wengi ni wale ambao wametoroka.

    Ramani ya eneo la tukio
  9. Mashindano ya CECAFA yang'oa nanga Kigali huku kukiwa na changamoto ya corona

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili
    CECAFA

    Mashindano ya CECAFA kwa vijana walio chini ya Umri wa miaka 17 yameanza kutimua vumbi nchini Rwanda ,zikishiriki timu kutoka mataifa 6 ya ukanda wa Afrika mashariki.

    Kenya na Ethiopia zilitoka sare katika mechi ya kwanza na leo Rwanda inacheza dhidi ya Tanzania.

    CECAFA

    Kulingana na shirikisho la soka Afrika Mashariki na kati CECAFA, mashindano haya yalikumbwa na changamoto kubwa ya Covid19 kiasi kwamba ilibidi mechi ya ufunguzi Jumamosi kuahirishwa na mechi ya jana kati ya Kenya na Ethiopia kuchelewa kwa zaidi ya saa nzima kwa kusubiri matokeo ya vipimo vilivyofanyiwa wachezaji, katibu mkuu wa CECEFA, Auka Gecheo anasema :

    ‘’Sheria za CAF zinasema kwamba lazima timu zifanyiwe vipimo saa 48 kabla ya mechi, hii ndiyo maana hata mechi ya Rwanda na Tanzania Jumamosi iliahirishwa na hatungekuwa na mechi mbili kwa kuwa muda wa vipimo vyao ulikuwa umemalizika, ni sheria iliyopo ya kulinda watu. Matokeo ya vipimo kwa mchezo huu wa Kenya na Ethiopia pia yalichelewa kwa sababu lazima kwanza ziwekwe katika mfumo uliopo, hatungetaka pia kukiuka sheria za nchi’’.

    CECAFA

    Ni shindano ambalo mashabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani ili kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

    Pamoja na hayo CECEFA iliamuru mashindano hayo kuchezwa katika mji mmoja, mjini Rubavu badala ya kuchezwa pia katika mji wa Huye kusini mwa Rwanda kwa hofu ya maambukizi.

    Kuhusu matokeo ya mechi ya ufunguzi jana Kenya na Ethiopia zilitoka sare ya kufungana mabao 2 kwa 2 kundi lao likishirikisha pia Uganda na leo Rwanda inakipiga dhidi ya Tanzania katika kundi B linaloshirikisha pia timu ya Djibuti.

    Timu ya Sudan Kusini iliondolewa baada ya vipimo (MRI Test) kubainisha kuwa wachezaji wake 4 wanazidisha umri wa miaka 17.

    Fainali inatarajiwa kupigwa tarehe 22 mwezi huu wa 12.

  10. Tundu Lissu atoa tuzo aliyopewa kwa chama na wafuasi ‘waliotoweka’

    Tundu Lissu

    Makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema nchini Tanzania, Tundu Lissu ametoa tuzo ya uhuru aliyopewa na taasisi ya 'Bush Thatcher' kwa ajili yake binafsi, lakini yeye ameamua kuitoa kwa chama chake na wafuasi wa chama hicho wasiojulikana walipo kwa miaka kadhaa ambao ni bwana Alphonce Mawazo na Ben Saanane.

    Akizungumza katika hafla ya kupokea tuzo hiyo Lissu, alisema kuwa tuzo hiyo inaonesha utambuzi wa kimataifa wa kujitolea kwake binafsi na kwa watu wengine kwa ujumla nchini Tanzania kupambana kwa ajili ya demokrasia na kulinda uhuru wa watu wa kimsingi.

    “Hizi ni hatua muhimu kuelekea mapambano kwa ajilii ya demokrasia, utawala wa kisheria na haki za binadamu nchini’’, alisema Ijumaa kupitia mtandao katika hotuba yake fupi baada ya kupokea tuzo hiyo.

    Bw Lissu yuko nchini Ubelgiji ambako anaishi baada ya kuondoka nchini Tanzania kwa kile alichosema kuwa anahofia maisha yake.

  11. Waziri Mkuu wa Eswatini afariki baada ya kupatika na corona

    Waziri Mkuu Ambrose Dlamini

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waziri Mkuu Ambrose Dlamini alipatikana na virusi vya corona mwezi Novemba

    Serikali ya Eswatini imesema kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ambrose Dlamini amefariki dunia, wiki nne baada ya kupatikanava virusi vya corona.

    Taifa ya serikali imesema kuwa Bw Dlamini, mwenye umri wa miaka 52, alifariki dunia Jumapili mchana hospitalini nchini Afrika Kusini.

    Hakuna sababu ya kifo iliyotajwa, lakini hivi karibuni Dlamini alitibiwa maradhi ya Covid-19 nchini Afrika Kusini.

    Dlamini amekuwa waziri Mkuu wa Eswatini, zamani ikiitwa Swaziland, tangu mwezi wa Oktoba 2018.

    Nchi hiyo ndogo iliyopo kusini mwa Afrika ni moja ya nchi chache ambazo bado zinatawaliwa kifalme duniani.

    Ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni moja tayari imerekodi visa 6,768 vya virusi vya corona na vifo127 vilivyohusishwa na corona, kwa mujibu wa Wizara ya afya.

    Dlamini alitangaza kuwa amepatwa na virusi vya corona tarehe 16 Novemba. Wakati huo alisema kuwa hakuwa na dalili na alikuwa anajihisi vizuri.

    Wiki chache baadaye , tarehe 1 Disemba, serikali ya Eswatini ilisema kuwa Dlamini amehamishiwa katika hospitali ya Afrika Kusini kwa matibabu , kwa lengo la kuharakisha kupona kwake.

    Lakini Jumapili serikali ilisema kuwa Dlamini amefariki "wakati alipokuwa akipokea matibabu katika hospitali ya Afrika Kusini ", bila taarifa zaidi .

    "Serikali kwa ushirikiano na familia itaendelea kulifahamisha taifa kuhusu mipango kadri inavyoendelea," Naibu Waziri Mkuu Themba Masuku alisema katika taarifa.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  12. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatatu tarehe 14.12.2020