Waziri Mkuu wa Msumbiji akataa kuwapa silaha raia kupambana na wanamgambo

Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos do Agostinho, amepinga wito wa kuwapa raia silaha katika jimbo la Cabo Delgado ili kupambana na wanamgambo wa Kiislamu.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi and Dinah Gahamanyi

  1. Padri maarufu wa Nigeria awatukana wanahabari wa BBC

    Padre Ejike Mbaka

    Chanzo cha picha, Adoration Ministry

    Padri maarufu wa kanisa katoliki nchini Nigeria Ejike Mbaka na baadhi ya waumini wa kanisa lake wamewatukana wafanyakazi wa BBC na watu wengine waili katika jimbo la kusini mashariki la EnuguJumatano jioni.

    Waandishi wa BBC Chioma Obianinwa na Nnamdi Agbanelo, pamoja na dereva wao, Ndubuisi Nwafor, walikuwa wameandamana padre mwingine wa kanisa katolik, Father Cajethan Obiekezie na naibu wake Solomon Orakam, kwenda kwa kanisa la padri Mbaka jumatano asubuhi.

    Padri Obiekezie alikuwa amepanga mahojiano na padri Mbaka, lakini haikuweza kufanyika kwasababu alikuwa akiongoza misa.

  2. Mkusanyiko wa taarifa za corona duniani

      • Author, Caro Robi
      • Nafasi, BBC Swahili
    Waziri wa Afya Zweli Mkhize anaongoza ita dhidi ya  Covid-19 Afrika Kusini

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waziri wa Afya Zweli Mkhize anaongoza ita dhidi ya Covid-19 Afrika Kusini

    Afrika Kusini imetangaza rasmi kukumbwa na wimbi la pili la maambukizi baada ya hapo jana kurekodi visa 7,000 vya maambukizi mapya. Vijana ndiyo wanalaumiwa kwa kuchochea wimbi hilo la pili katika taifa ambalo ndilo lililoathiorika zaidi na Covid 19 barani Afrika.

    Waziri wa afya nchini humo Zweli Mkhize amesema zaidi ya maambukizi mapya yanaathiri wale wenye umri kati ya miaka 15 na 19 na inahofiwa kuwa katika baadhi ya maeneo Afrika Kusini, maambukizi ni makubwa hata kuliko yaliyoshuhudiwa katika wimbi la kwanza la mwezi Julai.

    Zaidi ya watu elfu 22 wamefariki dunia Afrika Kusini kutokana na Corona. Nchi nyingine za Afrika kama Zimbabwe na Kenya pia zinaripoti maambukizi mapya.

    Hata hivyo mpaka sasa, bara Afrika kwa jumla limenusurika kutumbukia katika hali mbaya ya mamabukizi na vifo kama inayoshuhudiwa Marekani na barani Ulaya. Shirika la afya duniani WHO hata hivyo linaonya kuwa katika kipindi cha siku saba zilizopita, Afrika imerekodi ongezeko la zaidi ya asilimia saba ya maambukizi.

    Visa vipya 100,000 vimerokodiwa na watu 100 wamefariki dunia wiki moja iliyopita. Nchi zinazojumiusha asilimia sabini ya maambukizi Afrika ni Afrika Kusini, Morocco, Misri, Tunisia na Ethiopia. Morocco imepokea dozi milioni mbili ya chanjo ambayo wahudumu wa afya na walio na matatizo ya kiafya watapewa kipaumbele. Chanjo hiyo itapeanwa bila malipo.

    Mhudumu wa afya Marekani

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kimataifa, Marekani imerekodi zaidi ya vifo elfu tatu katika kipindi cha siku moja pekee, hiyo ikiwa ni idadi ya juu zaidi ya vifo kwa siku vitokanavyo na Covid 19 kuwahi kurekodiwa kokote ulimwenguni. Nayo Afrika Kusini inaripoti wimbi jipya la maambukizi, vijana wakilaumiwa kwa kusababisha wimbi hilo.

    Marekani inasalia kuwa nchi iliyoathirika zaidi na maradhi ya Covid 19 ulimwenguni, huku mamilioni wakiwa wameambukizwa na takriban watu laki tatu wakiwa wamefariki dunia nchini humo kutokana na virusi hivyo vya Corona ambavyo vimeutikisa ulimwengu kwa karibu mwaka mmoja sasa tangu vilipozuka nchini China mwezi Desemba mwaka jana.

    Tukitupia macho muenendo wa Corona katika mataifa ya Ulaya, siku moja baada ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel kuwatolea wito Wajerumani kukubali hatua kali zaidi za sitisho la shughuli ili kudhibiti kuenea kwa maambukizi, visa elfu 23 mia sita sabini na tisa vipya vimerekodiwa katika taifa hilo imara zaidi kiuchumi barani Ulaya.

    Waziri mkuu wa jimbo la Bavaria Markus Soder amesema sitisho kamili linapaswa kutekelezwa kuanzia Krisimasi hadi tarehe 10 Januari.

    Nchi jirani na Ujerumani, Waziri mkuu wa Ufaransa Jean Castex anatarajiwa kutangaza kulegezwa kwa masharti yaliyowekwa na serikali mwezi uliopita kudhibiti maambukizi, serikali ya Ufaransa ilikuwa imetarajia maambukizi yatapungua hadi chini ya elfu tano kwa siku lakini hapo jana, maambukizi mapya elfu kumi na nne yaliripotiwa nchini humo, kwa hiyo kumbi za burudani zitasalia kufungwa kwa muda kiasi.

  3. ‘Zaidi ya tai 2,000 waliuawa kwa ajili ya ibada’

    Jogoo

    Chanzo cha picha, AFP

    Utafiti nchini Guinea-Bissau umebaini kuwa vifo vya tai zaidi ya 2,000 walichinjwa kwa ajili ya kutumiwa katika ibada za kishirikina.

    Mkuu wa utafiti huo Mohammed Henriques, ameliambia shirika la Habari la Ufaransa RFI kwamba miguu na tumbo la tai hutumiwa kwa ibada na matambiko ya imani za kishirikina Afrika Magharibi.

    Alisema kuwa wengi kati ya tai hao ambao miili yao ilipatikana tangu mwezi wa Februari walipatikana vichwa vyao vikiwa vimekatwa.

    "Baadhi wanaamini kuwa vichwa vya tai hao vinaleta ," Henriques alinukuliwa na RFI akisema.

    Imefichuliwa kuwa wengi wa tai hupewa sumu ya methiocarb, ambayo imepigwa marufuku barani Ulaya kabla ya vichwa vyao kukatwa.

  4. Kenya yaamuriwa kuwalipa fidia waathiriwa unyanyasaji wa kingono

    At least 1,000 people were killed in the violence

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Karibu watu 1,000 waliuawa katika ghasia hizo

    Mahakama Kuu nchini Kenya ameamuru serikali kuwalipa fidia ya karibu $30,000 watu wanne kwa kushindwa kuwapatia ulinzi dhidi ya unyanyasaji wa kingono na kijinsia wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi zilizokumba nchi hiyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2007-2008.

    Uamuzi huo unaonekana kuwamkubwa, huku Naitore Nyamu-Mathenge – mkuu wa madaktari wa kundi la kutetea haki za binadamu akiunga mkono hatua hiyo ya mahakama-akisema hatiamye haki imetekelezwa.

    Hata hivyo ametoa wito kwa serikali kuongeza juhudi za kuzuia vitendo kama hivyo kutokea tena siku zijazo.

    Akitua hukumu hiyo Jaji Weldon Korir alisema manusura hao wana haki ya kuishi maisha na kwamba walinyanyaswa wakati waliposhambuliwa.

    Pia aliongeza kuwa serikali ilishindwa kuwalinda dhidi ya mateso, unyama na udhalilishaji waliyofanyiwa.

    Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch linakadiria kuwa watu 1,000 waliuawa na wengine zaidi ya 500,000 kufurushwa makwao.

    Pia kulikuwa na ripoti kadhaa za ubakaji na mateso.

    Ghasia zilizuka baada ya Mwai Kibaki- rais wa wakati huo kutangazwa mshindi wa uchaguzi. Mpinzani wake Raila Odinga alisema kura zimeibwa.

    Rais wa sasa Uhuru Kenyatta – ambaye alimuunga mkono Bwana Kibaki – na naibu wake William Ruto – ambaye alimuunga mkono Bwana. Odinga – walishtakiwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai, ICC kwa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu baada ya kutuhumiwa kwa kuchochea ghasia.

  5. Ethiopia inaanza upimaji wa bure wa Covid-19

    Serikali ya Ethiopia imetangaza upimaji wa bure wa Covid-19 katika vituo 34 mjini, Addis Ababa.

    Taasisi ya afya ya umma ya nchi hiyokwa ushirikiano na Wizara ya Afya imechapisha orodha ya vituo ambayo inajumuisha hospitali za kibinasi na za umma.

    Haijabainika ikiwa huduma hiyo itapelekwa katika maeneo mengine nje ya mji mkuu.

    Vituo vya afya vimekuwa vikitoza ada ya Birr 1,250 sawa na ($32) kufanya vipimo vya Covid-19.Kuna maeneo ambayo yanatoza hadi Birr 1,500 za Ethiopia.

    Awali waliokuwa wakifanyiwa vipimo vya bure ni wale ambao walitambuliwa wakati wa kuwatafuta watu waliotangamana na wale walioambukizwa.

    Tangazo hilo linakuja wakati ambao kumekuwa na ongezeka la watu ambao hawazingatii uvaaji wa barakao katika maeneo ya umma.

    Kwa mujibu wa kituo ya kudhibiti na kuzuia magonjwa Afrika(CDC), na Taasisi ya kiufundi ya muungano wa Afrika, Ethiopia ni miongoni mwa nchi za Afrika zilizo na idadi ya juu y amaambukizi na Covid-19.

    Kufikia sasa nchi hiyo imethibitisha kuwapima watu karibu milioni 1.7. Watu 114,834 wamethibitishwa kuwa na virusi vya corona na wengine 1,769 kufariki kutokana na virusi hivyo, kwa mujibu wa wizara ya afya.

  6. Waziri Mkuu wa Msumbiji akataa kuwapa silaha raia kupambana na wanamgambo

    ms

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri Mkuu wa Msumbiji, Carlos do Agostinho, amepinga wito wa kuwapa raia silaha katika jimbo la Cabo Delgado ili kupambana na wanamgambo wa Kiislamu.

    Wakazi wa eneo hilo wakati wote wamekuwa wakiomba silaha ili kuvisaidia vikosi vya usalama.

    Waziri Mkuu ametupilia mbali mawazo hayo wakati wa kikao cha masuala ya usalama kilichofanyika mji mkuu, Pemba.

    Alisema kuwa hatua hiyo itakuwa ‘’hatari na isiyohimilika’’.

    Alisisitiza silaha zinapaswa kuwa katika mikono ya ‘’watu wanaofaa’’, akimaanisha vikosi vya ulinzi na usalama na wale wanaowaamini.

    Bwana do Rosario amesema raia wanapaswa kuwa na jembe la kulima na ardhi na kalamu ya kuchangia maendeleo ya taifa lao.

  7. Godbless Lema apewa hifadhi Canada

    lema

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema, apata nafasi ya hifadhi ya kisiasa nchini Canada.

    Lema aliondoka jana nchini Kenya akiwa na familia yake, wakili wake George Luchiri Wajackoyah athibitisha.

    Mwezi uliopita Godbless Lema, polisi nchini Kenya walimkamatwa kwa madai ya kuingia nchini humo kinyume na sheria na kumuachia huru baada ya muda mfupi.

    Kwa mujibu wa wakili wake, George Wajackoyah, Lema ambaye alikua ameambatana na familia yake alikua akielekea jijini Nairobi kwa ajili ya kutafuta makazi ya muda baada ya kutishiwa maisha.

  8. Rais wa zamani wa Malawi ‘apinga kuzuiwa kwa akaunti zake ‘

    Reuters

    Chanzo cha picha, Reuters

    Rais wa zamani wa Malawi Peter Muthatika ametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya benki ya nchini humo baada ya akaunti zake kuzuiwa na chombo cha taasisi ya kupambana na rushwa mwezi Agosti, Gazeti la the Nation nchini humo limeripoti.

    Gazeti hilo limeelezea barua kutoka kwa mwanasheria wa Mutharika inayosema kuwa muda wa notisi ya zuio la akaunti zake umekwisha.

    Taasisi ya kupambana na rushwa (ACB) ilizuia akaunti za Bw. Mutharika na mkewe kutokana na ‘’utoaji fedha uliokanganya’’ wakati wa uchunguzi wa ukwepaji kodi wakati wa kuingiza mifuko 800,000 ya cement.

    Makosa hayo yanadaiwa kufanywa mwaka 2018 na 2019 wakati Bwana Mutharika alipokuwa madarakani.

    Mutharika alikana kufanya makosa hayo

  9. Mawaziri waonywa dhidi ya selfie na makundi ya whatsapp

    Rais wa Tanzania John Magufuli amewaonya mawaziri wapya dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

    "Sitaki mitindo ile ya kisasa ya kupiga selfie kwa kila unachofanya, unapaswa kufanya kazi na ajenda nyingine ni za siri .

    ''Teknolojia mpya ni nzuri lakini ni muhimu kwa kuzingatia maadili ya kazi zenu.Ndani ya serikali ni vyema kufanya kazi kwa uadilifu , kuna makundi mengi katika mitandao ya kijamii .

    Ndani ya serikali ni vyema kuzingatia siri na maadilli tulio nayo. Idara zote ni muhimu katika taifa letu. Alisema Magufuli

    "Kuna kaugonjwa serikaini kameingia , kila kitu kinaingia kitu mnaweka katika makundi ya WhatsApp. Baadhi ya siri za serikali zinavuja," rais Magufuli alisema.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Magufuli alichaguliwa tena mwezi Oktoba kuwa rais kwa miaka mingine mitano.

    Rais alipata 84% za kura.

  10. Habari...karibu katika matangazo ya moja kwa moja hii leo 10/12/2020