Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Makabiliano makali yaibuka ndani ya bunge la DRC
Kumekuwa na makabiliano makali ndani ya Bunge la taifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kati ya wanaharakati wa chama cha kabila na chama chaRais Felix Tshikedi Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema.
Moja kwa moja
Esther Namuhisa, Dinah Gahamanyi and Ambia Hirsi
Makabiliano yaibuka ndani ya bunge la Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Mbelechi Msochi
- Nafasi, BBC Swahili
Kumekuwa na makabiliano makali ndani ya Bunge la taifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kati yawanaharakati wa chama cha kabila na chama chaRais Felix Tshikedi. Watu kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano hayo.
Kundi la wanaharakati wa chama cha rais mtaafu Joseph Kabila walikuja kuzuia kikao cha wabunge ambao wanataka spika wa bunge aondolewe.
Picha za video zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha watu wakirushiana viti na kuharibu baadhi ya vifaa ndani ya bunge hilo lililopo mjini Kinshasa, huku polisi wakiwakimbiza.
Mzozo uliibuka wakati wabunge wanaomuunga mkono Rais Felix Tshikedi katika nia yake na kuanza kuwashawishi wabunge ili apate idadi kubwa ya wabunge kabla ya kuunda serikali yake mpya.
Kundi hilo la wawakilishi wa raia walikuja kuwasilisha, kura zao za maoni jana za kutaka Spika wa bunge Bi Jeanine Mabunda ambae ni mwanachama wa chama cha Bw Kabila aondolowe wakimtuhumu kuongoza bunge vibaya, lakini Spika wa bunge hakuwepo bungeni.
Ghadhabu hiyo ni ishara ya hali ya wasiwasi na uhasama unaoendelea kuongezeka baina ya Rais Tshisekedi na mtangulizi wake, Joseph Kabila – ambaye washirika wake bado wana ushawishi mkubwa ndani ya bunge na baraza la mawaziri nchini humo.
Rais Tshisekedi alitangaza siku ya Jumapili kwamba mpango wake wa mageuzi unawekewa pingamizi na alitaka kuunda serikali mpya ya muungano au kutangaza uchaguzi upya.
Unaweza pia kusoma:
Burundi yawapokea wawakilishi wa EU
Burundi na Muungano wa Ulaya (EU) zimekubali kurejelea tena mashauriano kwa lengo la kurejesha uhusiano wa kidiplomasia baada ya kusitishwa miaka mitano iliyopita, ofisi ya rais imetangaza.
Rais Evariste Ndayishimiye siku ya Jumatatu alikutana na wawakilishi wa EU nchini Burundi pamoja na mabalozi kutoka nchi za Ulaya.
Pande hizo mbili "zilikubaliana kusahau yaliyopita na kuangazia siku zijazo kwa kujenga upya uhusiano wao", kwa mujibu wa afisi ya rais.
Burundi ilikuwa imeilaumu EU kwa "kudhamini misukosuko" nchini humo kufuatia jaribio la mapinduzi lililotibuka mwezi Mei mwaka 2015. EU ilikatiza msaada wa bajeti kwa serikali kutoka na kile ilitaja kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu.
Rais Pierre Nkurunziza alikuwa madarakani wakati huo. Alifariki mapema mwaka huo na nafasi yake kuchukuliwa na rais Ndayishimiye.
Balozi wa EU mjini Bujumbura Claude Bochu ameweka picha ya mkutano huo katika Tweeter yake, na kusema kuwa ulifanyika katika "mazingira tulivu na ulikuwa wa kufana".
UN: Ethiopia sharti irejeshe utawala wa sheria Tigray
"Ni muhimu kurejesha haraka utawala wa sheria, kwa kuheshimu haki za binadamu" katika jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema.
Katika taarifa fupi aliongeza kuwa "anahofia hali ilivyo kwa sasa" katika jimbo hilo baada ya wiki nne za mapigano kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Tigray People's Liberation Front (TPLF).
Zaidi ya watu 40,000 wamevuka mpaka na kuingia Sudan na wengine wengi huenda wakalazimika kutoroka makwao.
Ndani ya Tigray kwenyewe kuna watu wengi wanahitaji misaada ya kibinadamu na Bwana Guterres ameomba "kufunguliwa kwa njia ya kuwafikia ".
Wiki iliyopita mamlaka nchini Ethiopia zilisema zitatoa njia salama ya kwa wafanyakaza wa kutoa msaada.
Ni vigumu kuthibitisha taarifa kutoka jimbo hilo baada ya mawasiliano ya simu na internrti kukatizwa katika maeneo tofauti.
Katika tamko lake la hivi punde kuhusu mzozo wa Tigray, Waziri Mkuu wa Abiy Ahmed amesema lengo la serikali ilikuwa "kurejesha sheria na utulivu" huko na kuwazuilia viongozi wa TPLF.
Kwa mara nyingine tena alipinga mpango wa kushauriana na uongozi wa TPLF.
Mjumbe huyo Muungano wa Ulaya wa masuala ya kibinadamu pia ametoa wito wa msaada wa kibinadamu:
Uganda yatuma maombi ya chanjo ya corona
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Isaac Mumema
- Nafasi, BBC Swahili
Uganda imewasilisha ombi la kupata chanjo ya covid19 kama inavyotakiwa na COVAX facility, wizara ya afya ya Uganda imethibitisha kuwasilisha ombi hilo.
Ombi hilo limetumwa wakati maambukizi ya virusi vya corona nchini Uganda yakizidi kupanda kwa kasi huku baadhi ya wanasiasa wakituhumiwa kusambaza virusi vya corona kutokana na muingiliano wa watu katika kampeni.
Maneja wa mipango ya taifa ya upanuzi wa chanjo katika wizara ya afya nchini humo bwana Alfred Driwale ameiambia BBC kuwa wameanza mchakato huo kwa majuma mawili na sasa wamekamilisha na wamewasilisha jana jioni kwa COVAX Facility:
"Uganda ikiwa moja ya mataifa ya uchumi wa chini yanayokwenda kunufaika kutoka kwa COVAX Facility. Kufikia sasa hakuna chanjo iliochaguliwa kutumiwa katika mataifa,isipokuwa kuna maendeleo na matarajio ya majaribio ya chanjo ya corona kila siku kwa wanachama wa COVAX Facility. Hivyo mara chanjo itakapopatikana itakuwa rahisi kusambaza kwa mataifa yenye mahitaji".
Dk.Driwale ameongeza kwamba chanjo hiyo itapewa watu waliomstari wa mbele katika kupambana na virusi vya corona pamoja na watu walio hatarini kuambukizwa virusi vya covid19 :
Kwa mujibu wa Shirika la afya duniani WHO, COVAX tayari imeshirikisha mataifa 186 duniani kati hayo 47 ni kutoka bara la Afrika.
Maalim Seif aapishwa kuwa makamu wa kwanza wa urais
Maalim Seif Sharif Hamad kutoka chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo amepishwa rasmi kuwa makamu wa rais wa kwanza wa Zanzibar.
Wakati akila kiapo hicho, Maalim Seif amehaidi kushirikiana na rais wa Zanzibar kwa hali na mali ili kuijenga Zanzibar kwa usalama na amani.
Maalim alitoa shukrani kwa wananchi wa Zanzibar na kusisitiza kuwa "imani ya wananchi wangu ndio wito mtakatifu unaonilazimisha kusimama kuwatumikia."
Aidha ameeleza kuwa uamuzi wa yeye Maalim pamoja na chama chake kufikia uamuzi wa kukubali kuingia katika serikali shirikishi ulikuwa mgumu sana ila nia ya rais Dkt.Hassan Mwinyi ndio iliwafanya wafikie uamuzi huo na kuweka pembeni madhila yote yaliyotokea.
Yeye amewakilisha chama kuja kutibu majeraha yaliokuepo.
Soma pia:
- Huu ndio mwisho wa Maalim Seif kisiasa?
- Upi mustakabali wa Zanzibar baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa?
Marekani yaiorodhesha Nigeria miongoni mwa nchi zinazokiuka uhuru wa dini
Marekani imeiweka Nigeria kwenye orodha ya nchi ambazo Washington haswa inakuwa na wasiwasi nazo kuhusu vitisho dhidi ya uhuru wa dini.
Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo hakutoa sababu kuhusu uamuzi huo alipoutangaza, lakini ripoti ya wizara hiyo iliripoti mwanzoni mwa mwaka huu uwepo wa vitendo vya kuwashikilia wafuasi wa madhehebu ya kishia na kukamatwa kwa waislamu wasiofuata sheria za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwenye orodha hiyo pia zimejumuishwa China, Iran, Pakistan, Myanmar, Korea Kaskazini na Saudi Arabia.
Nchi zilizo kwenye orodha zinaweza kukabiliwa vikwazo vya Marekani iwapo watahindwa kuchukua hatua ya kuboresha mazingira ya uhuru wa kidini.
Kifo cha daktari aliyefariki kwa corona Kenya chazua gumzo
Daktari mmoja nchini Kenya amefariki jana kutokana na ugonjwa wa Covid-19 huku akiwa hajalipwa mshahara kwa kipindi cha miezi mitano.
Umoja wa madaktari nchini Kenya umeeleza taarifa ya kifo hicho.
Stephen Mogusu aliyefariki akiwa na miaka 28 ,hakuwa na bima ya afya na familia yake ilianza kuchangisha katika mitandao ya kijamii mara alipoingia katka chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
Gavana wa kaunti ya Machakos, ambako Dkt Mogusu alikuwa anafanyia kazi ,alisema daktari huyo aliajiriwa chini ya mpango wa taifa wa afya.
"Si sawa kwa muajiri wake, ambaye ni serikali kutomlipa mshahara kwa miezi kadhaa .
Madaktari ambao wanaajiriwa na serikali huwa wanapokea mshahara wao na marupurupu yao kwa wakati na huwa na bima zote ,"Gavana Alfred Mutua aliandika katika kurasa yake ya tweeter.
Wakati Daktari, Mercy Korir,aliandika kwenye tweeter ya mwisho ya Dkt. Mogusu, "jilinde uwezavyo kwa sababu serikali haioni thamani ya maisha yako".
Madaktari wa Kenya wamekuwa wakilalamikia malipo duni , ukosefu wa vifaa vya kujikinga pamoja na huduma ya bima.
Madaktari walikuwa wafanye mgomo siku ya Jumatatu lakini waliamua kuipa serikali muda wa wiki mbili kufanyia kazi madai yao.
Ingawa wahudumu wengine wapatao 30,000 wakiwemo manesi walianza mgomo hapo jana.
Seif Sharif Hamad aapishwa leo kuwa makamu wa rais
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, anatarajiwa kumuapisha makamu wa kwanza wa rais kutoka chama cha upinzani cha ACT-Wazalendo,Maalim Seif Sharif Hamad.
Hata hivyo wadhifa huo si mpya kwa mkongwe huyo wa siasa za Tanzania.
Kabla ya mtafaruku wa kisiasa baada ya kufutwa matokeo ya uchaguzi wa 2015, Maalim Seif akiwa Chama cha Wananchi (CUF) alihudumu katika nafasi hiyo kutoka mwaka 2010 hadi 2015. Wakati huo Dkt. Ali Mohammed Shein wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa Rais.
Maalim ameamua kurudi tena kuwa makamu, kwa sasa akiwa chini ya Dkt. Hussein Ali Mwinyi. Swali linaloulizwa na wengi, kipi kikubwa anakwenda kuinufaisha upinzani kwa kuwa sehemu ya serikali?
Dkt. Mwinyi ameshusha tanga la safari ya kuiongoza Zanzibar chini ya muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Ni punde tu tangu taifa hilo lenye mamlaka ya ndani, kutoka katika uchaguzi uliogubikwa na mizengwe mingi.
Soma pia:
- Huu ndio mwisho wa Maalim Seif kisiasa?
- Upi mustakabali wa Zanzibar baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa?
Wakimbizi wa Burundi wadai kunyanyaswa Tanzania
Wawakilishi wa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania wameandika barua kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Guterres na Kamishna Mkuu wa umoja huo anayeshughulikia Wakimbizi Grandi kuomba makazi katika nchi nyingine.
Barua hiyo imesema kuwa baadhi ya wakimbizi wananyanyaswa na kurejeshwa kwao bila kufuata utaratibu maalum ndio maana wanaomba taifa lingine liweze kuwapokea.
Lakini mwanzoni mwa mwezi huu shirika la kutetea haki za binadamu Human Watch, ilitoa ripoti ya kukemea jambo hilo la kuwa Tanzania inawanyanyasa wakimbizi na kulitaka taifa hilo liwalinde kwa kufuata sheria za kimataifa.
Wakimbizi hao wanasema kuwa wameambiwa kuwa wanapaswa kurudi kwao kwa sababu sasa hivi taifa la Burundi liko salama.
Hata hivyo hapo nyuma, serikali ya Burundi na Tanzania zilifikia makubaliano ya wakimbizi kurudi nyumbani kwa kuwa kuna amani kwa sasa ingawa wakimbizi wenyewe wanasema, si serikali yoyote kati ya hizo mbili ndio wana haki ya kusema usalama upo au haupo.
Msemaji mkuu wa serikali ya Tanzania , Dkt Hassan Abas alisema hawajapokea barua yeyote kutoka kwa wakimbizi, "kama kuna changamoto yeyote kwenye usimamizi wa wakimbizi Tanzania kuna ofisi za shirika la umoja mataifa linalosimamia haki za wakimbizi, serikali ipo ,hizo changamoto tungeletewa na kuzitatua".
Aliongeza kusema "Tunachokisisitiza kuwa Tanzania haiwezi kuwatesa wakimbizi , Tanzania haiwezi kumdhuru mkimbizi, ambaye sisi wenyewe ndio tulimkubali, tungeweza kumkataa lakini tumemkubali na akapata kinga ya kimataifa ya kukaa nchini kwetu mpaka itakaporejea kuwa na amani, sasa tunashiriki vipi kumuhujumu."
- Zoezi la kuwaondoa wakimbizi wa Burundi laanza kwa kufunga masoko
Habari...karibu katika matangazo ya moja kwa moja leo hii ikiwa ni tarehe 8/12/2020.