NEC: Tumepokea majina ya viti maalum kutoka Chadema
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imesema ilipokea barua zenye majina ya mapendekezo ya wanawake wabunge na madiwani wa viti maalum kutoka Chadema.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo. Tukutane tena Jumatatu ijayo
Tunakuaga kwa video hii ya ssichana wa miaka 10 tu aliyewanunulia wazazi wake nyumba:
Akiwa na umri wa miaka 10 tu Emmanuella Samuel ametumia
mapato yake aliyoyatengeneza kupitia
mtandao wake wa You Tube kuwajengea wazazi wake nyumba. Amekuwa nyota katika
chaneli ya You Tube maarufu ya
mchekeshaji Mark Angel, tangu alipokuwa na umri wa miakamitano. Akimshukuru
mama yake Emmanulla amesema mama yake anafaa kupewa nyumba nyingi.
Maelezo ya video, Akiwa na umri wa miaka 10 tu Emmanuella Samuel amewajengea wazazi wake nyumba
NEC: Tumepokea majina ya viti maalum kutoka Chadema
Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imesema ilipokea barua zenye majina ya mapendekezo ya wanawake wabunge na madiwani wa viti maalum kutoka chama cha demokrasia na maendeleo-Chadema.
Tume imesema imepokea majina hayo tarehe 19, Novemba mwaka huu kutoka Chadema huku chama cha mapinduzi- CCM walikuwa wametuma majina yao Septemba 26.
Na Novemba 20, kikao kilikaa kuteuwa wabunge hao 19 kutoka katika chama hicho kwa mujibu wa katiba na sheria ya Tanzania.
Awali, Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika aliiambia BBC kuwa Chadema haijafanya uteuzi wa wabunge hao na vikao vya juu vya chama hicho vitakaa ili kufanya maamuzi.
Hata hivyo Chadema iligoma kuteua wabunge wa viti maalumu wakidai kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi uliopita wakisema ulikuwa na kasoro lukuki, tuhuma ambazo hata hivyo zimekanushwa na mamlaka nchini humo.
Abiy Ahmed akutana na ujumbe wa AU lakini ameuzuwia kwenda Tigray
Chanzo cha picha, @PMEthiopia
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amekutana na Tume ya
Muungano wa Afrika ambao uliwasili mjini Addis Ababa kujaribu kuleta upatanishi
baina ya serikali na vikosi vya Tigray
People's Liberation Front (TPLF) baada
ya zaidi ya wiki tatu za mzozo.
Awali Bw Abiy alisema
juhudi za kimataifa za kuleta pande mbili mezani kwa ajili ya mazungumzo "hazikaribishwi",
na tume ya AU haitaruhusiwa kukutana na maafisa wa Tigray.
Baada ya mkutano wa
Ijumaa na wajumbe watatu maalum wa AU, Bw Abiy amesema kuwa serikali yake inataka
kuhakikishaulinzi wa raia, inafungua
njia ya misaada ya kiutu, na itawakaribisha tena wakimbizi Waethiopia
waliokimbilia Sudan.
Hata hivyo, waziri
mkuu huyo amesema serikali yake itaendelea na juhudi zake dhidi ya za kile
alichokiita"kundi la TPLF ".
Wajumbe wa AU envoys
–Marais wa zamani Joaquim Chissano wa Msumbiji, Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia na Kgalema Motlanthe wa Afrika Kusini- hawataruhusiwa kusafiri kuelekea Tigray, serikali tayari imesema.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Mzozo wa Tigray Ethiopia: Waziri Mkuu Abiy Ahmed ni nani?
Chanzo cha picha, EPA
"Kwa mtazamo wangu, siamini Ethiopia inahitaji vita. Sitaki kujumuishwa miongoni mwa watu wanaopendelea suluhisho la kijeshi.
Hiyo ilikuwa kauli ya Waziri Mkuu Abiy mwezi Septemba wakati jimbo la Tigray linaloongozwa na TPLF iliamua kufanya uchaguzi kupinga amri iliyotolewa na serikali kuu...Soma zaidi taarifa hii.
Jimbo lateua ujumbe kwa ajili ya mazungumzo ya upatanishi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wakimbizi wanaotoroka mapigano Tigray wamepata hifadhi katika nchi jirani ya Sudan
Uongozi wa jimbo la Ethiopia la Tigray unasema kuwa umewateua wawakilishi
wake kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Muungano wa Afrika (AU) pamoja na mashirika mengine ya kimataifa kuhusu usitishwaji
wa mara moja wa mapigo na serikali ya Ethiopia.
Katika taarifa yake,
pia umetoa wito wakuwezeshwa kwa shughuli za misaada ya kiutu na kufanyika kwa
uchunguzi kuhusu madai ya uhalifu wa kivita.
Waziri Mkuu Abiy Ahmed anatarajiwa kukutanza na ujumbe wa Amani wa
AU, lakini amekataa upatanishi wa kimataifa katika mzozo huo.
Mapigano yameripotiwa
baina ya vikosi vyaWatigray na
wanajeshi wa serikali katika maeneo kadhaa ya Tigray, lakini mji
mkuu wa jimbo hilo Mekelle unasemekana kuwa katika hali ya utulivu.
Darasa la mapishi linalookoa maisha ya watoto Tanzania
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Aboubakar Famau
Nafasi, BBC News, Dar es Salaam
Nchini Tanzania, tatizo la utapiamlo kwa
watoto walio chini ya umri wa miaka mitano bado ni kubwa.
Miongoni mwa mikoa yenye idadi kubwa wa
watoto hao ni mkoa wa Shinyanga uliopo kaskazini Magharibi mwa Tanzania, ambapo
asilimia kumi na tano ya watoto wana uzito pungufu huku asilimia 32 wakiwa na
udumavu. Hii ni kwa mujibu Tafiti ya Taifa ya Lishe yani Tanzania National
Nutrition Survery ya mwaka 2018/2019.
Kundi la kina mama lenye watoto
wanaosumbuliwa na tatizo la utapiamlo uliosababishwa na upungufu wa madini
chuma na vitamin A hivyo kuwa na utizo pungufu limekamilisha mafunzo ya wiki
mbili ya mapishi bora yanayojumuisha makundi matano ya vyakula vyenye
virutubishi kwa watoto.
Baadhi ya akina mama kutoka kijiji cha
Wijiteleja kilichopo mkoani Shinyanga kaskazini magharibi mwa Tanzania,
wanaelezea jinsi mafunzo hayo yalivyoongeza uzito wa watoto wao.
Magdalena John Kumalia awali mtoto wake alikuwa
na kilo ambazo sio nzuri, lakini baada ya kumpikia vyakula vyenye virutubishi
hali ilibadilika.
“Mwanangu alikuwa na kilo saba tu, tukaanza
darasa la mapishi, tukaanza kumpikia. Tulikuwa tunapika uji, tunaweka karanga,
maziwa, tukiivisha, tunaepua na kuweka mbogamboga za majani, mpaka leo
tumepima, mwanangu ana kilo tisa,” anasema Magdalena.
Nae Agnes Ngelela anasema mbali na mtoto
wake kuwa na kilo moja alipozaliwa lakini pia aliandamwa kwa magonjwa kama vile
kuharisha na kutapika, lakini sasa magonjwa yote yameisha baada ya kupata lishe
bora.
Christian Ngowi ambae ni mganga mfawidhi wa zahanati ya Mundo
mkoani humo anasema mafunzo hayo yalilenga zaidi kutumia vyakula, mbogamboga na
matunda ambayo upatikanaji wake ni rahisi katika jamii inayozunguka.
“Tuliona katika kundi la mbogamboga, kuna changamoto kubwa ya
upatikanaji wa kundi hili kutokana na hali ya ukame inayozunguka wilaya yetu.
Kwa hiyo, tulishauriana na afisa kilimo na mtendaji wa kijiji na wahudumu wa
afya tukawafundisha kina mama kuwa na bustani za majumbani, kwa hiyo lile kundi
la mbogamboga sasa hivi kina mama wanalipata kwa wingi bila gharama na kupoteza
muda kwa kwenda sokoni,” anasema Dk. Ngowi.
Wakati huo huo, Dk Frank Mtimbwa kutoka Shirika la World Vision
nchini Tanzania ambalo ndilo linalodhamini mradi huu wa mafunzo ya mapishi kwa
kushirikiana na serikali na wadau wengine wa afya, anasema ili kutokomeza
tatizo la utapiamlo katika jamii imewalazimu kuwashirikisha na kina baba.
“Kwa jamii hizi tulizonazo, mwanaume anaweza akalima na mwanamke
na akauza chakula chote na kwenye familia ukasikia kuna njaa, lakini wakati wa
msimu wa kulima, walilima pamoja na walivuna sana. Kwa hiyo, sasa hivi wanafanya
kazi pamoja na mwisho wa siku wanaamua wauze nini na pesa inayopatikana ifanye
nini,” anasema Dk. Mtimbwa.
Mbali na darasa la mapishi, wanakijiji pia wamehamasishwa
kuanzisha bustani za nyumbani ili kurahisisha upatikani wa mbogamboga pamoja na
viazi lishe ambavyo wataalamu wanadai vina asilimia kubwa ya virutubishi kwa
watoto.
Wakenya waliokuwa wakielekea Dubai wakamatwa na stakabadhi gushi za corona
Chanzo cha picha, SIMON MAINA/AFP/GETTY IMAGES
Maafisa wa uwanja wa ndege nchini Kenya
wamewakamata wasafiri 21 ambao waliokuwa
wakielekea mjini Dubai, katika Muungano wa falme za kiarabu (UAE), kwa kutumia
vyeti gushi vya Covid-19.
Wasafiri hao wamekamatwa wakati wa msako wa vyeti hivyo uliokuwa ukifanyika
katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta katika mji mkuu, Nairobi.
Hii inakuja saa kadhaa baada ya UAE
kupiga marufuku utoaji wa vibali vya
kusafiria (visa) kwa wasafiri wanaotoka nchi kadhaa ikiwa ni pamoja na Kenya.
Vyombo vya habari nchini Kenya vinaripoti kuwa marufuku hiyo iliwekwa baada
ya wasafiri kutoka Kenya kupatikana na vyetu gushi vya Covid-19 walippowasili
katika taifa hilo la Ghuba.
Kenya imekuwa ikirekodi ongezeko la maambukizi ya Covid-19, huku jumla ya watu wenye maambukizi
ikifikia 80,102 vikiwemo vifo vya watu 1,427.
Binti wa Jerry Rawlings aonya kuhusu uchangishaji wa pesa za mazishi
Binti
mkubwa wa rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings ametoa onyo dhidi ya wezi wa
mtandaoni wanaodai kuwa wanachangisha pesa kwa ajili ya mazishi ya baba yake.
Katika
taarifa yake aliyoituma kwenye mtandao wa Facebook siku ya Alhamisi Zanetor
Rawlings, alisema akaunti gushi za
mitandao ya kijamii zimebuniwa kwa ajili ya kukusanya rambirambi ya baba yake.
Amesema
kuwa wezi wanawalenga wale wanaomtumia salamu za rambirambi kufuatia kifo cha
baba yake.
Bi
Rawlings ni mbunge wa jimbo la Klottey
Korle katika bunge la Ghana.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Tume ya uchaguzi Uganda yawataka polisi kutowazuia wagombea urais
Tume ya uchaguzi
nchini Uganda imewatahadharisha polisi nchini humo dhidi ya kuwazuia wagombea
wa urais kuendesha kampeni zao.
Tume hiyo imesema kuwa imepokea baadhi ya
malalamiko kutoka kwa wagombea wa urais na pia kuona taarifa za vyombo vya
habari kwamba polisi inazuia na kuvuruga kampeni zao .
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 1
Wakati huo huo katika taarifa ya pamoja ya mabalozi wa nchi za
Muungano wa Ulaya nchini humo, wameeleza kutofurahishwa kwao na ghasia
zilizotawala kampeni ya uchaguzi tarehe 18 na 19, Novemba nchini humo.
Wamesema Uganda ilishuhudia ghasia na maandamano pamoja na
matumizi yasiyofaa ya vikosi vya usalama dhidi ya raia na kuvitaka vyama vyote
vya kisiasa na wagombea wake kuwataka wafuasi wao kuacha ghasia na matumizi ya
lugha mbaya.
Wametoa wito wa kuchukuliwa kwa hatua kali za kisheria kumaliza
uchokozi unaolenga kuleta ghasia au kusababisha ukiukaji wa sheria.
Hii inajiri huku Kiongozi wa upinzani nchini humo Robert
Kyagulanyi al maarufu Bobi Wine akilalamikia kuzuiwa kuendesha kampeni zake
katika mji wa Hoima magharibi mwa nchi hiyo.
Katika ujumbe wake wa twitter Bobi Wine amesema kuwa polis
walifunga barabara za kuelekea katika mji huo ili kumzuwia kufika katika hoteli
aliyotarajia kupata malazi na kuziamuru hoteli zote katika mji huo zisimpokee
na timu yake, na hivyo kuwalazimisha kulala ndani ya magari:
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Kenya yapunguza idadi ya wageni wanaohudhuria harusi kutokana na corona
Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Chakula kitatolewa tu kwa wazazi na ndugu wa maharusi
Idadi ya wageni watakaoruhusiwa kuhudhuria harusi nchini Kenya
imepunguzwa hadi kufikia watu 50 pekee kutokana na ongezeko la maambukizi ya
virusi vya corona nchini humo.
Baraza linalojumuisha
dini mbalimbali nchini humo limesema kuwa chakula kinachotolewa katika harusi
kitakuwa kikiletwa kwa wazazi na ndugu wa karibu wa maharusi pekee.
Mwezi Agosti Rais
Uhuru Kenyatta aliongeza idadi ya wageni wanaoweza kuhudhuria harusihadi watu 100 alipolegeza masharti ya
kudhibiti maambukizi ya Covid-19.
Katika masharti
mapya yaliyotangazwa Alhamisi wiki hii, chakula kimepigwa marufuku katika
mazishi na idadi ya watu wanaoruhusiwa kuhudhuria mazishi imepunguzwa hadi watu
100 pekee.
Muda wa mazishi pia
umerekebishwa kwa kupunguzwa hadi saa moja pekee.
Huduma za kanisa pia hazitatolewa kwa zaidi ya dakika 90.
Wiki iliyopita mwenyekiti wa baraza la dini mbali mbali nchini Kenya, Anthony
Muheria, alitibiwa virusi vya corona katika hospitali moja mjini Nairobi.
Mwanasheria mkuu wa Tanzania aionya Chadema kuhusu wabunge walioteuliwa
Chanzo cha picha, Profesa Adelardus Kilangi
Maelezo ya picha, Profesa Adelardus Kilangi anasema wabunge wa viti maalum waliteuliwa halali kikatiba
Mwanasheria Mkuu wa Tanzania Profesa Adelardus
Kilangi amewaonya CHADEMA kutowabugudhi wabunge wa chama hicho wa viti
maalumkutoka chama hicho.
Profesa Kilangi amesema, mchakato wa Wabunge wa viti Maalum
kutoka CHADEMA umefuata Sheria na Katiba, hivyo hawapaswi kubugudhiwa.
Awali Spika wa bunge la
Tanzania Job Ndugai alisema, kanuni za
bunge zinamtaka kuwalinda Wabunge walio wachache na maslahi yao na kuahidi kufanya hivyo kwa nguvu zake zote.
Chanzo cha picha, BUNGE-TANZANIA
Maelezo ya picha, Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
Kuhusu Wabunge 19 wa viti Maalum kutoka CHADEMA Bw Ndungai
alisema wameteuliwa kihalali na kama
CHADEMA wana matatizo nao walipaswa kuwaita kwa heshima na kuwasikiliza badala
ya kuwahukumu.Amesema majina ya
wabunge wa viti maalum alipewa na na Tume ya Uchaguzi, na kazi yake ni kuwaapisha Wabunge hao na
ameshafanya hivyo.
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 27.11.2020