Uskochi kuwa taifa la kwanza kugawa pedi bure

Uskochi limekuwa taifa la kwanza duniani kufanya bidhaa za sodo/pedi kugawiwa bure kwa kila mtu. Wabunge walipitisha mswada huo bila kutoa taarifa siku ya Jumanne.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Mpaka hapa tumefika mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, tukutane tena hapo kesho.Shukrani!

  2. Uskochi kuwa taifa la kwanza kugawa pedi bure

    pad

    Uskochi limekuwa taifa la kwanza duniani kufanya bidhaa za sodo/pedi kugawiwa bure kwa kila mtu. Wabunge walipitisha mswada huo bila kutoa taarifa siku ya Jumanne.

    Na sasa mamlaka imetoa idhini kisheria kuhakikisha kuwa bidhaa hizo zinatolewa bure kwa yeyote anayehitaji. Mswada huo ulitmbulishwa na waziri wa ajira bi. Monica Lennon.

    Alikuwa anafanya kampeni ya kukomesha umaskini wa kununua bidhaa hizo tangu mwaka 2016.

    h

    Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

    Alisema kuwa ni suala linawezekana kufanyika na sheria tu ndio inaweza kutoa muongozo wa kila kitu na sasa ni muhimu zaidi kutokana na janga la corona.

    "Siku za hedhi haziachi kutoka wakati wa janga na kazi kubwa inapaswa kufanywa kuhakikisha pedi au sodo hizo zinatolewa bure," aliongeza.

    Umasikini wa sodo ukoje? Umasikini wa sodo ni pale watu wenye kipato cha chini kushindwa kununua pedi. Boksi moja la pedi zinazoweza kutumika siku tano zina gharama ya paundi 8 na baadhi ya wanawake hawawezi kugharamikia .

  3. Utafiti wabaini mengi ya mashambulio ya IS hufanyika Afrika

    Watoto wa Burkinafaso

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Watoto nchini Burkina Faso hujifunza hata jinsi wanavyopaswa kufanya wanaposhambuliwa na Jihad

    Tathmini ya mwaka ya ugaidi umebaini kuwa mataifa yaliyoko kusini mwa jangwa la sahara yalishuhudia mashambulio mengi yanayohusiana na kikundi cha uhusiano Islamic State na washirika wake.

    Utafiti huo uliofanywa na Global Terrorism Index, na kuendelezwa na taasisi ya uchumi na amani, ulibaini kuwa kulikuwa na vifo chini ya 14,000 tu kote duniani vilivyohusishwa na ugaidi- kwa mwaka wa tano mfulurizo idadi hiyo ilipungua.

    Ilibainika kuwa kupungua zaidi kwa vifo vitakanavyo na ugaidi kulikuwa katika mataifa ya Nigeria na Afghanistan.

    Ongezeko kubwa la matukio ya ugaidi lilitokea katika nchi yaBurkina Faso – ambako vifo vilipanda kwa 590%.

    Kulingana na kiwango hicho pia mataifa ya Msumbiji, Mali na Niger zilikuwa ni yalikuwa na ongezeko la kuhofiwa la mashambulio ya IS.

    Ilionya kuwa kudorora kwa hali ya uchumi kunaweza kuwafanya watu washawishiwe na propaganda za itikadi kali.

  4. Kenyatta alieleza sababu ya kuachana na mtandao wa Twitter

    Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa aliamua kuacha kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter kwasababu ya matusi.

    ‘’ Mimi nilitoka Twitter kwa sababu huko ni matusi tu...afadhali nipige story na mama, nilale, niamke nifanye kazi.’’ Amesema Bw Kenyatta,

    Bw Kenyatta ameyasema hayo alipokuwa akizindua mpango wa ukusanyaji wa saini za wakenya kwa ajili ya mchakato wa kuleta maridhiano nchini humo –BBI.

    Inatarajiwa kuwa walau saini 5000 zitakuwa zikikusanywa kwa kwa wiki moja.

    Kituo cha televisheni nchini Kenya cha NTV kilishirikisha video ya sehemu ya hotuba ya rais Kenyatta:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  5. Mbuzi wa Msumbiji watunukiwa cheti maalumu

    Mbuzi

    Chanzo cha picha, AFP

    Mbuzi maarufu wa Msumbiji amepewa cheti maalumu kama sehemu ya mipango ya kuulinda utambulisho wake atakaposafirishwa nje ya nchi kuuzwa kwenye soko la dunia.

    Waziri wa viwanda na biashara nchini humo, Carlos Mesquita, ameyasema hayo akiongeza kuwa, ishara ya utambulisho wa kijiografia katika nyama ya mbuzi utahakikisha sifa ya ubora wake inalindwa.

    Mbuzi huyo aina ya Tete yana umuhimu wa kipekee katika Msumbiji, kwasababu ya nyama yenye utamu wa kipekee.

    Nyama ya mbuzi inaweza kuliwa wakati wote nchini Msumbiji, lakini mara kwa mara huliwa katika sherehe za kitamaduni na kijamii, mkiwemo harusi na katika sherehe za mahafari.

    GI ni cheti kinachothibitisha kwamba bidhaa fulani inatoka katika eneo fulani linalofahamika kwa ubora wake, ikimaanisha kuwa bidhaa kutoka maeneo mengine hayawezi kutumia jina sawa na hilo - sawa na inavyofanyika katika pombe aina ya Champagne.

  6. Afisa wa wanyamapori Kenya amnusuru pundamilia saratani

    Afisa wa wanyamapori katika mbuga ya wanyama iliyopo jijini Nairobi nchini Kenya -Nairobi National Park, amefanikiwa kuuondoa uvimbe uliokuwa kwenye uso wa pundamilia ambao ulibainika baadaye kuwa ni aina nadra ya saratani ya ngozi.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Aina hiyo ya uvimbe wa saratani ambayo hufahamika kwa lugha ya kitaalamu kama 'squamous cell carcinoma', ulikuwa umevimba chini ya sikio la kushoto la pundamilia.

    Uvimbo huo uliondolewa kwa upasuaji, kulingana naShirika la huduma za wanyamapori la Kenya (KWS), na pundamilia huyo anatarajiwa kupona kabisa

  7. Elon Musk: Mambo 5 unayopaswa kuyafahamu kumuhusu mtu wa pili tajiri duniani

    Elon Musk

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mwaka 2020 pekee Elon Musk alipata zaidi ya dola bilioni 100

    Mkurugenzi mkuu waTesla CEO bilionea Elon Musk sasa amempita Bill Gates na kuchukua nafasi ya pili miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani.

    Utajiri wa jumla wa Musk umepanda na kufikia hadi ya dola bilioni 7.2mwezi Novemba 23 , kutokana na bei ya hisa za kampuni yake ya magari ya umeme-Tesla, kwa mujibu wa makadirio Bloomberg ya kiwango cha utajiri . Utajiri wa Elon Musk kwa sasa dola bilioni 127.9

    Katika umri wa miak 12 Musk aliuza programu ya kwanza ya  software  aliyobuni
    Maelezo ya picha, Katika umri wa miak 12 Musk aliuza programu ya kwanza ya software aliyobuni

    Elon Musk alizaliwa Juni 28, 1971 mjini Pretoria, Afika Kusini

    Akiwa mtoto, alikuwa na tabia ya fikra za ubunifu, jambo lililowafanya wazazi wake na ‘madaktari’ kumfanyia uchunguzi wa kusikia.

    Baada ya baba yake kutalikiana na mama yake, Musk akawa mtu anayependa sana kompyuta. Alijifunza mwenyewe kubuni wavuti akiwa na umri wa miaka 10. Aliuza softwareambayo aliitengeneza kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 12.

    Alianzisha software ya X.com mwaka 1999, ambayo baadae iliitwa PayPal, halafu mwaka 2002 akaanzisha SpaceX naTesla Motors mwaka 2003.

    Akiwa na umri wa miaka 20 alikuwa tayari milionea baada ya kuuza kampuni yake ya Zip2.

    2. Alikuwa namba 35 katika orodha ya wawekezaji wa dunia Januari 2020

    Elon Musk alipata theluthi tatu ya utajiri wake kupitia kampuni ya magari ya umeme ya  Tesla

    Chanzo cha picha, ROBYN BECK / AFP

    Maelezo ya picha, Elon Musk alipata theluthi tatu ya utajiri wake kupitia kampuni ya magari ya umeme ya Tesla

    Alipata ujuzi kwa kusoma vitabu

    Elon Musk

    Akiwa na umri wa miaka tisa, alikuwa mwana akiolojia Encyclopaedia Britannica kwasababu ya utafiti wake wa mara kwa mara kuhusu suala hilo.

    Hata sasa, akitaka kumuajiri mfanyakazi katika kampuni yake huhakikisha anafahamu asilimia kubwa ya mtu ya elimu binafsi ya mtu ili hata kama hatafanikiwa kupata kazi, uelewa wake uwe umeongezeka.

    4. Hataki kumiliki nyumba binafsi

    Nyuma ya Elon

    Chanzo cha picha, ZILLOW / MUSK

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Nyumba zake mbili alizoziweka sokoni moja ilikuwa na thamani ya dola milioni 40 na nyingine ilikuwa na thamani ya dola milioni 30.

    5. Alikuwa analala kwenye kiti cha ofisi

    Tajiri huyo huenda kufanya kazi katika kampuni yake kama mfanyakazi mwingine yoyote yule na hata amekuwa akilala ofisini kazi zinapokuwa nyingi.

    Hulala kwenye kiti cha ofisini kilichopo mkabala na godoro na kitanda, japo alikuwa akifanya hivyo akiamua.

  8. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa aitaka Ethiopia kuwalinda raia Tigray

    António Guterres

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres anahoia hali ya raia jimboni Tigray

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ana "hofu kubwa" kuhusu hali ya watu wa jimbo la Ethiopia la Tigray na anaunga mkono juhudi za Umoja wa Afrika za kutuliza hali katika eneo hilo, Msemaji wa Umoja wa mataifa, Stephane Dujarric amesema.

    Bw Guterres pia ametoa wito wa ulinzi wa raia kabla ya tishio la jeshi la Ethiopia la kuanza mashambulio dhidi ya mji mkuu wa jimbo hilo, Mekelle.

    "Tunafuatilia ripoti za uwezekano wa hatua ya kijeshi kwa hofu kubwa. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ana hofu kubwa kuhusu athari zitakazosababishwa na mashambulio hayo kwa raia, kuhusu uwezo wetu wa kusambaza misaada ya kiutu katika eneo ambalo ni vigumu kufanya hivyo ." Bw Dujarric amesema.

    "Amewataka viongozi wa Ethiopia kufanya kila liwezekanalo kuwalinda raia, kuzingatia haki za binadamu, na kuhakikisha misaada ya kibinadamu inaweza kusambazwa kwa watu wanaoihitaji."

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mapigano baina ya serikali kuu na vikosi katika jimbo laTigray yamekuwa yakiendelea kwa karibu wiki tatu.

    Mamia ya watu wameripotiwa kuuawa na wengine maelfu kwa maelfu kutoroka makazi yao ili kuepuka mapigano hayo.

    Waziri Mkuu Abiy Ahmed amekuwa kirudia mara kwa mara kuwa jeshi litawalinda raia katika mashambulio yake dhidi ya vikosi vya Tigray.

  9. Mwanaume afariki ghafla ndani ya basi la umma Kenya

    Mabasi

    Wasafiri waliokuwa wamepanda katika basi la umma katika mji mkuu wa Kenya Nairobi, waliingiwa na hofu, baada ya mwanaume mmoja kufa ghafla ndani ya basi hilo.

    Wasafiri na kondakta walitambua kuwa mwanaume huyo amefariki wakati walipojaribu kumuambia ampishe abiria mwenzake ambaye alikuwa anataka kutoka ndani ya gari lakini hakuweza kujibu lolote na alionekana kupoteza fahamu.

    Maafisa wa wizara ya afya waliitwa katika eneo la tukio baada ya polisi kukataa kusafirisha mwili kwa hofu ya uwezekano kuwa mwanaume huyo alikuwa na maambukizi ya Covid-19.

    Maafisa waliupulizia dawa mwili wa mwanaume huyo ulipokuwa ndani na baadaye waliondoka nao ndani ya mfuko.

    Televisheni ya Kenya NTV iliushirikisha umma video hii ya tukio:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  10. Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubashara ya leo tarehe 25.11.2020