Wabunge wa viti maalum Chadema waapa
Wabunge wateule wa viti maalum kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA wanaapishwa leo jijini Dodoma.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Wabunge wa viti maalum Chadema waapa
Wabunge wa viti maalum kupitia chama cha upinzani cha CHADEMA wanaapishwa leo jijini Dodoma.
Wabunge hao 19 wameongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha)Halima Mdee kula kiapo cha uaminifu mbele ya Spika Job Ndugai.
Awali, Chadema iligoma kuteua wabunge wa viti maalumu wakidai kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi uliopita wakisema ulikuwa na kasoro lukuki. Uongozi wa chama hicho ulidai kuwa na kutuma wabunge wa vti maalumu ni kuhalalisha uchaguzi huo.
Ruka YouTube ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazoMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Katika uchaguzi wa mwezi uliopita, Chadema ilipata mbunge mmoja tu wa kuchaguliwa jimboni, Bi Aida Kenani kutoka jimbo la Nkasi Kaskazini mkoani Katavi.
Fuatilia zaidi
- Je, mbunge pekee wa Chadema anaweza kwenda bungeni?
- Je, huu ni mwisho wa upinzani Tanzania?
Tanzania yajipanga kwa utalii wa Disemba
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Peter Mwangangi
- Nafasi, BBC Swahili

Chanzo cha picha, Getty Images
Bodi ya utalii ya Tanzania pamoja na wawekezaji katika sekta ya utalii wanasema wanaweka juhudi kubwa zaidi katika kuwavutia watalii kutoka Afrika Mashariki katika likizo ya Disemba ambapo watu wengi husafiri na kutumia fedha zao kuvinjari.
Sekta ya utalii imepata pigo kutokana na kupungua kwa watalii kutoka nje, na baada ya serikali nyingi kusitisha safari za ndege ili kuzuia kuenea kwa Covid-19.
Hata hivyo hatua hii imekuwa ya baraka kwa upande mwingine hususan utalii wa ndani.
‘’Kati ya miezi ya Machi na Agosti mwaka huu, mbuga ya wanyama ya Serengeti ambayo ni kivutio kikuu cha utalii ilipokea wageni 43,452 kutoka Afrika Mashariki na watalii 9,791 kutoka nje’’, anasema Joseph Sendwa ambaye ni Meneja wa masoko ya ndani na ya kikanda katika Bodi ya Utalii ya Tanzania.
Takwimu hizi zimefanya baadhi ya makampuni nchini Tanzania kuanza kulizingatia zaidi soko la nyumbani, anasema Nancy Cosmas Ngotea ni Afisa wa masoko katika kampuni ya utalii ya Zara Tours iliyopo eneo la Kilimanjaro.
‘‘Kampuni yetu ni kubwa na ilikuwa na wafanyakazi wengi sana ila imebidi watu kuachishwa kazi. Kwa wakati huu pia tumepata maombi mengi kutoka kwa watanzania na watu kutoka Afrika Mashariki, na tumeandaa vifurushi nafuu na kupunguza bei sana kwa mfano ukiwa na Tsh 1,200,000 (USD 517) unaweza kupanda mlima Kilimanjaro ambapo mwanzoni haikuwa hivo, na mkiwa wengi zaidi bei inapungua,’’ anasema Nancy.
Hata hivyo wapo wajasiriamali ambao wamekuwa wakilenga soko la ndani tangu zamani kama vile Juma Rasheed, mwanzilishi wa ExplorePhotoTrip. Kampuni hiyo imepata ufanisi mkubwa kwa kuwasafirisha watalii katika Pwani ya Kenya na nchini Tanzania.
Rasheed anasema: ‘‘tuliona pengo katika utalii wa ndani na tukaanza kutoa bei nafuu kwa Wakenya na raia wa Afrika Mashariki. Tulianzia Mombasa na kuenea hadi Kenya nzima na Tanzania. Tulipata mapokeo mazuri. Wakati huu wa Covid-19 tulipoteza biashara. Lakini kuanzia mwezi wa tano tulianza mambo kama vile kuendesha baiskeli na madau madogo madogo, na wengi waliweza kutulipa ili watalii nasi’’.
Je, bodi ya utalii ya Tanzania inafanya nini zaidi kuimarisha hali?
Sendwa anasema kuwa wametoautambulisho mpya kwa vivutio nchini humo kwa jina ‘Tanzania Unforgettable’ pamoja na kuweka matangazo ya kidijitali yaani dijital marketing kulenga masoko ya nje.
‘‘Sisi kikawaida matangazo yetu huwa tunaenda kwenye maonyesho ya ng’ambo kama vile ITB (Internationale Tourismus Börse) Berlin, WTM (World Travel Market) ila hilo sasa haliwezekani. Kwa hivyo sasa tunawahusisha mabalozi wetu katika nchi za nje, ’’ anasema Sendwa.
Umoja wa Mataifa wasema misaada ya kiutu inaisha Tigray

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Watoto wakicheza karibu na soko katika mji wa kaskazini wa Humera ambao ulichukuliwa na jeshi kutoka kwa wapiganaji wa Tigray Wafanyakazi wa misaada wa Umoja wa Mataifa wameonya kwamba misaada ya kiutu inaelekea kuisha katika jimbo la Ethiopia la Tigray baada ya wiki za mashambulio katika jimbo hilo.
Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya kiutu, Saviano Abreu, alisema kuwa shirika hilo limezuiwa kutuma wahudumu na misaada.
Katika mkutano na BBC, ametoa wito wa uhuru wa matembezi pamoja na kuwa huru kwa raia.
Shirika la huduma kwa wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema idadi ya raia waliovuka mpaka na kuingia Sudan imeongezeka na kufikia hadi watu 40,000.
Baraza lausalama la Umoja wa Mataifa linatarajia kufanya mkutanoJumanne kujadili mzozo wa mapigano wa Tigray.
Trump aweka sheria mpya kwa wasafiri kutoka baadhi ya mataifa ya Afrika

Chanzo cha picha, AFP
Raia wa nchi 15 za Afrika watatakiwa kutuma hawala za hadi dola 15,000 (£11,000) ili kuruhusiwa kuingia nchini Marekani, kwa mujibu wa sheria mpya za zitakazoanza kutekelezwa kuanzia tarehe 24 Disemba.
Mpango wa miezi sita wa majaribio-unaowalenga wale wanaotafuta Viza za matembezi na biashara-zitatumika kama malipo kwa wale watakaokaa zaidi ya vibali vyao vya kuishi nchini humo.
Rais Trump ambaye anaondoka madarakani,ambaye alishindwa katika azma yake ya kugombea muhula wa pili , aliweka masharti ya uhamiaji kama sehemu kuu ya mpango wake wa miaka minne madarakani.
Rais mteule wa Marekani Joe Biden,kutoka chama cha Democrat, ameahidi kubadilisha nyingi kati ya sera za Trump za uhamiaji, lakini mamia ya mabadiliko ya sheria hizo yanaweza kuchukua miezi au miaka kadhaa.
Sheria ya hawala ya Viza inazilenga nchi ambazo raia wake walikuwa na kiwango cha ‘’ kukaa zaidi ya muda wa unaokubalika’’ cha 10% au cha juu zaidi mwaka 2019 na sasa watatakiwa kulipa hawala ya dola 5,000, 10,000 au milioni 15,000 ambazo wanaweza kurudishiwa..
Huku nchi hizo zikiwa na viwango vya juu vya kuishi zaidi ya muda, raia wake wanaosafiri kwenda Marekani ni wachache, linasema Shirika la habari la Reuters.
Nchi za Afrika zinazoathriwa na sheria hii mpya ya Trump ni pamoja na: Angola, Burkina Faso, Chad, Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Djibouti, Eritrea, Gambia, Guinea-Bissau, Liberia, Libya, Mauritania, Sudan, Sao Tome na Principe, Cape Verde, na Burundi.
Mbwa kutumia kuwatambua wenye mambukizi ya corona Rwanda
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Yves Bucyana
- Nafasi, BBC Swahili

Chanzo cha picha, @RBCRwanda
Rwanda na Ujerumani wamesaini makubaliano ya ushirikiano katika mradi wa kutumia mbwa kuwatambua walioambukia virusi vya Corona.
Makubaliano hayo yamesainiwa kati ya Balozi wa Rwanda nchini Ujerumani Dkt Thomas Kurz na Mkuu wa kituo cha kitaifa cha utambuzi wa utambulisha wa watu (RBC) Dkt Nzanimana Sabin.

Mradi huo uliopewa jina la ‘’ utambuaji wa harufu’’ (scent Identification) utawahusisha mbwa waliopewa mafunzo maalum ya utambuzi wa watu wenye maambukizi ya Covid -19 na hivyo kuharakisha juhudi za kuzuwia usambaaji zaidi wa virusi vya corona.
Elon Musk ampiku Bill Gates na kuwa mtu wa pili tajiri zaidi duniani

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Utajiri wa Elon Musk, umetoana na kupanda kwa bei ya hisa za kampuni yake Baada ya kumpiku Mkurugenzi mkuu na muasisi wa Facebook, Mark Zuckerberg katika orodha ya watu tajiri zaidi duniani — Mkurugenzi mkuu waTesla CEO bilionea Elon Musk sasa amempitaBill Gates na kuchukua nafasi ya pili miongoni mwa watu tajiri zaidi duniani.
Utajiri wa jumla wa Musk umepanda na kufikia hadi ya dola bilioni 7.2mwezi Novemba 23 , kutokana na bei ya hisa za kampuni yake ya magari ya umeme-Tesla, kwa mujibu wa makadirio Bloomberg ya kiwango cha utajiri . Utajiri wa Elon Musk kwa sasa dola bilioni 127.9
Hii ni moja ya faida ya utajiri miongoni mwa watu 500 matajiri zaidi duniani .
Musk aliongeza zaidi ya dola bilioni100.3 juu ya utajiri aliokuwa nao mwaka huu.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Elon Musk (kushoto) sasa ndiye anayechukua nafasi ya pili ya mtu tajiri zaidi akimfuata Jeff Bezos (kulia) Mwezi Januari mwaka 2020, alikuwa nambari 35 katika orodha ya matajiri duniani , lakini kuongezeka kwa bei ya hisa za kampuni yake ya Tesla kumemfanya awapite mabilionea wengine duniani. Kupanda kwa utajiri wa Musk kunakuja huku soko la hisa za magari ya umeme -Tesla zikiongezeka na kufikia karibu milioni 500 Jumatatu.
Hii ni mara ya pili katika historia ya orodha ya mabilionea ya Bloomberg ambapo Bill Gates ameshuka chini ya namba mbili.
Gates alishikilia nafasi ya kwanza kabla ya nafasi hiyo kunyakuliwa na muasisi wa kampuni ya mauzo ya mtandanoni, Amazon, Jeff Bezos mwaka 2017.

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Utajiri wa Bill Gates umepungua baada ya kuutumia kwa shughuli za misaada Bill Gates kwa sasa ana jumla ya utajiri wa thamani yadola bilioni 127.7, na angekuwa wa kwanza asingetoa msaada kwa mashirika ya misaada ya kiutu kwa miaka mingi. Gates ametoa msaada wa zaidi ya dola bilioni 27 kupitia Wakfu wa Bill & Melinda Gates, tangu mwaka 2006, kwa mujibu wa Bloomberg.
Si Musk peke yake aliyeongeza utajiri. Mwaka huu umekuwa wa neema kwa matajiri zaidi duniani licha ya janga la corona kukwamisha biashara nyingi.
Unaweza pia kusoma:
Ni kwanini wakazi eneo la Kunduchi Mtongani Tanzania wanashauriwa wahame?

Maelezo ya picha, Athari za hali ya kijiolojia inayofahamika kitaalamu kama liquefaction nchini Indonesia Wakazi wa Kunduchi Mtongani Jijini Dar es Salaam wameshauriwa kuhama maeneo yao baada ya kutokea kwa hali ya kijiolojia inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama 'Liquefaction'.
Akizungumza na BBC mtaalamu wa jiolojia nchini Tanzania, Gabriel Mbogoni amesema hali hii hutokana na mabadiliko ya jiolojia ambayo mara nyingi hutokea sehemu ambayo kuna mchanga au udongo ambao haujajishindilia vyema na hivyo kunakuwa na sehemu za wazi katika udongo ambazo huchanganyikana na maji na hivyo kutengeneza tope linalojitokeza juu ya ardhi.

Maelezo ya picha, Nchini Indonesia Liquefaction ilihamisha eneo lote la kijiji Kwa kawaida udongo huwa na chembechembe, lakini katika eneo kama la Kunduchi Mtongani chembechembe za udongo huacha nafasi ambazo hujazwa na maji na hivyo kuifanya ardhi kutokuwa thabiti kuweza kuhimili uzito wa vitu kama majengo ya nyumba, na shughuli mbalimbali za binadamu na wanyama, anasema Bw Gabriel Mbogoni.
Aidha anasema kutokana na hali hii ya kijiolojia maeneo kama Kunduchi Mtongani yana uwezekano mkubwa wa kupata matetemeko ya ardhi na hivyo kuhatarisha nyumba zilizojengwa katika ardhi ambayo sio imara.
‘’ Wakazi wa maeneo haya wanashauriwa kuondoka mahali hapo kwasababu ardhi ya hapo kutoweza kuhimili uzito wa majengo’’, amesema Bw Mbogoni.
Jumapili Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw Aboubakar Kunenge aliwaelekeza baadhi ya Wakazi wa eneo la Kunduchi Mtongani ambao nyumba zao zimepitiwa na uji uji wa tope linalofuka kutoka ardhini , hivyo kuhama mara moja ili kujikinga na maafa wakati Serikali inaendelea kufanya utafiti wa kujua ukubwa wa eneo lililoathirika ndio jambo muhimu.
Bunge la Uingereza laidhinisha vikwazo dhidi maafisa wa Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Maandamano ya kupinga ukatili wa polisi nchini Nigeria yalisababisha vuguvugu kubwa la kijamii Bunge la Uingereza limepiga kura ya kuunga mkono uwezekano wa serikali wa kuwawekea vkwazo maafisa wa Nigeria waliohusika katika madai ya matumizi ya nguvu dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani mwezi uliopita ya kupinga ukatili wa polisi.
Kura hiyo ilikuwa ni matokeo ya ombi lililoletwa mbele ya bunge la Uingereza ambalo lilisainiwa na watu zaidi ya 220,000.
Maafisa nchini Nigeria wameendelea kukanusha kwamba vikosi vya usalama viliwafyatulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiandamana kwa amani.
Wabunge wa Uingereza walisema kuwa vikwazo dhidi ya Nigeria vinaweza kuumiza umma wa Wanigeria.
Kwahiyo walitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kuhusiana na unyanyasaji na wakaitaka serikali ya Uingereza kuwalenga maafisa waliohusika katika ufyatuaji wa risasi dhidi ya waandamanaji katika maandamano ya mwezi uliopita dhidi ya ukatili wa polisi.
Wabunge walirejelea mara kwa mara madai ya matumizi ya nguvu ya polisi dhidi ya waandamanaji katika eneo la Lekki tollgate mjini Lagos.
Pia walilaani kitendo cha kufuja akaunti za benki za waandalizi wa maandamano ya amani ambayo yalikuwa ni muhimu kwa demokrasia.
Baadhi ya wabunge walihoji nafasi ya Uingereza katika kutoa mafunzo kwa vikosi vya Nigeria na silaha kwa kwa nchi hiyo.
Mbunge aliyezungumza kwa niaba ya waziri wa Uingereza wa masuala ya Afrika aliafiki uamuzi wa Nigeria wa kuchunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu na kuvunjwa kwa kikosi tata cha polisi- cha kukabiliana na ujambazi.
Lakini bila utelezwaji wa wazo la kuweka vikwazo Wabunge walisema Uingereza itaendelea kushinikiza serikali ya Nigeria kuheshimu haki za binadamu.
Chanjo ya corana kuuzwa kwa bei nafuu kwa nchi masikini

Chanzo cha picha, Getty Images
Shirika la Unicef limetangaza kuhusu mkakati wake wa kusambaza chanjo ya Covid-19 kwa Kenya na nchi nyingine zinazoendelea, limeripoti gazeti la daily Nation nchini Kenya.
Chanjo zote zitakazonunuliwa kupitia Covax zitauzwa kwa shilingi 300 za Kenya (takriban dola 3) kwa nchi zinazoendelea.
Shirika hilo la watoto duniani linasema kuwa limefanya mkataba na zaidi ya ndege 350 na makampuni mengine ya safari za anga kwa ajili ya kusambaza sindano bilioni billion na chanjo.
Takriban sindano milioni 500 za chanjo zitaletwa mwaka ujao. Shirika hilo Jumatatu lilisema kuwa hii itakuwa ni operesheni kubwa na ya haraka ya aina yake kuwahi kufanywa na shirika hilo.
Wataalamu wa Kenya wanatarajia kupokea chanjo za Covid-19 kwa asilimia 20 kwa ajili ya Wakenya. Wahudumu wa afya watakuwa wa kwanza kunufaika kwa kuchanjwa, wakifuatiwa na makundi yaliyomo katika hatari zaidi kama vile wazee.
Likiwa ni mnunuzi mkubwa wa chanjo duniani, Unicef kwa kawaida hununua zaidi ya dozi zaidi ya bilioni mbili kwa mwaka kwa ajili ya chanjo ya kawaida na kwa ajili ya milipuko ya magonjwa kwa niaba ya karibu nusu ya nchi 100.
Jumatatu, Chuo kikuu cha Oxford na Astrazeneca pia walitangaza matokeo ya hatua ya tatu ya uchunguzi wa chanjo zao. Hii ndio chanjo ambayo inafanyiwa majaribio katika eneo la Kilifi, lakini matokeo yaliyotangazwa hayajumuishi data kutoka Kenya.
Hujambo na karibu tena kwa matangazo yetu mubasha leo tarehe 24.11.2020
