Undertaker ajiuzulu mieleka

Mchezaji maarufu wa mchezo wa mieleka- Undertaker amethibitisha rasmi kujiuzulu kutoka WWE baada ya miaka 30.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho.

  2. Jaribio laonesha chanjo Oxford ina ufanisi wa juu

    Chanjo ya  Oxford/AstraZeneca sasa imefikia hatua ya mwisho ya vipimo

    Chanzo cha picha, OXFORD UNIVERSITY/JOHN CAIRNS

    Maelezo ya picha, Chanjo ya Oxford/AstraZeneca sasa imefikia hatua ya mwisho ya vipimo

    Chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford ina ufanisi wa hali ya juu katika kuzuia watu dalili za Covid-19, majaribio ya chanjo hiyo yanaonesha.

    Data zilizopatikana zinaonesha kuwa chanjo hiyo ina kinga ya 70%, lakini watafiti wanasema kiwango hicho kinaweza kuwa zaidi 90% kwa kubadilisha kidogo dozi.

    Matokeo hayo yataonekana kama ushindi, lakini yanakuja baada ya chanjo za Pfizer na Moderna kuonesha uwezo wa kinga kwa asilimia 95%.

    Hatahivyo, chanjo hiyo ni ya garama ya chini zaidi, na ni rahisi kuitunza, na inaweza kusambazwa katika kila kona ya dunia kuliko Pfizer na Moderna.

    Kwa hivyo chanjo hiyo itakuwa na fursa kubwa katika kukabiliana na janga la corona, iwapo itaidhinishwa na wasimamizi wa viwango.

  3. Ni nani anayepigania kujitenga kwa Tigrey na Ethiopia?

    Debretsion Gebremichael,

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Debretsion Gebremichael

    Mbabe wa kivita wa zamani ambaye alikuwa akivuruga mtandao wa mawasiliano ya majeshi ya Ethiopia Debretsion Gebremichael sasa anaongoza mapigano dhidi ya serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kudhibiti eneo la kaskazini la Tigray, linalotajwa kama "uzao" wa nchi . Bonyeza hapa kupata taarifa zaidi:

  4. Biden amteua waziri wa mambo ya nje

    Anthony Blinken

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Duru za kisiasa nchini Marekani zimeripoti kuwa rais mteule wa Marekani Joe Biden amemteua Anthony Blinken kuwa Waziri wa mamno ya nje, atakapochukua kiti cha urais rasmi.

    Bw. Blinken ana uhusiano wa karibu na Bw Biden kwa takriban miaka 20 na ana uzoefu wa masuala ya kigeni.

    Anafahamika kama mtu anayeunga mkono ushirika dhabiti na mataifa mengi, akisema mapema mwaka huu kwamba matatizo kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, janga la corona na utengenezaji wa silaha hatari hayawezi kutatuliwa na Marekani peke yake.

    Wakati mmoja aliwahi kuwa Naibu waziri wa mambo ya nje chini ya utawala wa rais wa zamani Barack Obama ambapo alisaidia kuboresha masuala ya ushirikiano na mataifa yaMashariki ya kati.

    Bw Bilken, mwenye umri wa miaka 58, alisomea Ufaransa, na baadaye katika Chuo Kikuu cha Harvard University na Cho Kikuu cha Sheria cha Colombia.

  5. Jaji kuwasilisha malalamiko ya uhalifu dhidi ya Zuma

    Jacob Zuma alilazimishwa kujiuzulu mwaka2018 baada ya kukumbwa na madai ya ufisadi

    Chanzo cha picha, G

    Maelezo ya picha, Jacob Zuma alilazimishwa kujiuzulu mwaka 2018 baada ya kukumbwa na madai ya ufisadi

    Jaji anayeongoza uchunguzi wa ufisadi nchini Afrika Kusini amesema kuwa malalamiko ya ufisadi yatawasilishwa dhidi ya Rais Jacob Zuma baada ya kuondoka nje ya kikao cha kamati kilichokuwa kikifanya uchunguzi dhidi yake.

    Bw Zuma alijaribu kuhakikisha Naibu Jaji Raymond Zoro anaondolewa katika uchunguzi huo, akimtuhumu kuwa na upendeleo.

    Lakini wakati lengo lake lilipogonga mwamba, rais huyo wa zamani na wakili wake hawakurejea tena mbele ya kikao hicho kukabiliana na maswali kuhusu ufisadi.

    Takriban mashahidi 34 wamemshutumu kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja Bwa Zuma. Alikana kufanya kosa lolote lile.

    Kamati, ambayo imekuwa ikisikiliza ushahidi tangu mwaka 2018, imesema kuwa iliwasiliana mara moja na Mahakama ya juu zaidi ya Afrika Kusini, Mahakama ya Katiba, katika juhudi za kumlazimisha Bw Zuma aitikie wito wa kuhojiwa.

  6. Idadi ya watu waliokufa katika maandamano Uganda wafikia 45

    Maandamano Uganda

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi nchini Uganda imesema kuwa idadi ya vifo vilivyotokea katika maandamano ya wiki iliyopita imeongezeka na kufikia watu 45.

    Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumatatu, msemaji wa polisi Fred Enanga, amesema waliokufa ni wanaume 39 na wanawake sita.

    Chombo kimoja cha habari nchini humo kimevinukuu vyanzo vya usalama vikisema kuwa ufyatuaji mkubwa wa risasi ulifanywa na watu ambao hawakuwa wamevaa sare, ambao walirekodiwa na umma wakinadi bunduki kwenye mitaa.

    Waandamanaji walikuwa wakidai kuachiliwa huru kwa Bobi Wine
    Maelezo ya picha, Waandamanaji walikuwa wakidai kuachiliwa huru kwa Bobi Wine

    Waziri wa usalama nchini humo Jenerali Elly Tumwiine aliwaambia waandishi wa habari Ijumaa kuwa polisi na vikosi vingine vya usalama wana haki ya kufyatua risasi na kuua. Kama waandamanaji "wanafikia kiwango fulani cha ghasia ."

    Polisi ilisema kuwa maafisa wa polisi 11 walishambuliwa na kujeruhiwa na waandamanaji.

    Maandamano yaliibuka katika maeneo mbalimbali katika mji mkuu Kampala, huku waandamanaji wakitoa wito wa kuachiliwa huru kwa mgombea wa urais Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ambaye alikuwa amekamatwa katika mkutano wa kampeni.

    Baada ya kushikiliwa kwa siku mbili mahabusu, alishitakiwa kwa kukiuka sheria za kudhibiti virusi vya corona, na kupewa dhamana. Kwa sasa amerejea katika msururu wa kampeni.

  7. Watoto wa shule waliolaghaiwa Kenya wapewa ushauri nasaha

    Polisi  wa Kenya

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mzazi mmoja wa kati ya watoto 44 waliokamatwa na maafisa wa upelelezi katika nyumba moja usiku, baada ya kulaghaiwa ameiambia BBC kuwa wanapewa ushauri nasaha.

    Mwishoni mwa juma wapelelezi kutoka idara ya upelelezi wa makosa ya jinai nchini Kenya (DCI) waliwakamata watoto hao wa shule 44 na mwenyeji wao , na kukamata aina tofauti za vileo na bangi katika nyumba iliyopo jijini Nairobi.

    Watoto hao wavulana 26 na wasichana 18 –wana umri kati ya miaka 14 na 17.

    Mzazi huyo amesema ushauri huo nasaha unatolewa kwa wiki nzima kwa wazazi na watoto kwa pamoja, na wameshauriwa wasiwakaripie wala kuwapiga watoto wao.

    Ameongeza kuwa watoto hao wanafanyiwa vipimo vya kimatibabu, ikiwa ni pamoja na kuchunguzwa iwapo walidhalilishwa kingono.

    Hii inaendelea huku uchunguzi ukiendelea Idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI nchini Kenya, ikiendelea na uchunguzi kuhusu "genge la mtandaoni" ambalo linalenga wasichana wa shule waliokwama majumbani kwa sababu ya virusi vya corona na kuwashawishi katika kile maafisa wanakielezea ni kuwadanganya na kuwapotosha kimaadili.

    Kulingana na DCI watakao patikana na hatia ya kuwalaghai watoto hao wanakabiliwa na kifungo cha miaka isiyo chini ya miaka saba.

  8. Wanafunzi wa kidato cha nne Tanzania waanza mtihani

    Wanafunzi wa kidato cha nne Tanzania waanza mtihani leo

    Jumla ya wanafunzi 490,103 ndio waliotarajiwa kufanya mtihani kuo wa kumaliza awamu ya kwanza ya elimu ya sekondari, huku watakaofaulu vyema wakitarajiwa kuendelea hadi kidato cha sita kabla ya kujiunga na vyuo vikuu.

    Kulingana na ratiba ya mtihani huo leo wanafanya mtihani wa Kiswahili na Geografia:

    Mwaka huu kuna ongezeko la 0.9% ikilinganisha na waliofanya mtihani huo 2019 Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum ni 893.

    Mtihani huu unafanyika baada ya Baraza la Mitihani nchini Tanzania (NECTA) kutangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba.

  9. Uganda itawaruhusu raia wake kusafiri Tanzania

    KMPALA COUCH

    Wafanyabiashara, wanafunzi na wasafiri wengine wanaovuka mpaka kutoka Uganda kuelekea Tanzania sasa wanaweza kusafiri kwa mabasi kama kawaida, limeripoti gazeti la Daily Monitor Uganda

    Wafanyabiashara, wanafunzi na wasafiri wengine wanaovuka mpaka kutoka Uganda kuelekea Tanzania sasa wanaweza kusafiri kwa mabasi kama kawaida.

    Usafiri wa basi ulikuwa umepigwa marufuku tangu mwezi Machi wakati serikali ya nchi hiyo ilipofunga mipaka yake na kupiga marufuku safari za umma ili kukabiliana na Covid-19, ambapo hadi sasa umekwisha wauwa watu zaidi ya140 nchini humo.

    Wasafiri wanaoingia nchini Uganda hupitia mpaka wa Mutukula kwa kutumia mabasi yanayopita katika nchi za Tanzania, Burundi, Rwanda na Zambia.

  10. Ethiopia yatakiwa 'kuwaepusha rais wa Tigray na madhara'

    Shirika la kutetea haki za binadamu -Rights group Human Rights Watch (HRW), limeitaka Ethiopia kuwalinda raia wanaoishi katika mji mkuu wa jimbo la Tigray, Mekelle, huku vikosi vya serikali vikisonga mbele kuelekea katika mji huo.

    Waziri wa Ethiopia Mkuu Abiy Ahmed Jumapili alivipa vikosi vya Tigray muda wa saa 72 viwe vimejisalimisha lakini vikosi hivyo – Tigray People's Liberation Front (TPLF), ambavyo vinalidhibiti jimbo hilo lililoko katika maeneo ya milima, vimeapa kuendelea na mapigano.

    Mkurugenzi mkuu wa Human Rights Watch, Kenneth Roth, ametuma tweet akisema wanajeshi wa Ethiopia "wanapaswa kuwaepusha na mathara watu wote hata wale wanaoishi katika mji wa Mekelle, lisitishie tu kwamba 'hakutakuwa na huruma'".

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Awali jeshi la Ethiopia liliwaonya wakazi wa Mekelle 500,000 kwamba jeshi lita "zingira " mji wao na kuushambulia kwa makombora.

    Mzozo huo unaripotiwa kuwaua mamia ya wa watu na kuwasambaratisha maelfu wengine katika wiki za hivi karibuni. Umoja wa Mataifa umeonya kuwa unaweza kusababisha mzozo wa kibinadamu.

  11. Mchezaji mashuhuri wa mcheza mieleka Undertaker ajiuzulu

    Undertaker

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mchezaji maarufu wa mchezo wa mieleka- Undertaker amethibitisha rasmi kujiuzulu kutoka WWE baada ya miaka 30.

    Aliingia ulingoni kwa mchezo wa mwisho katika mchezo wa mwisho wa Survivor Series Jumapili usiku, ambapo aliuhutubia umma wa mashabiki wa WWE Universe kwa mara ya mwisho.

    Undertaker

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wakati wa hotuba yake, Undertaker ambaye jina lake halisi ni Mark Calaway –alieleza ni kwanini ameamua kujiuzulu.

    "Kwa miaka 30 nimekuwa nikiingia ndani ya ulingo huu taratibu na kuwaangusha watu mara kwa mara," alisema.

    "Sasa wangu muda umefika. Muda wangu umefika wa kumuacha Undertaker apumzike... kwa ... amani."

    undertaker

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Calaway anajiuzulu akiwa ndiye mchezaji bora wa WWE kuwahi kushuhudiwa katika mashindano hayo na amekuwa ulingoni kwa miongo mitatu na atakumbukwa na mashapiki wake daima.

  12. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatatu tarehe 23.11.2020