Aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, kwa tiketi ya Chadema, Lazaro Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga.
Moja kwa moja
Lizzy Masinga
Mchezaji wa zamani mashuhuri wa soka Samuel Eto'o anusurika kwenye ajali ya gari
Chanzo cha picha, Getty Images
Mshindi mara nne wa tuzo ya mchezaji bora AfrikaSamuel Eto’o amenusurika katika ajali siku ya
Jumapili wakati akielekea mji wa kibiashara nchini Cameroon wa Douala, kwa
mujibu wa wanafamilia wake.
Alikuwa akirejea
kutoka mji wa Bafoussam, Magharibi mwa Cameroon, ambako alihudhuria tamasha
mwishoni mwa juma.
Dereva alisema kuwa
alishindwa kulidhibiti gari na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa kwenye
msafara wa Eto’o.
Msemaji wake
alizungumza na BBC idhaa ya Pidgin kuwa anaendelea vizuri na kuwa gari lake
liliharibika.
Alikataa kujibu maswali zaidi.
Kampeni kuelekea uchaguzi Uganda zaanza
Chanzo cha picha, Getty Images
Kampeni za kuelekea uchaguzi kumpata rais ajaye zimeanza nchini
Uganda.
Wagombea 11 akiwemo rais aliyekaa madarakani kwa muda mrefu,
Yoweri Museveni ambaye atawania tena nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika
katika kipindi cha miezi miwili.
Masharti makali ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona
vimewekwa kwenye kampeni, lakini utekelezaji wake umekuwa mgumu.
Rais Museveni
ameanza kampeni katika eneo liitwalo Luweero triangle, eneo ambalo lilikuwa
kitovu cha vita vya msituni vya miaka mitano vilivyomuweka madarakani mwaka
1986.
Mwanamuziki ambaye
sasa ni mwanasiasa Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine yuko njiano kuelekea mji
wa West Nile, kuanza kampeni siku ya Jumanne.
Polisi mji wa Mashariki wa Jinja umewatawanya wafuasi wa chama
cha Forum for Democratic Change(FDC) cha mgombea Patrick Amuriat Oboi kwa
kutumia vitoa machozi. Walikusanyika njiani kumshangilia akielekea eneo la
Mashariki kuanza kampeni yake.
Masharti ya afya
wakati huu wa kampeni yanawataka wanasiasa kuepuka mikusanyiko mikubwa kwa kuwa
na mkutano wa watu wasiozidi 70.
Lakini suala hili
limeonekana kuwa gumu kama ilivyoshuhudiwa wakati wa uteuzi juma lililopita,
wakati wafuasi wa karibu wagombea wote walipokusanyika kwa wingi kwenye mitaa
mbalimbali na kwenye vituo vya biashara.
Kinyang’anyiro cha
urais pia kinawahusisha majenerali wawili wa jeshi na mhitimu wa Chuo kikuu
mwenye miaka 24 ambaye hana ajira.
Raia wa Uganda watapiga kura kuchagua rais na wawakilishi tarehe
14 mwezi Januari.
Lazaro Nyalandu azuiwa kuvuka mpaka wa Namanga
Aliyekuwa
mgombea ubunge jimbo la Singida Kaskazini, kwa tiketi ya Chadema, Lazaro
Nyalandu amezuiwa kutoka nchini kupitia mpaka wa Tanzania na Kenya wa Namanga
baada ya kukosa nyaraka muhimu.
Kwa
mujibu wa gazeti la Mwananchi Mkuu wa Wilaya Longido, Frank Mwaisumbe amesema
mwanasiasa huyo alikuwa akitaka kuondoka nchini humo lakini hakuwa na nyaraka zinazohitajika.
"Ni
kweli maofisa wa uhamiaji mpakani wamemzuia kutoka nchini, kwani alikuwa hana
nyaraka kadhaa ikiwamo za gari na vitu vingine ambavyo alikuwa anaondoka
navyo,"Mwananchi lilimnukuu Mkuu huyo wa Wilaya.
Amesema
kwa sasa vitu alivyotaka kuvuka navyo bado vinashikiliwa mpaka wa Namanga na
ametakiwa kuwasilisha nyaraka zake.
"Tumemtaka
alete nyaraka muhimu zinazohitajika na tumemuachia akalete, lakini akishindwa
atafikishwa mahakamani,"alilieleza gazeti la Mwananchi.
Vijana wa Nigeria watishia kufanya maandamano mapya
Chanzo cha picha, EPA
Ripoti za kuwepo kwa maandamano mapya nchini Nigeria
zimechapishwa na vyombo vya habari vya nchini humo.
Vitisho hivyo vya maandamano mapya dhidi ya ukatili wa polisi
vimejitokeza baada ya mahakama kutoa amri kuipa haki mamlaka Benki Kuu ya Nigeria
kuzuia akaunti za watu 19 na kampuni zilizohusishwa na maandamano ya #EndSARS.
Makundi tofauti,
ikiwemo ya haki ya kiislamu (Muric), wamewataka watu wasishiriki kwenye
maandamano mapya.
Serikali ya Lagos
pia imetahadharisha wakazi wake kutoshiriki maandamano.
Jopo liliundwa kuchunguza matukio ya ukatili wa polisi limekuwa
likiwasikiliza waathirika.
Polisi imetoa tahadhari kuwa hairuhusu maandamano nchini humo.
Mchekeshaji Elsa Majimbo ashinda tuzo za watu za E!
Chanzo cha picha, Elsa Twitter
Mchekeshaji wa Kenya Elsa Majimbo amewapiku wasanii kutoka
nchi mbali mbali Afrika na kupata ushindi katika tuzo za E! people’s kipengele cha Nyota wa mitandao ya kijamii Afrika.
Mwanadada huyo machachari alikuwa akiwania kipengele hicho
na watu saba akiwemo msanii nyota wa Afrika Kusini Sho Madjozi huku wengine ni Karl Kugelmann, Dimma Umeh, Wian,
Lydia Forson, Thuso Mbedu na Zozi Tunzi.
Tuzo hizo ambazo hufanyika nchini Marekani mwaka huu
zilifanyika kupitia mkutano wa Video utokana na janga la virusi corona.
Godbless Lema akamatwa baada ya kukimbilia Kenya
Chanzo cha picha, Getty Images
Bw. Lema alikamatwa wakati akiendeshwa na
mwanasheria wake katika mji mkuu wa nchi hiyo, Nairobi.
Alikuwa amefuatana na mke wake na watoto.
Polisi wa Kenya waliwakamata katika eneo karibu kilometa 45 (maili 28) kutoka mpakani baada ya kutahadharishwa na wenzao wa Tanzania, gazeti la Standard linaripoti.
Mbunge huyo wa zamani anaripotiwa kukataa
kutoa pasi yake ya kusafiria kwa maafisa wa uhamiaji wa Tanzania.
Mwanasheria, George Luchiri Wajackoyah, alinukuliwa na gazeti akisema
alitaka kumpeleka mwanasiasa huyo kwenye ofisi ya tume ya haki za binadamu
ya Umoja wa Mataifa (UNHCR).
‘’Sasa hivi , niko na mke wanguNeema, mtoto wangu wa kiume mwenye miaka 14 Allbless,
Brilliance( binti) kitindamimba wangu Terrence. Sijui kesho yetu itakuwaje. Sasa
ninatafuta hifadhi,’’ Bwana Lema alinukuliwa na gazeti hilo akisema
Bw. Lema alikuwa
miongoni mwa viongozi watatu walioachiwa juma lililopita baada baada ya
kuitisha maandamano kutaka kufanyika upya kwa uchaguzi.
Kiongozi wa Tigray aitaka AU kuingilia kati mzozo wa Ethiopia
Chanzo cha picha, Getty Images
Kiongozi wa jimbo la Tigray Kaskazini mwa Ethiopia ametoa wito kwa Umoja wa Afrika kuingilia kati mgogoro nchini humo usifikie hatua ya kuingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika taarifa aliyoitoa kwa njia ya televisheni, Debretsion Gebremichael alisema Tigray itaendelea kujitetea mpaka pale serikali itakapokubali kufanya mazungumzo.
Lakini Waziri Mkuu wa Ethiopia , Abiy Ahmed, amesema kuwa vitendo vya viongozi wa Tigray vilivyovuka mpaka vimemfanya achukua hatua za kijeshi.
Ripoti kutoka mji jirani wa Amhara zinasema wanajeshi 100 wa serikali walikuwa wakipatiwa tiba ya majeraha.
Awali, Bwana Abiy bila kutoa maelezo amewafuta kazi mkuu wa jeshi, mkuu wa idara ya Intelijensia na waziri wa mambo ya nje
Mkuu mpya wa jeshi Berhanu Jula amesema kuwa vikosi vya serikali vimedhibiti miji minne Magharibi mwa Tigray.
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Polisi yawafurusha waandamanaji Georgia
Chanzo cha picha, EPA
Polisi katika mji mkuu wa jimbo la Georgia, Tbilisi, wamewafurusha
makundi ya watu waliokuwa wakiandamana kupinga matokeo ya wabunge katika
uchaguzi wa juma lililopita.
Maelfu
ya watu walikusanyika nje ya jengo la Tume ya uchaguzi kutaka mchakato wa kura
kufanyika upya, baada ya kushutumu chama tawala wa wizi wa kura.
Chama
cha Dream cha Georgia kimekana shutuma za udanganyifu.
Waangalizi
wa kimataifa wamesema “kura zimepigwa kwa kuheshimu uhuru” lakini walikosoa
sehemu ya mchakato
Chama
cha Dream,ambacho kilianzishwa na bilionea Bidzina Ivanishvili , kilichokuwa
madarakanitangu mwaka 2012, kilipata 48%
ya kura kwenye uchaguzi wa tarehe 31 mwezi Oktoba.
Ushindi
huo unakipa chama hicho haki ya kuunda serikali ijayo.
Lakini
maelfu ya waandamanaji walioandamana Tbilisi walikataa matokeo na kutaka ,mkuu
wa polisi na wa tume kujiuzulu.
Habari! karibu katika matangazo ya moja kwa moja Jumatatu 09.11.2020