Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020: Biden aongoza Pennsylvania na Georgia kwa mara ya kwanza
Mgombea wa chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais wa Marekani Joe Biden amechukua uongozi wa jimbo hilo kwa mara ya kwanza.
Moja kwa moja
Asha Juma
Habari za hivi punde, Jimbo la Georgia kurudia hesabu ya kura za urais
Waziri wa
masuala ya kigeni katika jimbo la Georgia Brad Raffensberger ametangaza kwamba
jimbo hilo litahesabu upya kura zake za urais.
Anasema kwamba kura 4169 hazijahesabiwa na kwamba kura 8000
za wanajeshi bado zimo katika barua na kwamba sitahesabiwa zitakapowasili
mwisho wa siku.
Joe Biden achukua uongozi wa jimbo la Pennsylvania
Sio muda mrefu sasa, usiku kucha , Joe Biden amempiku Donald
Trump katika mji wa Georgia .
Na huku matokeo ya kura yakitolewa, Biden amechukua
uongozi dhidi ya Trump katika jimbo la Pennsylvania.
Georgia yenye wajumbe 16 inatosha kumfanya Biden kupata
matokeo sawa na Trump katika idadi ya wajumbe, huku akisubiri matokeo maengine kutoka majimbo mengine.
Pennsylvania itamfanya Biden kuingia katika Ikulu ya
Whitehouse.
habari zetu mubashara zinaendelea
Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020:Itakuwaje ikiwa wagombea urais watapata kura sawa za wajumbe?
Chanzo cha picha, EPA
Kura za wajumbe zikiwa
538 ni nadra sana wagombea kupata kura sawa yaani 269.
Hata hivyo ni jambo
linaloweza kutokea.
Ikiwa ni iwe hivyo,
Donald Trump atahitajika kushinda katika majimbo ya Arizona, North Carolina,
Nevada na Pennsylvania, lakini ashindwe katika jimbo la Georgia.
Ikiwa hivyo, kipi kitatokea?
Ikiwa hakuna mgombea kati yao aliyepata wingi wa kura
za wajumbe, Bunge ndio litakaloamua.
Bunge la wawakilishi
litapiga kura kuamua nani atakuwa rais, huku kila wabunge wa jimbo wakiwa na
kura moja.
Ili kupata wingi wa
kura, mgombea atahitajika kupata kura 26.
Naibu rais
atachaguliwa na bunge la Seneti huku maseneta wote 100 wakihitajika kupiga
kura.
Wabunge waliochaguliwa
katika uchaguzi wa 2020 ndio watakaoshiriki mchakato huo – lakini hadi kufikia
sasa kuna baadhi ya majimbo ambayo hayajamaliza kupiga kura.
Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020: Vichwa vya habari Duniani vyajikita katika ‘vurugu za Marekani’
Chanzo cha picha, The Standard
Marekani bado shughuli
ya kuhesabu kura inaendelea, lakini vyombo vya habari vya dunia vinaangazia
hatua za kisheria zilizochukuliwa na Donald Trump na kuendeleza mjadala wa
vurugu zinazokumba shughuli ya kuhesabu kura.
Tuanze na nchini Kenya
ambapo gazeti la The Standard kichwa chake cha habari kinasoma "Vurugu
hadi mwisho".
Gazeti la Punch nchini
Nigeria liliangazia taarifa yenye kichwa "wasiwasi na mvutano" Marekani.
Gazeti la China la
Global Times limesema kura zinazoendelea kuhesabiwa zimesababisha "mgawanyiko,
ghasia na machungu makali" nchini Marekani. China, inasema
uchaguzi huo umekuwa kama "burudani", "jamii iliyokumbwa na
ghasia", gazeti hilo limeongeza.
Kwengineko shirika la habari la Iran limeangazia ghasia
zilizotokea mitaani wakati shughuli ya kuhesabu kura inaendelea katika majimbo
kadhaa. Radio Iran (VIRI) imesema "Sintofahamu iliyokumba matokeo nchini Marekani,
huku ghasia za uchaguzi zikiongezeka".
Nchini Urusi, uchaguzi wa Marekani haukuwa tena gumzo
badala yake vituo vyote vilijikita katika matamshi ya Trump ya wizi wa kura
bila kutaja ushahidi wowote.
Na gazeti la Corriere della Sera nchini Italia limesema
uchaguzi wa mwaka huu ni "mtihani mkubwa sana kwa demokrasia”, na unaoonesha
"uimara na udhaifu wa mfumo wao wa upigaji kura" Marekani.
Habari za hivi punde, Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020:Biden anaongoza Georgia kwa mara ya kwanza
Georgia, moja ya majimbo muhimu ambapo kura bado
zinaendelea kuhesabiwa, wanaofuatilia uchaguzi kwa karibu pamoja na chombo cha habari
cha CNN kimesema kwamba mgombea wa Democrat Joe Biden amechukua uongozi wa
jimbo hilo kwa mara ya kwanza.
Biden anaongoza kwa kura kidogo huku ikisemekana kwamba
asilimia 99 ya kura tayari zimehesabiwa.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 1
Aidha, vyombo vya habari vya eneo pia vinaonesha kwamba
Biden yuko mbele ya Donald Trump kwa zaidi ya kura 900 kulingana na kura zinazohesabiwa
katika kituo cha kaunti ya Clayton.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe, 2
Bwana Trump
hana njia mbili zaidi ya kupata ushindi wa jimbo la Georgia ili aweze kubaki na
mwanya wa kupata ushindi.
Kulingana na
data ya hivi karibuni Bwana Biden anaongoza huku kura nyingi zikiwa zimeshahesabiwa.
Jimbo la Georgia
lina kura za wajumbe 16 , na kushinda jimbo hilo kutafanya Bwana Biden kusalia
na kura moja pekee ya kumuwezesha kufikia kura 270 za wajumbe zinazohitajika
ili aweze kupata ushindi.
Ikiwa Bwana
Trump atashindwa kupata ushindi wa jimbo la Georgia, kura za wajumbe ambazo
anaweza kupata itakuwa ni 269 ikimaanisha kwamba hatakuwa amefikisha idadi ya
kura zinazohitajika.
Watani wa jadi Yanga na Simba kumaliza ubishi kesho
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Eagan Salla
Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam
Chanzo cha picha, Simba Sports Club
Ni mchezo
unaovuta hisia za mashabiki wengi wa soka Tanzania na kwingineko duniani
kutokana na ukubwa wa vilabu hivi viwili nchini Tanzania.
Wawili hao
wamekuwa wakitambiana kila mmoja akijivunia ubora wa kikosi chake msimu huu
mara ya mwisho simba ili iliigaragaza Yanga 4 – 1 kwenye mchezo wa nusu fainali wa
kombe la ligi (Azam Federation Cup).
Mara hii Yanga ikiwa chini ya kocha Mrundi
Cedric Kaze watakuwa nyumbani kwenye dimba la Mkapa jijini Dar es salaam
kuiakaribisha Simba inayonolewa na kocha Mbelgiji Sven Vandenbroeck.
Chanzo cha picha, Yanga sports club
Kaze ameshaiongoza Yanga kwenye michezo minne na kati yake ameshinda mitatu na kutoa suluhu mmoja huku Scven yeye amekuwa na Simba toka msimu uliopita.
Yanga wamezoeleka kucheza mpira ya pasi ndefu na kasi huku Simba wao wakipiga pasi nyingi mpaka golini, kwenye mchezo wa kesho Yanga wanaingia wakivunia kuwa na ukuta imara zaidi wakiwa hawajafungwa mchezo hata mmoja msimu huu huku wakiwa wameruhusu magoli mawili tu.
Chanzo cha picha, Simba Sports Club
Simba wao wanaingia kifua mbele wakiwa na safu imara zaidi ya ushambuliaji wakiwa wameshajikisanyia jumla ya magoli 21 mpaka sasa huku watani wao wakiwa na magoli 11 tu.
Mchezo wa kesho utachezeshwa na waamuzi sita wawili wakiwa nyuma ya magoli, mtendaji mkuu wa bodi ya ligi Almasi Kasongo alitangaza azma hiyo kutokana na kuwepo kwa malalamiko ya mara kwa mara kutokana na makosa yanayofanya na waamuzi kwenye micheozo ya ligi kuu.
Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020:Kwanini baadhi ya Republicans wangefurahi kumuona Trump akipoteza Urais?
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Profesa wa somo la Sheria katika Chuo Kikuu cha Southampton, Jacob Eisler, ameiambia
BBC Radio 5 Live kwamba kesi zilizowasilishwa na kampeni ya Trump ni
"dhaifu".
Aliongeza kuwa
ana wasiwasi kwamba Trump huenda akang'ang'ania madarakani.
"Kile kinamshinikiza
kufanya hivyo [Trump] ni maslahi yake binafsi," amesema.
"Trump, ana fursa
ya kukabiliana na mtihani huu huku akiendelea kuwa na ushawishi mkubwa katika
chama cha Republican."
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020:'Usalama waimarishwa' kwa Biden
Chanzo cha picha, Getty Images
Usalama umeimarishwa kwa Joe Biden kuanzia Ijumaa
wakati inatarajiwa kuwa huenda akatangazwa kuwa mshindi, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la Washington.
Bwana Biden ataongezewa idadi ya maafisa wa usalama
baada ya timu yake ya kampeni kuiambia idara husika kwamba anaweza akatoa
hotuba muhimu Ijumaa, gazeti hilo limeandika kwa kunukuu watu wenye ufahamu wa mipango
hiyo.
Bwana Biden na timu yake ya kampeni wamekuwa katika
kituo cha Wilmington, Delaware.
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Polisi yachunguza njama za kuvamiwa kwa kituo cha kuhesabiwa kura cha Philadelphia
Polisi huko
Philadelphia inachunguza njama ya kuvamia kituo kikuu cha kuhesabu kura cha Pennsylvania,
ambako kura zinahesabiwa.
Shirika la utangazaji
la ABC News limesema kundi la watu – ambalo huenda likawa familia – lilikuwa kuvamia
kituo hicho kutoka Virginia kwa kutumia gari aina ya Hummer SUV kutekeleza
shambulio hilo.
Polisi wameshika gari
hilo na kumkamata mwanaume mmoja, taarifa hiyo inasema.
Philadelphia sasa hivi
ni moja ya miji michache inayofuatiliwa kwa karibu katika kinyang’anyiro cha
kuingia Ikulu.
Wakati shughuli ya
kuhesabu kura inaendelea, kura zile alizopata Trump katika jimbo hilo ambazo zilionesha
anaongoza kwa kura nyingi zaidi zinazidi kupungua hatua ambayo imefanya timu ya
kampeni yake kutaka shughuli ya kuhesabu kura kusitishwa.
Hata hivyo, licha ya
rais kuchukua hatua za kisheria akitaka shughuli ya kuhesabu kura kusitishwa, kwa kukosa imani na matumaini dhidi ya wafuasi wa Joe Biden katika jimbo hilo imekuwa ambao wameanza hata kusherehekea nje ya kituo kikuu cha kuhesabu kura.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Diamond Platnumz akutana na watoto wake kwa mara ya kwanza tangu 2018
Mwanamuziki maarufu nchini
Tanzania Diamond Platnumz hatimaye amekutana na watoto wake kwa mara ya
kwanza tangu mwaka 2018.
Aliyekuwa mke wake
Zari aliwasili Tanzania Alhamisi usiku pamoja na watoto wao Tiffah na Nillan.
Picha za Video zinazosambaa
kwenye mitandao ya kijamii zinamuonesha Diamond Platnumz akiwalaki watoto wake
wawili.
Baada ya watoto hao kupokelewa, mmoja aliulizwa na wanahabari "umemletea nini
baba na bibi yako?" na kujibu ‘’Pizza’’.
Matokeo ya uchaguzi Marekani 2020: Usalama waimarishwa katika kituo cha kuhesabu kura Nevada
'“Hatutamruhusu yeyote kutuzuia kutekeleza jukumu letu
la kuhesabu kura,” hayo ni maneno ya Joe Gloria, msajili wa eneo la Clark huko
Nevada, amewaambia wanahabari.
Amesema maafisa wa usalama wamepelekwa eneo hilo huku
hatua zingine za kiusalama zikichukuliwa kuhakikisha wafanyakazi wako salama
kuendelea na shughuli ya uhesabuji wa kura.
Lakini pia ameongeza kuwa masanduku ya mwisho ya kura yanayotarajiwa
kuwasilishwa baadae huenda matokeo yakatolewa wiki ijayo kabla ya matokeo
kamili kufahamika.
Joe Biden sasa hivi anaongoza kwa kura kidogo huko
Nevada, na kampeni ya Trump imetishia kuwasilisha kesi ya madai ya udanganyifu mahakamani
ingawa hadi kufikia sasa hakuna ushahidi wowote uliotolewa.
Akijibu madai ya udanganyifu wa kura, Bwana Gloria
alisema: "Hatufahamu lolote kuhusu uhesabu wa kura zisizostahili."