Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi Jumapili

Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii.

Moja kwa moja

Asha Juma and Esther Namuhisa

  1. Rais mteule wa Tanzania 2020-2025

    magu
  2. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania:Tundu Lissu aibuka kuwa mshindi wa pili

    Lissu
  3. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Magufuli kukabidhiwa cheti cha ushindi Jumapili

    mAGUFULI

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii.

    Magufuli mgombea kutoka chama tawala CCM ameshinda kwa kupata kura milioni 12.5 akifuatiwa na Tundu Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura milioni 1.9.

    Jumla ya kura zilizopigwa ni milioni 15.9.

    Waliojiandikisha kupiga kura walikuwa milioni 29.7.

    Rais Magufuli atapewa cheti chake cha ushindi pamoja na mama Samia Suluhu , siku ya Jumapili.

  4. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020:Matukio katika picha

    gett

    Chanzo cha picha, Getty Images

    ccm

    Chanzo cha picha, Getty Images

    uchaguzi
    c

    Chanzo cha picha, Getty Images

    ccm

    Chanzo cha picha, Getty Images

  5. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Wanasiasa maarufu waliopoteza majimbo yao

    hALIMA

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Halima Mdee

    Mwanasiasa na mbunge machachari kwa tiketi ya Chadema, ameangushwa na Mchungaji Josephat Gwajima. Halima Mdee alikuwa mbunge wa viti maalum kwa miaka mitano n mbunge wa kawe kwa miaka 10.

    Mbowe
    Maelezo ya picha, Freeman Mbowe

    Freeman Mbowe

    Mwenyekiti wa chama cha upinzani Chadema ambaye pia alikuwa mbunge wa Jimbo la Hai huko Moshi.

    Freeman Mbowe ameshindwa kutetea kiti chake, baada ya kushindwa kwenye sanduku la kura na mgombea wa CCM, Saashisha Mafuwe.

    Freeman Mbowe amekuwa mbunge wa Chadema kwa miaka 10.

    zitto

    Zitto Kabwe:

    Alikuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo.

    Zitto amekuwa mbunge kwa miaka 15, miaka 10 jimbo la Kigoma Kaskazini, na miaka mitano jimbo la Kigoma mjini ambalo alikuwa akitetea kiti chake.

    Esther Bulaya

    Esther amekuwa mbunge kwa miaka 10, miaka mitano mbunge wa viti maalum na mitano mbunge wa jimbo la Bunda mjini kupitia Chadema.

    mbilinyi

    Joseph Mbilinyi

    Joseph Mbilinyi maarufu Mr.Two au Sugu amekuwa mbunge wa Mbeya mjini kupitia chama cha upinzani cha chadema nchini humo tangu mwaka 2010 mpaka 2020.

    Godbless Lema

    Godbless Lema wa Chadema ameshindwa kutetea jimbo lake la Arusha mjini baada ya kushindwa na mgombea wa CCM, Mrisho Gamba.

    Lema amekuwa mbunge kwa kipindi cha miaka 10.

    J

    Chanzo cha picha, Prof Jay Instagram

    Joseph Haule:

    Msanii wa Bongo Fleva Joseph Haule maarufu Profesa Jay wa chama cha CHADEMA ameshindwa kutetea jimbo la Mikumi, ambalo alikuwa mbunge kwa kipindi cha miaka mitano.

    Mchungaji Peter Msigwa

    Alikuwa akilishikilia jimbo la Iringa mjini ameshindwa kutetea kiti chake cha ubunge kupitia Chadema, alichokuwa amekikalia kwa miaka 10.

    MBATIA

    Chanzo cha picha, HISANI

    James Mbatia

    Aliyekuwa Mbunge wa Vunjo kwa tiketi ya chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia, ameshindwa kuitetea nafasi hiyo.

  6. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: Magufuli amwacha mbali Lissu katika matokeo ya awali

    Magufuli (kushoto) Lissu (kulia)

    Matokeo ya uchaguzi kwa ngazi ya urais yanaendelea kutangazwa nchini Tanzania huku rais aliye madarakani na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiongoza katika matokeo ya awali.

    Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Magufuli anaongoza kwa asilimia 85 katika matokeo ya majimbo 226 yaliyotangazwa matokeo yake na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kufikia sasa.

    Mgombea wa Chama kikuu cha upinzani Chadema Tundu Lissu ana asilimia 12.

    Tanzania ina majimbo 264 ya uchaguzi hivyo bado matokeo ya majimbo 62 tu ili matokeo rasmi yatangazwe.

    Hata hivyo, Lissu ametangaza kutoyakubali matokeo ya uchaguzi wa Jumatano akidai kuwa kulikuwa na udanganyifu pamoja na mawakala wa upizani kuzuiwa kuingia vituoni.

    Lakini madai hayo yametupiliwa mbali na NEC.

  7. Tetemeko kubwa lapiga Ugiriki na Uturuki

    tetemeko

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Tetemeko kubwa la ardhi limetokea Uturuki katika pwani ya Aegean n magharibi mwa fukwe ya Ugiriki ya Samos.

    Tetemeko hilo lilikuwa na ukubwa wa 7.0 lilipiga jimbo la Uturuki la Izmir , Watafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS) wamesema kuwa lilisikika kwa mbali huko Athens na Istanbul.

    Maofisa wa Uturuki wanasema hakuna ripoti ya waliojeruhiwa mpaka sasa lakini majengo sita yameanguka katika mji wa Izmir.

    Uturuki na Ugiriki zinakabiliana na matetemeko ya ardhi mara kwa mara.

    uturuki

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Ripoti ya tetemeko la ardhi liliripotiwa fukwe ya Ugiriki ya Crete.

    Video katika mitandao ya kijamii zinaonyesha jinsi watu wanavyotafuta wenzao katika majengo yaliyoanguka.

    Walioshuhudia tukio hilo mjini Izmir walitawanyika katika mitaa mbalimbali wakati tetemeko hilo lilipopiga.

    uturuki

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwezi Januari mwaka huu, watu 30 waliuawa na wengine 1,600 walijeruhiwa na tetemeko lililopiga Uturuki katika jimbo la Elazig.

    Julai mwaka jana, tetemeko lilipiga katika eneo kubwa la mji wa Athens huko Ugiriki.

    Tetemeko lingine kubwa kupiga Uturuki lilipiga Izmit, karibu na Istanbul, mwaka 1999 na kuua watu 17,000.

  8. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020:'Bwege' au 'Uliskia Wapi' apoteza ubunge

    Selemani Bungala, ambaye ni maarufu kwa jina la Bwege nchini Tanzania ama 'Ulisikia Wapi' nchini Kenya amepoteza kiti chake cha ubunge katika jimbo la Kilwa Kusini.

    Bungala, ambaye amegombea kupitia chama cha ACT Wazalendo amepoteza kiti chake baada ya kupata kura 10,096 dhidi ya mpinzani wake wa CCM Ally Kasinge ambaye amepata kura 22,521.

    Selemani Bungala

    Chanzo cha picha, YOUTUBE

    Bwana Bungala alikuwa maarufu kwenye mitandao ya kijamii kwa matamshi yake ambayo yamebadilishwa kwa kila aina ya utani mitandaoni na hata kutengenezwa vibonzo vya aina yake.

    Video yake iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii alikuwa anajibu madai kwamba amejiunga na chama cha CCM kinachoongozwa na Rais Magufuli.

    “We ulisikia wapi!? We ulisikia wapi!? Mheshimiwa ulisikia wapi!? Niliingia katika Chama Cha ACT nataka muelewe hivo,” Bwana Bungara alisema.

    Siku ya uchaguzi Jumatano, raia wa Kenya walijitokeza na kumtakia kila la kheri Bwana Bungala wakati anagombea ubunge kwa mara ya tatu.

  9. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020:Je majimbo yaliyosalia yanaweza kuukomboa upinzani?

    chadema

    Chanzo cha picha, Mwananchi

    Mpaka sasa matokeo ya uchaguzi nchini Tanzania yanaonyesha kuwa kuna majimbo mawili pekee ndio yamekwenda upinzani.

    Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi, kati ya matokeo ya majimbo 220 yaliyotangazwa ni majimbo 118 chama tawala CCM kimeibuka na ushindi.

    Jimbo la Nkasi Kaskazini limechukuliwa na CHADEMA, baada ya Aida Khenan kupata kura 21,226 na kumshinda Ally Kessy aliyekuwa akitetea kiti chake cha ubunge lakini aliambulia kura 19,972.

    Chama kingine cha upinzani kilichoweza kupata kiti kimoja kufikia sasa ni CUF baada Shemsia Mtamba kuibuka mshindi katika jimbo la Mtwara Vijijini kwa kura 26,215 na kumpiku Hawa Ghasia wa CCM aliyepata kura 18,564.

    Tanzania ina jumla ya majimbo 264 pekee kwa nchi nzima.

    Hivyo ni majimbo 44 tu ndio yamesalia kutangaza majibu yake.

  10. Matokeo ya Uchaguzi Tanzania 2020: John Magufuli aongoza katika matokeo ya awali

    CCM

    Matokeo ya uchaguzi kwa ngazi ya urais yanaendelea kutangazwa nchini Tanzania huku rais aliye madarakani na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) akiongoza katika majimbo yote yaliyotangazwa.

    Matokeo hayo yanatangazwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) Jaji Semistocless Kaijage kutoka katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

    Kwa mujibu wa gazeti la serikali la Daily News, mpaka kufikia saa mbili usiku jana Alhamisi Magufuli alikuwa naongoza kwa asilimia 81 huku Tundu Lissu wa Chadema akifuatia kwa asilimia 15. Matokeo hayo yalikuwa ni kutoka majimbo 94.

    Matokeo bado yanaendelea kutangazwa na kuna dalili kuwa matokeo ya mwisho huenda yakatangazwa ndani ya siku mbili.

  11. Uganda yapiga marufuku kundi la uangalizi wa uchaguzi

    Bobi Wine

    Chanzo cha picha, Getty

    Mamlaka nchini Uganda wamepiga marufuku zaidi ya mashirika 60 yaliyobuniwa kuchunguza uchaguzi mkuu wa mwaka 2021 kwa misingi kwamba sio halali.

    Ofisi ya Kitaifa ya Uganda ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali - ambayo inadhibiti shughuli za mashirika yasiyokuwa ya kiserikali imesema shirika la kitaifa la uangalizi wa uchaguzi halijasajiliwa.

    Ofisi hiyo imesema baadhi ya mashirika chini ya muungano huo hayajasajiliwa wala hayana kibali cha kuhudumu nchini humo

    Mkuu wa ofisi hiyo, Stephen Okello, amesema kundi hilo linatakiwa kusitisha shughuli zake mara moja ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa umma.

    Raia wa Uganda watashiriki uchaguzi mkuu wa urais na ubunge mwezi Januari mwaka 2021.

    Shirika la kimataifa la Action Aid nchini Uganda, katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wake, limesema kundi hilo lilianzishwa mwezi uliopita kukuza uadilifu katika uchaguzi kuongeza imani ya raia na ushiriki.

    Serikali ya Uganda imekuwa ikikosoa mashirika yasiokuwa ya kiserikali kwa kufanya kazi kwa maslahi ya nchi za kigeni kurejelea kazi ya serikali na kuhudumia katika mazingira yasiyoeleweka.

    Mwaka 2017, polisi walivamia ofisi za mashirika matatu ya aina hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli haramu za kifedha na uasi ili kudhoofisha nchi.

  12. Lil Wayne azua tafrani mtandaoni

    Lil Wayne

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Lil Wayne

    Rapa kutoka nchini Marekani Lil Wayne amezua tafrani mtandaoni baada ya kutangaza kuwa amekutana na rais wa Marekani Donald Trump huku akiafikiana na mpango wa Rais huyo unao fahamika Kama "Platinum Plan" unao lenga kuwasaidia wamarekani wenye asili ya Afrika.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    “Nilikuwa na kikao na Trump ukiachana na yale aliyofanya mpaka sasa mpango wake “The plutnum plan” unakwenda kuipa jamii umiliki halali.

    Amesikiliza tulichotaka kusema na ametuhakikishia atatekeleza.”

    Mapokeo ya wafuasi wake hasa nchini Marekani yalikua ni ya kumzomea na kumcheka huku wengine wakimtengenezea vibonzo vya kumdhihaki.

    Pia wapo ambao walihisi ukurasa wake wa twitter umedukuliwa.

    Lil Wayne

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Lil Wayne

    Hata hivyo baadhi ya wafuasi wa Trump wamefurahishwa huku wakiamini ni fursa hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa Marekani.

    Rapa wengine wenye asili ya Afrika walio wahi kumuunga mkono trump ni Kanye West ambaye baadae alibadili mawazo na kuamua kusimama kama mgombea urais nchini Marekani.

    Mwingine ni 50 Cent ambaye pia alibadili mawazo akisema “Sijawahi kumpenda”

  13. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Mtandao waminywa kwa siku ya nne mfululizo

    watumiaji wa simu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, watumiaji wa simu

    Raia wa Tanzania leo wameingia siku ya nne wakiwa bado na changamoto ya kutumia mitandao ya kijamii.

    Mitandao iliyoathirika zaidi ni ya Twitter, WhatsApp, Instagram na YouTube.

    Nembo ya mtandao wa WhatsApp

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Nembo ya mtandao wa WhatsApp

    Siku za nyuma, mashirika kama vile la Netblocks na VPN linalofanya kazi kama mtandao wa kibinafsi wenye uwezo wa kufikia mtandao mwingine binafsi katika mitandao yote ya umma pia ilionesha lililalamikia kuminywa kwa intaneti.

    Tanzania inaingia miongoni mwa nchi nyingine kama vile Ethiopia na Cameroon barani Afrika ambazo zimewahi kuzima mitandao ya kijamii kwa wakati wao wenyewe.

  14. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Hamis Mwijuma 'Mwana FA' awa mbunge mpya

    'Mwana FA'
    Maelezo ya picha, 'Mwana FA'

    Mwanamuziki wa Bongo fleva nchini Tanzania Hamis Mwijuma, maarufu kama Mwana FA, ni mbunge mpya wa jimbo la Muheza,Tanga.

    Mwana FA aligombea ubunge kwa tiketi ya chama cha CCM na kushinda kura 47,578.

    Mpinzani wake Yosepher Komba wa chama cha upinzani Chadema alipata kura 12,034.

  15. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Mdee aangushwa na Gwajima

    chadema

    Chanzo cha picha, The Citizen

    Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kawe Halima Mdee aliyegombea kupitia CHADEMA amepata kura 32,524.

    Hivyo basi, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemtangaza Gwajima mbunge mteule.

    Josephat Gwajima amegombea ubunge kwa chama cha CCM katika Jimbo hilo na kumshinda mpinzani wake kwa kupata kura 194,833.

  16. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: CHADEMA yapata jimbo moja pekee

    Aida Khenani (CHADEMA) ameshinda Ubunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini kwa kupata kura 21,226 akifuatiwa na Ally Keissy wa (CCM) aliyepata kura 19,972.

    Ushindi huo ulithibitishwa na msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo la Nkasi Kaskazini.

    Aida Khenani

    Chanzo cha picha, TBC

    Maelezo ya picha, Aida Khenani
  17. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Hisia za wagombea wengine baada ya Dkt Hussein Mwinyi kutangazwa mshindi

    Dkt Hussein Mwinyi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Dkt Hussein Mwinyi rais mteule wa Zanzibar

    Baada ya Tume ya uchaguzi Zanzibar kumtangaza Dkt Hussein Mwinyi kuwa mshindi wa urais Zanzibar, wafuasi wake wa chama cha Mapinduzi walipokea ushindi huo kwa furaha na shangwe.

    Lakini je wapinzani wake wamepokea vipi matokeo hayo?

    Hapo jana kulipoanza kuonesha dalili kuwa Dkt Hussein Mwinyi anaelekea kushinda, chama kikuu cha upinzani kikiongozwa na mwenyekiti wake na aliyekuwa mgombea urais Maalim Seif Sharif kupitia chama cha ACT Wazalendo, wao walizungumza na waandishi wa habari wakiashiria kupinga matokeo hayo kiasi cha kujitokeza barabarani kutaka kuandamana.

    Lakini baadhi ya viongozi wengine wa upinzani walisema wameridhia ushindi wa Dkt Mwinyi na kuahidi kumpa ushirikiano.

    Juma Ali Khatib kupitia chama cha ADA TADEA alisema kuwa yeye na chama chake wameridhika.

    ‘’Sasa ni wakati wa kufanya kazi na kujenga nchi yetu.’’

    Hamad Muhammed Ibrahim mgombea urais wa chama cha UPDP alisema:

    ‘’Matokeo haya mimi nasema ni maamuzi ya Wazanzibari, mimi kama mgombea kutoka UPDP nitashirikiana naye wakati wowote.’’

    Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia Makini, Ameri Said Ameri yeye anamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumaliza uchaguzi salama na kwa amani na ameahidi kushirikiana na Dkt Hussein Mwinyi ili kuhakikisha maendeleo ya Zanzibar yanapatikana.

  18. Matokeo ya uchaguzi Tanzania 2020: Maalim Seif ameachiwa kwa dhamana

    Maalim Seif Sharif

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Maalim Seif Sharif

    Mwenyekiti wa ACT Wazalendo ambaye alikuwa mgombea wa urais visiwani Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad ameachiwa kwa dhamana na sasa yuko nyumbani.

    Kwa mujibu wa kiongozi wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe, amesema Maalim Seif pamoja na Profesa Omar Fakih wameachiwa lakini asubuhi ya leo wanatakiwa kuripoti katika kituo cha polisi cha Madema saa mbili asubuhi.

    Maalim Seif alikamatwa jana majira ya asubuhi kwa mara nyingine tena muda mfupi baada ya kutangaza kuongoza maandamano ya amani ili kutetea haki yao ya kidemokrasia.

    Aidha, Jumanne Maalim Seif alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha mtoni Garagara na kuachiliwa saa kadhaa baadaye katika hatua ambayo ilishtumiwa vikali na viongozi wa upinzani.

    Hapo jana, Kamanda wa polisi mkoa wa mjini Magharibi Hawadhi Juma, aliwataka Watanzania kupuuza wito wa kujitokeza na kufanya maandamano na kuongeza kuwa matokeo ya nani ameshinda ni maamuzi ya wananchi.

  19. Habari ya asubuhi na karibuni katika matangazo yetu ya moja kwa moja hii leo ikiwa ni tarehe 30.10.2020.