Zitto Kabwe: 'Nitampigia Kura Tundu Lissu awe rais wa Tanzania'
Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe ametoa tamko kuwa kura yake itaenda kwa mgombea wa chama cha upinzani cha Chadema.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Zitto Kabwe: 'Nitampigia Kura Tundu Lissu awe rais wa Tanzania'

Kiongozi wa chama cha upinzani cha ACT-wazalendo, Zitto Kabwe ametoa tamko kuwa kura yake itaenda kwa mgombea wa chama cha upinzani cha Chadema.
Anasema kamati ya Uongozi ya Chama chake cha ACT imeshauriana na kuona kuwa huu ni mwaka wa kihistoria kwa Watanzania, mwaka wa kuamua hatma ya Maisha yao.
"Kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mimi Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe nitampigia kura kwa ndugu Tundu Antipas Mughwai Lissu. Huyu ndiye Mgombea wa Upinzani ambaye ana nguvu ya kumshinda mgombea wa chama tawala."
Anasema hatua hii ya kumuunga mkono mgombea wa chama kingine imesukumwa na dhamira yake ya kuleta mabadiliko ya kumchagua Lissu.
Kabwe ameyaeleza hayo katika hotuba yake ya kampeni Bangwe, Kigoma na kuwataka wafuasi wa chama hicho pia kumpigia kura Lissu.

Mwezi Septemba Mwenyekiti wa ACT Maalim Seif Shariff Hamad, alitangaza kumuunga mkono Lissu kwenye kinyang'anyiro cha Urais.
ACT katika kinyang'anyiro cha urais imemsimamisha aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania, Benard Membe, ambaye mpaka sasa hajajitokeza hadharani kumuunga mkono Lissu.

Mara baada ya Maalim Seif kutangaza kumuunga mkono Lissu, Mmembe alisisitiza kuwa yeye ndiye mgombea halali wa ACT.
Chadema kwa upande mwengine kimetangaza kumuunga mkono Maalim kwenye kinyang'anyiro cha urais wa Zanzibar.
Hata hivyo, ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa vimeoynya juu ya ushirikiano wa vyama hivyo ikisema ni kinyume na sheria.
Soma zaidi:
Kawaida maji ya juu ya ziwa yakiwa baridi - kwasababu ya hali joto ya baridi au mito inayobeba theluji iliyoyeyuka, kwa mfano, - maji hayo baridi ambayo ni mazito huzama na yale ambayo sio mazito hupanda juu ya ziwa. Bofya kiunganishi hiki kusoma taarifa hii zaidi..https://bbc.com.im/swahili/54568727%3C/a%3E%3C/p%3E%3C/div%3E%3C/div%3E%3C/article%3E%3C/li%3E%3Cli class="css-xxlek1">
Mfanyabiashara haramu ya binadamu akamatwa Libya
Polisi akamatwa kwa kuwashambulia waandamanaji Nigeria
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Gavana Sanwo-Olu pia amesema kwamba jimbo limetenga naira milioni 200 (dola 521,000) kwa ajili ya kufidia waathiriwa wa ukatili wa polisi.
Serikali ya kitaifa imepiga marufuku maandamano katika mji mkuu, ili kutekeleza maadili ya kukabiliana na Covid-19.
Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yamefanyika katika miji yote nchini Nigeria katika kipindi cha wiki iliyopita.
Maandandamano yameendelea licha ya kuvunjwa kwa kikosi tatacha polisi kinachotuhumiwa kwa ukatili wa raia maarufu kama (Sars).
Wakulima waadhimisha siku ya chakula Tanzania

Wakulima waadhimisha siku ya chakula Tanzania ambapo wadau mbalimbali wakiwemo wakulima, wataalamu wa lishe bora, watafiti na maafisa ugani wamekutana leo jijini Dodoma katikati mwa Tanzania kwa lengo la kuangazia suala la upatikanaji wa chakula na lishe bora.
Ingawa katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania, licha ya chakula kupatikana kwa wingi lakini bado kuna tatizo la utapiamlo.
Pelagia Gaudence ambae ni mkulima kutoka Arusha amesema tatizo kubwa la utapiamlo linasababishwa na ukosefu wa elimu katika jamii kuhusu lishe bora.
Wakati huo huo, Elibarika Joseph ambae pia ni mkulima anasema kukosa elimu ya lishe bora kumemfanya amekuwa miongoni mwa waathirika wa lishe bora kutokana na ulaji wake kutozingatia virutubisho vinavyotakiwa.

Maelezo ya picha, Baadhi ya wakulima waliohudhuria kongamano hilo wameonekana kutilia mkazo matumizi ya mbegu za asili Maadhimisho haya pia yanaenda sambamba na miaka 75 ya shirika la chakula duniani FAO.
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa zaidi ya nusu ya watu duniani hushiriki kuzalisha chakula, lakini chini ya nusu ya watu duniani hupata chakula bora.
Yanga yamkaribisha Tanzania kocha Mrundi

Chanzo cha picha, Young Africans
Maelezo ya picha, Kaze amefika Tanzania Timu ya soka nchini Tanzania Young Africans imemkaribisha kocha raia wa Burundi Kaze Cedric nchini Tanzania leo kwa ajili ya kuanza kuifunza timu hiyo.
Young Africans imetoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wa mtandao wake wa kijamii wa Twitter. Na Cedric Kaze alieleza kufurahishwa kwake na kazi mpya katika kikosi cha Yanga:
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kaze anachukua nafasi ya mtangulizi wake Mserbia, Zlatko Krmpotic ambaye aliifunza timu hiyo kwa siku 37 pekee.
Kaze anaanza kazi siku chache tu baada ya mchezaji wa Burundi Saido Ntibazonkiza kusajiriwa na timu ya Yanga wiki hii.
Kaze mwenye umri wa miaka 40, ni miongoni mwa makocha Warundi wenye umri mdogo na ana kibali cha FIFA cha kuifunza timu ya daraja la kwanza.
Zamani alikuwa mchezaji wa safu ya kati ya Prince Louis Rwagasore FC ya mjini Bujumbura, na baadaye akawa mkufunzi wake.
Alionesha umahiri wa kazi hiyo alipokuwa mkufunzi wa Atletico Olympic FC iliyoshinda kombe la mashindano ya kitaifa ya soka nchini Burundi, na baadaye akawa kocha wa mwaka 2010/2011.
Baadaye alikwenda nchini Rwanda ambako alikuwa mkufunzi wa timu ya Mukura VS (2013 - 2014) kabla ya kwenda kufundisha soka katika shule ya mpira wa miguu ya Canada Barcelone (FC Bescola Soccer School).
Rusesabagina 'ameandika barua' kutoka jela

Vincent Lurquin, wakili Mbelgiji amesema alipokuwa mjini Kigali alipata barua kutoka kwa Paul Rusesabagina inayosema kuwa mawakili anaowataka ni wawili , ambao ni miongoni mwa mawakili saba waliopangwa na familia yake.
Mapema leo asubuhi ‘’shujaa huyo wa filamu ya Hoteli Rwanda’’ alikataliwa dhamana, na anashikiliwa katika gereza kuu la Kigali akisubiri kesi ya mashitaka ya ugaidi dhidi yake, ambayo hajayakubali bado.
Bw Rusesabagina anasaidiwa na mawakili wawili wa Rwanda ambao waendesha mashitaka wa Rwandawalisema walichaguliwa na mshukiwa binafsi.
Familia yake iliwakataa ikihoji uhuru wao.
Katika kikao na waandishi wa habari kilichofanyika kwa njia ya video Alhamisi mawakili wawili kati ya saba waliopangwa na familia yake waliwaambia waandishi wa habari kuwa walipokuwa Kigali walizuiwa kumuona Bw Rusesabagina.

Maelezo ya picha, Paul Rusesabagina anakabiliwa na mashitaka 13 Bw Lurquin alisema kuwa amekuwa wakili wa Bw Rusesabagina nchini Ubelgiji naalikuwa mjini Kigali kumuona mteja wake na kupata haki ya kumuwakilisha.
“ Kwa miaka miwili iliyopitaUbelgiji imekuwa ikichunguza kesi dhidi ya Bw Rusesabagina, na nimekuwa wakili wake tangu wakati huo” - Bw Lurquin alisema.
“Sioni ni kwanini Rwanda ilinizuwia kumuona na kumsaidia mteja wangu, raia wa Ubelgiji juu ya kesi ambayo ilianzia Ubelgiji.” Aliongeza.
Wakati alipokuwa Kigali Bw Lurquin alisema kuwa alipata barua kutoka gerezani iliyoandikwa na Bw. Rusesabagina akiwakubali mawakili Gatera Gashabana, wakili anayeishi Rwanda Vincent Lurquin, kama mawakili aliowachagua binafsi kumuwakilisha katika kesi dhidi yake.
Amesema kuwa katika kipindi cha wiki mbili atarejea Rwanda na timu ya mawakili kushinikiza haki ya kumuwakilisha mteja wake.
Africa ‘haiwezi kuhimili’ wimbi la pili la virusi vya corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Nchi nyingi za Afrika zimelegeza masharti ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona Shirika la afya duniani (WHO) limeonya kuwa Afrika haiwezi kuhimili wimbi la pili laCovid-19, likisema kuwa litakuwa na athari kubwa hususan za kiuchumi.
Onyo hilo linatolewa wakati maambukizi yakiendelea kuongezeka katika nchi nyingi ambazo zililegeza sheria za kupambana na maambukizi hayo hivi karibuni.
WHO linasema virusihavitaweza kudhibitiwakama mataifa ya Afrika yataendelea kufungua shughuli zakebila kuweka tahadhari za kuzuwia maambukizi ya virusi vya Corona.
Imeonya pia juu ya kurejea kwa vipindi vya amri za kutotoka nje ambazo inasema Afrika haiwezi kuvihimili.
Mkurugenzi wa Who kanda ya Afrika, Matshidiso Moeti, pia amesema hatua zimewekwa kuhakikisha bara hilo linapata sehemu yake ya ya chanjo yoyote inayotengenezwa.
Afrika imeripoti zaidi yavisa milioni 1.6 vya virusi vya corona tangu mlipoko huo ulipoanza huku watu 39,000 wakifa kutokana na maradhi hayo.
Maalim asimamishwa kufanya kampeni za urais Zanzibar
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Aboubakar Famau
- Nafasi, BBC News, Dar es Salaam

Maelezo ya picha, Maalim anashutumiwa kwa kuwahamasisha watu kujitokeza kupiga kura tarehe 27 Oktoba Mgombea urais wa chama cha ACT Wazalendo kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesimamishwa kufanya kampeni na Kamati ya maadili ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar- ZEC kwa muda 5.
Adhabu hiyo imetolewa jana jioni baada ya kamati hiyo kukaa na kusikiliza malalamiko yaliyo wasilishwa na Chama cha Demokrasia Makini ambapo imemtuhumu mwanasiasa huyo mkongwe kwa kuhamasisha watu kujitokeza na kupiga kura tarehe 27 ambayo kwa mujibu wa sheria imetengwa kwa watu maalumu.
ACT Wazalendo kimeituhumu Tume ya uchaguzi ya Zanzibar kwa kuwa na upendeleo. Akizungumza na BBC Afisa wa habari na uenezi- Salim Bimani amesema:
‘’Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC inatumika na inatumika vibaya dhidi ya chama cha ACT Wazalendo, tuna ushahidi kwasababu masuala mengi ambayo tumekuwa tukiyadai, tukiyaeleza na kuyalalamikia tume hata siku moja haijapata kujibu, haijapata kutekeleza, taijapata kuwa wazi, kile kinachotakikana kwenye CCM ndicho wanachokifanya.
Kuna mifano mingi kabisa kuwa ZEC imekuwa ikibeba upande mmoja na huu ndio ushahidi wa wazi.’’

Matamko ambayo yanadaiwa kwenda kinyume na kanuni za uchaguzi za mwaka 2020.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa Uchaguzi Zanzibar Thabit Faina ameiambia BBC kwamba mgombea huyo wa ACT Wazalendo anaweza kukata rufaa.
ACT Wazalendo wanafanya mkutano kujadili suala hilo leo
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Ijumaa tarehe 16.10.2020



