Serikali ya Tanzania kutumia ndege kuzima moto Mlima Kilimanjaro
Serikali ya Tanzania inatazamiwa kutuma helikopta na ndege katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kujaribu kuuzima moto unaendelea kuwaka kwa siku ya saba sasa.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Uholanzi yaruhusu mauaji ya huruma kwa watoto

Chanzo cha picha, Getty Images
Serikali ya Uholanzi imeidhinisha mipango ya kuruhusu kifo cha mapema au mauaji ya huruma kwa watoto wenye ugonjwa usiopona kati ya mwaka 1 na miaka 12 ...Kwa habari zaidi bofya kiunganishi hiki:https://bbc.com.im/swahili/54556899%3C/a%3E%3C/p%3E%3C/div%3E%3C/div%3E%3C/article%3E%3C/li%3E%3Cli class="css-xxlek1">
Ujerumani yarekodi idadi kubwa zaidi ya waliopatwa na corona kwa siku
Nigeria yapiga marufuku maandamano dhidi ya polisi ‘katili’
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Katika taarifa hiyo serikali imesema kuwa serikali imeelezea hofu yake juu ya kusambaa kwa maandamano ambako kumesababishashinikizo kwa raia wanaoheshimu sheria, licha ya Mkuu wa polisi kutangazwa kuvunjwa kwa kikosi kinachodaiwa kutekeleza ukatili dhidi ya raia
Ufisadi na ukosefu wa heshima vimekuwa vikitumiwa na serikali kuzima maandamano.


Genge la watu wenye mapanga lawashambulia waandamanaji Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Maandamano dhidi ya ukatili wa polisi yamekuwa yakiendelea katika miji mikubwa kote Nigeria Waandamanaji dhidi ya ghasia za polisi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja wameshambuliwa na wanaume wasiojulikana waliokuwa wamebeba mapanga.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema mamia ya waandamanaji kadhaa walikuwa wamekusanyika katikati ya mji huo wakati shambulio lilipotokea.
Muandamanaji mmoja amesema baadae baadhi ya wavamizi hao walikamatwa na kukabidhiwa kwa maafisa.
Maandamano yamekuwa yakifanyika katika miji mbalimbali kote nchini Nigeria kwa wiki nzima iliyopita.
Ghasia zimeendelea licha ya kuvunjwa kwa kikosi tata cha polisi- cha kukabiliana na wizi kinachofahamika kama Sars.
Waandamanaji wameapa kuendelea kuwepo mitaani.
Shule zafunguliwa tena leo Uganda
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Isack Mumena
- Nafasi, BBC Swahili Kampala

Maelezo ya picha, Wanafunzi wanazingatia agizo la kukaa mbali darasani Shule na taasisi nchini Uganda zimefunguliwa hii leo kote nchini humo baada ya kipindi cha miezi saba kufuatia janga la COVID-19.
Wanaoruhusiwa kurejea shuleni ni watahiniwa wanaokamilisha masomo yao huku shule na taasisi zikitakiwa kufuata kanuni za kudhibiti maambukizi ya corona.
Hata hivyo, shule kadhaa binafsi zinalalamikia kutosaidiwa na serikali kuweza kufadhili mahitaji ya wanafunzi kama vile vitakasa mikono na vipima joto, anasema mwandishi wa BBC Issaac Mumena.

Maelezo ya picha, Baadhi ya wanafunzi wameshindwa kufika shuleni baada ya kukosa fedha za kununua vifaa vya kudhibiti maambukizi Mwezi Septemba, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitangaza kufunguliwa kwa shule kwa watahiniwa wa darasa la saba, kidato cha nne, kidato cha sita, wanafunzi wa vyuo vikuu, vyuo vya ufundi na bishara wanaomaliza mwaka wao wa mwisho kuanzia leo.
Shule hizo zinatakiwa kufunguliwa kwa kufauta masharti ya wataalam wa afya ya kudhibiti Covid-19.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya St Daniel Yumbe kaskazini mwa Uganda , Aziku Mosese anasema wamejiandaa kwa ajili ya masomo.
Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wanasema wameieleza BBC kuwa hawako tayari kuhudhuria masomo leo kwasababu ya changamoto ya kushindwa kununua vifaa vya kujikinga na maambukizi ya corona kutokana na ukosefu wa fedha.
Shule zinafunguliwa Uganda kufuatia kulegezwa kwa mashariti ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.
Rashford apongeza mpango wa ugawaji wa chakula kwa watoto Wales.

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Marcus Rashford alitunukiwa tuzo kwa kampeni yake ya kupata chakula cha bure kwa ajili ya watoto wakati wa likizo nchini Uingereza Chakula cha bure shuleni kitakuwa kikitolewa kwa watoto wakati wa likizo katika eneo la Wales hadi mwezi Aprili 2021, imetangazwa .
Mchezaji soka wa England Marcus Rashford, ambaye alifanikiwa katika kampeni ya suala la ugawaji wa chakula kwa wanafunzi nchini Uingereza, amepongeza mpango huo.
Waziri wa elimu wa Uingereza Kirsty Williams amesema pauni milioni 11 zitalipia mpango wa utoaji wa chakula kwa wanafunzi ikiwa ni pamoja hadi wakati wa likizo ya Pasaka mwaka 2021.
Nyota huyo wa Manchester United amesema mpango huo utasaidia "watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini humo".
Zaidi ya wanafunzi 75,000 wenye umri kati ya miaka mitano na 15 kutoka familia zenye kipato cha chini wanastahili kupata chakula cha bure kote Wales.
Mpango huo pia uko wazi kwa watoto wadogo zaidi wanaohudhuria masomo ya chekechea kwa siku nzima.
Kampeni zaanza Ivory coast kwa ajili ya uchaguzi wa urais

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Raia wa Ivory Coast wamekua wakikusanya kadi za kupigia kura kabla ya uchaguzi Kampeni zimeanza leo Alhamisi nchini Ivory Coast kabla ya uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika tarehe 31 Oktoba.
Vyama vya upinzani vimetoa wito unaowataka ukaidi wa raia ili kupinga azma ya rais aliyeko madarakani, Alassane Ouattara, ya kugomea muhula wa tatu. Wapinzani wameitaja azma hiyo kuwa kinyume cha sheria.
Maelfu ya watu waliandamana dhidi ya hatua hiyo katika mji wa kibiashara, Abidjan, siku ya Jumamosi.
Kuna jumla ya wagombea wanne wanaowania kiti cha urais. Wapinzani wakuu akiwemo rais wa zamani na waziri mkuu wa zamani, walizuiwa kugombea baada ya kushindwa kutimiza vigezo vya uchaguzi.
Bw Ouattara alikuwa rais miaka 10 iliyopita katika uchaguzi ulioibua mgawanyiko na kukumbwa na ghasia.
Helikopta kupelekwa katika mlima Kilimanjaro kusaidia kuuzima moto

Maelezo ya picha, Upepo na nyasi zilizokauka vimetajwa kuwa sababu ya kusambaa zaidi kwa moto katika Mlima Kilimanjaro Serikali ya Tanzania inatazamiwa kutuma helikopta na ndege katika mlima Kilimanjaro nchini humo kujaribu kuuzima moto unaoendelea kuwaka kwa siku ya saba sasa.
Hayo ameyasema Waziri wa utalii nchini humo Dkt Hamis Kigwangala baada ya moto kuendelea kuwaka katika mlima huo .
Jumatano, Waziri Kigwangala alitangaza kuwa wameweza kuudhibiti moto huo, lakini baadaye moto huo ulisaambazwa zaidi na upepo uliovuma katika mlima huo.
Katika ujumbe wake wa Twitter Waziri Kigwangala amethibitisha kuwa moto unaendela kuwaka Katika mlima huo mrefu zaidi barani Afrika.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Unaweza pia kutazama:

Bobi Wine adai polisi 'walichukua' nyaraka za uteuzi wake wa urais

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanasiasa na mwanamuziki wa Uganda, Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi Wine, ameiambia BBC kuwa nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya uteuzi wake wa kugombea urais zimepotea katika ofisi yake baada ya uvamizi wa ofisi hiyo wa vikosi vya usalama siku ya Jumatano mchana.
Moja ya masharti ya wagombea ni kuwasilisha sahihi za wafuasi wao 100 waliojisajiliwa kupiga kura kutoka katika walau theluthi mbili ya wilaya za Uganda.
Bobi Wine anasema timu yake ilikuwa tayari imekusanya sahihi milioni sita lakini hizi sasa zimepotea.
“Serikali ya Museveni inajaribu kunizuwia kuteuliwa kama mgombea wa urais. Kuanzia kuhoji nyaraka zangu, kuhoji umri wangu - na sasa wanafanya kila juhudi kukwamisha uteuzi wangu na ninaamini kuwa ndio maana walichukua saini .”
"Hatutakata tamaa, tumekwisha ripoti mara moja kwa matawi yetu kuhakikisha wanaanza kukusanya saini mara moja na tunatumaini kufikia Ijumaa tutakuwa na saini zinazohitajika ,” alisema.
Mbunge huyo alikuwa akizungumza na BBC baada ya kutoroka kutoka katika ofisi yake wakati makumi kadhaa ya askari na polisi walipowasili kufanya msako.
Pia alisema milioni 23 za Uganda milioni ($6,200 ) zilichukuliwa. Anasema pesa hizi zilichangishwa kusaidia kulipia garama za uchaguzi kwa ajili ya wanachama wanaotaka kugombea ubunge.
Polisi hawakujibu wito wa BBC wa kuzungumzia madai ya Bobi Wine. Awali walikana kuwa uvamizi huo ulichochewa kisiasa.
Tume ya uchaguzi iliwapatia wagombea siku ya Ijumaa kuwa muda wa mwisho wa kuwasilisha fomu zao za uteuzi..
Msemaji wa tume anasema hawezi kuzungumzia juu ya madai ya Bobi Wine ya kutoweka kwa nyaraka lakini anasema muda wa mwisho unaweza kuongezwa kwa mgombea iwapo wataifahamisha tume rasmi.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Alhamisi tarehe 15.09.2020

