Ofisi ya Bobi Wine yavamiwa Uganda
Ofisi ya chama cha mgombea wa Urais nchini Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi imevamiwa na makumi ya wanajeshi wenye silaha pamoja na maafisa wa polisi.
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Je nini kilichomkera Kim Jong-un wakati wa hotuba?
Maelezo ya video, Je ni kwanini rais Kim Jong-un alikuwa na hasira wakati wa hotuba hii? Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alijawa na hisia chungu nzima wakati wa hotuba katika hafla ya gwaride la kijeshi wikendi iliopita.https://bbc.com.im/swahili/habari-54534724%3C/a%3E%3C/p%3E%3C/div%3E%3C/div%3E%3C/article%3E%3C/li%3E%3Cli class="css-xxlek1">
Wakuu wa shule Kenya watahadharishwa dhidi ya kuwanyunyizia 'dawa' wanafunzi
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Ofisi ya Bobi Wine yavamiwa

Chanzo cha picha, Bobi Wine Twitter
Maelezo ya picha, Kofia anayoivaa Bobi Wine na wafuasi wake ilitangazwa na serikali ya Uganda kama sare ya jeshi Ofisi ya chama cha mgombea wa Urais nchini Uganda Robert Kyagulanyi, al maarufu Bobi imevamiwa na makumi ya wanajeshi wenye silaha pamoja na maafisa wa polisi.
Nyaraka zimeripotiwa kuchukuliwa kutoka kwenye ofisi pamoja na kofia yenye muundo wa kijeshi na magwanda vimechukuliwa. Kamera za CCTV pia zimechukuliwa.
Mmoja wa washauri wa Bobi meiambia BBC kuwa maafisa hawakuwasilisha kibali walipokua wakiingia kukusanya nyaraka na mavazi.
Msemaji wa polisi nchini Uganda Fred Enanga ameiambia BBC, ‘tunafanya operesheni juu ya utumiaji mbaya wa sare za kijeshi.
Septemba mwaka jana, serikali iliidhinisha kofia nyekundu sawa na anayovaa Bobi Wine na wafuasi wake ni sare ya jeshi-ikimaanisha kuwa yeyote anayeonekana ameimiliki au kuivaa kinyume cha sheria anaweza kushitakiwa.
Bwana Enanga amesema operesheni inaendelea na kwamba maafisa watasaka maeneo mengine pamoja na ofisi za National Unity.
Bobi Wine amesema kuwa nguvu za dola zinamlenga na chama chake wakati akijiandaa kukabiliana na Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi ujao wa mwaka 2021.
Lakini msemaji wa polisi anasisitiza kuwa operesheni hiyo haijachochewa kisiasa.
Moto uliowaka katika Mlima Kilimanjaro umedhibitiwa, asema Waziri Kigwangala

Maelezo ya picha, Waziri Hamis Kigwangala amesema eneo lililoathiriwa na moto ni ngazi ya tatu ya msitu ambayo huwa ina vichaka Asilimia moja nukta sita ya eneo la hifadhi ndilo liloathiriwa na moto na hakuna madhara makubwa ya kiekolojia na bado mpaka sasa chanzo cha moto huo hakija bainika na bado wanaendela na uchunguzi na hivyo hawataki kumnyooshea yeyote kidole kwa sasa.
Waziri wa mali asili na utalii nchini Tanzania Hamis Kigwangala amesema moto unaendelea kuwaka kwenye msitu wa mlima Kilimanjaro kwa siku ya nne sasa tayari umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa na mvua iliyonyyesha usiku wa kuamkia hii leo imesaidia jitihada za kukabiliana na moto huo.
Waziri Kigwangala amesema eneo lililoathiriwa na moto huo ni ngazi ya tatu ya msitu ambayo huwa ina vichaka na msitu mzito wa mlima haujaathiriwa kwa namna yoyote.
Waziri Kigwangala anasema amesha ielekeza mamlaka ya hifadhi za mali asili nchini Tanzania (Tanapa) kununua vifaa vya kutoshha vya kuzima moto ikiwemo helkopta ili kujiweka tayari iwapo kutaibuka janga jingine kama hilo siku zijazo.
, Facebook 'kukabiliana na taarifa za upotoshaji' kabla ya uchaguzi wa Tanzania

Chanzo cha picha, Getty Images
Facebook imezindua programu kadhaa za kukabiliana na taarifa potofu na uingiliwaji wa uchaguzi nchini Tanzania kabla ya uchaguzi wa mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu, limeripoti gazeti la Citizen.
Mkuu wa sera wa kampuni hiyo kubwa ya mtandao wa habari wa kijamii katika eneo la Afrika Mashariki na upande wa Afrika, Mercy Ndegwa, ametangaza uzinduzi wa siku ya kumbukumbu ya uchaguzi katika Facebook na Instagram.
Uzinduzi huo utahusisha utoaji wa taarifa rasmi za upigaji kura na kuwaruhusu Watanzania kushirikisha uzoefu wao wa kupiga kura.
Bi Ndegwa anaripotiwa kusema kuwa Facebook itahakikisha matangazo ya kibiashara ya kampeni katika majukwaa yake yanathibitishwa kwa ajili ya uwazi.
Vikwazo vya vyombo ya habari vimeongezeka tangu Rais Magufuli anayewania muhula wa pili aingie madarakani mwaka 2015.
Wanasayansi waonya juu ya kutokea kwa ‘mkasa mwingine wa volkano’ DRC
Wanasayansi wanaonya kuwa ziwa la lava linajaa kwa kiwango cha kutishajuu katika Mlima wa volcano wa Nyiragongo uliopo juu ya mji wa Goma Mashariki mwa Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo.
Mwezi Januari 2002, lava iliyomwagika kutoka Mlima Nyiragongo kwa kasi hadi katika mji wa Goma na kusababisha vifo vya watu 250 na kuharibu 20% ya mji wa Goma.
Kikundi cha wanasayansi wanaochunguza matukio ya milima, wameonya kuwa “mwamba unaoyeyuka unaweza kulipuka tena kupitia kuta za ziwa la volkano”, imesema taarifa ya jarida la kisayansi.
“ Sasa, hali inaonyesha dalili za mkasa mwingine” Dario Tedesco, mtaalamu wa volcano na milima aliliambia jarida la masuala ya kisayansi.

Maelezo ya picha, Mtoto akitembea kando ya lava iliyoyeyuka katika uwanja wa ndege wa Goma, mwaka 2002 Tathmini yao inaonesha kuwa hatari kubwa zaidi yam lima huo itatokea katika kipindi cha miaka 4, ingawa wanaamini tetemeko la ardhi linaweza kusababisha mlipuko huo mapema.
“Hii ni volkano hatari zaidi duniani!” Profesa Tedesco aliongeza. Watu wapatao milioni moja wanaishi katika mji wa Goma.
Muasisi wa Taifa la Tanzania hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere akumbukwa
Leo Tanzania inaadhimisha miaka 21 toka kufariki kwa muasisi na raisi wa kwanza wa Taifa hilo Mwalimu Julius Nyerere.
Mwalimu Nyerere alifariki Oktoba 14, 1999 jijini London, Uingereza alipokuwa akipatiwa matibabu.
Watu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania wanatumia mitandao ya kijamii kumkumbuka Mwalimu Nyerere kwa falsafa na nukuu zake:
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Ruka X ujumbe, 4Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Kikosi kipya cha polisi chaundwa kuchukua nafasi ya kikosi 'katili' Nigeria

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Kiosi maalumu cha kupambana na wiziSpecial Anti-Robbery Squad -kilishutumiwa kwa ukatili Mkuu wa polisi nchini Nigeria amesema kikosi kipya kimeundwa ili kuchukua nafasi ya kikosi tata maalumu cha polisi cha kukabiliana na wizi kinachofahamika kama Sars, ambacho kilivunjwa kufuatia maandamano ya ukiukaji wa haki za binadamu dhidi yake.
Kikosi kipya kitajulikana kama 'Swat' au kikosi maalumu cha cha silaha na mbinu – (Special Weapons and Tactics Team).
Waandishi wa habari wanasema Wanigeria wengi hawana Imani na wanaendelea kuandamana wakitaka yafanyike mageuzi makubwa katika polisi ya nchi hiyo.
Katika juhudi za kutatua kuondoa hofu miongoni mwa Wanigeria mkuu wa polisi amesema kuwa polisi wote kutoka katika kikosi kilichovunjwa watapitia uchunguzi wa kisaikolojia na kimatibabu kabla ya kupata mafunzo zaidi na kupelekwa tena katika sehemu za kazi.
Pia aliagiza kuachiliwa huru bila masharti yoyote kwa watu wote waliokamatwa wakati wa maandamano.
Rwanda yahalalisha mauzo ya nje ya bangi kwa matumizi ya dawa

Rwanda imehalarisha kisheria ukulima na mauzo ya nje ya nchi ya mmea wa bangi kwa ajili ya matumizi ya tiba ili kupata fedha, wamesema maafisa wa nchi hiyo.
Kikao cha baraza la mawaziri kilichokaa Jumatatu kiliidhinisha “miongozo juu ya ukulima, usindikaji na mauzo ya nje ya mimea ya matibabu ya thamani ya juu nchini Rwanda ”.
Akizungumza na televisheni ya taifa hilo Jumatano waziri wa afya wa Rwanda Dkt. Daniel Ngamije alisema mimea hiyo inajumuisha bangi.
Taifa hilo lililopo Afrika mashariki limehalalisha bangi baada ya nchi kama Malawi, Lesotho, Afrika Kusini, Zambia na Zimbabwe kuhalalisha kisheria mauzo ya bangiau matumizi ya mmea huo.
Bwana Ngamije amesema Rwanda inataka “kutoa mchango wake kwa vituo vya utafiti na sekta ya madawa kwa kutoa raslimali ili tupate faida ya fedha…”
Mwaka jana, soko la bangi la dunia lilidhaniwa kuwa na thamani ya dola bilioni 150 billion, kulingana na Benki ya Barclays.
Ni wakulima waliopewa leseni ambao wataruhusiwa kuzalisha zao hilo “uvutaji wa bangi bado unazuiwa ”, kulingana na bodi ya maendeleo ya Rwanda imesema.
Iwapo utapatikana unalima au kuuza bangi nchini Rwanda unaweza kuadhibiwa hadi kifungo cha maisha jela , huku mvutaji akikabiliwa na kifungo cha miaka miwili jela nchini Rwanda.
Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatano tarehe 14.10.2020
