Je unalifahamu jina jipya la Museveni?

Rais wa Uganda, anayejulikana kama Yoweri Kaguta Museveni, amebadilisha rasmi majina yake, kujumuisha jina lake la utoto, Tibuhaburwa.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo haya ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. Shughuli za utalii 'Mlima Kilimanjaro' zinaendelea

    Mamlaka ya wanyapori nchini Tanzania imetoa wito kwa wenyeji na wageni kuondoa hofu na kuendelea na shughuli za utalii kama kawaida kwenye hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.

    Video hii inaonesha hali ilivyo huku jitihada za kuzima moto zikiendelea.

    Maelezo ya video, Shughuli za utalii Mlima Kilimanjaro zinaendelea
  3. Muuza maparachichi Kenya ataka madai ya dhuluma kuchunguzwa

    Parachichi

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Muuzaji wa maparachichi nchini Kenya katika soko la kimataifa amemtaka mwendesha mashtaka mkuu wa nchi hiyo achunguze madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye mashamba yake siku moja baada ya shirika la uuzaji la Uingereza Tesco kusimamisha huduma zake.

    Kakuzi, ambayo ni mzalishaji mkubwa wa parachichi nchini, anasema ni mwathiriwa wa kampeni inayolenga kuiharibia sifa.

    Inakabiliwa na madai kwamba walinzi wake katika kipindi cha muongo mmoja uliopita wamewashambulia na kuwabaka wanakijiji wa eneo hilo na wakati mmoja kumuua mtu aliyetuhumiwa kuiba parachichi.

  4. Kijana wa Kiitaliano kuwa 'Mtakatifu wa kwanza wa milenia' kanisa katoliki

    Wazazi wa Carlo Acutiswalihudhuria sherehe ya kutawazwa kwake siku ya Jumamosi

    Chanzo cha picha, PA Media

    Maelezo ya picha, Wazazi wa Carlo Acutiswalihudhuria sherehe ya kutawazwa kwake siku ya Jumamosi

    Kijana wa Italia ambaye alitumia mtandao kueneza imani yake amekuwa mtakatifu wa kwanza wa milenia wa Kanisa Katoliki.

    Carlo Acutis, ambaye alifariki kutokana na saratani ya damu(leukemia) mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 15, tayari amepewa jina "mtakatifu mlinzi wa wavuti".

    Siku ya Jumamosi, alitunukiwa heri katika sherehe za mji wa Assisi na kusogea hatua moja karibu na utakatifu.

    Acutis ni mwenye heri wa kwanza wa "millenia hii " aliyetumia mtandao kutumika katika kanisa, aliyeonesha mfano wa teknolojia inavyoweza kutumika vizuri sana katika kanisa.

    Aliwekwa kwenye njia ya utakatifu baada ya Vatican kuamuru kwamba aliokoa maisha ya kijana mwingine kimiujiza.

  5. 'Nilifungwa jela kwa kufichua vitendo vya rushwa'

    Hopewell Chin'ono

    Chanzo cha picha, Reuters

    Katika mfululizo wa barua kutoka kwa waandishi wa habari, mwanahabari wa Zimbabwe Hopewill Chin'ono anaeleza namna gani alikabiliana uso kwa uso na athari za kusaidia kufichua kashfa ya rushwa mwanzoni mwa mwaka huu.

  6. Mkuu wa polisi akamatwa Afrika Kusini kwa tuhuma za ufisadi

    Afisa wa polisi wa ngazi ya juu nchini Afrika Kusini amekamatwa Jumatatu asubuhi,kufuatia tuhuma za ufisadi kwa mujibu wa kitengo cha upelelezi nchini humo.

    Afisa huyo, naibu kamishena wa polisi ambaye jina lake limebanwa ni wa hivi punde kukamatwa kuhusiana na zabuni ya mamilioni ya fedha za kununua vifaa vya dhararu.

    Kamishena wa kitaifa wa polisi, Khomotso Phahlane, ni miongoni mwa wale waliohusishwa na kesi hiyo. Hata hivyo amepinga tuhuma dhidi yake.

    Maafisa wengine wa ngazi ya juu wameshitakiwa kwa tuhuma za ufisadi, ubadhirifu wa fedha, wizi na utakatishaji.

    Naibu huyo wa kamishena wa polisi anatarajiwa kufunguliwa mashitaka leo Jumatatu.

  7. Je unalifahamu jina jipya la Museveni?

    Yoweri Museveni
    Maelezo ya picha, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni

    Rais wa Uganda, anayejulikana kama Yoweri Kaguta Museveni, amebadilisha rasmi majina yake, kwa kujumuisha jina lake la utoto,Tibuhaburwa.

    Jina la Tibuhaburwa katika kabila lake la Banyankore, linaweza kutafsiriwa kama "yule ambaye hawezi kuchukua ushauri au kuongozwa / kurekebishwa".

    Hatua ya Museveni kubadilisha jina imezua uvumi na utani miongoni mwa Waganda katika mitandao ya kijamii, baadhi yao wakihoji kazi ya washauri wake.

    Rais alisaini tamko kama inavyotakiwa na Sheria ya Usajili wa Watu, ili kujulikana rasmi kama Yoweri Tibuhaburwa Kaguta Museveni.

    Ingawa jina hilo limetajwa katika katika mazingira tofauti juu ya utawala wake wa miaka 34, hajawahi kulitumia hadharani.

    Kulingana na hati ya upeanaji wa hati ya tarehe 6 Oktoba, rais anasema kwamba jina hilo limetumiwa kwenye vyeti vyake vya masomo.

    Lakini inaaminika kuwa hatua hiyo inafuata mahitaji kutoka kwa Tume ya Uchaguzi, kwa wagombea wa uchaguzi 2021 kuhakikisha kuwa majina kwenye hati zao za uteuzi zinalingana na zile zilizo kwenye rekodi zao za masomo.

    Tume ya uchaguzi hivi karibuni ilitangaza kuwa wagombeaji ambao majina yao kwenye karatasi zilizowasilishwa si sawa na wale walio kwenye karatasi zao za masomo hawatateuliwa.

    Mnamo mwaka wa 2017, uamuzi wa mahakama ulibatilisha ushindi wa mbunge kwa misingi kwamba amebadilisha majina yake kwenye hati tofauti rasmi.

  8. Rwanda yawachukulia hatua mapadri kwa kukiuka muongozo wa kuzuia corona

    Padri Emmanuel Ndagijimana  na padri Felicien Nsengiyumva

    Chanzo cha picha, Rwanda National Police

    Maelezo ya picha, Padri Emmanuel Ndagijimana na padri Felicien Nsengiyumva

    Mamlaka nchini Rwanda imewachukulia hatua ya kinidhamu mapadri wa Kanisa Katoliki kwa kuendesha misa bila kuzingatia muongozo wa usalama wa kuzuia maambukizo ya virusi ya corona.

    Parokia ya Kanisa Katoliki la Ruhengeri kaskazini mwa nchi hiyo, ambayo pia ni makazi ya mapadri hao inakabiliwa na tishio la kufungwa.

    Mapadri hao, Emmanuel Ndagijimana na Felicien Nsengiyumva, wanasemekana hawakuzingatia idadi ya waumini waliotakiwa kuhudhuria misa kama iliyowekwa na serikali.

    Polisi walikumbana "hali ya msongamano "katika kanisa na "kila mtu alikuwa katika hatari ya kupata maambukizi ya virusi", kwa mujibu wa taarifa ya serikali.

    "Tunawakumbusha viongozi wa kidini hasa wale waliyoruhusiwa kurejelea ibada kufuata muongozo wa usalama uliyowekwa na mamlaka husika," taarifa hiyo ilisema.

  9. Ethiopia yaimarisha vita dhidi ya makundi ya nzige

    Nzige wamevamia nchi kadhaa za Afrika Mashariki

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nzige wamevamia nchi kadhaa za Afrika Mashariki

    Waziri wa Kilimo wa Ethiopia, Oumer Hussien, amesema ndege zaidi za kunyunyiza dawa zitapelekwa kukabiliana na makundi ya nzige wanaovamia mashamba nchini humo.

    Hii ni baada ya ndege za kupuliza dawa kuanguka mapema mwezi Oktoba na kurudisha nyuma jitihada za kupambana na wadudu hao waharibifu.

    Waziri amesema nzige katika maeneo manne wamepulizwa dawa kwasababu wamekuwa tishio kwa usalama wa chakula nchini Ethiopia.

    Amesema Wizara inaendeleza mchakato wa kubaini mashamba yaliyoathiriwa zaidi na uvamizi wa nzige ili kuwapa usaidizi wenye mashamba hayo.

    Nzige walionekana katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki ambako wamesababisha uharibifu wa mimea.

    Wataalamu wametaja uvamizi wa sasa wa nzige kuwa mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 60.

  10. Tanzania yapambana na moto wa mwituni kwenye Mlima Kilimanjaro

    Mlima Kilimanjaro

    Mlima Kilimanjaro ulio mrefu zaidi Afrika unawaka moto, sababu ya moto huo unaowaka umbali wa mamia ya mita kutoka usawa wa bahari bado hazijajuikana.

    Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini Tanzania, mashuhuda wamesema kuna jitihada za wakazi wa eneo hilo kuuzima moto huo lakini changamoto inayolikumba zoezi hilo ni umbali ambao moto huo upo.

    Miale ya moto ilikuwa ikionekana kutoka mji wa Moshi umbali wa makumi ya kilomita kutoka eneo la mlima kulikotokea tukio hilo.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    The Citizen limenukuu Taarifa ya hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro (Kinapa) ikisema kuwa moto huo ulitokea siku ya Jumapili majira ya jioni Tarehe 11 mwezi Oktoba, kisha taarifa hiyo ilithibitishwa na afisa habari wa Shirika la hifadhi la Taifa (TANAPA)Patrick Shelutete na kusema kuwa taarifa kwa kina itatolewa kuhusu tukio hilo.

  11. Uingereza na Kenya kukusanya $ 5bn kufadhili elimu baada ya Covid-19

    Uhuru na Borris

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Waziri Mkuu wa Uingereza na Boris Johnson na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wanatarajiwa kuzindua mpango utakaosaidia kukusanyadola bilioni tano sawa na (£3.8bn) kwa ajili ya kuwasomesha watoto kutoka jamii masikini duniani

    Idadi ya wanafunzi walioacha shule imeongezeka zaidi wakati wa janga la Covid-19.

    Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na utamaduni (Unesco) linakadiria kuwa hadi wanafunzi bilioni 1.3 duniani billioni wameacha shule huku wataalamu wakionya kuwa baadhi yao huenda wasirudi kutokana na hali ya kiuchumi ya nchi zao.

    Viongozi hao wawili pia watatangaza mpango wa kuandaa kwa pamoja kongamano kuu la elimu nchini Uingereza katikati yam waka ujao kutafuta ungwaja mkono.

    Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais Uhuru Kenyatta watawashawishi viongozi kuhakikisha wanaenda shulewa kuwekeza zaidi katika mpango huo unaofahamika kama Global Partnership for Education.

  12. Karibu katika matangazo mubashara Jumatatu 12.10.2020