Rihanna aomba msamaha kwa kutumia Hadithi ya Kiislamu

Rihanna aomba msamaha kwa kutumia Hadithi ya Kiislamu kwenye onesho la nguo za ndani za kampuni yake ya Fenty

Moja kwa moja

Asha Juma

  1. Na hadi kufikia hapo ndio natamatisha matangazo ya leo ya moja kwa moja. Kwaheri.

  2. Baadhi ya picha zinazoadhimisha mwezi wa historia ya mtu mweusi Uingereza

    JULIO ETCHART

    Chanzo cha picha, JULIO ETCHART

    Maelezo ya picha, Julio Etchart anakumbusha tamasha la Notting Hill lililofutwa mwaka kwasababu ya janga la corona.

    Mkusanyiko wa picha za watu weusi zilizo chaguliwa katika maonesho yanayoadhimisha umuhimu wa historia ya watu weusi Uingereza mwezi huu wa Oktoba.

    Zaidi ya picha 100 zimewasilishwa kwa waandalizi na zilizochaguliwa zinalenga kuzungumzia maisha ya siku za nyuma na ya sasa ya mtu mweusi na masuala yanayowakabili.

    Picha ya Dina Asher-Smith iliyopigwa na Frederic Aranda

    FREDERIC ARANDA

    Chanzo cha picha, FREDERIC ARANDA

    Maelezo ya picha, FREDERIC ARANDA

    Frederic Aranda ni msanii aliyejifunza mwenyewe na kujikita kwenye uchoraji. Amechora wengi wenye ushawishi kama Margaret Thatcher, Prince Philip, Sir Ian McKellan, Rosamund Pike na Pharrell Williams.

    Picha hii ilichukua medali katika Olimpiki ya Uingereza.

    Kina dada watatu na Hussina Raja

    HUSSINA RAJA

    Chanzo cha picha, HUSSINA RAJA

    Maelezo ya picha, HUSSINA RAJA

    Hussina Raja ni msanii wa kike wa Uingereza, mwelekezi wa filamu, mpigaji picha na pia anafanya maonesho.

    Katika picha yake ya kina dada watatu, Raja anaonesha wasanii wanaoibuka wa kike Joyce Omotola, Akuc Bol na Bel Adawa wakati wanafanya filamu ya ‘The Last King of Scotland’ huko Sheffield.

    Picha hii ya mtu aliyenyoosha mkono akiwa amekunja ngumi imepigwa na Felix Schmilinsky

    Felix Schmilinsky ni mpiga picha za filamu Mwingereza kwenye asili ya Ujerumani mwenye makao yake London.

    Picha hii ilipigwa wakati kukiwa na maandamano ya Black Lives Matter mapema mwaka huu. Schmilinsky anasema: "gari lilisimama katikati ya mkusanyiko wa waandamanaji waliokuwa mbele ya ofisi ya ubalozi wa Marekani. Alijitokeza akasimama na kuinua mkono wake huku akiwa amekunja ngumi bila kusema lolote."

    Picha ya Esther kutoka Rwanda iliyopigwa na Jenny Matthews

    JENNY MATTHEWS

    Chanzo cha picha, JENNY MATTHEWS

    Maelezo ya picha, JENNY MATTHEWS

    Jenny Matthews amekuwa mpiga picha kwa miaka 30 akiangazia migogoro na masuala ya kijamii katika magazeti ya Uingereza.

    Matthews amepiga picha za matukio ya kihistoria kama vita vya gorilla, uhuru wa Eritrea na mapigano ya kimbari Rwanda.

    Picha hii ni ya Esther, manusura wa vita vya kimbari nchini Rwanda ni kutoka kwa moja ya kazi zake.

    Picha ya Laurence iliyopigwa na Ade "Àsìkò" Okelarin

    Mpiga picha na msanii Ade "Àsìkò" Okelarin alizaliwa London, lakini miaka ya utoto wake alikuwa Lagos, Nigeria kabla ya kurejea London. Kazi yake inadhihirisha utambulisho, utamaduni, mila na desturi na pia amekuwa akifanyakazi katika mtindo wa fasheni na tasnia ya muziki.

    ADE "ÀSÌKÒ" OKELARIN

    Chanzo cha picha, ADE "ÀSÌKÒ" OKELARIN

    Maelezo ya picha, ADE "ÀSÌKÒ" OKELARIN

    Picha hii ni ya mwanamke mweusi kuashiria hisia zao kwenye ngozi, na kuangazia masuala kama ubaguzi wa rangi na imani.

    "Alama za kwenye ngozi na michoro ya tattoo inaashiria ukuaji wa imani na kuthamini asili yangu.

  3. Somalia yakanusha kuachiwa huru kwa madaktari wa Cuba

    Waziri wa mambo ya nje nchini Somalia amekanusha taarifa zinazomesema madaktari wawili wa Cuba waliotekwa nyara nchini Kenya na kupelekwa nchi jirani ya Somalia kwa karibu mwaka mmoja na nusu wameachiliwa huru.

    Madaktari hao wawili walitekwa nyara Aprili 2019 kaskazini mwa Kenya mji wa Mandera na walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Kiislamu wa kundi la al-Shabab.

    Kisha wakapelekwa katika mpaka wa Somalia ambapo wamekuwa wakizuiliwa tangu wakati huo.

    Ripoti zinasema kwamba maafisa waandamizi wa kijasusi nchini Somalia wameshiriki mazungumzo ya kuachiliwa kwao huru kutokana na ombi la serikali ya Cuba.

    Shirika la habari la Reuters limemnukuu Waziri wa mambo ya nje wa Cuba, Bruno Rodriguez, akithibitisha kuachiliwa kwao na kushukuru serikali ya Somalia kwa kuingilia kati na kuhakikisha mateka hao wameachiliwa huru.

    Hata hivyo Mawaziri wa mambo ya nje wa Cuba na Somalia wamekanusha taarifa hizo za kuachiliwa huru kwa wawili hao.

    Madaktari wa Cuba walikuwa nchini Kenya chini ya mpango wa mabadilishano uliotiwa saini mwaka 2018 ambapo madaktari zaidi ya 100 wa Cuba walipekewa nchini Kenya kusaidia Wizara ya Afya huku madaktari kadhaa wa eneo nao pia wakipelekwa nchini Cuba kwa mafunzo zaidi.

  4. Wachezaji nyota Afrika waliojiunga na timu mpya Ulaya

    Dirisha la usajili kwa Ligi kubwa za Ulaya kusajili wachezaji wapya lilifungwa Oktoba 5.

    Vilabu vya Ligi ya Primia bado vinaweza kufanya usajili baina ya vilabu hadi Oktoba 16.

    Je baadhi ya nyota wa Afrika waliojiunga na timu mpya ni kina nani?

    Tuanze na Nahonda wa timu ya Tanzania Mbwana Samatta aliondoka Aston Villa alikokuwa kwa miezi tisa tu baada ya kujiunga na Ligi ya Primia kutoka Genk mwezi Januari.

    Mbwana Samatta

    Chanzo cha picha, FENERBAHCE/TWITTER

    Maelezo ya picha, Mbwana Samatta amejiunga na Fenerbahce ya Uturuki

    Mchezaji huyo, 27, alijiunga na timu ya Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo na uwepo wake wa muda mrefu wakiwa na makubaliano ya kumnunua.

    Hatua ya kiungo wa kati wa Ghana Thomas Partey kuhamia Arsenal ilishangaza wengi lakini ndio uhamisho uliotambuliwa zaidi wakati dirisha la usajili linafungwa.

    Thomas Partey
    Maelezo ya picha, Arsenal ilifanikiwa kumsajili Thomas Partey kutoka Atletico Madrid

    Atletico Madrid haikutaka mchezaji huyo wa miaka 27 kuondoka lakini Arsenal ilitimiza yote yaliohitajika na kulipa dola milioni 59.

    Manchester united ilisajili wachezaji watano siku ya mwisho wakiwemo vijana wawili wazaliwa wa Afrika.

    Ililipa dola milioni 35 kwa ajili ya winga wa Ivory Coast Amad Diallo, 18 ambaye atajiunga nao Januari kutoka Atalanta.

    Pia imekubali kulipa zaidi ya dola milioni 4 kwa mchezaji, 16, mzaliwa wa Kinshasa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Willy Kambwala kutoka Sochaux.

    Choupo-Moting

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Choupo-Moting alifunga magoli 10 kwa PSG

    Siku ya mwisho mshambuliaji wa Cameroon Eric Maxim Choupo-Moting aliondoka Paris St-Germain na kuelekea Bayern Munich kama mbadala wa Robert Lewandowski.

    Victor Osimhen

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen alijiunga na timu ya Napoli kutoka Lille

    Awali, mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen aliondoka timu ya Ufaransa ya Lille na kuelekea Napoli huku baadhi ya vyombo vya habari vikiripoti kwamba makubaliano yake yalikuwa ya dola milioni 95.

    Chelsea ilitumia dola milioni 250 kwa wachezaji wapya akiwemo mlindalango wa Senegal Edouard Mendy kutoka Rennes kwa dola milioni 29.

    Edouard Mendy

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Edouard Mendy mchezaji mpya wa Chelsea

    Na aliyekuwa mshambuliaji wa Ivory Coast na Chelsea Salomon Kalou alijiunga na timu ya Brazil ya Botafogo Julai baada ya kuondoka Hertha Berlin kwa misimu sita.

  5. Washukiwa wa shambulizi la ugaidi la Westgate wapatikana na hatia Kenya

    Washukiwa wawili wapatikana na hatia katika shambulizi la ugaidi la Westgate Kenya

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Washukiwa wawili wapatikana na hatia katika shambulizi la ugaidi la Westgate Kenya

    Mahakama nchini Kenya imewapata washukiwa wawili na hatia ya kupanga njama ya kutekeleza ugaidi na kusaidia kundi la magaidi katika jukumu lao walilotekeleza kwenye shambulizi la Westgate mwaka 2013 mjini Nairobi.

    Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu 67.

    Mshukiwa wa tatu – mkimbizi kutoka Somalia ambaye kaka yake alikuwa mmoja wa washambuliaji ameachiliwa huru.

    Liban Abdullahi ana kitambulisho cha Kenya na ameondelewa shitaka la kuwa nchini Kenya kinyume cha sheria.

    Serikali imesema wanamgambo wanne waliotekeleza shambulizi hilo walipatikana wamefariki dunia kwenye vifusi vya jengo hilo.

    Zaidi ya watu 140 walitoa ushahidi kwenye kesi hiyo. Aidha washukiwa walikanusha madai ya njama ya kutekeleza ugaidi.

    Hakimu ametoa uamuzi kwamba washukiwa wawili wote raia wa Kenya, watahukumiwa Oktoba 22.

    Mwandishi wa BBC Ferdinand Omondi mjini Nairobi amesema kuwa hukumu yao itakuwa inasubiriwa katika nchi ambayo bado iko katika hali ya tahadhari kuu ya uwezekano wa kutokea kwa mashambulizi ya al-Shabab.

    Kundi hilo lenye kuhusishwa na kundi la al-Qaeda lina makao yake nchini Somalia na limetekeleza mashambulizi kadhaa nchini Kenya.

    Kenya ina wanajeshi nchini Somalia kusaidia kukabiliana na wanamgambo hao.

  6. Polisi Afrika Kusini yakanusha kupanga njama ya kumkamata afisa wa juu wa ANC

    Ace Magashule

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Bwana Magashule alikuwa anaongoza mkoa wa Free State

    Afrika Kusini imekanusha taarifa kwamba imetoa kibali cha kukamatwa kwa katibu mkuu wa chama tawala ANC, juu ya madai ya ufisadi.

    Msemaji Hangwani Mulaudzi, katika taarifa amesema ripoti hiyo ilikuwa na nia mbaya ya kushusha uadilifu wa polisi.

    Afisa wa Chama cha taifa cha African National Congress (ANC) Ace Magashule, amekiambia chombo cha habari cha eneo kwamba kuna uvumi kuwa kunaenda kutolewa kibali cha kukamatwa kwake.

    Bwana Magashule alikuwa anaongoza mkoa wa Free State wakati inaposemekana kwamba pesa zilizotengwa kwa ajili ya wakulima zilipoelekezwa kwengineko.

    Hata hivyo aliwahi kunanusha madai hayo wakati wa nyuma.

    Uwezekano wa kukamatwa kwake huenda kukasababisha apoteze kazi yake kwenye chama, kulingana na taarifa iliyochapishwa na chombo cha habari cha Reuters.

    Siku za hivi karibuni, Afrika Kusini imeshuhudia matukio ya kukamatwa kwa watu mashuhuri wenye kuhusishwa na madai ya ufisadi.

  7. Wanamgambo Mali wawaachia huru Mfaransa na mwanasiasa mkongwe

    Sophie Pétronin,

    Chanzo cha picha, LIBERONS SOPHIE/FACEBOOK

    Maelezo ya picha, Sophie Pétronin, 75, alitekwa nyara nchini Mali Desemba 2016

    Familia ya raia wa mwisho wa Ufaransa aliyetekwa nyara na wanamgambo wa Kiislamu nchini Mali imesema ameachiliwa huru.

    Familia hiyo imethibitisha Sophie Pétronin – mwenye umri wa miaka 75, mfanyakazi katika shirika la kutoa msaaada – yuko njiani anaelekea mji mkuu wa Bamako – Ingawa serikali ya Ufaransa bado haijathibitisha hilo.

    Bi. Pétronin alitekwa nyara na kundi la kigaidi la al-Qaeda- lenye kuhusishwa na wanaume wenye silaha kaskazini mwa mji wa Gao ambako amekuwa akiendesha shirika la kutoa msaada.

    Soumaïla Cissé

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Soumaïla Cissé alitekwa nyara akiwa kwenye msafara wa kampeni

    Taarifa huko Mali zinasema kwamba raia mwingine aliyeshikwa mateka mwanasiasa mkongwe na aliyekuwa mgombea urais Soumaïla Cissé, 70, pia nae ameachiliwa huru na wanamgambo hao.

    Mwanasiasa huyo amekuwa akizuiliwa tangu mwezi Machi.

    Inasemekana kwamba kuachiliwa kwao huru ni sehemu ya makubaliano yanayojumuisha kuachiliwa huru kwa wapiganaji wa jihadi zaidi ya 100 na mamlaka.

  8. Rais Lazarus Chakwera awasili Tanzania

    Rais Lazarus Chakwera akiwasili Tanzania

    Chanzo cha picha, Matangazo ya moja kwa moja TBC

    Maelezo ya picha, Rais Lazarus Chakwera akiwasili Tanzania

    Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ameshawasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku ya mbili.

    Rais Chakwera amepokelewa na mwenyeji wake rais John Pombe Magufuli ambaye anachukua mapumziko ya kampeni kabla ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

    Rais Chakwera akipokelewa na mwenyeji wake  Rais Magufuli

    Chanzo cha picha, Matangazo ya moja kwa moja TBC

    Maelezo ya picha, Rais Chakwera akipokelewa na mwenyeji wake Rais Magufuli

    Bwana Chakwera ni rais wa tatu kufanya ziara rasmi nchini Tanzania baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  9. Rihanna aomba radhi kwa kutumia 'Hadith' ya Kiislamu

    Rihanna

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rihanna aomba msamaha kwa kutumia Hadith ya Kiislamu kwenye onesho lake

    Rihanna aomba msamaha kwa kutumia Hadith ya Kiislamu kwenye onesho la nguo za ndani za kampuni yake ya Fenty.

    Alianza kukosolewa vibaya mtandaoni kwa kutumia wimbo uaojulikana kama Doom wa msanii Coucou Chloe, ambao unajumuisha maudhui ya Kiislamu yanayofahamika kama Hadith.

    Rihanna amesema utumiaji wa nyimbo hiyo ulikuwa "ukosefu wa umakini."

    Hadith ni sehemu ya baadhi ya maneno ambayo yanaaminika kuzungumzwa na mtume Muhammad.

    Baada ya kitabu takatifu cha Quran, Hadithi inachukuliwa kuwa baadhi ya meneno muhimu kwenye dini ya Kiislamu.

    Mashairi ya Kiarabu ya wimbo huo ni sehemu ya Hadith kuhusu siku ya kiyama.

    Baadhi ya wafuasi wake wa Kiislamu walianza kuhoji matumizi ya wimbo huo kwenye onesho lake lilioneshwa moja kwa moja kupitia mtandao wa Amazon Oktoba 2.

    Aidha, Coucou Chloe pia ameomba msamaha na kusema hakujua kwamba wimbo huo una mashairi ya dini ya Kiislamu.

    Lakinihii sio mara ya kwanza Rihanna kushutumiwa kwa kufanya mambo yasiokubalika yanayolenga dini ya Kiislamu.

    Mwaka 2013, aliombwa kuondoka katika msikiti mmoja huko Adu Dhabi baada ya kuonekana akipiga picha zisizofaa".