Baadhi ya wanafunzi kurejea shuleni juma lijalo, Kenya
Baada ya kufungwa kuanzia Machi mwaka huu, shule nchini Kenya zimepangiwa kufunguliwa Jumatatu ijayo, Oktoba, 12 kwa wanafunzi wa darasa la 4, 8 na kidato cha nne.
Moja kwa moja
Asha Juma
Je Cavani ataiokoa au ataiangusha Manchester United?

Maelezo ya picha, Je, Edinson Cavani ndio muokozi wa Manchester United? Wakati kandarasi ya Edinson Cavani na Paris St-Germain haikuongezwa mnamo mwezi Juni, huo ndio ulikuwa mwisho wa miaka saba katika klabu hiyo ya Ufaransa.
Wakati ambapo wengi wanaweza kusema walitabiri ujio wa hatu hiyo, baada ya kipindi chake msimu huo kutawaliwa na majeraha, kusalia kwenye benchi, lakini ni kidogo sana waliofikiria kwamba atajitosa kwenye mchezo wa baleti.
"Soka na densi ni mambo mawili yanayofanana kwa karibu sana kuliko vile dunia inavyofikiria," alisema hivyo Septemba wakati anasaidia kukuza kipaji cha mchezo huo kwa watoto wa eneo lake la nyumbani.
"Inapoanza, soka na densi zote zinahitaji utulivu na kuwa makini."
Na siku ya mwisho ya usajili, amechukuliwa na Machester United.
Cavani alichukulia mchezo huo na kuulinganisha na mshambuliaji ambaye amefunga zaidi ya magoli 300 kwa klabu na nchi yake alipoingia kwenye baleti.
Baadhi ya wanafunzi kurejea shuleni juma lijalo, Kenya

Maelezo ya picha, Wanafunzi kurejea shuleni Kenya Baada ya kufungwa kuanzia Machi mwaka huu, shule nchini Kenya zimepangiwa kufunguliwa Jumatatu ijayo, Oktoba, 12 kwa wanafunzi wa darasa la 4, 8 na kidato cha nne.
Tangazo hilo limetolewa na Waziri wa Elimu George Magoha huku akisisitiza kwamba mtihani wa kitaifa uliotarajiwa kufanyika Oktoba na Novemba mwaka huu utafanyika Machi 2021.
Wakati anasisitiza kwamba kutokaribiana bado ni changamoto kubwa katika taasisi nyingi, Waziri wa Elimu alisema hatua stahiki ikiwemo utumiaji wa barakoa, kudumisha kiwango cha juu cha usafi na ufuatiliaji wa kiwango cha joto mara kwa mara kutatekelezwa.
Waziri alitangaza kwamba taasisi ambazo zilitumika kama karantini tayari zimeshanyunyizwa dawa na kuagiza zingine zipulizwe dawa kabla ya wanafunzi kurejea.
Katika awamu ya kwanza ya shule kufunguliwa, watoto watakuwa na wiki moja tu ya mapumziko mwezi Desemba kabla ya shule kufunguliwa tena Januari.
Waziri aliwasihi walimu kutoa usaidizi wa kiakili na kiimani kwa wanafunzi wakati wa kipindi hiki cha janga la corona.
Tangazo hilo limetolewa wakati ambapo wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa chuo kikuu wameanza kurejea kwenye taasisi zao.
Aidha, serikali bado haijatangaza tarehe ya kufunguliwa tena kwa shule kwa wanafunzi wengine waliosalia.
Simba wafariki Kenya kwa mitego ya wawindaji
Simba watatu wamefariki katika mbuga ya Wanyama ya Maasai Mara baada ya kunaswa kwenye mitego iliyowekwa na wawindaji wakijaribu kutafuta nyama ya wanyama wa mwituni, mamlaka imesema.
Fisi wanne ni miongoni mwa waliouawa.
“Inasikitisha sana kutangaza kifo cha Rafiki, Lenkume [na] mmoja wa kijana wa Lenkume,” Mradi wa Uhifadhi wa Mara wa Wanyama Wawindaji umesema kwenye ukurasa wao wa Facebook, akimaanisha simba.
Mamlaka imeanza kusafisha eneo hilo kuondoa mitego iliyotegwa na kuchunguza nini hasa kilichotokea.
Baada ya miaka kadhaa ya matukio ya uwindaji haramu, idadi ya simba ilikuwa 2,000 pekee nchini Kenya mara ya mwisho wanahesabiwa, mwaka 2017.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Waziri wa Sierra Leone amesimamishiwa kazi juu ya ufisadi
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amewasimamisha kazi watumishi wa umma waliotajwa kwenye ripoti iliyoangazia ufisadi.
Walioathirika ni pamoja na waziri wa kilimo Dennis Vandi na katibu makamu rais, Baba Fortune.
Ripoti hiyo inayoangazia ufisadi iliyotolewa na tume maalum ya kuchunguza kubaini ukweli wa mambo imewahusisha watu kadhaa waliokuwa watumishi wa umma na wa sasa na wizi wa fedha za umma.
Waziri Vandi amesema kwamba yeye hana hatia na hakupewa fursa na tume hiyo ya kujitetea.
Wote waliotajwa wamepewa miezi mitatu kukata rufaa.
Baadhi ya waliokuwa mawaziri na maafisa kadhaa wamepigwa marufuku kuondoka nchini humo juu ya madai ya ufisadi.
Aidha, aliyekuwa rais, Ernest Bai Koroma, yuko kwenye orodha ya watu 102 waliohusishwa na madai ya ufisadi yaliyochapishwa na gazeti la Sierra Leone Telegraph.
Rais Bio ameahidi kurejesha pesa zinazodaiwa kufunjwa na mtangulizi wake.
Walioathirika na mafuriko Afrika Mashariki waongezeka mara sita zaidi

Chanzo cha picha, EPA
Maelezo ya picha, Sudan imeshuhudia mvua kubwa zaidi katika kipindi ch akarne moja Idadi ya walioathirika na mafuriko ya msimu katika eneo la Afrika Mashariki imeongezeka mara sita katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, kulingana na takwimu iliyopewa BBC na Umoja wa mataifa.
Karibu watu milioni 6 tayari wameathirika mwaka huu huku wengine milioni 1.5 wakiwa wamehama makazi yao.
Baadhi ya sehemu zinashuhudia mvua kubwa kuwahi kurekodiwa katika kipindi cha karne moja.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa yenye Kuratibu Masuala ya Kibinadamu eneo hilo, imekuwa na jukumu la msingi katika kukabiliana na hali ya dharura wakati kunapotokea mafuriko.
Na takwimu ilizokusanya inatia hafu.
“Mwaka 2016, zaidi ya watu milioni 1 waliathirika na mafuriko – hii ikimaanisha kwamba nyumba zao au biashara zao ziliharibika au walihitajika kutafuta hifadhi. Mwaka 2019, idadi hiyo iliongezeka na kufikia milioni 4.
Mwaka huu idadi hiyo tayari imefika milioni 6.
Hii ikiwa ni kabla hata ya msimu wa mvua fupi kuanza ambayo hushika kasi Novemba na hunyesha katika maeneo mengi ya Afrika mashariki.
Karibu majimbo yote nchini Sudan yameshuhudia mafuriko tangu Julai. Hali ni hiyo hiyo katika maeneo ya Ethiopia na Sudan Kusini.
Wanasayansi wanaamini kwamba joto katika bahari Hindi linaongeza kiwango cha mvua. Utafiti wa hivi karibuni kutoka chuo kikuu cha Texas, unaonesha kiwango cha mvua wakati wa vipindi vifupi kinaweza kuongezeka maradufu kufikia mwisho wa karne hii.
Madagascar yaondoa hatua ya kutotoka nje usiku iliyowekwa kwasababu ya Covid-19

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Madagascar iliweka sheria ya kutotoka nje usiku kwasababu ya kuongezeka kwa idadi ya maambukizi ya virusi vya corona. Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameondoa hatua ya kusalia ndani usiku iliyowekwa kukabiliana na usambaaji wa virusi vya corona.
Rais alitangaza kwamba shughuli za michezo zitaruhusiwa lakini kwa idadi ya watu isiozidi 200.
Aidha, watu wanaopanda ndege kwa safari za ndani ya nchi watahitajika kupimwa kuthibitishwa kuwa hawana virusi vya corona saa 48 kabla ya kuondoka na mtu ataruhusiwa tu kupanda ndege ikiwa atathibitishwa kuwa salama dhidi ya virusi hivyo.
Uwanja wa ndege mmoja tu ndio ulioidhinishwa kwa ajili ya safari za ndege za kimataifa mwezi huu kukiwa na miongozi mikali iliyowekwa kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona.
Kuvaa barakoa na hatua ya kutokaribiana bado vinaendelezwa kote nchini humo.
Madagascar ilirekodi idadi kubwa ya virusi vya corona mnamo mwezi Julai na kulazimisha serikali kuanzisha tena hatua ya kutotoka nje katika mji mkuu wa Antananarivo.
Rais Rajoelina alikuwa amepigia debe matumizi ya dawa ya miti shamba ambayo alisema kwamba inatibu virusi vya corona vya Covid-19 lakini Shirika la Afya Duniani limedumisha kwamba hakuna tiba ya ugonjwa huo.
Dawa hiyo sasa hivi inatengenezwa kwa muundo wa vidogo na inaendelea kugawanywa kote nchini humo.
Rais wa Malawi akiri kushindwa kubuni ajira milioni moja

Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Rais Lazarus Chakwera alichaguliwa tena katika uchaguzi uliorudiwa Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ameangazia ahadi yake aliotoa wakati wa kampeni ya kutengeneza ajira milioni moja na kusema kwamba serikali inaweza tu kutengeneza ajira 200,000.
Rais Chakwera alisema serikali haikuweza kutimiza ahadi peke yake na kuwa ilihitajika usaidizi kutoka kwa sekta za kibinafsi.
Alisema kwamba kila mjasiriamali alihitajika kuajiri watu wengi zaidi.
Rais alisema hayo wakati wa kusherehekea siku 100 tangu serikali yake ilipoingia madarakani hapo Jumatatu.
Ahadi ya kutengeneza ajira milioni moja ndio ilikuwa gumzo kwa Muungano wa Tonse uliochaguliwa katika uchaguzi wa urais uliorejelewa.
Wakosoaji wake wameambia vyombo vya habari kwamba muungano huo haukuwa na mpango wa kutengeneza ajira na ulikuwa tu unautumia kama mkakati wa kampeni.
Jeshi la Mali lachukua nyadhifa muhimu katika serikali mpya ya Mali

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Jeshi lachukua nyadhifa muhimu Mali Rais wa mpito nchini Mali, Bah Ndaw, ameteua serikali ya watu 25 ambapo maafisa waandamizi wa jeshi wamepewa nyadhifa muhimu.
Kulingana amri ya rais iliyosomwa kupitia kituo cha televisheni cha taifa, wizara za ulinzi, usalama, utawala wa maeneo na maridhiano ya kitaifa zote zikiwa zinaongozwa na makanali wa jeshi la Mali.
Bwana Ndaw – ambaye aliongoza jeshi la anga – alichaguliwa kuwa rais wa nchi na kiongozi wa mapinduzi.
Kufuatia kuchaguliwa kwa waziri mkuu ambaye ni raia, mamlaka za kikanda kama vile ECOWAS – inatarajiwa kuondolea nchi hiyo vikwazo ilivyoiwekea baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Agosti.
kanali Sadio Camara, mmoja wa viongozi wa waliopindua serikali, atakuwa waziri wa ulinzi, huku msemaji wa jeshi wa kundi hilo hilo, kanali Maj Ismaël Wagué, akipewa fursa ya kusimia maridhiano ya kitaifa.
Baadhi ya nyadhifa nyingine muhimu pia ziliwaendea aliyekuwa mwendesha mashtaka, Mohamed Sidda Dicko, akipewa nafasi ya idara ya sheria.
Na nyadhifa nne tu zilizopewa wanawake huku mbili tu zikitengwa kwa upinzani, M5, ambao uliongoza maandamano yaliyopelekea kumng’oa madarakani Rais Ibrahim Boubacar Keïta aliyepinduliwa na jeshi.
Mumeamkaje na karibuni katika matangazo ya moja kwa moja
