Aliyekuwa mbunge wa Burundi anashikiliwa na mamlaka kwa jaribio la kupindua serikali

Aliyekuwa mbunge wa Burundi Fabien Banciryanino anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa kile ambacho inasemekana ni jaribio la kupindua serikali, kwa mujibu wa familia.

Moja kwa moja

Asha Juma

  1. Leo ni siku ya Walimu Duniani nakuacha na video ya Mwalimu Bora Duniani mwaka 2019.

    Maelezo ya video, Vidokezo vya namna ya kufunza watoto nyumbani na Mwalimu Peter Tabichi

    Mwalimu Peter Tabichi ndio aliyetambuliwa kuwa bora duniani mwaka 2019. Tukutane kesho kwa matangazo ya moja kwa moja.

  2. George Weah ashambulia vijana kwa maneno kwa kuomba pesa

    George Weah rais wa Liberia
    Maelezo ya picha, George Weah aliingia madarakani kama rais wa Liberia Januari 2018

    Rais wa Liberia George Weah amesema akiwa kanisani kwamba anapokea ujumbe wa matusi kutoka kwa watu wanaodai kuwa ni wafuasi wake wenye hasira kwa madai kwamba hawasaidii.

    Weah aliyekuwa mchezaji soka mwenye umri wa miaka 54 anakaribia nusu ya muhula wake madarakani huku wengine wakilalamika kuwa serikali yake imeshindwa kutengeneza fursa za ajira alizoahidi alipokuwa anawania urais.

    Kupitia gazeti la FrontPage Africa, Rais amenukuliwa akiwaambia waumini kuwa kati ya jumbe 1000 anazopokea, 999 ni matusi.

    Aidha, rais ameahidi kwamba hatatoa usaidizi wowote kwa watu wanaoendelea kumtukana na kuonesha kutomheshimu kupitia ujumbe mf,upi.

    “Unamdharau na unaomba kufanyiwa kitu; Siwezi kutekeleza. Huwezi kuwa unaomba usaidizi na wakati huohuo unamtukana rais,” Bwana Weah amenukuliwa akisema.

    Pia aliwashambulia vijana wa miaka 19-20 kwa maneno wenye hamu ya kuanza kujitegemea.

    “Munajua kwamba nilikuwa na miaka 18 nikilala sakafuni? Kwanini munakimbilia maisha?” aliuliza.

  3. Aliyekuwa mkuu wa polisi Afrika Kusini afikishwa mahakamani

    Aliyekuwa mkuu wa polisi Afrika Kusini mkoa wa KwaZulu Natal amefikishwa nahakamani akihusishwa na kesi ya ufisadi.

    Kibali cha kukamatwa kwa Bi. Mmamonnye Ngobeni kilitolewa Ijumaa baada ya kutofika mahakani ingawa alihudhudria kikao cha Jumatatu.

    Mama huyo anakabiliwa na madai ya ufisadi yenye kuhusishwa na rushwa ambapo inasemekana alilipwa ajaribu kutafuta taarifa kuhusu zabuni iliyotolewa kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA ili isitishwe, kulingana na kituo cha eneo cha habari cha EWN

    Mwanahabari aliyetuma ujumbe kupitia mtandao wa Twitter aliyekuwa mahakamani amesema wakili wa Bi. Ngobeni alisema ana matumaini "kwamba ataondolewa mashtaka.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Aliyekuwa mbunge wa Burundi anashikiliwa na mamlaka kwa jaribio la kupindua serikali

    Fabien Banciryanino akiwa mbunge

    Chanzo cha picha, BUNGE LA BURUNDI

    Maelezo ya picha, Fabien Banciryanino anafahamika sana kwa kukosoa utawala wa aliyekuwa rais Pierre Nkurunziza akiwa mbunge

    Aliyekuwa mbunge wa Burundi Fabien Banciryanino anazuiliwa katika kituo cha polisi kwa kile ambacho inasemekana ni jaribio la kupindua serikali, kwa mujibu wa familia.

    Bwana Banciryanino alikamatwa Ijumaa baada ya mkutano na wanahabari aliokuwa ameuitisha siku hiyo kufutwa, mwanafamilia wa karibu amezungumza na BBC.

    Alichukuliwa na polisi kutoka nyumbani kwake katika mji mkuu wa Bunjumbura, mwanafamilia huyo aliongeza.

    Polisi bado haijasema lolote kuhusu tamko hilo.

    Mwanaume huyo aliyekuwa mbunge alikuwa mkosoaji wa aliyekuwa rais Pierre Nkurunziza, aliyefariki dunia Juni mwaka huu. Aidha, alipinga sheria yenye kumwezesha Bwana Nkurunziza kunufaika baada ya kustaafu kwake ikiwemo kuwa "kiongozi mkuu wa uzalendo".

    Mkutano wake na wanahabari Ijumaa ulikuwa ni kuhusu kuzungumzia madai ya kituo kimoja cha eneo cha YouTube kwamba alimtukana rais, Evariste Ndayishimiye, kulingana na mwana familia.

  5. Balozi Amina Mohamed wa Kenya augwa mkono na EAC kugombea nafasi ya WTO

    Balozi Amina Mohamed wa Kenya
    Maelezo ya picha, Balozi Amina Mohamed wa Kenya anagombea wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani

    Jumuiya ya Afrika Mashariki imemuidhinisha mgombea wa Kenya Amina Mohamed kuongoza Shirika la Biashara Ulimwenguni, ikiwa ni nguvu mpya aliyopata katika kinyang’anyiro hicho.

    Idhinisho hilo limetangazwa Jumapili ikiwa ni siku mbili tu kabla ya wagombea kuingia kwenye kwenye duru ya mwisho ya kufanyiwa majaribio.

    Waziri wa mambo ya nje wa Rwanda Vincent Biruta, ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la mawaziri la EAC, alisema Jumapili kwamba Bi. Mohamed amepata uungwaji mkono kutoka kwa nchi washirika kufuatia ombi la mwenyekiti wa EAC Rais Paul Kagame wa Rwanda la kumuidhinisha.

    "Tunarejelea majibu kutoka kwa nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki… juu ya ombi la kumuunga mkono mgombea wa Kenya katika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani.

    "Ningependa kuwafahamisha kwamba Balozi Amina C Mohamed ameidhinishwa kama mgombea wa Afrika Mashariki katika wadhifa wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani," Dkt Biruta aliandika kwa wanachama wenzake Kenya, Burundi, Uganda, Tanzania na Sudani kusini.

    Bi. Amina ni miongoni mwa wagombea watano waliofaulu kuingia kwa duru ya pili ya kutafuta wadhifa huo na matokeo yanatarajiwa kutangazwa Oktoba 6 kwa kutajwa kwa majina ya wawili walioingia kwenye fainali.

  6. Watu watano wafariki dunia katika ajali nchini Tanzania huku wengine 10 wakijeruhiwa

    Ajali Tanzania

    Chanzo cha picha, THE CITIZEN

    Maelezo ya picha, Ajali Tanzania

    Watu watano wamefariki dunia huku wengine 10 wakijeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha basi dogo la abiria na lori la mchanga.

    Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo katika eneo la mataa ya Chang’ombe, wilaya ya Temeke, Jijini Dar es salaam.

    Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema waliokufa ni pamoja na wanaume watatu na wanawake wawili waliokufa papo hapo.

    Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, chanjo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa basi hilo kwa kushindwa kuzingatia taa za barabarani.

    Kwa mujibu wa mashuhuda, ambao wengine walikuwa sehemu ya abiria kwenye basi hilo lililokuwa linatoka Temeke kwenye Muhimbili, wamesema pamoja na kumsisitiza dereva kuzingatia alama hizo, alipuuza kabla ya basi hilo kugongana na lori kwenye makutano.

    Daktari Meshack Shimwela, Mganga Mkuu Hospitali ya Rufaa ya Temeke amesema kuwa wengine wanne waliojeruhiwa walipata huduma ya kwanza na tayari wamepelekwa hospitali ya Muhimbili kwa tiba zaidi huku wengine wakiendelea kupata matibabu katika hospitali ya Temeke.

  7. Wachimbaji migodi Zambia 'waliowekwa karantini na mwajiri wao mchina waachiliwa huru'

    Kundi la wachimbaji migodi raia wa Zambia walioshikiliwa na mwajiri wao Mchina kwa miezi mitano kama hatua ya kiusalama kukabliana na virusi vya corona wameachiliwa huru, kulingana na taarifa ya tovuti ya gazeti la Lusaka Times.

    Kuachiliwa kwao huru Jumapili kumetokea baada ya mbunge wa eneo kuingilia kati.

    Walikuwa wamekamatwa ndani ya migodi 9 kuzuia wasipate maambukizi ya virusi vya corona na kuwaambukiza wasimamizi wao raia wa China.

    Makamu rais Saulos Chilima aliliambia bunge wiki mbili zilizopita kwamba serikali haikuwa na ufahamu wa kuzuiliwa kwao, ripoti ya tovuti hiyo inasema.

    Inasemekana mameneja wa China waliondoka kwenye mgodi huo pale ujumbe wa maafisa wa serikali uliwasili kuwaachilia huru wachimbaji hao midogi.

    Hadi kufikia sasa, Zambia imethibitisha

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  8. Uamuzi wa kesi ya shambulizi la ugaidi Westgate waahirishwa Kenya

    Wanamgambo wa al-Shabab walisema wametekeleza shambulizi hilo 2013
    Maelezo ya picha, Wanamgambo wa al-Shabab walisema wametekeleza shambulizi hilo 2013

    Hukumu ya kesi inayowakabili wanaume watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya kusaidia wanamgambo walioshambulia jumba la Westgate nchini Kenya katika mji wa Nairobi imeahirishwa hadi hapo kesho.

    Hakimu Francis Andayi amesema kwamba kulikuwa na baadhi ya vifungu katika uamuzi wake vyenye mwanya unaohitajika kuzibwa.

    Takriban watu 67 waliuawa katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa mwaka 2013, katika jumba la manunuzi la Westgate.

    Wanamgambo wa Kiislamu wenye makao yao nchini Somalia walikiri kutekeleza shambulizi hilo. Aidha serikali ilisema kwamba wanamgambo waliotekeleza shambulizi hilo waliuawa.

    Zaidi ya watu 140 walitoa ushahidi kwenye kesi hiyo ambapo washitakiwa walikanusha kufanya njama ya kutekeleza ugaidi.

    Kutolewa kwa hukumu kutahamasisha nchi ambayo bado ipo katika tahadhari ya juu kwa uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la kigaidi, na ambayo jeshi lake bado liko nchini Somalia kukabiliana na vikosi vya al-Shabab kutoka kwenye kambi zao.

  9. Ethiopia 'yapiga marufuku safari za anga juu ya bwawa la mto Nile'

    Bwawa la GERD

    Ethiopia imepiga marufuku safari za anga katika angala lake juu ya bwana iinalojenga la Grand Ethiopian Renaissance Dam (GERD) kwasababu za kiusalama, kulingana na tovuti inayomilikiwa na mwanahabari wa kujitegemea.

    "Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Ndege la Safari za Anga nchini Ethiopia, Col Wesenyeleh Hunegnaw, amemuambia mwanahabari huyo kwamba kufuatia mashauriano na mashirika husika ya usalama, anga la eneo la jimbo la Benishangul-Gumuz [kaskazini -mashariki mwa Ethiopia] ambapo bwawa hilo linajengwa ni karibu na safari zote za ndege," ripoti hiyo imesema.

    Alisema kwamba hakuna ndege ya abiria au za mizigo zitakazoruhusiwa kusafiri juu ya anga hilo lakini huenda pengine ruhusa ikatolewa kwa atakayewasilisha ombi.

    Mkuu wa jeshi la Anga, Meja Jenerali Yilma Merdasa, pia wiki iliyopita alionya kwamba kikosi cha anga kimeboresha ndege zake za kivita na inauwezo wa kulinda bwana hilo kutokana na shambulio lolote la adui.

    Bwawa hilo ambalo limezua utata linalotarajiwa kuwa kubwa zaidi Afrika, limeendelea kuzorotesha uhusiano wa Ethiopia na Misri pamoja na Sudan kwa kiasi fulani.