Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kenya yaandaa kongamano la kitaifa kujadili hali ya Covid 19
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wakuu serikali wanakutana jijini Nairobi kujadili hali ya janga la Covid-19 nchini humo.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Ethiopia yawafuta kazi maafisa wa majimbo kufuatia ghasia
Karibu maafisa 40 wa mamlaka za majimbo katika eneo la Benishangul-Gumuz nchini Ethiopia wamefutwa kazi kufuatia msururu wa ghasia, chama tawala cha Prosperity Party (PP) kimesema.
Makumi ya maafisa hao sasa wanachunguzwa, kiliongeza kusema bila kutoa maelezo zaidi.
Wilaya tano katika jimbo hilo la magharibi zimewekwa chini ya ulinzi wa majeshi ili kudhibiti ghasia ambazo zimesababisha vifo kadhaa huku mamia ya wakazi wakiachwa bilamakao wiki iliyopita.
Tume ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Ethiopia amesema kuwa imesikitishwana ghasia hizo zinazowalenga raia.
Katika shambulio la Ijumaa alfajiri , karibu watu 15 miongoni mwao wanawake waliuawa
Mashambulio mengine yaliyofanyika mapema mwezi huu yalisabisha vifo vya watu 30, japo wanaharakati wanasema idadi hiyo huenda ikafikia 80.
Baadhi ya walioathiriwa katika mashambulio hayo wanasadikiwa kutoka jamii za Amhara na Agew.Haijabainika waliotekeleza mashambulio hayo.
Siku ya Jumapili, mamlaka katika Jimbo la Amhara zililaumu maafisa wa Benishangul-Gumuz kwa kutofanya juhudi za kutosha kukabiliana na ghasia hizo .
Msemaji wa Jimbo la Amhara aliongeza kuwa jimbo hilo ‘’limeanza "kuishiwa na uvumilivu".
Ghasia zinazohusishwa na mzozo wa kikabili zimeongezeka nchini Ethiopia. Hali hiyo inaonekana kuwa changamoto kubwa inayomkabi Waziri Mkuu Wa Ethiopia na mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel Abiy Ahmed.
Kenya yaanda kongamano la kitaifa kujadili hali ya Covid 19
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na maafisa wengine wa serikali wanakutana jijini Nairobi kujadili hali ya janga la Covid-19 nchini humo.
Mkutano huo wa kitaifa, unajiri baada ya miezi sita ya kufungwa kwa shughuli za kiuchumi kama sehemu ya zilivyowekwa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona.Rais Kenyatta anatarajiwa kulegeza masharti ambayo Kenya iliweka baada ya kuripoti kisa cha kwanza cha ugonjwa wa corona mnamo Machi 13.
Lengo lake ni kutathmini kama hatua zilizochukuliwa na nchi hiyo kukabiliana na Covid -19 zilifikia malengo yake na jinsi kutafuta mbinu ya itakayotumiwa kuendelea mbele na shughuli za kawaida licha ya kuwepo kwa janga la corona.
Baadhi ya hatua hizo ni pamoja nakafyu ya kitaifana kudhibiriwa kwa shughuli za hoteli, migahawa, vilabu, maduka makubwa na mikusanyiko ya umma.
Kufikia Jumapili, Kenya ilikuwa imethibitisha watu 38,115 wameambukizwa virusi vya corona ikiwa ni pamoja na watu 24,621 waliopona na vifo 691.
Nchi hiyo imefanyia uchunguzi sampuli 540,308 za watu walioshukiwa kuwa na ugonjwa huo.
Mfahamu bilionea aliyetoa mali yake yote kwa masikini
Charles "Chuck" Feeney ni bilionea ambaye alikuwa na ndoto za kumaliza mali yake yote akiwa hai, kwa kutoa fedha zake zote kwa mashirika ya hisani.
Mfanyabiashara huyo wa Marekani mwenye umri wa miaka 89 , hatimaye amefikia lengo lake siku chache ziliopita alipotoa dola ,milioni 8,000 kusimamia miradi ya hisani duniani.
TikTok yaponea kupigwa marufuku Marekani
Mahakama nchini Marekani imesitisha kwa muda agizo la serikali la kupiga marufuku mtandao wa kijamii wa TikTok.
Jaji Carl Nichols wa Mahahakama ya Wilaya ya Columbia alitoa agizo hilo Jumapili jioni baada ya kusikiliza kesi kwa dakika 90.
TikTok imeridhika na uamuzi huo na kuapa kuwa itaendelea kutete haki yake.
"Tunashukuru kwamba mahakama imekubaliana na hoja zetu za kisheria na kuzuia hatua ya serikali kupiga marufuku programu ya TikTok," ilisema katika taarifa.
Watumiaji wa sasa wa programu hiyo wangeruhusiwa kuendelea kuitumia lakini wale ambao huenda waliifuta katika simu zao hawwengeliweza kuipakuwa tena kwenye simu za Adriod ama Google play store
Wafanyakazi wa KNH wagoma kushinikiza nyongeza ya mishahara
Huduma za afya katika hospital kuu ya rufaa ya Kenyatta nchini Kenya(KNH) zimekwama baada ya zaidi ya wafanyakazi 4000 wa afya kuanza mgomo wao siku ya Jumatatu kushinikiza nyongeza ya mishahara.
Mgonjwa mmoja ameripotiwa kufariki huku wengine kadhaa wakiachwa bila njia mbadala ya kupata huduma ya afya.
Wafanyakazi wa KNH wanalalamikia hatua ya Tume ya mishahara kutekeleza nyongeza ya mishahara yao ya shilingi milioni 301 iliyopitishwa na bunge na kuidhinishwa na hazina ya kitaifa mwaka 2012.
Katibu Mkuu wa Muungano wa Wauguzi nchini Kenya Seth Panyako, amesema Tume ya SRC imekataa kutekeleza nyongeza mishahara yao licha ya asasi mbali mbaii za serikali kuipatia idhini ya kufanya hivyo.
Virusi vya corona: Madaktari wa China wawasili Zimbabwe
Kundi la madaktari 10 kutoka China limewasili nchini Zimbabwe kusaidia nchi hiyo kupambana na janga la virusi vya .
Madaktari hao watahudumu katika hospitali za Parirenyatwa kwa miezi 12 zijazo,kwa mujibu wa ripotiya gazeti la serikali la Herald.
Mkuu wa madaktari hao, Dkt Luo Weiqiang, amenukuliwa akisema madaktari hao pia watanadi tiba asilia kutoka.
Ubalozi wa China uliweka picha ya madaktari hao kwenye Twitter yake:
Tume ya Uchaguzi Tanzania yamtaka Lissu kufika mbele yake kujieleza
Tume ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imemtaka mgombea wa urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kufika mbele ya kamati ya maadili ya Taifa kutoa ushahidi kuhusu madai aliyotoa dhidi yake.
Mkurugenzi wa wa Uchaguzi Dkt Charlse Muhera amesema kuwa Tume hiyo imesikitishwa na taarifa za uwongo, uzushi na upotoshaji zilizotolewa na mgombea wa urais wa upinzani Tundu Lissu siku ya Jumamosi, akisema kwamba Rais John Magufuli aliitisha kikao cha wasimamizi wa uchaguzi wa majimbo yote nchi nzima mjini Dodoma kwa lengo la kuhujumu uchaguzi.
NEC imesema baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli.
‘’Kitendo cha baadhi ya wagombea wa Rais hasa mgombea wa Chadema Tundu Lissu kuikashifu Tume kwamba itaiba kura zake ni kitendo cha kuidhalilisha Tume na kutaka kuitisha Tume ili isifanye kazi zake kwa uhuru’’ alisema Dkt Muhera Charlse.
Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imetoa taarifa kukanusha madai hayo.
Bw. Lissu mwenyewe amethibitisha kuwa Jumatatu asubuhi Msajili wa Vyama vya Kisiasa nchini humo ameandikia CHADEMA akitaka chama hicho kueleza kwa nini mgombea wake wa urais anatishia amani.
Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Mali ateuliwa kuwa Waziri Mkuu
Rais wa mpito wa Mali Bah Ndaw amemteua waziri Mkuu mpya.
Bw. Ndaw amemteua mwanadiplomasia wa Moctar Ouane kuchukua nafasi hiyo.
Ouane alihudumu kama Waziri wa Mambo ya nje wa Mali kati ya 2004 na 2011.
Alikuwa mjumbe wa kudumu wa Mali katika Umoja wa Mataifa kuanzia 1995 hadi 2002 na baadae kuwa mshahuri masuala ya kidiplomasia wa Muungano wa kiuchumi wa nchi za Afrika Magharibi, Ecowas.
Uteuzi wake huenda ukachangia Mali kuondolewa vikwazo iliyowekewa na Ecowas kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi uliopita.
Kiongozi wa mapinduzi hayo Kanali Assimi Goita alikuwa amemteua Bw.Ndaw – ambaye aliidhinishwa rasmi Ijumaa iliyopita – kuwa rais wa mpito.
Rwanda yajiandaa kufungua shule licha ya Covid-19
Serikali ya Rwanda imesema shule zote zitafunguliwa ifikapo mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa Waziri wa Elimu Valentine Uwamariya uamuzi wakufungua shule utaanza na Vyuo Vikuu.
‘’Shule zitafungua kwa awamu tofauti kuanzia ngazi ya Vyuo Vikuu ambavyo tubatarajia vitafungua milango mwezi ujao. Shule nyingine kama sekondari, shule za msingi na chekechea tunatarajia kwamba zitakuwa zimeshafunguliwa’’ alisema Bi Uwamaria
Wizara ya Elimu inasema shule zitatakiwa kuzingatia masharti yaliyopo ya kujilinda na Covid -19 kama kuwa na sehemu ya kuosha mikono, kuvaa barakoa kwa kila mwanafunzi na kuacha nafasi ya mita moja kati ya wanafunzi.
Karibu katika matangazo Mubashara Jumatatu 28.09.2020