Tanzania yaondoa marufuku dhidi ya ndege za Kenya

Tanzania imeondoa marufuku ya safari za ndege za Kenya iliyokuwa imeiweka mwezi uliopita

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja, tukutane tena kesho.

  2. Taji alilovaa Notorious B.I.G lauzwa maelfu ya dola

    Taji la Notorious B.I.G

    Chanzo cha picha, G

    Taji alilovaa msanii maarufu wa mtindo wa Hip hop, marehemu Notorious B.I.G alilovaa katika picha aliyopigwa muda mfupi kabla ya kuuawa kwake,limenunuliwa dola 594,750, kwa mujibu wa kampuni ya biashara Sotheby iliyoliuza.

    Mauzo ya taji hilo yamefanyika katika mnada uliofanyika usiku wa Jumanne mjini New York ambapo pia barua za mapenzi za Tupac Shakur alipokuwa kijana mdogo ziliuzwa.

    Mwezi uliopita , kampuni ya Sotheby's ilikuwa imesema taji hilo litagharimu kati ya dola 200,000 na dola 300,000, za Marekani na sasa limeuzwa kwa karibu mara mbili ya thamani iliyokadiriwa awali.

    Notorious B.I.G au Biggie alivaa taji hili siku tatu tu kabla ya kupigwa risasi hadi kufa tarehe 09/03/1997, akiwa na umri wa miaka 24.

    Barua za Tupac Shakur alizomuandikia mpenzi wake waliyekuwa wakisoma pamoja katika shule ya Baltimore, ziliuzwa dola 75,600.

  3. Je kuna chembechembe za uhai katika sayari ya Venus?

    Wazo kwamba viumbe wanaoishi wanaelea katika mawingu ya sayari ya venus ni uwezekano uliopo.

    Lakini hilo ni kwa mujibu wa wataalamu wa angani baada ya kugundua kitu kilichopo angani ambacho hakiwezi kuelezeka.

    Ni gesi kwa jina Phosphane PH3, molekyuli ilioundwa kutokana na atomu moja ya Phosphorous na tatu za Hydrogen... Soma zaidi taarifa hii

  4. Kuna matumaini madogo ya ukuaji wa uchumi wa Kenya

    Kiwanda cha nguo Kenya

    Chanzo cha picha, AFP

    Shirika linaloongoza kwa utoaji wa viwango linasema uchumi wa Kenya utakua kwa asilimia moja mwaka 2020, kikiwa ni kiwango cha chini cha matarajio ya ukuaji kilichotolewa awali.

    Awali Shirika hilo Moody lilibashiri kuwa kiwango cha uchumi wa taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi Afrika Mashariki kingefika asilimia sita kabla ya kuwasili kwa virusi vya corona.

    Sekta ya utalii imeathiriwa kwa kiwango kikubwa na janga la corona, na huenda isiweze kurejea katika hali yake ya awali kwa miaka mitatu.

    Hatahivyo Moody linasema kutakuwa na ukuaji wa uchumi wa takriban asilimia tano katika mwaka 2021.

    Limeonya, hatahivyo, juu ya kuongezeka kwa hasara kwasababu ya kushuka kwa kiwango cha kodi ya mapato na kubanwa kwa matumizi ya serikali.

    Shirika la fedha duniani IMF limebashiri kuwa chumi za mataifa yote ya bara la Afrika zitapungua kwa asilimia moja nukta tano katika mwaka 2020.

  5. Marekani yamuwekea vikwazo mke wa rais zamani wa Gambia

    Yahaya Jammeh na mkewe Zenab Jammeh

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Zineb Jammeh, mke wa rais wa zamani wa Gambia, Yahya Jammeh.

    Zineb anaaminiwa kusaidia au kuruhusu shughuli za ufisadi wakati wa utawala wa mume wake wa miaka 22 katika taifa hilo la magharibi mwa Afrika.

    "Zineb Jammeh alitumia nafasi yake kusaidia kwa mali, kudhamini, au kutoa usaidizi kwa mume wake. Alitumia wakfu na misaada kama chambo kusaidia usafirishaji haramu wa pesa kwa mume wake," taarifa ilisema.

    Rais huyo wa wa zamani aliiongoza Gambia kwa miaka 20. Alitoroka nchi baada ya kushindwa katika uchaguzi wa mwaka 2017 na sasa anaishi Equatorial Guinea.

  6. Ecowas inatumai utawala wa kiraia utarejea Mali ' ndani ya siku kadhaa'

    Viongozi wa Mali na ECOWAS

    Chanzo cha picha, EPA

    Rais wa Ghana, Nana Akufo- Addo, amesema viongozi wa magharibi mwa Afrika wana matumaini ya kuiona serikali inayoongozwa na raia ikiwekwa nchini Mali katika kipindi cha siku kadhaa.

    Alizungumza baada ya mazungumzo baina ya viongozi wa kikanda na wanamgambo wa Junta ambao walichukua mamlaka nchini Mali mwezi uliopita.

    Bwana Akufo- Addo alisema kuwa jumuiya ya kiuchumi ya nchi zilizoko magharibi mwa Afrika Ecowas, wataondoa vikwazo " mara moja " pale raia watakapochukua mamlaka nchini Mali.

    Viongozi wa Ecowas walikutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kwa mazungumzo juu ya mzozo wa kisiasa wa Mali.

    Viongozi wa jeshi la Mali junta, Kanali Assimi Goita, pamoja na wawakilishi kutoka Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika pia walihudhuria.

    Viongozi wa mataifa ya Afrika magharibi wanahofia kwamba hali ya usalama nchini Mali inaweza kuharibiwa zaidi na kudhoofishwa kwa juhudi zilizofanyika kuyashinda makundi ya wapiganaji wa kiislamu.

    Jumamosi, upinzani unaofahamika kama M5-RFP ulipinga pendekezo la jeshi la mchakato wa kipindi cha mpito cha miezi 18.

  7. Kituo cha habari cha Tanzania chapata watazamaji bilioni moja katika YouTube

    Chombo cha habari za mtandaoni nchini Tanzania Millard Ayo kimekuwa cha kwanza barani Afrika kupata watazamaji bilioni moja katika mtandao wa YouTube.

    Mmiliki wake-ambaye ana jina hilo hilo- Millard Ayo amewashukuru wale wanaokitazama kituo chake kwa ajili ya kupata habari.

    Ali Tweet picha yake ya kusherehekea mafanikio yake:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  8. Ndege za Kenya kupaa katika anga za Tanzania tena

  9. Watuhumiwa 32 washitakiwa kuwa wapiganaji wa kikundi cha uhalifu

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili
  10. Polisi Uganda kupima DNA za familia inayodai mtoto aliyekatwa kichwa ni wao

  11. ‘Shujaa' wa filamu ya Hoteli Rwanda atapewa haki kisheria, yasema Rwanda