Joseph Kabila arejea rasmi ndani ya siasa za DRC baada ya kustaafu
Rais wa zamani wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Joseph Kabange Kabila amewasili leo katika bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza rasmi kama Seneta
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Jack Grealish asaini mkataba mpya na Aston Villa

Chanzo cha picha, Getty Images
Nahodha wa Aston Villa, Jack Grealish amesaini mkataba mpya na wa miaka mitano na klabu hiyo.
Mchezaji huyo nyota mwenye umri wa miaka 25- kutoka England alikuwa amehusishwa na taarifa za kuhama kutoka Villa Park msimu huu, lakini alitangaza kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
Grealish amekuwa katika klabu hiyo ya nyumbani tangu alipokuwa na umri wa miaka minane ambapo alicheza kwa mara ya kwanza mwaka matika msimu wa 2013-14.
"Ni kwabu yangu, nyumbani kwangu na ninafuraha sana," alisema Grealish baada ya kuukubali mkataba mpya leo Jumanne.
Kiungo huyo wa safu ya mashambulizi ya kati, ambaye alicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya England dhidi ya Denmark wiki iliyopita, amesaini mkataba hadi mwaka 2025
Alexei Navalny kurejea Urusi baada ya kupewa sumu

Chanzo cha picha, @NAVALNY
Maelezo ya picha, Navalny alituma picha hii kwenye Instagram kutoka kwenye kitanda cha hospitali nchini Ujerumani Mpinzani wa Urusi aliyepewa sumu Alexei Navalny atarudi Urusi, amesema msemaji wake.
"Inanishangaza ni kwanini mtu yeyote anaweza kufikiria ," Kira Yarmysh aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.
Bwana Navalny pia alituma picha kwenye Instagram ka mara ya kwanza tangu apewe sumu, akitangaza kwamba alikua anapumua bila usaidizi wa mashine ya kusaidia kupumua (ventilation).
Alianguka alipokua safarini ndani ya ndege alipokuwa akitoka Siberia tarehe 20 Agosti. Vipimo vya kimatibabu vimeonesha kuwa alipewa sumu kali ya neva ya Novichok
Alihamishiwa katika hospitali ya Charité iliyopo katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin.
Washirika wake walidai kuwa alipewa sumu kwa maaagizo ya rais wa Urusi Vladimir Putin. Serikali ya Kremlin ilikana kuhusika.
Rais mstaafu wa DRC Joseph Kabila awasili bungeni kama seneta

Chanzo cha picha, Cellule communication senat
Maelezo ya picha, Bwana Kabila (wa pili kutoka kushoto) anakuwa seneta wa maisha, kulingana na katiba ya DRC Rais wa zamani wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Joseph Kabange Kabila amewasili leo katika bunge la nchi hiyo kwa mara ya kwanza rasmi kama Seneta.
Kwa mujibu wa katiba ya DRC kwasababu ni rais mstaafu moja kwa moja anakuwa seneta wa maisha.

Chanzo cha picha, Cellule communication senat
Bw. Kabila mwenye umri wa miaka 49, alikuwa rais wa wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kati ya Januari 2001 hadi 2019, alipoondoka madarakani baada na Uongozi wa nchi hiyo kuchukuliwa na rais wa sasa Felix Tshisekedi baada ya uchaguzi uliotawaliwa na vurugu na maandamano.

Chanzo cha picha, PARLIAMENT DR CONGO
Wengi wanamuona Bwana Kabila kama mtu mwenye ushawishi wa kisiasa katia taifa hilo na kwamba huenda akarejea tena mamlakani.
Chama cha kabila kinataka sheria ya uchaguzi nchini humo ifanyiwe mabadiliko makubwa na uchaguzi wa rais ufanyike bungeni, badala ya rais kuchaguliwa na wananchi.

Chanzo cha picha, EPA
Mjumbe wa Marekani katika mkutano wa kutafuta amani nchini Afghanstan ameiambia BBC kuwa "hafurahii" makubalino yenye utata ya kuwaachia huru wafungwa 5,000 wa Talban ili kufanikisha mazungumzo ya amani ya kihistoria.
Hatahivyo mwakilishi huyo Lyse Doucet, Zalmay Khalilzad aliongeza kuwa "Inabidi kufanya maamuzi magumu". Soma zaidi taarifa hii
Rais Yoweri Museveni aadhimisha siku ya kuzaliwa
Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo amefanya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa.
Bwana Museveni ambaye leo ametimiza umri wa miaka 76, ni miongoni mwa marais wa Afrika waliohudumu kwa miaka mingi ambapo aliingia mwaka 1986.
Bwana Museveni ametangaza nia yake ya kuwania kiti hicho baada ya kuidhinishwa na chama chake cha NRM kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa mwaka ujao..
Mtoto wa Museveni wa kiume Muhoozi Kainerugaba alikuwa ni miongoni mwa raia wa Uganda waliotuma ujumbe wa kumtakia kile la heri katika siku ya kuzaliwa kupitia mitandao ya kijamii:
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Ruka X ujumbe, 3Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Ruka X ujumbe, 4Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Corona imerudisha maendeleo ya dunia nyuma miaka zaidi ya 20

Chanzo cha picha, REUTERS
Ripoti ya utafiti wa wakfu wa Bill & Melinda Gates imebainisha kuwa kusambaa vya virusi vya corona kote duniani kumerudisha nyuma maendeleo ya dunia kwa miaka zaidi ya 20.
Kulingana na utafiti huo, mamilioni ya watu duniani wamezidi kuishi zaidi katika maisha yanayotofautiana, magonjwa na umasikini.
Wakfu huo wa Bill & Melinda Gates unasema kuwa hali hiyo inaathiri malengo mengi ya Umoja wa mataifa yanayolenga kuleta maendeleo duniani.
Akizungumza na BBC, Bill Gates alisema kuwa chanjo ya Covid-19 iliyotengenezwa na kufikia kiwango stahiki huenda ikapatikana mwaka ujao wa 2021.
Rais wa zamani wa Ivory Coast azuiwa kugombea urais

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Wafuasi wa Laurent Gbagbo walikuwa wamewasilisha nyaraka zake za kugombea urais Mahakama ya katiba nchini Ivory Coast aimemzuwia rais wa zamani wa nchi hiyo, Laurent Gbagbo, na waziri mkuu wa zamani, Guillaume Soro, kugombea urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika nchini humo mwezi ujao.
Tume ya uchaguzi ilikuia tayari imekwishasema kuwa yeyote mwenye rekodi ya uhalifu atazuiwa kugombea.
Kwa pamoja Laurent Gbagbo na Guillaume Soro walipatikana na hatia.
Awali, maandamano yaliibuka katika miji kadhaa kupinga uamuzi wa Rais Alassane Ouattara wa kugombea muhula wa tatu, kitu ambacho katiba ya Ivory Coast inazuwia.
Watu kumi na watano walikufa katika ghasia tangu mwezi uliopita alipotangaza kwamba atagombea tena urais.
Alichukua uamuzi huo baada ya mrithi wake aliyemchagua kufa ghafla mwezi Julai.
Umoja wa Ulaya kutoa Bilioni 70 kusaidia Tanzania kupambana na corona

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Rais Magufuli alisema kuwa shetani alitaka kuitawala dunia kupitia virusi vya corona Umoja wa Ulaya umesema uko tayari kutoa kiasi cha Euro milioni 27 sawa na takriban shilingi bilioni 70 za Tanzania kwa lengo la kusaidia mipango ya kukabiliana na janga la Covid 19 na madhara yake ya kiuchumi, imesema taarifa ya Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Nia ya msaada huu wa Umoja wa Ulaya unakuja wakati Tanzania ikiwa imekwisha tangaza kumalizika kwa ugonjwa wa Corona nchini humo.
Akihutubia Jumatatu katika mkutano wa kampeni za uchaguzi, Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alisema kuwa shetani alitaka kuitawala dunia kupitia virusi vya corona lakini hana nafasi nchini Tanzania.
Magufuli alisema kuwa ''haiwezekani kwa uchumi wa dunia kufungwa kwasababu ya ugonjwa’'
Akizungumza katika mkutano huo Chato Geita, Magufuli alisema, bahati nzuri, serikali yake haikukubali shinikizo la kufunga shughuli za kiuchumi na kukaa nyumbani ’’lockdown’’.
Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Bw. Charles Michel, alisema fedha hizo zinalenga kutumika kuweka miundombinu ya umeme na maji katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizojengwa na rais Magufuli katika maeneo mbali mbali ya nchi kama hatua ya Muungano huo ya kuunga mkono juhudi zilizofanywa na serikali katika kupambana na virusi vya corona.
Taratibu za kutolewa kwa fedha hizo ziko katika hatua za mwisho, imesama taarifa hiyo inasema.
Trump aapa kulipiza mara '1,000' shambulio la Iran dhidi ya balozi wa Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Rais wa Marekani Donald Trump ameapa kujibu mara "1,000’," kwa shambulio lolote la Iran.
Hii ni baada ya taarifa kwamba Iran ilikuwa inapanga kumuua balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini, Lana Marks.
"Shambulio lolotela Iran, la muundo wowote, dhidi ya Marekani litakutana na shambulio dhidi ya Iran ambalo litakuwa ni kubwa mara 1,000 !" Bwana Trump alitweet Jumatatu.
Ruka X ujumbe, 1Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Ruka X ujumbe, 2Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje wa Iran Saeed Khatibzadeh amepuuzilia mbali taarifa juu ya mpango wa mauaji ambao kwanza uliripotiwa na Politico.
Iliripoti kuwa Iran ilikuwa inapanga kumuua Balozi wa Marekani, ambaye ni rafiki wa muda mrefu wa Rais Trump, katika hatua yake ya kujibu mauaji ya Jenerali Qasem Soleimani mwezi januari.
Gen Soleimani aliuawa katika shambulio za ndege za Marekani zisizokuwa na rubani Baghdad mwezi Januari.
Waliohusika na ajali ya moto katika shule ya Kyerwa Tanzania kuwajibishwa

Mkuu wa polisi nchini Tanzania Inspekta Jenerali Simon Siro ameapa kuwawajibisha waliohusika na ajali ya moto iliyowauwa watoto 10 shule ya Byamungu English Medium Primary School iliyoko wilayani Kyerwa.
Bwana Siro amesema tayari Mmiliki wa shule hiyo amekamatwa, lakini akasema wahusika wengine pia watawajibishwa:
''Ukiliona jengo lenyewe sijui kama wakaguzi...afisa elimu alijua kama watoto walikuwa wanalala katika hali hii. Ukiangalia wayaring iliyofanywa ni ya kienyeji sana'', amesema Inspekta Jenerali Siro alipozungumza na waandishi wa habari.
Bwana Siro amesema matofali yaliyojenga shule hiyo yako dhaifu sana: ''Kikubwa Hatujafahamu nini chanzo hasa ni nini, lakini kwa haraka inaonekana jengo halikuwa madhubuti. Ndio maana tumemkamata mwenye shule...lakini pia nimesema watafute Afisa elimu na Wakaguzi wote waliokuwa wanakuja kukagua hii shule walikuwa wanaona watoto wanakaa wapi?, jengo lilia imara?, ni lazima hapa tuwe wakali kwasababu tayri maisha ya watu yamekwisha ondoka'', aliongeza.

Chanzo cha picha, Credo radio
Maelezo ya picha, Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni wakati ajali ya moto ilipotokea Bwana Siro amesema kuwa wanajaribu kutafuta vyanzo ikiwa ni pamoja na uwezekano wa adui wa nje kutumia mwanya kufanya jambo hilo.
Amewataka wakazi wa Kyerwa kushirikiana kutoa taarifa zozote juu ya chanzo cha ajali hiyo.
Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo, na mpaka sasa chanzo cha moto hakijajulikana.
Hujambo na karibu kwa matangazo mubashara leo tarehe 15.09.2020
