Lissu amtaka Rais Magufuli ashiriki mdahalo wa televisheni

Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amemtaka Rais John Magufuli ashiriki p kabla ya uchaguzi mkuuwa mwezi Oktoba.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho

  2. Akamatwa mbele ya bunge la Uganda akiwa na kichwa cha mtoto

    The Parliament of Uganda

    Chanzo cha picha, The Parliament of Uganda

    Polisi nchini Uganda imemkamata mbele ya bunge la taifa hilo mwanaume mmoja aliyekuwa amebeba kikapu kilichokuwa na kichwa cha mtoto.

    Hata hivyo haijawa wazi ni ujumbe gani aliotaka kuufikisha kwa wabunge.

    Haijafahamika piani wapi na ni kwa vipi alipata kichwa hicho.

    Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa katika idara ya upelekezi wa makosa ya jinai , ambako anahojiwa.

    Chanzo cha habari katika Idara ya upelelezi nchini humo kimesema kwamba kisa cha kutoweka kwa mtoto kiliripotiwa katika wilaya ya Masaka, kusini mwa Kampala, siku ya Jumapili. Mwili wa mtoto ambao haukuwa na kichwa pia ulipatikana siku hiyo hiyo wilayani humo.

    Wachunguzi wanataka kubaini iwapo tukio hilo lina uhusiano na kichwa ambacho mwanaume huyo amekamatwa nacho.

    Katika miaka ya 90 hadi mapema 2000 na zaidi, Uganda ilishuhudia wimbi la utekaji nyara na mauaji ya watoto, ambapo iliaminiwa kuwa miili yao ilitumiwa kama kafara.

    Na katika miaka ya hivi karibuni, kumekuwa na matukio ya wananaharakati wanaotupa vitoto vya nguruwe katika maeneo ya bunge, kama ishara ya kupinga ufisadi na ukosefu wa ajira kwa vijana.

  3. Lissu amtaka Rais Magufuli ashiriki mdahalo wa televisheni

    LISSU

    Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu amemtaka Rais John Magufuli ashiriki kabla ya uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

    Rais Magufuli anawania muhula wa pili wa miaka mitano, huku hofu ikiendelea kuongezeka ya ukandamizaji dhidi ya vyama vya upinzani.

    Bado Bwana Magufuli hajajibu kuhusu wito huo kutoka kwa Lissu.

    Hii si mara ya kwanza kwa Bwana Lissu kumtaka Rais Magufuli ashiriki mdahalo wa wagombea wa urais.

    Bwana Lissu, ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani Chadema, alisema kuwa mdahalo wa televisheni wa wagombea wa urais utakuwa ni "afya kwa demokrasia ya nchi hiyo".

    Aliuambia mkutano wa kampeni kwamba rais hapaswi kuogopa kufanya mdahalo na mtu ambaye hajawahi kuwa rais kama yeye.

    Alituma picha ya video hii katika mkutano wa kampeni:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  4. Joto lapasua barafu katika ncha ya dunia

    Mabadiliko ya hali ya hewa katika Greenland

    Sehemu kubwa ya barafu imemeguka kutoka katika hifadhi kubwa ya theluji iliyosalia ya - 79N, au Nioghalvfjerdsfjorden – katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Greenland.

    Sehemu iliyomeguka inachukua karibu kilomita 110 za mraba; picha za setilaiti zinaionesha likiwa limemeguka katika vipande vidogo vidogo.

    Wanasayansi wanasema kuyeyuka zaidi kwa theluji hiyo ni ushahidi wa mabadiliko ya haraka ya hali ya hewa katika eneo hilo la Greenland.

    "Hali ya hewa katika kanda hiyo imekuwa ya joto kwa kiwango cha nyuzi joto 3 tangu mwaka 1980," amesema Dkt Jenny Turton.

    Barafu inashambuliwa  na joto kutoka juu na chini yake

    Chanzo cha picha, COPERNICUS DATA/ESA/SENTINEL-2B

    Maelezo ya picha, Barafu inashambuliwa na joto kutoka juu na chini yake

    "Na miaka ya 2019 na 2020, kanda hiyo ilirekodi vipimo vya hali ya juu vya joto kuwahi kurekodiwa katika msimu wa majira ya joto ," alisema mtafiti wa maeneo ya ncha ya dunia katika chuo Kikuu cha Friedrich-Alexander nchini Ujerumani akiungumza na BBC.

    Eneo lililofunikwa na theluji katika nchi ya dunia linalofahamika kama Nioghalvfjerdsfjorden- lina urefu unaokadiriwa kuwa sawa na kilomita 80 na upana wa kilomita 20 na lina theluji au barafu inayoenea hadi Kaskazini magharibi mwa ukanda wa barafu wa Greenland - ambako inamwagika kwenye ardhi hadi baharini na kuelea tena.

  5. Ethiopia yaanza kutumia noti mpya za benki

    Ethiopia inaanza kutumia noti mpya za benki katika hatua ambayo Waziri Mkuu wa nchi hiyo Abiy Ahmed anasema itasaidia kukabiliana na uhisani wa shughuli haramu na ufisadi.

    Miundo mipya ya noti za thamani ya Birr 10, 50 na 100 zilifichuliwa pamoja na noti mpya za thamani ya Birr 200.

    Bwana Abiy alitweet pesa mpya. Alisema zimetengenezwa kwa muundo unaoimarisha usalama wa pesa ili kuepuka noti gushi:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  6. Kwa picha: Tuzo za picha za vichekesho vya wanyamapori

    Tabasamu,  Picha hii iliyopigwa na Arthur Telle Thiemann  El Hierro, katika visiwa vya Canary

    Chanzo cha picha, ARTHUR TELLE THIEMANN

    Maelezo ya picha, Tabasamu, Picha hii iliyopigwa na Arthur Telle Thiemann El Hierro, katika visiwa vya Canary

    Tuzo za picha za vichekesho za wanyamapori 2020 zimefichuliwa. Picha ya samaki anayeonekana kutabasamu, dubu akipepea kutoka mbali na kila aina ya kobe wa majini ni miongoni mwa picha zilizofuzu kufikia mchujo wa fainali kitengo cha picha za kuchekesha.

    Tuzo ya picha za wanyamapori- The Comedy Wildlife Photography ilianzishwa na Paul Joynson-Hicks na Tom Sullam, wote wakiwa ni wapigapicha waliosomea na wahifadhi wa wanyamapori wanaoipenda kazi hiyo. Hizi ni baadhi ya picha zilizofikia fainali:

    Terry the Turtle - kobe wa majini, ilipigwa na  Mark Fitzpatrick, katika eneo la Lady Elliot Island, Queensland, Australia

    Chanzo cha picha, MARK FITZPATRICK

    Maelezo ya picha, Terry the Turtle - kobe wa majini, ilipigwa na Mark Fitzpatrick, katika eneo la Lady Elliot Island, Queensland, Australia
    Picha ya nyani  iliyopigwa na  Martin Grace.  karibu na mto Chobe nchini Botswana

    Chanzo cha picha, MARTIN GRACE

    Maelezo ya picha, Picha ya nyani iliyopigwa na Martin Grace. karibu na mto Chobe nchini Botswana
    Picha ya nyani wa maeneo theruji Japan -Picha iliyopigwa na  Wei Ping Peng.

    Chanzo cha picha, Wei Ping Peng

    Maelezo ya picha, Picha ya nyani wa maeneo theruji Japan -Picha iliyopigwa na Wei Ping Peng
    Kuibia picha, Picha ya twiga hawa ilipigwa na Brigitte Alcalay Marcon katika mbuga ya wanyama ya Etosha, Namibia

    Chanzo cha picha, BRIGITTE ALCALAY MARCON

    Maelezo ya picha, Kuibia picha, Picha ya twiga hawa ilipigwa na Brigitte Alcalay Marcon katika mbuga ya wanyama ya Etosha, Namibia
  7. Miili yaondolewa katika mgodi wa dhahabu Kivu Kisini DRC

    Kumekuwa na matukio mengi ya ajali katika migodi midogo ya madini DRC

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Kumekuwa na matukio mengi ya ajali katika migodi midogo ya madini DRC

    Wahudumu wa uokozi wamegundua miili ya wachimba migodi waliokufa wakati mgodi wa madini ulipoporomoka karibu mji wa Kamituga katika jimbo la Kivu Kusini katika Jamuhuri ya kidemokrasi ya Kongo.

    Takriban watu 50 wanahofiwa kufa katika tukio hilo lililotokea Ijumaa, kwa mujibu wa idadi iliyotolewa na maafisa wa eneo hilo.

    “Tayari tumeiondoa miili 19,” Mwandishi wa BBC wa Mashariki mwa DRC , Byobe Malenga amesema.

    Kwa mujibu meya wa mji wa Kamituga , Alexandre Bundya familia 19 zinawatafuta watu waliopotea katika mgodi huo, lakini hakuweza kuthibitisha ni idadi kamili ya wachimba migodi waliokuwemo ndani ya mgodi wakati ulipoporomoka.

  8. Kesi ya Paul Rusesabagina yaanza Rwanda.

    Paul Rusesabagina alipata umaarufu kutokana na filamu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Paul Rusesabagina alipata umaarufu kutokana na filamu ya mauaji ya kimbari ya Rwanda

    Kesi ya Paul Rusesabagina imeanza kusikilizwa rasmi leo katika mahakama ya mjini Kigali Rwanda.

    Hali ya usalama imeimarishwas katika eneo la mahakama hiyo na waandishi waliofuatilia kesi hiyo walipimwa virusi Covid-19 asubuhi kabla ya kuruhusiwa kwenda mahakamani.

    Bwana Rusesabagina alikamatwa mjini Dubai katika Muungano wa nchi za kiarabu tarehe 27 Agosti na tarehe 31 mwezi huo ofisi ya upelelezi nchini Rwanda RIB ikatangaza kuwa yupo katika mahabusu zake baada ya kumuonesha waandishi wa habari.

    Rusesabagina ambaye alipata umaarufu kutokana na filamu ya mauaji ya kimbari Hotel Mille Collines, Paul Rusesabagina, ni kiongozi wa muungano wa kisasa MRCD-Ubumwe ambacho Rwanda inauhusisha na mashambulio ya ugaidi yaliyowaua Wanyarwanda katika kituo cha polisi cha mjini Kigali.

    Mapema leo alifikishwa kwenye mahakama ya Kicukiro iliyopo mjini Kigali kwa ajili ya kesi hiyo.

    Maelezo ya video, Paul Rusesabagina akifikishwa katika mahakama ya Kicukiro jijini Kigali

    Baraza la kimataifa kuhusu msaada wa kibinadamu nchini Rwanda lililalamika kwamba Bwana Rusesabagina hana wakili aliyemchagua binafsi kumuwakilisha katika kesi dhidi yake

  9. Mchezaji tenisi awashukuru mababu zake kwa ushindi

    Naomi Osaka

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mchezaji filamu maarufu wa Japan Naomi ambaye amefanikiwa kushdna shindano la US Open mwishoni mwa Juma, amewashangaza wengi baada ya kuwashukuru mababu zake kwa ushindi huo.

    "Ningependa kuwashukuru mababu zangu kwasababu kila wakati, ninapokumbuka kuwa damu yao inapita katika mishapa yangu inanikumbusha kuwa siwezi kushindwa ," nyota huyo alituma ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Jumapili.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Mama yake ni Mjapani huku baba yake akiwa ni mwenye asili ya Haiti.

    Katika kila mechi katika shindano la mwaka huu la US open, Osaka alivalia barakoa yenye jina la mhanga mweusi wa ghasia zinazodaiwa kufanywa na polisi au za ubaguzi wa rangi nchini Marekani.

    Jumamosi alivaa barakoa yenye jina la Tamir Rice, aliyeuliwa na polisi kwa risasi katika eneo la Cleveland akiwa na umri wa miaka 12 mwaka 2014.

    "Ninahisi kuwa ni wakati wa kuwafanya watu kuanza kuongea," alisema Osaka, mwenye umri wa 22, ambaye anaishi Marekani, lakini anachezea timu ya Japan.

    Inadaiwa kua binafsi Osaka amekuwa akikumbwa na ubaguzi wa rangi.

  10. Wanafunzi 10 wafariki katika ajali ya moto Tanzania

    Ajali ya moto

    Chanzo cha picha, Fedeco Radio

    Maelezo ya picha, Moto ulianza kuwaka kwenye bweni jana usiku

    Wanafunzi 10 wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya bweni la shule yao ya Byamungu English Medium Primary School iliyoko wilayani Kyerwa kuteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

    Jumla ya wanafunzi 74 walikuwepo kwenye bweni hilo, na mpaka sasa chanzo cha moto hakijajulikana

    Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amesitisha shughuli za malazi katika shule hiyo kwa muda. "Nachukua hatua nyingine za ziada, hatua ya kwanza na ya awali kabisa tunasitisha huduma za malazi katika shule hii watoto wote waliokuwa wakilala katika huduma ya hosteli au bweni huduma hiyo sasa imesitishwa mpaka itakavyoelekezwa vinginevyo’’, amesema Brigedia Jenerali Marco Gaguti alipotembelea eneo la tukio.

    Umati wa wanavijiji  katika eneo la tukio

    Chanzo cha picha, Fedeco Radio

    Maelezo ya picha, Umati wa wanavijiji katika eneo la tukio

    Mkuu wa Mkoa wa Kagera ameelekeza kamati za usalama za ngazi zote katika mkoa wa Kagera kufanya mapitio upya ya shule zinazotoa malazi, kuhakiki kwamba shule hizo kama zinavyo vibali halali vya serikali na ubora wa majengo yanayotumiwa na wanafunzi, na kuangalia mifumo ya uzimaji moto na kujiokoa inapo.

    Mapema mwezi Julai, wanafunzi watatu wa shule ya sekondari ya Ilala Islamic walipoteza maisha baada ya shule yao hiyo iliyo jijini Dar es Salaam kuungua moto.

  11. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu mubashara leo Jumatatu tarehe 14.09.2020