Msumbiji yahimizwa kuchunguza madai ya mateso Cabo Delgado

Shirika la kutetea haki la Amnesty International limetoa wito kwa serikali ya Msumbiji kuanzisha uchunguzi huru kuhusiana na madai ya mateso yanayohusishwa na oparesheni za kijeshi katika eneo la Cabo Delgado lenye utajiri wa gesi kaskazini mwa nchi hiyo.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo ya moja kwa moja kwa leo. Kwaheri.

  2. Kambi ya watalii Kenya inavyozuia uhamaji wa nyumbu Masai Mara

    Nyumbu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Watu kadhaa nchini Kenya wamekuwa wakitumia mtandao wa kijamii wa Twitter kuelezea ghadhabu zao kufuatia kanda ya video iliyowekwa kwenye mtandao huo na Waziri wa Utalii Najib Balala, kuonesha jinsi uhamaji wa kila mwaka wa nyumba ulivyoathiriwa na kambi ya kitalii iliyojengwa kando ya mto Mara.

    Mmoja wao aliita ‘’chukizo’’ na mwengine kusema ni ‘’uharibifu mkubwa wa turathi yetu ".

    Bw. Balala aliandika katika Twitter akisema kwamba amezungumza na Gavana wa eneo hilo kuomba kambi hiyo ya watalii ‘’kuondolewa’’ kando ya mto huo ili kutoa njia ya wanyama hao kupita.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Video hiyo iliyowekwa mtandaoni bwana Balala kwenye Twitter inaonesha jinsi nyumbu walivyokwama katikati ya mto huo baada ya wale waliokuwa wamefanikiwa kuvuka kurudishwa nyuma na kundi la watu.

    Uhamaji mkubwa wa nyumbu ni moja wapo ya Maajabu Saba mpya duniani.

  3. Aliyefanyiwa jaribio la chanjo ya corona augua

    Mhudumu wa Afya

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Majaribio ya mwisho ya kimatibabu kwa ajili ya chanjo ya virusi vya corona , iliyotengenezwa na AstraZeneca pamoja na Chuo Kikuu cha Oxford yamesitishwa baada ya mshiriki kuugua kutokana na athari za majaribio hayo.

  4. Msumbiji yahimizwa kuchunguza madai ya mateso Cabo Delgado

    Msumbiji

    Chanzo cha picha, AFP

    Shirika la kutetea haki la Amnesty International limetoa wito kwa serikali ya Msumbiji kuanzisha uchunguzi huru kuhusiana na madai ya mateso yanayohusishwa na oparesheni za kijeshi katika eneo la Cabo Delgado lenye utajiri wa gesi kaskazini mwa nchi hiyo.

    Shirika hilo lisilokuwa la kiserikali linasema limethibitisha kanda ya video na picha kutoka eneo hilo zinazoonesha jinsi watu waliozuiliwa wanavyoteswa .

    Video na picha hizo za kutisha zinaonesha jaribio la wafungwa kukatwa vichwa huku wafungwa wengine wakifanyiwa madhila makubwa,liliongeza kusema.

    Shirika hilo pia linasema picha hizo zinaonesha wapiganaji wa upinzani wakikatwa katwa, katika kile kinaashiria mauaji ya kiholela na usafirishaji wa idadi kubwa ya maiti ambayo huenda inazikwa katika kaburi la pamoja.

    Amnesty linasema walioonekana wakitekelezamates ohayo wanaonekana katika video wakiwa wamevalia sare za jeshi la ulinzi la Msumbiji na polisi wa kukabiliana na hali ya daharura.

    Wanaotekeleza mateso hayo wanawaita waliokamatwa kama al - Shabab, likimaanisha jina la kawaida linalotumiwa na makundi ya Kiislamu yaliyojihami na ambayo yanaendesha oparesheni zake katika eneo la Cabo Delgado.

  5. Mafuriko yatishia kuharibu maeneo ya kale Sudan

    Pyramid

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka nchini Sudan inajaribu kuokoa maeneo ya kale kuharibiwa na maji ya mafuriko kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika nchi hiyo.

    Viwango vya maji katika mto Nile ulio karibu na maeneo hayo vimepanda kuliko vya kawaida.

    Kuta zimejengwa katika eneo hilo na shughuli za kutoa maji kwa kutumia mashine imekuwa ikiendelea kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

    Eneo hilo linahifadhi mabaki ya majengo ya kale ya zaidi ya miaka 2,300.

    Mafuriko yanayoshuhudiwa karibu kila pembe ya nchi yamesababisha vifo vya karibu watu 100 huku maelfu ya wengine wakiachwa bila makao.

    Mto Nile huvunja kingo zake mara kwa mara na maji yake yamekuwa yakitumiwa kwa shughuli za kilimo. Lakini mafuriko ya mwaka huu sio ya kawaida.

  6. Rufaa za wagombea zatolewa na Tume ya Uchaguzi Tanzania

      • Author, Munira Hussein
      • Nafasi, BBC Africa

    Huku Kampeni zikiendelea na zikiwa zimebaki wiki chache kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, Tume ya taifa ya uchaguzi NEC imeanza kutoa majibu ya rufaa zilizokatwa na wabunge ambao walienguliwa kutokana na sababu mbalimbali katika nafasi hizo za wagombea.

    Rufaa 55 zimetolewa za ubunge,15 kati yao wamerudi kwenye nafasi zao za ugombea.

    Zoezi hili linaendelea hadi hapo kesho.

    ‘’Zoezi la kuzijadili na kuzitolea uamuzi linaendelea hapa katika Tume, na tutakua tunawajulisha wahusika kadri zoezi litakavyoendelea. Wahusika wa rufaa hizo wameanza kujulishwa kwa njia ya barua kuanzia leo'' ,anasema Dkt.Wilson Mahera mkurugenzi wa uchaguzi NEC.

    Hata hivyo NEC imepokea rufaa 557 kutoka kwa wagombea ubunge na udiwani kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi hizo katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba mwaka huu wa 2020.

    Rufaa hizo zinatokana na baadhi ya wagombea ubunge na udiwani kutoridhika na maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi.

  7. Kura zaanza kupigwa katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia

    TPLF imeonya juu ya machafuko ikiwa uchaguzi utazuiliwa

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, TPLF imeonya juu ya machafuko ikiwa uchaguzi utazuiliwa

    Shughuli ya upigaji kura imeanza katika eneo la Tigray kaskazini mwa Ethiopia katika hatua inayodai wa kukaidi mamlaka za nchi na kutishia mzozo wa kisiasa katika taifa hilo la pili Afrika kwa idadi kubwa ya watu

    Chama cha Tigray People Liberation Front (TPLF), ambayo imeongoza serikali za Ethiopia kwa miongo kadhaa kimeonya kuongezeka kwa ghasia zinazoendelea sasa ikiwa utawala wa muungano unaoongoza utajaribu kuvuruga uchaguzi huo wa kimaeneo.

    Mpiga kura

    Waziri Mkuu Abiy Ahmed amepuuza umuhimu wa kura hizo, akisema TPLF imerefusha muda wake madarakani kwa mujibu uamuzi uliofikiwa na bunge la juu mwezi Juni.

    Hii ni baada ya uchaguzi wa kitaifa kucheleweshwa kutokana na janga la corona.

    Pia alisema uchaguzi wa sasa haitabadilisha chochote dhidi ya uamuzi huo.

  8. Zimbabwe yaondoa vibali vya uchimbaji katika mbuga ya wanyama

    Tembo

    Serikali ya Zimbabwe imepiga marufuku shughuli zote za uchimbaji madini katika mbuga ya kitaifa ya Hwange magharibi mwa nchi hiyo.

    Kampuni mbili za China zilipewa leseni za kuchimba mkaa wa mawe ndani ya mbuga ya wanyama ya Zimbabwe, ambayo inahifadhi tembo zaidi ya 40,000, pamoja na faru weusi, na simba miongoni mwa wanyama wengine.

    Lakini wahifadhi mazingira waliwasilisha ombi la dharura wakisema kwamba aina yoyote ya uchimbaji utakuwa na athari kubwa kwa mazingira hali ambayo inaweza kuua sekta ya utalii nchini.

  9. Kipindi cha uhalisia cha 'Keeping up with The Kardashian' kumalizika

    Familia ya Kardasian

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Kipindi cha uhalisia cha muda mrefu cha familia ya Kardashian maarufu ‘’Keeping up with The Kardashian’’ kinamalizika, Kim Kardashian West ametangaza.

    Kipindi hicho kimekuwa kikipeperushwa kwa miaka 14 kimeipatia familia hiyo umaarufu kimataifa.

    Akitoa shukrani zake kwa "maelfu ya watu binafsi na wafanyabiashara" waliohusika katika mpango huo, Kim pia aliongeza: "Ninashukuru sana kwa kila mtu ambaye alinitazama na kuniunga mkono mimi na familia yangu miaka 14 iliyopita."

    Baadhi ya jamaa wa familia hiyo walikuwa hawajulikani wakati kipindi hicho kilipoanza 2007.

    Msimu wa mwisho ambao utakuwa wa 21, utarushwa mapema 2021.

  10. Semenya apoteza rufaa ya kizuizi cha viwango vya homoni

    Semenya

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya amepoteza rufaa dhidi ya kizuizi cha viwango vya homoni ya kiume kwa wanariadha wa kike aliyowasilisha mbele ya mahakama ya juu zaidi ya riadha nchini Uswizi.

    Semenya haruhusiwi kushiriki mbio za kati ya mita 400 na maili moja bila kutumia dawa za kupunguza viwango vya homoni ya kiume, uamuzi uliofikiwa 2019 na shirikisho la riadha duniani.

    "Nimesikitika sana," alisema mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 29.

    Shirikisho la riadha liliweka sheria kwamba wanariadha walio na tofauti za ukuaji wa kijinsia lazima watumie dawa maalum ili kushindana katika mbio za mita 400 hadi maili moja la sivyo wakimbie mbio ndefu zaidi.

  11. Karibu katika matangazo mubashara