Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Mbunge wa Kenya 'aliyemtukana rais' kushitakiwa

Mkurugenzi wa mashitaka ya umma nchini Kenya Noordin Hajji ameidhinisha mbunge Jonah Ng'eno afunguliwe mashitaka.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo ya moja kwa moja kwa leo.

  2. Wakfu wa Mandela wamjibu Trump

    Wakfu wa Nelson Mandela umejibu tamko lililodaiwa kutolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kumhusu shujaa wa kupinga ubaguzi wa rangi Nelson Mandela.

    Maneno hayo yameangaziwa katika kitabu kipya cha wakili wa zamani wa Bw Trump, Michael Cohen, ambacho kilichotolewa Jumanne.

    Katika kitabu hicho, Bw Cohen anadai Rais Trump alitoa maoni ya kibaguzi kumhusu Nelson Mandela, akidaiwa kusema rais wa Afrika Kusini aliyefariki "hakuwa kiongozi".

    Ikulu ya Marekani inasema wakili huyo anasema uwongo.

    Taasisi ya Nelson Mandela imesema haiamini kwamba "viongozi wanaojiendesha kwa njia ambayo bwana Trump anafanya wako katika nafasi ya kutoa ufafanuzi wenye mamlaka juu ya maisha na kazi ya Madiba"

  3. Kutana na mwanamke wa kwanza Afrika kufanya kazi NASA

    Fadji Maina amekuwa mwanasayansi wa kwanza kutoka nchini Niger kufanya kazi na Shirika la Anga za Juu,NASA.

    Bi maina mwenye umri wa miaka 29 alipata shahada ya uzamifu(PHD) mwaka 2016 na alijiunga na shirika hilo maarufu la anga za juu nchini Marekani mwisho wa mwezi uliopita.

    Ameiambia BBC atatumia kazi yake mpya kurudishia shukurani sio tu nchi yake bali pia kwa bara zima la Afrika.

    ''Nawaasa wanawake wenzangu wasikate tamaa kufikia ndoto zao kwa sababu hakuna mtu angelifikiria mwanamke kutoka Niger, au msichana mdogo kutoka Niger, anataweza kufika mahali kama hapa. Siri ni kujiamini na kutafuta mazingira ambayo itakusaidia kufikia ndoto yako'' alisema katika mahojiano yake na BBC.

  4. Fahamu umuhimu wa uchaguzi wa Tanzania ndani na nje ya taifa hilo

    Jicho la ulimwengu lipo Tanzania wakati huu ikielekea katika uchaguzi mkuu. Vyama vya kisiasa kile tawala na vile vya upinzani, vinaendelea kuchuana kwa sera katika majukwaa.

  5. TikTok mbioni kuondoa video ya mtu akijitoa uhai

    Matandao wa kijamii wa TikTok unajitahidi kuondoa kanda ya video inayomuonesha mtu akijjitoa uhai.

    Video hiyo ambayo imekuwa ikisambazwa kwenye mtandao huo kwa siku kadhaa, ilianzia kwenye Facebook na sasa imeanzakusambazwa Twitter na Instagram.

    TikTok ni maarufu kwa vijana wadogo – na baadhi yao wameripotiwa kutazama video hiyo na wamepata usumbufu wa kimwazo.

    Mtandao huo umesema utawapiga marufuku akaunti za watu watakaoendelea kusambaza video hiyo mara kadhaa.

    ''Tunawashukuru wafuatiliaji wa mtandao wetu ambao wameripoti kuhusu video hiyo na kuwatahadharisha wengine dhidi ya kuitazama ama kushirikisha maudhui kama hayo kwenye jukwaa lolote, kwa heshima ya mtu huyo na familia yake'' mwakilishi wa TikTok alisema.

    Kwa upande wake Facebook imeiambia BBC: "Tulifuta video hiyo mwezi uliopita kwenye mtandao Facebook, siku iliyooneshwa moja kwa moja, na kutumia mfumowa teknolojia kufuta nakala za video zinazochapishwa kutoka wakati.

    "Tunatoa pole zetu kwa familia ya Ronnie na marafiki wakati huu mgumu."

  6. Rais wa Zambia aongoza nchi kuomboleza kifo cha samaki

    Zambia inaomboleza kifo cha samaki wake mkubwa katika chuo kikuu cha umma cha Copperbelt (CBU).

    Samaki huyo aliyejulikana kama Mafishi – ameombolezwa na rais Edgar Lungu na kiongozi wa upinzani Hakainde Hichilema.

    Neno Mafishi limekuwa likisambaa kwa kasi katika mtandao wa Twitter nchini Zambia kufuatia kifo cha samaki huyo Jumatatu usiku.

    Samaki huyo alikuwa akiishi katika kidimbwi cha chuo kikuu na baadhi ya wanafunzi waliokuwa wakimtembelea kabla ya kufanya mtihani ili kuomba wapite.

    Wanafunzi wengine wanasema aliwasaidia kujiondolea msongo wa mawazo .

    Rais Lungu alitumia nukuu ya Mahatma Gandhi kumuomboleza samaki huyo kwa kuandika:"ukuu wa taifa na maendeleo ya maadili yake yanaweza kuhukumiwa kutokana na jinsi anavyowatendea wanyama wake."

    Bwana Hichilema aliandika: "Tunaungana na jamii ya wanafunzi wa sasa na wazamani wa chuo kikuu cha CBU, kufuatia kifo chasamaki wao Mafishi."

    Samaki huyo alikuwa sehemu ya mpango wa turathi ya viumbe wa majini na anasemekana ameishi ndani ya kidimbwi cha chuo hicho kwa karibu miaka saba, kwa mujibu wa kituo cha kibinafsi cha televisheni, Diamond.

    Tazama wanafunzi walivyomuomboleza samaki huyo usiku wa Jumatatu:

  7. Mkulima asimulia jinsi ngiri maji ilivyovunja ndoto yake

    Hujafa hujaumbika. Ni maneno ya wahenga. Hii inaonekana dhahiri katika maisha ya kijana Matayo Kudenya, mkazi wa kizota, jijini Dodoma. Kwa maelezo zaidi tazama video ifuatayo.

  8. Mbunge wa Kenya 'aliyemtukana rais' kushitakiwa

    Mkurugenzi wa mashitaka ya umma nchini Kenya Noordin Hajji ameidhinisha mbunge Jonah Ng'eno afunguliwe mashitaka.

    Mbunge Johanna Ng’eno alikamatwa siku ya Jumatatu kufuatia matamshi aliyotoa dhidi ya Rais Uhuru Kenyatta wikendi iliyopita, kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

    Bwana Ng’eno anatuhumiwa kwa kutumia maneno ya matusi kumdhalilisha rais, kulingana na taarifa ya gazeti la Daily Nation inayonukuu ripoti ya polisi.

    Kanda ya video inayomuonesha mbunge huyo akizungumzia mgogoro kati ya rais Kenyata na naibu wake William Ruto imezua gumzo kali katika mitandao ya kijamii.

    Mbunge huyo anasikika akimwambia rais avunje serikali ikiwa ameshindwa kufanya kazi na bwana Ruto.

    Hali ya taharuki ilishuhudiwa wakati wa kukamatwa kwa mbunge huyo wa Emurua Dikirr, katika eneo la bonde la ufa huku tukio hilo likioneshwa moja kwa moja katika ukurasa wake wa Facebook.

    Baada ya kukamatwa kwa bwana Ng'eno, naibu wa rais aliandika ujumbe katika Twitter yake akisema "viongozi wanapaswa kujizuia na kuepuka kutumia lugha ya matusi dhidi ya Wakenya wengine".

  9. Buhari alaani hatua ya viongozi wa Afrika Magharibi kugombea muhula wa tatu

    Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa wito kwa viongozi wa Afrika Magharibi kuzingatia mihula yao ya madarakani kwa mujibu wa katiba.

    Tamko lake linafuatia uamuzi wa Rais wa Ivory coas Alassane Ouattara na Rais wa Guinea Alpha Condé kugombea mihula ya tatu katika nchi zao.

    Maoni ya Rais Buhari yalitolewa wakati wa mkutano wa viongozi wa kikanda wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (Ecowas), uliofanyika Niamey, mji mkuu wa Niger.

    Uamuzi wa Rais Ouattara kuwania muhula wa tatu kufuatia kifo cha ghafla cha aliyempendelea kuwa mrithi wake ulisababisha maandamano nchini Ivory Coast. Wakosoaji wake wanasema kuwa hatua hiyo ni kinyume na katiba.

    Maandamano ya ghasia pia yameshuhudiwa katika nchi jirani ya Guinea ambapo Rais mwenye umri wa miaka 82 anataka kugombea muhula wa tatu wa kutatanisha katika uchaguzi mkuu ujao.

  10. Wanajeshi wa Mali wapewa wiki moja kuteua uongozi wa kiraia

    Viongozi wa kijeshi walioongoza mapinduzi ya kumuondoa madarakani rais wa Mali wamepewa hadi Septemba 15 kuteua kiongozi wa kiraia kuongoza kipindi cha mpito.

    Viongozi wa Jumuia ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), wanataka watakaopendekezwa kuwa rais na waziri mkuu kuongoza nchi hadi uchaguzi mpya utakapoandaliwa.

    Viongozi wa kijeshi bado hawajatoa tamko lolote kuhusiana na tangazo hilo lililotolewa siku ya Jumatatu katika mkutano uliohudhuriwa na wakuu wanane wa nchi katika jimbo la Niamey, mji mkuu wa Niger.

    Ecowas inataka kipindi cha mpito kikamilishwe ndani ya mwaka mmoja lakini wanajeshi waliwahi kusema wanataka "muda wa kutosha" na kupendekeza angalau miaka miwili.

  11. Karibu katika matangazo mubashara