Tunakamilisha matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo.
Lakini tunakuacha na taarifa ya duka la urembo nchini Afrika Kusini kuvamiwa kwa kutoa tangazo la ‘kibaguzi'
Hii ni baada ya waandamanaji kulalazimisha maduka kadhaa ya urembo yanayomilikiwa na kampuni ya Click kufungwa kufuatia tangazo la biashara lililotolewa na kampani hiyo ambalo wanadai kuwa na ujumbe wa kibaguzi.
Tangazo hilo lilikuwa na picha inayolinganisha nywele ya mwafrika na mzungu ikiashiria kuwa nywele ya mwafrika imekauka na kuharibika ilihali ya mzungu ni laini, nyororo na ya kuvutia.
Chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) kimetaja tangazo hilo kuwa la"kibaguzi" na la "kudhalilisha".