Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afrika kupokea dozi milioni 220 za chanjo ya Covid-19
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema chanjo ya Covid-19 itakapoaidhinishwa, Afrika itapata karibu dozi milioni 220 za awali.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
KLM na Etihad miongoni mwa ndege zilizopigwa marufuku kuingia Nigeria
Nigeria imepiga marufuku mashirika ya ndege kutokanchi kadhaa kuhudumu nchini humo kuanzia Jumamosi hii.
Mashirika kumi ya ndege yamezuiliwa kuhudumu- Ikiwemo Air France, KLM kutoka Uholanzi, Lufthansa kutoka Ujerumani, na Etihad Airways ya Milki za kiarabu.
Hii ni kwasababu Wanigeria walio na viza ya watalii hawaruhusiwi kuingia katika nchi hizo..
Nigeria ilisema kwamba italipiza kisasi hatua ya kuwapiga marufuku raia wake kuingia katika nchi hizo.
Baadhi ya mashirika ya ndege yamezuiliwa kuhudumu nchini Nigeria kwasababu nchi zao hazijarejelea safari za abiri kimataifa.
Lakini mashirika 14 ya ndege yataruhusiwa kuhudumu nchini humo mionngo mwa hzo ni British Airways, Virgin Atlantic, Turkish Airlines, Qatar Airways na Ethiopian Airlines.
Abiria wataruhusiwa nchini humo chini ya mashari makali.
Wapiganaji waasi wa DR Congo waingia mkoa wa Ituri
Wapiganaji wa waasi waliojihami vikali wameingia eneo la Bunia, makao makuu ya mkoa wa Ituri mashaki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Hatua hiyo ya kundi la waasi wa Codeco imezua hofu lakini maafisa wanasema hawakufanya mashambulio na kuongeza kwamba walisindikizwa na kuingizwa mjini humo na polisi.
Katika wiki za hivi karibuni serikali imekuwa ikijaribu kuwashawishi wapiganaji hao kujisalimisha.
Umoja wa Mataifa unalaumu kundi hilo kwa kutekeleza ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo mauaji, kuwakata watu vichwa na ubakaji.
Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita Codeco, ambalo wanachama wake wengi wanasadikiwa kutoka jamii ya Walendu, limeongeza mashambilizi yake.
Karibu watu 1,000 wameuawa huku wengine nusu milioni wakitoroka makwao.
Namibia kutumia mbwa kugundua virusi vya corona
Chuo Kukuu cha Namibia kitengo cha sayansi ya mifugo kinawafundisha mbwa kubaini virusi vya corona kwa kunusa.
Mpango wa nchi hiyo ni kuwapelea mbwa hao katika viwanja vya ndege na vituo vya mpakani, kwa mujibu wa mtandao wa The Namibian.
Mbwa wamethibitishwa kuwa na uwezo wa kubaini virusi vya corona kwa aslimia 95, mhadhiri wa somo la tiba ya wanyama Alma Raath anasema.
Mradi huo ulianzishwa miezi miwili iliyopita, inasema taarifa ya mtandao huo wa The Namibian, lakini haujataja ni lini mbwa hao watakuwa tayari kufanya kazi.
Mtandao wa The Namibian unasema nchi hiyo itakuwa ya kwanza kutumia mbwa kubaini virusi vya corona.
Pia unaweza kusoma:
Vifurushi 21 vya msaada wa Jack Ma 'havikufika' Kenya
Mamlaka nchini Kenya imekiri kwamba mchango muhimu katika vita dhidi ya Covid-19 kutoka kwa bilionea wa China Jack Ma haikuwasili nchini.
Naibu wa waziri wa uchukuzi wa, Chris Obure amefichua kuwa vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vilivyotolewa na wakfu wa Jack Ma mwezi Machi kama msaada wa kukabiliana na Covid 19 haikufika Kenya.
Bwana Obure alisema hayo siku ya Alhamisi mbele ya kamati ya bunge ya afya japo hakudokeza ni vifaa vya aina gani vilikuwa ndani ya vifurushi hivyo.
Aliongeza kuwa vifaa hivyo havikuwahi kuwawasili nchini kutoka Ethiopia ambako misaada ya Jack Ma katika eneo hilo ilitumwa kwa ajili ya kusambazwa katika nchi zingine.
Wizara ya uchukuzi iligundua kuwa vifurushi 21 havikuwepo baada ya kuthibitisha hilo katika stakabadhi za kuegesha kutoka China.‘’Binafsi niliongea na maafisa wakuu wa Wizara ya Afya na walinithibitishia kuwa wanafuatilia suala hilo’’ alisema bwana Obure.
Kumekuwa na madai kwamba misaada ya Covid-19, ikiwemo ile kutoka kwa Jack Ma ilitumiwa vibaya au kutoweka katika njia za kutatanisha.
Maelezo zaida:
Ifahamu sumu ya Novichok iliyotumiwa kumshambulia mpinzani wa Rais Vladimir Putin
Msemaji wa Urusi anataka Ujerumani kuishirikisha katika taarifa zake zote huku msemaji wa wizara ya mambo ya nje Maria Zakharova akilalamika kwamba madai ya Novichok hayakuambatinishwa na ushahidi wowote.
Raia wa Ghana awa mwanamke wa kwanza Afrika kushinda tuzo ya uhandisi
Mfanyabiashara wa teknolojia nchini Ghana Charlette N’Guessan, ameshinda tuzo ya mwaka huu ya uhandisi Afrika.
Charlette N’Guessan ni mwanamke wa kwanza barani Afrika kushinda tuzo hiyo na wa kwanza kutoka Ghana.
Bi N’Guessan mwenye umri wa miaka 26 na kundi lake la wavumbuzi, Bace API, wanatumia utambuzi wa usoni na akili bandia kuthibitisha utambulisho kwa mbali, ilisema taasisi ya uhandisi ya Royal Academy.
Inatumia picha za moja kwa moja ama video fupi zilizonaswa kwa kutumia kamera ya simu kutambua ikiwa picha hiyo ni ya mtu halisi, ama picha ya kitu kilichopo.
Taasisi mbili za kiuchumi tayari zinatumia programu hiyo kuthibitisha utambulisho wa wateja wao.
Bi N’Guessan alipewa zawadi ya dola 33,000 kwa kuibuka mshindi.
Mshindi alipigiwa kura na watazamaji wa moja kwa moja wakati wa hafla ya tuzo iliyofanyika Alhamisi ambapo wahitimu wanne waliwasilisha kazi zao.
Macron 'kukutana na rais wa Ivory Coast ' licha ya mzozo wa uchaguzi
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atakutana na mwenzake wa Ivory Coast Alassane Ouattara mjini Paris leo Ijumaa, kwa mujibu wa taarifa ya shirka la habari la AFP inayonukuu vyanzo vy ahabari katika ofisi ya rais wa Ufaransa.
Uamuzi wa bwana Ouattara kugombea muhula wa tatu wa urais katik auchaguzi utakaofanyika mwezi Octoba umezua taharuki na maandamano nchini.
Awali alikuwa amesema hatogombea, lakini akabadili msimamu huo kufuatia kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly,aliyekuwa ameteuliwa na chama tawala kuwa mrithi.
Wapinzani wake wanasema jaribio lake la kugombea muhula wa tatu linakiuka katiba.
Afrika kupokea dozi milioni 220 za chanjo ya Covid-19
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema chanjo ya Covid-19 itakapoaidhinishwa, Afrika itapata karibu dozi milioni 220 za awali.
Sehemu ya kwanza ya chanjo hiyo itapewa wafanyakazi wa afya na makundi yaliohatarini, kwa mujibu wa meneja mkuu wa mradi huo katika WHO Afrika, Richard Mihigo.
Amesmea usambazaji wa chanjo hizo utategemea idadi ya watu katika kila nchi.
Bwana Mihigo amesema nchi zote 54 barani humo zimeonesha nia ya kutaka chanjo ya Covid-19.
Afrika ina zaidi ya wato bilioni 1.3.
Mpango wa chanjo duniani unaofahamika kama COVAX, inakusudia kusaidia kununua na kusambaza kwa usawa dozi bilioni mbili za chanjo zilizoidhinishwa ifikapo mwisho wa mwaka 2021.
Mpango huo una chanjo tisa ambazo zinafanyiwa majaribio duniani
Chanjo mbili kati ya hizo zinafanyiwa majaribio Afrika, kwa mujibu wa mkuu wa muungano wa ubunifu wa maandalizi dhidi ya majanga (CEPI) bwana Richard Hatchett.