Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mamba alivyowapa 'ulinzi wa kipekee' wanawe
Picha inayomuonesha mamba akiwabeba watoto wake mgongoni kwa kutumia mbinu isiokuwa ya kawaida inaendelea kuzua gumzo mitandaoni.
Moja kwa moja
Ambia Hirsi
Uamuzi wa rufaa ya Kabuga kutolewa mwsho wa Septemba
Mahakama ya juu zaidi inayotoa uamuzi wa mwisho wa kesi za rufaa nchini Ufaransa inatarajiwa kutoa uamuzi wake ikiwa Félicien Kabuga ambaye anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda afikishwe mbele ya mahakama maalum ya Umoja wa mataifa iliopo Tanzania Septemba 30, kulingana na ripoti ya AFP.
Bwana Kabuga alikamatwa mwezi Mei viungani mwa mji wa Paris baada ya kwenda mafichoni kwa zaidi ya miongo miwili.
Anatuhumiwa kwa kufadhili mauaji ya kimbari ya 1994 nchini Rwanda ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya Watutsi 800,000 na Wahutu wenye misimamo ya kadiri
Mnamo mwezi Juni, akijibu mashitaka dhidi yake katika mahakama ya rufaa, Bwana Kabuga alisema "Huo wote ni uwongo."
Awali Mahakama iliamua Kabuga,87, ahamishiwe mahakama maalum ya Umoja wa Mataifa kuhusu Rwanda mjini Arusha lakini mawakili wake wakapinga uamuzli huo.
Siku ya Jumatano shirika la habari la AFP liliripoti kuwa wakili wake waliambia mahakama kwamba mteja wake anaugua maradhi ya kisukari, shinikizo la damu na tatizo la ubongo lilnaojulikana kama ‘leukoaraiosis’,na kwamba ni mgonjwa sana “kusafirishwa kilomita 7,000” mjini Arusha, Tanzania.
Maelezo zaidi:
Maafisa wa uhifadhi wapandishwa vyeo kupambana na ujangili Tanzania.
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Munira Hussein
- Nafasi, BBC Africa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imewapatia vyeo maafisa wahifadhi 225 na Askari 1,568 sawa na asilimia 99 ambao wamekidhi vigezo wametunukiwa vyeo hivyo na jeshi la uhifadhi Tanzania.
Katika hafla ya kuwapatia vyeo hivyo, Kamishena wa mamlaka ya TAWA Fredrick Ambwene amesema kuwa kupewa vyeo kwa maafisa hao, kutasaidia sana katika harakati za kupambana na ujangili.
‘’Tanzania haijamaliza ujangili kwa asilimia mia moja, hivyo hawa maafisa wetu wapo mbele kupambana na ujangili’’ anasema Ambwene.
Kwa mujibu wa Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori (WWF)
Tanzania imepoteza zaidi ya asilimia 60 ya Tembo wake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.
Kenya Airways yatoa ofa ya nauli kwa wahudumu wa afya
Wahudumu wa afya kote duniani sasa wanaweza kusafiri popote kwa hadi nusu ya nauli wanayotozwa kwa hisani ya shirika la ndege la Kenya Airways.
Shirika hilo limesema hatua ya kupunguza nauli kwa hadi asilimia 50 ni njia ya kuwazawadia wahudumu wa afya kutokana na juhudi zao wakati wa janga la corona.
Kenya Airways ilipata hasara ya dola milioni 133 miezi sita ya mwanzo wa mwaka.
Shirika hilo lilikuwa likijizatiti kuhudumu licha ya kupata hasara na ushindani kutoka kwa mashirika mengine ya ndege kabla ya mlipuko wa virusi vya corona, hali ambayo iliifanya serikali kusitisha safari zake.
Mamba alivyowapa 'ulinzi wa kipekee' wanawe
Picha inayomuonesha mamba akiwabeba watoto wake mgongoni kwa kutumia mbinu isiokuwa ya kawaida inaendelea kuzua gumzo mitandaoni.
Picha hiyo ya kuvutia ilinaswa na mpiga picha Dhritiman Mukherjee katika hifadhi ya Uttar Pradesh nchini india.
Miito imekuwa ikitolewa kupendekeza mpiga picha huyo apewe tuzo ya mwaka huu ya picha bora ya wanyhama pori.
Dhritiman anasema mamba kwa kawaida huwabeba watoto wao kwa (makini) wakitumia mdomo, lakini mbinu iliyotumiwa na mamba huyu ni ya kustaajabisha na ni vigumu kwake kuwapa ulinzi watoto.
"Ili kujiokoa watoto walilazimika kujishikilia katika eneo la kichwa cha mama na hata wengine kupanda mgongoni ili kuwa salama," anasema.
Thuluthi tatu ya mamba hao wanapatikana katika hifadhi ya Uttar Pradesh, hali ambayo huenda ikawa jambo la muhimu kwa mamba wadogo kujilinda kwa njia isiokuwa ya kawaida wanapobebwa na mama zao.
Akon kusonga mbele na ujenzi wa 'Akon City' Senegal
Msanii Akon wa muziki wa R&B nchini Marekani na ambaye amekuwa akizungumzia kujenga mji mpya nchini Senegal tangu 2018 amesema shughuli ya ujenzi itaanza mwaka ujao.
Akon hakuwatambulisha wawekezaji katika mradi huo lakini amefichua kwamba ufadhili wa thuluthi tatu ya dola bilioni sita umepatikana.
Mchoraji ramani wa mji huo mpya, Hussein Bakri, amesema idadi ya watu katika mji huo inakadiriwa kufika 300,000.
Akon, ambaye jina lake halisi ni Alioune Badara Thiam, aliwashirikisha moja kwa moja Wamarekani weusi katika mauzo ya mradi huo.
Alisema kuwa ametangamana na "Waafrika wenye asili ya Marekani ambao hawaelewi utamaduni wao, Kwa hivyo nilitaka kujenga mji ama kubuni mradi kama huu ambao utawapa motisha ya kuwa na makazi katika nchi yao," Shirika la habari la AFP lilimnukuu msanii huyo aliyezaliwa Marekani kutokana na wazazi raia wa Senegal, akisema.
"Unapoamua kuishi Marekani,Ulaya ama mahali kwengine ughaibuni na ungelipendelea kuzuru Afrika, tunataka Senegal iwe kituo chako cha kwanza," alisema.
Bobi Wine ashitakiwa kwa kuhadaa kuhusu umri wake
Mahakama nchini Uganda imemtaka mwanasiasa wa upinzani Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, kufika mbele yake kujibu tuhuma za kutoa taarifa za uwongo kuhusu umri wake kwa Tume ya Uchaguzi.
Bobi Wine anatakiwa kufika mbele ya mahakama hiyo kabla ya Septemba 16 kujibu kesi iliyowasilishwa na wakili, Male Mabirizi.
Katika ombi lake la Agosti 3, bwana Mabirizi anadai vyeti vya masomo vya Bobi Wine vinaonesha alizaliwa tarehe 12 Februari 1980, tofauti na tarehe iliyonakiliwa katika pasipoti yake na pamoja na fomu aliyowasilisha kwa tume ya uchaguzi mwaka 2017 wakati alipoteuliwa kugombea kiti cha ubunge.
Pasipoti ya Bobi Wine inaonenesha kuwa alizaliwa Februari 12,1982.
Pia anakabiliwa na mashitaka ya "kupata usajili kwa njia ya udanganyifu" katika mahakama hiyo.
Mjadala kuhusu miaka ya mtia nia huyo wa kugombea kiti cha urais na uhalisia wa vyeti vyake vya elimu umezua gumzo katika mitandao ya kijamii kwa majuma kadhaa.
Bobi Wine aliweka ujumbe katika mtandao wa Facebook Siku ya Jumatatu, akisema kesi ya hivi punde dhidi yake ni sehemu ya muendelezo wa njama ya serikali kuhujumu upinzani.
Rais wa Mali aliyeng'atuliwa madarakani 'alazwa hospitali'
Rais wa Mali aliyeng'olewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi Ibrahim Boubacar Keïta amelazwa katika hospitali moja mji mkuu wa Bamako, kwa mujibu wa Shirika la habari la Associated Press.
Lilinukuu vyanzo katika viwili kliniki ambako kiongozi huyo wa zamani anaripotiwa kutibiwa.
Mwanasiasa huyo wa miaka 75 alizuiliwa kwa siku kumi na wanajeshi kabla atangaze kujiuzulu na baaadae kuachiliwa huru..
Wakati wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa mzozo wa kisiasa nchini Mali Bwana Keita alinukuliwa kusema kuwa hana haja ya mamlaka ya urais.
Kwa miezi kadhaa upinzani ulikuwa ukimshinikiza kujiuzulu na kumlaumu kwa kurudisha nyuma uchumi wa nchi, kudhibiti ufisadi na kushindwa kukabiliana na makundi ya kijihadi.
Watu 90 wafariki kutokana na mafuriko makubwa Sudan
Takriban watu tisini wamefariki na wengine karibu elfu 400 kuachwa bila makao kufuatia mafuriko makubwa Sudan.
Umoja wa Mataifa unasema mafuriko hayo yamesababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha nchini humo tangu mwisho wa mwezi Julai..
Viwango vya maji katika ziwa vimepanda hadi karibu mita 17.5 kiwango ambacho ni cha juu zaidi kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka 100.
Maeneo yaliyoathirika vibaya ni mji mkuu wa Khartoum, Sudan Mashariki, White Nile na Darfur ambako maelfu ya watu sasa wanahitaji msaada wa dharura.
Baadhi ya watu walioathiriwa na mafuriko hayo ni wale ambao walikuwa wametoroka makwao kutokana na mzozo na tayari walikuwa wamepoteza njia za kujipatia kipato kufuatia janga la corona.
Umoja wa Mataifa unasema ukosefu wa maji safi wakati huu wa janga la virusi vya corona unawaweka katika hatari ya kupata maambukizi.
Makadirio ya awali ya Umoja huo inasema karibu vyanzo 2,000 vya maji vimechafuliwa ama havifanyi kazi.