U.N. yaonya maisha ya mshindi wa tuzo ya Nobel DR-Congo yako hatarini

Wiki iliyopita Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi aliamuru Bw. Mukwege mwenye umri wa miaka 65 kupewa ulinzi wakati uchunguzi wa tisho la mauaji dhidi yake ukiendelea.

Moja kwa moja

Ambia Hirsi

  1. Mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja. Tukutane tena kesho.

  2. Simulizi ya mwanamke Mnaigeria mwenye macho ya bluu na wanae

    Tazama Video ifuatayo kwa maelezo zaidi:

    Maelezo ya video, Mwanamke wa Mnigeria mwenye macho ya bluu na wanae
  3. Maonyesho ya tiba asilia ya mwafrika yaanza Tanzania

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC Africa, Dar es Salaam
    Wahusika
    Maelezo ya picha, Wahusuka

    Wataalamu mbalimbali wa tiba asili na tiba mbadala wanakutana jijini Dodoma katika maadhimisho ya wiki moja ya Tiba Asili ya Mwafrika kitaifa.

    Maadhimisho hayo yana lengo la kuangalia mafanikio yaliyopatikana katika sekta hiyo katika kipindi cha miongo miwili iliyopita. Wataalamu kadhaa wamejitokeza ili kuonyesha bidhaa zao.

    Maadhimisho haya yanafanyika wakati ambapo dunia iko mbioni kutafuta tiba au hata chanjo ya Covid19. Na baadhi ya wataalamu wa tiba asili nao wamekuwa mbioni katika kufanya uvumbuzi wa dawa hiyo.

    Baadhi ya bidhaa katoka maonesho hayo
    Maelezo ya picha, Baadhi ya bidhaa katoka maonesho hayo
  4. Ethiopia yaitaka Marekani kuelezea madai ya kuipunguzia ufadhili

    Ujenzi wa Bwawa hilo ulianza 2011

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Ujenzi wa Bwawa hilo ulianza 2011

    Serikali ya Ethiopia inataka ufafanuzi kutoka kwa Marekani kuhusu madai kwamba imepunguza ufadhili wake kwa nchi hiyo mzozo wa ukiendelea kuhusu bwawa kubwa la uzalishaji umeme katika mto Nile.

    Wiki iliyopita jarida moja linaloangazia sera za kigeni liliripoti kuwa Waziri mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo ameidhinisha kuzuiliwa kwa msaada wa hadi dola 130 milioni kwa Ethiopia katika juhudi za kuishinikiza ifikie mkataba na Misri kuhusu bwawa hilo

    Kwa karibu muongo mmoja, Ethiopia na Misri zimekuwa zikishauriana kuhusu bwawa hilo.

    Misri, ambayo inategemea maji ya mto Nile kwa 80%, ina hofu kuwa bwawa hilo litaathiri mfumo wa usambazaji maji na kuifanya Ethiopia kuwa na mamlaka juu ya usambaaji wa maji ya mto mkubwa Afrika.

    Nchi hizo pamoja na Sudan zinashauriana kuhusu kiwango cha maji kitakachoachiwa kupitia bwawa hilo

    Balozi wa Ethiopia nchini Marekani, Fitsum Arega, ameandika kati Twitter yake ujumbe uanaosema Marekani imeahidi kutoa maelezo kuhusu suala hilo (18:30 GMT). Lakini hakuna uthibitisho kuwa ufadhili umekatwa.

    Maelezo zaidi:

    • Mzozo kati ya Misri na Ethiopia: Nani anayemiliki mto Nile
  5. Chama cha ACT Wazalendo chazindua ilani yake

    Viongzi wa Chama cha ACT Wazalendo
    Maelezo ya picha, Viongzi wa Chama cha ACT Wazalendo

    Chama cha upinzani cha ACT Wazalendo nchini Tanzania kimezindua ilani yake leo Jumatatu kinapojiandaa kuanza kampeini ya kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

    Kiongozi wa Chama hicho, Zitto Kabwe amemkabidhi ilani hiyo Mgombea Urais wa chama hicho Benard Membe pamoja na Mgombea Mwenza wake Omar Fakih Hamad.

    Baadhi ya masuala waliopewa kipaumbele katika Ilani hiyo ni pamoja na:

    • Ujenzi wa Demokrasia na Utaoji Haki za Watu
    • Uhuru wa Kila Mtu
    • Elimu Bora ya kivumbuzi bila malipo
    • Ajira mpya milioni 10
    • Ushirika wa kisasa kwa maendeleo jumuishi
    • Ufanisi na Ubora wa Huduma za Jamii

    Katika mtandao wake wa Twitter Chama hicho pia kimesema:

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Chama hicho kinatarajiwa kuzindua rasmi kampeni yake kesho mkoani Lindi Kusini mwa Tanzania.

    Chama Tawala cha CCM kilizindua kampeni yake mjini Dodoma siku ya Jumamosi huku Chadema nayo ikifanya uzinduzi wa kampeni yake Ijumaa wiki iliyopita.

    Uchaguzi Mkuu wa Tanzania utafanyika Oktoba 28, 2020.

  6. Sudan yafikia mkataba wa amani na waasi

    Hafla ya kutia saini mkataba wa amani ilifanyika Sudan Kusini

    Chanzo cha picha, Catholic Radio Network

    Maelezo ya picha, Hafla ya kutia saini mkataba wa amani ilifanyika Sudan Kusini

    Serikali ya mpito ya Sudan imetia saini mkataba wa amani na makundi ya waasi katika hafla iliyoandaliwa nchi jirani ya Sudan Kusini.

    Mkataba huo unalenga kumaliza mzozo wa mika 17 katika maeneo ya magharibi mwa Darfur na majimbo ya kusini.

    Hii ni hatua kubwa kuelekea kutafuta ufumbuzi wa mizozo kadhaa nchi humo,anasema mwandishi wa BBC Anne Soy.

    Hata hivyo makundi mawili muhimu ya waasi yamekataa kutia saini mkataba huo ambao unaangazia masuala ya kama vile umiliki wa ardhi, ugawanaji mamlaka na jinsi mamilioni ya watu waliotoroka makwao kutokana na mapigano watakavyorejea nyumbani.

    Makundi ya waasi mjini Darfur yalianza kupigana na vikosi vya serikali 2003

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Makundi ya waasi mjini Darfur yalianza kupigana na vikosi vya serikali 2003

    Makubaliano yaliopita ya amani yaliolenga kukomesha mzozo huo wa muda mrefu yalitibuka.

    Mapigano kati ya vikosi vya serikali na waasi yalianza 2003 na yamesababisha vifo vya maelfu ya watu huku mamilioni ya wengine yakifurushwa makwao.

    Mazungumzo ya Amani yalicheleweshwa mara kadhaa kufuatia kifo cha waziri wa ulinzi wa zamani wa Sudan, Jamaleldin Omar, na janga la Covid-19.

  7. Shujaa wa Hotel Rwanda akamatwa kwa tuhuma za ugaidi

    Paul Rusesabagina

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha ya Paul Rusesabagina 2004 filamu ya Hotel Rwanda ilipotolewa

    Mwanamume ambaye jukumu lake la kuwaokoa Wanyarwanda dhidi ya mauaji ya kimbari liliangaziwa katika filamu ya Hotel Rwanda,amekamatwa kwa tuhuma za ugaidi.

    Paul Rusesabagina amekamatwa ughaibuni ambako alikuwa anaishi mafichoni.

    Shirika la upelelezi la Rwanda linasema alikamatwa kupitia waranti ya kimataifa kwa kuunda na kuongoza "vuguvugu la kigaidi" linaloendesha shughuli zake katika eneo hilo.

    Bw. Rusesabagina, 66, alitunukiwa medali ya Rais wa Marekani ya Uhuru 2005, miongoni mwa tuzo zingine za haki za binadamu.

    Hajatoa tamko lolote kuhusu tuhuma za sasa dhidi yake lakini amekuwa mkosoaji wa serikali ya Rwanda.

    2011, alituhumiwa kuwafadhili wajumu wa serikali ya Rwanda, lakini hakufunguliwa mashitaka yoyote.

    Wakati huo, Bw. Rusesabagina alipinga tuhuma dhidi yake na kudai ilikuwa njama ya kumharibia sifa.

    Mwaka 2004 filamu ya Hotel Rwanda iliangazia jinsi Bw. Rusesabagina, Mhutu wa aliyemuoa mwenye Tutsi, alivyotumia ushawishi wake - na rushwa- kuwashinikiza maafisa wa kijeshi kumpatia njia salama ya kuwatorosha karibu watu 1,200 kutafuta makazi katika Hoteli ya Mille Collines mjini Kigali.

    Kundi la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Ibuka liliwahi kusema kuwa alitilia chumvi jukumu lake la kuwasaidia wakimbizi kujificha hotelini hapo siku 100-ya mauaji ya kikatili mwaka 1994.

  8. U.N. yasema maisha ya mshindi wa tuzo ya Nobel DR-Congo yako hatarini

    Dkt Denis Mukwege

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Dkt Denis Mukwege, Mashindi wa Tuzo ya Amani ya Noble 2018

    Umoja wa Maitaifa umeonya kuwa maisha ya daktari wa Dr-Congo aliyeshinda Tuzo ya Nobel 2018 yako hatarini baada ya kupokea msururu wa vitisho vya mauaji vinavyotolewa dhidi yake.

    Kamishena wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amelaani vitisho hivyo na kutoa wito Dkt. Denis Mukwege na familia yake kupewa ulinzi.

    Bachelet pia amezishinikiza mamlaka nchini DRC kuidhinisha rasimu ya sheria ya ulinzi inayodhibiti shughuli za wanaharakati wa kutetea haki za binadamu "kwa kuzingatia viwango vya kimataifa."

    Wiki iliyopita Rais wa DR Congo Felix Tshisekedi aliamuru Bw. Mukwege mwenye umri wa miaka 65 kupewa ulinzi wakati uchunguzi wa tisho la mauaji dhidi yake ukiendelea.

    Daktari Mukwege(Aliyevalia miwani) akiwa na madaktari wenzake

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Dkt Denis Mukwege (Aliyevalia miwani) akiwa na madaktari wenzake

    Denis Mukwege ni daktari anayeshughulikia afya ya wanawake nchini DRC. Yeye na wenzake walikuwa wamewahudumia waathiriwa 30,000 wa ubakaji kufikia mwaka 2013.

    Anasema: "Nilijiuliza - ni nini haswa kilikuwa kinaendelea? Huu ulikuwa tu si uhalifu bali mikakati mahsusi. Kuna wakati ambapo watu wengi wangebakwa kwa mpigo, tena wazi mbele ya watu wengine - kijiji kizima kingebakwa usiku. Basi wanapofanya hivyo hawaumizi tu wanaowabaka bali jamii nzima inayolazimishwa kuwatizama.

    Vita Mashariki mwa DRC vimewalazimisha mamia kutoroka makwao hali inayohatarisha maisha yao.

  9. Rwanda yaitaka Ufaransa kumkamata mshukiwa wa mauaji ya kimbari

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili
    Aloys Niwiragabo

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Picha ya Aloys Niwiragabo kwenye tarakilishi

    Rwanda imeitaka Ufaransa kumkamata Aloys Niwiragabo anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

    Mtuhumiwa huyo alikuwa kanali wa jeshi, aliyehusika na upelelezi katika enzi za utawala wa hayati Juvenal Habyarimana.

    Mwendesha mashitaka mkuu wa Rwanda Aimable Havugiyaremye ametangaza kwamba Rwanda tayari imetoa waranti wa kutaka Kanali Aloys Ntiwiragabo akamatwe.

    ‘’Kwa sasa tunafanya kazi kwa ushirikiano na kundi la wapelelezi wa makosa ya uhalifu wa kivita nchini Ufaransa.Wapepelezi hao tayari wameishaanza uchunguzi wao na kazi inaenda kama ilivyopangwa.’’

    Kwa mjibu wa mwendesha mashtaka mkuu wa Rwanda Bw. Ntiwiragabo, anatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kimbari japo hakutoa maelezo zaidi.

    Kanali Aloys Ntiwiragabo mwenye umri wa miaka 72 alikuwa mkuu wa idara ya upelelezi wa jeshi wakati wa utawala wa hayati Juvenal Habyarimana.

    Kanali huyo alikuwa miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu katika jeshi la hayati Juvenal Habyarimana, lakini hayupo kwenye orodha ya watuhumiwa wakuu wa mauaji ya kimbari ambao bado wanasakwa na mahakama ya kimataifa kwa ajili ya Rwanda.

    Wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni Protais Mpiranya aliyekuwa kamanda wa kikosi cha ulinzi wa Habyarimana na Augustin Bizimana aliyekuwa waziri wa ulinzi lakini yeye imethibitishwa kufariki nchini Congo Brazaville.

    Waranti wa kumkamata mtuhumiwa huyo umetolewa ukifwatia kukamatwa kwa mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya kimbari Felicien Kabuga aliyekamatwa nchini Ufaransa mwezi Marchi baada ya kujificha kwa miaka 26.

  10. Rais wa Afrika Kusini kuchunguzwa kuhusiana na mchango wa kampeini

    Cyril Ramaphosa

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

    Maafisa wa chama tawala nchini Afrika Kusini wamesema Rais Cyril Ramaphosa atafika mbele ya Tume ya Uadilifu kujibu maswali kuhusiana na mchago tata wa kampeini.

    Lakini Jessie Duarte, mwanachama wa ngazi ya juu wa chama cha African National Congress, ANC, hakufafanua ikiwa Bwana Ramaphosa atajiwasilisha mwenyewe mbele ya kamati hiyo ya chama

    Katika ripoti yake, mamalaka ya kupambana na ufisadi inadai kuwa Bw Ramaphosa alipotosha bunge kuhusumchango aliopokea mwaka 2017, ya thamani ya zaidi ya dola 35,955.

  11. Tembo 12 wafa katika mazingira ya kutatanisha Zimbabwe

    Tembo

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Tembo

    Mamalaka ya hifadhi ya wanyama nchini Zimbabwe zinachunguza jinsi tembo 12 walivyokufa katika mbuga ya kitaifa ya Hwange.

    Tembo hao walipatikana wakiwa wamekufa wakiwa na pembe zao.

    Mamlaka zinasema hazina hofu kwamba huenda wametiliwa sumu ya cyanide - ambayo pia hutumiwa na wawindaji haramu badala ya silaha- kwani hakuna wanyama wengine walioathirika

    Sampuli ya damu imechukuliwa kutoka kwa tembo hao kuchunguza kilichosababisha vifo vyao.

    Mbuga ya kitaifa ya Hwange National inakaribia mpaka wa Botswana ambako mamia ya mizoga ya tembo ilipatikana mwaka huu.

  12. Karibu kwa matangazo yetu mubashara 31.08.2020