Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Chadema wazindua kampeni za uchaguzi rasmi Tanzania

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania Oktoba mwaka huu, baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kuzindua rasmi kampeni za kuwanadi wagombea wao wa viti vya ubunge, uwakilishi, udiwani na Rais.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena Jumatatu.

    Tunakuacha na video hii ya kanisa linaloruhusu unywaji wa pombe kanisani.

  2. Kanisa 'linaloruhusu unywaji pombe wakati wa ibada'

  3. Uzinduzi rasmi wa kampeni za uchaguzi 2020 za Chadema kwa picha:

  4. Chadema wazindua kampeni za uchaguzi rasmi Tanzania

      • Author, Munira Hussein
      • Nafasi, BBC Africa

    Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania Oktoba mwaka huu, baadhi ya vyama vya siasa vimetangaza kuzindua rasmi kampeni za kuwanadi wagombea wao wa viti vya ubunge, uwakilishi, udiwani na Rais.

    Kwa upande wa Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wao wanazindua kampeni kitaifa, kanda ya Pwani, siku ya leo.

    Chama cha mapinduzi (CCM) kinatarajia kuzindua kampeni zake kesho, katika mjii mkuu wa nchi hiyo Dodoma.

    Kwa upande wa chama cha ACT Wazalendo wao bado hawana uhakika wa kampeni zao zitaanza lini ama kufanyika wapi.

    Kwa upande wa vyama vingine vya siasa, bado hawajatoa taarifa rasmi za utaratibu wa kampeni zao.

    Uchaguzi wa Tanzania unatarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba 2020.

  5. Je FIFA ni inaweza kuwa kimbilio la Drogba?

    Matumaini ya Didier Drogba ya kuwa rais rais ajaye wa shirikisho la soka la Ivory Coast (FIF) yanaweza kurejeshwa.

    Fifa imeombakusitishwakwa shughuli zote zinazohusiana na uchaguzi hadi itakapopokea nyaraka mbalimbali.

    Kutokana na kwamba mchakato wa uchaguzi unaweza kuwa wa huru na haki , Shirikisho la soka duniani limeiomba tume ya uchaguzi ya FIF, iwe imelitumia faili tano kufikia Ijumaa "28 Agosti 2020 bila kuchelewa ".

    "Wakati tukisubiri nyaraka zenu na taarifa, tunawaomba muahirishe shughuli zote zinazohusiana na mchakato wa uchaguzi hadibaadae ," Katibu Mkuu wa FIfa Fatma Samoura amesema.

    Barua ya Samoura ilitumwa Alhamisi siku ambayo nahodha wa zamani wa Ivory Coast na nyota wa Chelsea Drogba alikataliwa kugombea nafasi hiyo.

    Siku ya Alhamisi, Tume ya uchaguzi iliwachagua wagombea wawili tu kuwania nafasi ya rais ajaye waFIF- Sory Diabate,ambaye ni makamu rais wa sasa wa shirikisho na Yacine Idriss Diallo ambaye ni makamu wa tatu wa zamani wa shirikisho hilo.

  6. Mwafrika aliyefanywa 'maonyesho' Marekani

    Ota Benga alitekwa nyara kule ambako sasa hivi kunafahamika kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 1904 na kupelekwa Marekani lengo likiwa nikumfanya kuwa onyesho.

    Mwadishi wa habari Pamela Newkirk, ambaye ameandika mengi kuhusu suala hilo, anaangalia matukio kadhaa ya kuficha ukweli wa kile kilichotokea. Unaweza kuisoma taarifa hii zaidi katika mtandao wetu

  7. Radi yawauwa watoto 10 Uganda

    Radi imepiga na kuwauwa watoto 10 katika mkoa wa kaskazini-magharibi mwa Uganda wa Arua.

    Mkoa huo umekuwa na mvua kubwa zinazoambatana na radi.

    Mvua kubwa iliyonyesha Alhamisi iliwalazimisha watotowaliokua wakicheza mpira wa miguukujikinga mvua hiyo ndani ya nyumba ya nyasi iliyokuwa kando ya uwanja.

    Nyumba hiyo ilipigwa na radi, watoto tisa waliokuwa kati ya umri wa miaka 13 na 15, wakafa mara moja, na mwingine mmoja alikufa alipokua njani kuelekea hospitali.

    Watatu walionusurika wanapata matibabu katika hospitali ya mkoa.

    Hili ni tukio baya zaidi la aina yake kutokea nchini Uganda tangu 2011.

    Mwaka 2011, watoto 18 walikufa baada ya kupigwa na radi na kufa katika shule iliyoko katikati mwa jimbo la magharibi.

    Kwa ujumla watu 28 walikufa kutokana na walikufa kwa radi katika kipindi cha wiki moja mwaka huo.

  8. Mwandishi wa habari wa Kenya aliyekamatwa Ethiopia aamua kubaki huko

    Mwandishi wa habari ambaye aliachilia huru nchini Ethiopia amechagua kubakia na marafiki zake nchini Ethiopia, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Kenya.

    Yassin Juma alikamatwa katika nyumba ya mwanaharakati wa upinzani wa Jawar Mohammed mapema mwezi Julai wakati wa ghasia za maandamano kufuatia mauaji ya mwanamuziki maarufu Hachalu Hundessa.

    Aliachiliwa huru mwezi huu baada ya wizara ya mambo ya nje ya Kenya kuingilia kati na kuchukuliwa katika kituo cha karantini kinachomilikiwa na serikali mjini Addis Ababa baada ya kupatikana na virusi vya Covid-19 alipokua mahabusu.

    Mwandishi huyo alikamilisha siku 14 katika karantini na akaruhusiwa kutoka kwenye kituo cha karantini baada ya kupimwa na kutopatikana na maambukizi, kwa mujibu wa taarifa ya waziri wa Kenya.

  9. Safari ya Wakimbizi wa Burundi walliorejea nyumbani kutoka Rwanda kwa picha

  10. Rais Ndayishimiye awakaribisha wakimbizi wa Burundi nyumbani

    Wakimbizi wa Burundi waliokua wakiishi katika ya wakimbizi nchini Rwanda, wamepokelewa nyumbani ‘’kwa mikono miwili’’.

    “Nimefurahi sana kurudi nyumbani, Nilikimbia na watoto wangu watatu na nimerudi nyumbani na watoto watano na mama yao, sote tuko salama,” Emmanuel Bizimana aliiambia BBC alipokua akipanda basi.

    Wakimbizi hao 493 ni sehemu ya kwanza ya wakimbizi wapatao 72,000 ambao walikimbilia Rwanda mwaka 2015 kufuatia ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

    6,000 kati yao wamekuwa wakiishi katika kambi ya wakimbizi ya Mahama iliyopo mashariki mwa Rwanda huku wengine wakiishi katika Miji ya Kigali na Huye, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa mataifa la wakimbizi UNHCR.

    Miongoni mwa maafisa waliowapokea ni Waziri wa mambo ya ndani wa Burundi Gervais Ndirakobuca na waziri wa afya Dkt Thaddée Ndikumana.

    Katika ujumbe wake wa Twitter, Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiya aliwakaribisha alisema: ‘’Karibu ndugu zetu waliotoka ukimbizini mahama. Nifuraha kubwa kwa familia zao na kwa Burundi. Wahusika wanaombwa kuwasaidia katika mchakato wa kurejea katika maisha ya kawaida. Tunawataka nawngine wanaotaka kurejea warudi, Burundini yetu sote. Karibu kweni pazuri!’’, aliandika Ndayishimiye.

  11. Safari za ndege za kimataifa zaahirisha Nigeria

    Mafisa nchini Nigeria wameahirisha ufunguzi wa safari za ndege za kimataifa kwa wiki moja.

    Safari hizo sasa zitafunguliwa tena tarehe 5 Septemba badala ya tarehe iliyotangazwa awali 29 Agosti.

    Wanasema kucheleweshwa kwa safari hizo kunatokana na matatizo ya vifaa na hakuhusiani na masuala ya anga- wakisema kuwa ni pamoja na masharti ya usalama wa virusi vya corona.

    Wizara ya usafiri wa anga nchini humo imesema kuwa inasikitishwa na kucheleweshwa kwa safari hizo lakini maafisa wameielezea tarehe mpya ya ufunguzi wa safari hizo kama "muhimu sana ".

    Nigeria ilisimamisha kwa muda safari za kimataifa za ndege mwezi Machi kama sehemu ya hatua za kudhibiti janga la virusi vya corona.

    Safari za ndege za ndani ya nchi zilifunguliwa mwezi uliopita.

  12. Museveni atangaza maombi ya corona Uganda

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza Jumamosi kuwa siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19.

    Rais huyo amesema kuwa alipata wazo kutoka kwa raia wa Ugandaambaye alikuwa na "maono kutoka kwa Mungu ".

    "Mungu alikua amemuambia katika moano kwamba ninapaswa kuanda maombi, yaandaliwe kisayansi, ili Mungu atuponye na Covid-19...Ninatangaza tarehe 29 Agosti, 2020, siku ya maombi ya kitaifa na siku ya mapumziko ya umma. Kaeni majumbani mwenu au kwenye viwanja vya nyumba zenu na muombe," Bwana Museveni alisema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.

    Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana vifo 28.

    Serikali iliweka masharti ya kudhibiti maambukizi baada ya kuthibitisha kisa cha kwanza mwezi Machi.