Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Aliyedhaniwa kuwa ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi afariki

Mwanaume wa Afrika Kusini aliyedhaniwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116.

Moja kwa moja

Dinah Gahamanyi

  1. Na mpaka hapo ndio tunafiia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja, tukutane tena kesho.

  2. Polisi Ufaransa wanawashikilia mashabiki 148 baada ya PSG kukosa kombe la Ulaya

    Polisi nchini Ufaransa inasema imewatia nguvuni watu 148 kufuatia ghasia zilizoibuka katika mji mkuu wa Ufaransa Paris, baada ya timu ya St-Germain Kushindwa na timu ya Ujerumani ya Bayern Munich Jumapili.

    Jumapili usiku PSG walifungwa 1-0 na Bayern Munich ya Ujerumani ambao sasa ni mabingwa wa Ligi ya Ulaya.

    Kulikua na makabiliano baina ya polisi na mashabiki wa timu hiyo waliozua ghasia katika mitaa ya Champs-Élysées na karibu na uwanja wa michezo wa PSG, Parc des Princes, ambako mashabiki walikua wamekusanyika kutazama mpambano kati ya timu yao na Bayern Munich.

    Katika ghasia hizo, magari yalichomwa moto na madirisha ya maduka yakavunjwa, kulingana na polisi.

    PSG ilikuwa inawania kupata kombe hilo kwa mara ya kwanza katika historia yake, lakini haikufanikiwa.

  3. Shughuli za michezo ‘kufufuliwa’ tena Kenya

    Shughuli za michezo zinatarajiwa kufunguliwa tena nchini Kenya katikati ya mwezi wa Septemba.

    Hii ni baada ya serikali kutoa muongozo wa awali wa namna matukio ya michezo yatakavyokuwa yakifanyika kufuatia kufungwa mwezi Machi kutokana na COVID-19.

    Baadhi ya wanariadhawalikua tayari wameanzakushiriki mashindano ya kimataifana sasa Wizara ya michezo nchibni inatarajiwa kufungua tena mashindano ndani ya nchi.

    Kulingana na Mapendekezo ya awali juu ya udhibiti wa viwanja, mazoezi na mpangilio wa mashindano Vitatathminiwa na mashirikisho.

    Mpanglio huo ni pamoja na uchunguzi na vipimo vya afya vitakavyochukuliwa kwenye maeneo yote ya kuingilia kwenye matukio ya michezo, uvaaji wa barakoa kwa wanamichezo wakati wote na udhibiti wa vyumba vya kubadilisha jezi katika maeneo ya matukio ya michezo. Kusalimiana kwa mikono, kukumbatiana na kusherehekea timu pia ni marufuku.

  4. Mtu aliyedhaniwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi afariki

    Mwanaume wa Afrika Kusini aliyedhaniwa kuwa ndiye mwenye umri mkubwa zaidi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 116.

    Nyaraka za utambulisho wa Fredie Blom zinaonesha kuwa alizaliwa katika jimbo Eastern Cape mwezi Mei 1904, ingawa hilo halikuwahi kuthibitishwa na rekodi za Guinnes za dunia(Guinness World Records).

    Alipokuwa kijana mwenye umri wa barehe, watu wote wa familia yake walikufa kutokana na jana la mafua -Spanish flu, mwaka 1918. Aliishi na kunusurika vita ya kwanza ya dunia pamoja na vita vya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.

    Bwana Blom ambaye alikua mvutaji wa sigara, aliiambia BBC mwaka 2018 kwamba hakuna siri maalumu ya kuishi maisha marefu.

    "Kuna kitu kimoja tu-ni mwanaume aliye juu (Mungu). Ana mamlaka yote. Sina chochote. Ninaweza kufa wakati wowote lakini bado amenishikilia,"

    Bwana Blom aliishi maisha ya kufanya kazi za kawaida - ikiwemo kazi ya kilimo katika shamba na baadae katika kiwanda cha ujenzi – alistaafu akiwa na umri wa miaka zaidi ya 80.

    Familia ya Bwana Blom amesema alikufa kifo cha kawaida mjini Cape Town Jumamosi.

  5. Video ya panya yawatia matatani maafisa wa hospitali Zambia

    Picha ya video ya panya wanaotambaa huru sakafuni katika moja ya hospitali kubwa zaidi nchini Zambia imewatia matatani wasimamizi wa hospitali hiyo.

    Picha hiyo inaonesha panya wakitoka katika mfuko wa plastiki huku mgonjwa aliyekuwa amelazwa tkatika wodi akionekana kando ya plastiki hiyo.

    Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya alifanya ziara ya ghafla katika hospitali kuu ya Kitwe iliyopo katika jimbo la Zambia Copperbelt baada ya video hiyo kusambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii:

    Waziri ameagiza hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya mameneja wa hospitali.

    Amesema kuwa hiyo ni aibu kwa serikali na wote wanaohusika lazima wajibu juu ya ni kwanini panya wako wodini.

  6. Rwanda yarekodi idadi kubwa zaidi ya watu wenye Covid-19

      • Author, Yves Bucyana
      • Nafasi, BBC Swahili

    Watu 200 wamepatikana na maambukizi ya virusi vya corona Jumapili - ikiwa ni idadi ya juu zaidi kuwahi kurekodiwa na taifa hilo kwa siku moja tangu liliporipoti kisa chake cha kwanza mwezi Machi.

    Idadi kubwa ya visa vya maambukizi mapya viliripotiwa katika mji mkuu Kigali.

    Idadi hiyo mpya imeleta jumla ya kesi zaidi ya 3,000 zikiwemo kesi mpya zilizorekodiwa katika wiki mbili zilizopita ambapo watu 12 walikufa kutokana na ugonjwa huo.

    Wiki iliyopita ,sheria ya kubaki nyumbani ilitangazwa tena katika baadhi ya maeneo ya mji mkuu wa Kigali ambao sasa una shuhudia wimbi jipya la maambukizi.

    Miongoni mwa maeneo ya biashara yaliyofungwa ni masoko mawili makubwa ya mjini .

    Wimbi jipya la maambukizi haswa mjini Kigali limeibua wasi wasi wa vikwazo vipya vinavyoweza kuwekwa na serikali.

    Afisa mkuu wa wizara ya afya Dr Sabin Nsanzimana amesema kuna wasi wasi wa kutokea maafa makubwa ikiwa waakazi wataendelea kupuuza ugonjwa huo na mikakati iliyowekwa ya kujilinda:

    ‘’Nikiangalia idadi ya maambukizi inayozidi kupaa kila uchao,nina wasi wasi .kasi ya maambukizi ikiendelea ilivyo hususan mjini Kigali, tutashuhudiaidadi kubwa ya vifo. Hali hii ikiendelea tutakuwa tunaelekea pabaya. ’’

    Rwanda, imekuwa nchi ya kwanzachini ya jangwa la Sahara kulazimisha wananchi kutotoka nyumbanimnamo mwezi Machi kwa kipindi cha siku 45.

  7. Kenya kushuhudia idadi kubwa ya watoto wa ‘Covid-19 ‘ mwishoni mwa mwaka

    Kenya itashuhudia idadi kubwa ya watoto watakaozaliwa mwishoni mwa mwaka huu, limeripoti gazeti la The Standard nchini humo.

    Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya afya kuhusu athari za virusi vya corona kwa huduma muhimu, kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanawake na wasichana wanaopata uja uzito tangu mwezi Machi mwaka huu wakati taifa hilo lilipoweka hatua za kudhibiti maambukizi ya corona baada ya janga kutangazwa.

    Janga la virusi vya corona lilisababisha kuwekwa kwa masharti makali ya matembezi ya watu na kuwalazimisha watu kukaa nyumbani na maagizo kutoka kwa wataalamu yalisababisha kufungwa kwa shule zote, makanisa, na shughuli zote za burudani zinazofanyika katika maeneo ya kijamii.

    Kwa mujibu wa wizara hiyo uchunguzi wa tathmini ya viashiria vilivyochaguliwa kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2018, kulikua na ongezeko la wanawake wanaotembelea hospitalini kupata huduma za afya ya ujauzito mwezi Juni mwaka 2020.

  8. 'Watoto wanaozaliwa na matatizo ya midomo watibiwe mapema'

      • Author, Aboubakar Famau
      • Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam

    Wataalamu wanashauri kuwa ni vyema watoto wanaozaliwa na matatizo ya 'kasoro' za midomo watibiwe mapema kuanzia miezi miwili.

    Ushauri huo umetolewa na Madaktari wataalamu wa upasuaji wa midomo wazi au midomo sungura ambao wameweka kambi kwa muda wa wiki moja ambapo watoto kadhaa waliozaliwa na tatizo hilo watafanyiwa upasuaji Katika mji mkuu wa Tanzania Dodoma.

    Huduma hii inayotolewa bure inafanyika kwa ushirikianio wa Hospitali ya Mkoa Dodoma na taasisi isiyo ya kiserikali ya Same Quality Foundation.

    Dr. Athanase Masele ambae ni daktari bingwa wa kinywa na meno ameniambia kwamba mwitikio ni mkubwa mkoani Dodoma kwa sababu awali walikuwa na malengo ya kuwafanyia upasuaji watoto 20, lakini mpaka sasa waliojiorodhesha ni zaidi ya hao

    Hata hivyo, licha ya kutokuwepo kwa takwimu zinazoonyesha ukubwa wa tatizo la watoto kuzaliwa na midomo sungura, imeelezwa kwamba kanda ya kaskazini mwa Tanzania kuwa na idadi kubwa ya watoto hao.

  9. Ecowas wafikia 'baadhi ya mapatano' na viongozi wa mapinduzi Mali

    Ujumbe kutoka Jumuiya yakiuchumi ya nchi zilizoko magharibi mwa Afrika, Ecowas, na wajumbe wa jeshi la Malijunta wanasema wamefikia makubalianokuhusu masuala kadhaa, siku moja baada ya mazungumzo yanayolenga kurejesha utawala wa kiraia.

    Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuendela leo Jumatatu.

    "Tumeweza kukubaliana juu ya masuala kadhaa lakini bado hatujajadiliana ," amesema rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, anaongoza harakati za upatanishi alipozungumza na Reuters.

    Viongozi wa kijeshi wamependekeza taasisi ya kijeshi iongoze kwa muda wa miaka mitatu "kutathmnini msingi wa taifa la mali ", taarifa za shirika la habari la AFP limemnukuu afisa katika ujumbe wa Ecowas.

    Jeshi la Mali junta pia limekubali kumuachilia rais aliyepinduliwa Boubacar Keïta, kulingana AFP.

    Ecowas imeomba mara kwa mara Bwana Keïta arejeshwe mamlakani, lakini maelfu ya raia wa Mali waliingia mitaana kuandamanakatika mji Mkuu Bamako kuunga mkono mapinduzi.

  10. Hujambo na karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo Jumatatu tarehe 24.08.2020