Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Viongozi wa mapinduzi Mali waapa kufungua mipaka tena
Viongozi wa kijeshi ambao walichukua mamlaka nchini Mali baada ya kumpindua Rais wametangaza kuwa mipaka ardhini na anga itafunguliwa tena leo Ijumaa
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Hospitali yazuia umma kuitembelea kutokana na corona Rwanda
Hospitali ya rufaa nchini Rwanda imezuia watu kuwatembelea wagonjwa madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo wakipatwa na virusi vya corona, maafisa wamesema.
Dkt Edgar Kalimba, afisa katika hospitali hiyo, King Faisal hospital, ameiambia televisheni ya taifa kwamba madaktari watano na wauguzi kadhaa walipata maambukizi ya virusi hivi karibuni.
Hospitali hiyo huwapokea wagonjwa kati ya 600 na 1,000 kwa siku na ina wafanyakazi 500.
Katika kipindi cha siku saba zilizopita, maambukizi ya Covid-19 yameongezeka mara tano nchini Rwanda ikilinganishwa na wiki za awali. Vifo vinavyotokana na virusi vimefikia hadi watu 11 katika kipindi cha majuma mawili yaliyopita.
Zaidi ya watu 2,700 wamethibitishwa kupata maambukizi ya Covid-19 nchini Rwanda, kwa mujibu wa data za wizara ya afya.
Madaktari waanza mgomo katika mji mkuu wa Kenya
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Rhoda Odhiambo
- Nafasi, BBC Africa, Nairobi
Zaidi ya madaktari 300 wnaofanya kazi katika hospitali za umma katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wameanza mgomo.
Wahudumu hao wa afya wanataka malipo bora na kuboreshwa kwa hali zao za kazi ikiwa ni pamoja na vifaa vya kujikinga na maambukizi (PPE).
Mji wa Nairobi ndio wenye idadi kuwa ya watu wenye maambukizi ya virusi vya corona zaidi nchini humo.
Madaktari wanasema kuwa wamekuwa na subira kwa serikali ambayo inahusika na huduma za afyamjini Nairobi.
Mwenyekiti wa madaktari Thuranira Kaugira alitweet kuwa wafanyakazi wa afya wamekuwa masikini vya kutosha:
Madaktari wanataka kulipiwa bima kamili ya matibabu na vifaa bora vya kujikinga wanapowashughulikia wagonjwa wa Covid-19.
Hii si mara ya kwanza kwa madaktari wa Kenya kufanya mgomo wakidai malipo na hali bora za kazi.
Wahudumu wa afya 700 ni miongoni mwa watu zaidi ya 30,000 waliopata maambukizi ya Covid-19 kwa ujumla nchini Kenya. Wahudumu kadhaa wa afya ni miongoni mwa watu waliokufa kutokana na virusi vya corona.
Waandamanaji wakamatwa na kufyatuliwa gesi za kutoa machozi Kenya
Polisi nchini Kenya wamewakamata na kuwafyatulia gesi za kutoa machozi waandamanaji waliokua wakipinga matumizi mabaya ya pesa za Covid-19.
Waandamanaji hao walikua wamekusanyika kwenye eneo maarufu la Bustani ya Uhuru (Uhuru Park), katika mji mkuu Nairobi.
Mmoja wa waandamanaji amesema kuwa watu 12 wamekamatwa:
Kampeni ya mtandaoni-hashtag #ArrestCovid19Thieves, inayohamasisha kukamatwa kwa wezi wa pesa za Covid-19 imeenezwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya huku wanaharakati wakidai uwajibikaji wa pesa za Covid-19.
Maandamano hayo yamekuja baada ya ripoti za madai ya matumizi mabaya ya fedha za misaada zilizotolewa kwa ajili ya kupambana na jana la virusi vya corona.
Serikali hata hivyo imekanusha kuwepo kwa matumizi yoyote mabaya ya pesa hizo, licha ya miito ya kutaka uchunguzi ufanyike juu ya madai hayo.
Mwanaume wa Nigeria ‘aliyefungwa na familia yake kwa miaka 30’ aokolewa
Polisi katika jimbo la kaskazini mwa Nigeria la Kano wameumuokoa mwanaume mwenye umri wa mika 30 ambaye alifungwa na familia yake kwa miaka 30 kwasababu alikua na ugonjwa wa akili, mwanaharakati wa haki za binadamu Sani Shuaibu meiambia BBC.
Mwanaume huyo alikuwa amefungiwa kwa miongo kadhaa huku miguu yake ikifungwa pamoja kwa chuma kilichoingizwa kwenye gogo la mti, ndani ya chumba ambacho hakikuwa na dirisha wala mlango,amesema BwanaShuaibu kutoka mtandao wa haki za binadamu (HRN).
Aliwafahamisha polisi juu ya maisha ya mwanaume huyo baada ya kujulishwa na mtu, na akajiunga na harakati za kumuokoa kutoka makazi yao yaliyopo katika mji wa Rogo.
“Ana matatizo ya kiakili, alikuwa na fujo na badala ya kuomba msaada mwaka 1990 baba yake akaamua kuwa jambo bora la kufanya ni kumfunga ," Bwana Shuaibu aliiambia BBC.
“Wakati baba yake alipokufa miaka kadhaa iliyopita kaka zake wawili, wadogo zake waliendelea kumfunga lakini leo ni mwanaume huru. Baadhi ya majirani walioifahamu hali yake walikuwa ni watu muhimu katika uokoaji huu ,” aliongeza.
Kwa sasa mwanaume huyo yuko katika hospitali kuu ya Rogo ambako anapewa matibabu, huku kaka zake wakihojiwa na polisi.
Huu ni uokoaji wa tatu wa hali ya juu katika kipindi cha wiki mbili wa watu wenye matatizo waliofungwa na familia zao katika eneo hilo la kaskazini mwa Nigeria.
Mawe mawili ya dhahabu yenye thamani ya $350,000 yapatikana Australia
Mawe mawili yenye thamani ya takriban dola 350,000 yamegunduliwa na wachimba mgodi kusini mwa Australia.
Brent Shannon na Ethan West aliyapata mawe hayo karibu na mji wenye machimbo ya madini wa Tarnagulla uliopo katika jimbo la Victoria.
Wawili hao walioneshwa kwenye kipindi cha televisheni cha Aussie Gold Hunters, kinachopeperushwa kila siku ya Alhamisi, huku wakiwa wamayabeba mawe yao hayo ya thamani.
Wanaume hao walichimba ardhi na kutumia ving’amuzi vya dhahabu katika eneo.
"Bila shaka huu ni moja ya ugunduzi wa muhimu sana ," Ethan West alisema, kwa mujibu wa CNN. " Kuwa na mawe makubwa mawili kwa siku moja inafurahisha ."
Waliyapata mawe hayo moja lenye uzito wa kilo 3.5 ndani ya masaa kadhaa tofauti kwa usaidizi wa baba yake na Bwana West, kwa mujibu wa kipindi cha televisheni ya Discovery Channel kilichohfuatilia taarifa hiyo.
Viongozi wa Afrika walaani mapinduzi ya kijeshi Mali
Viongozi wa Afrika wamelaani vikali mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini Mali Jumanne wiki hii na wametaka rais Boubacar Keita.
Wakati wa mapinduzi rais Ibrahim Boubacar Keita alikamatwa na wanajeshi waasi. Wakiongozwa na mwenyekiti wa Muungano wa Afrika, rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, viongozi hao wametoa wito wa kuachiliwa mara moja kwa Keïta na maafisa wa ngazi ya juu wa utawala wake miongoni mwao Waziri mkuu Boubou Cissé.
Kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya video pia kilihudhuriwa na wawakilishi wa Jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Mateka wa Iran walioshikiliwa Somalia waachiliwa
Raia watatu wa Iran waliokua wametekwa nyara na maharamia wa kisomali kwa miaka mitano iliyopita wameachiliwa huru.
Mpatanishi kati ya mharamia na mateka, John Steed, ameiambia BBC kuwa wanaume hao walikua ni wa mwisho kuokolewa miongoni mwa wahudumu wa meli ya uvuvi ya Iran ambayo ilikamtwa na maharamia mwaka 2015.
Alisema kuwa kuachiliwa kwao ni mwisho wa maumivu na mateso ya mateka waliosahaulika wa Somalia.
WHO na Unicef zataka shule zifunguliwe Afrika
Shirika la afya duniani (WHO) na Shirika la Umoja wa mataifa la watoto- Unicef yameyazitaka serikali za Afrika kufungua shule zenye mazingira salama wakati huu wa janga la corona.
Wanasema kufungwa kwa shule kwa muda mrefu kuna madhara kwa wanafunzi na mashirika hayo yanazitaka serikali kuwekeza katika huduma za usafi ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona katika taasisi za masomo.
Mashirika hayo mawili yamesema kuwa wanafunzi wanawekwa katika hatari ya lishe duni, mimba za utotoni na ghasia wakati huu wa kurefushwa kwa muda wa kukaa nyumbani.
Shule katika bara la Afrika ni "mahala salama " kwa watoto, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kanda ya Afrika wa WHO Matshidiso Moeti.
"Hatupaswi kusahau juhudi zetu za kudhibiti Covid-19. Wakati nchi zinafungua shughuli za kila siku kwa kuzingatia usalama, tunaweza kufungua tena shule ," alisema katika mkutano wa video Alhamisi.
Kufungwa kwa muda mrefu kwa shule kunaathiri maisha ya baadae ya watoto na jamii, kwa mujibu wa Mkurugenzi mkuu wa Unicef wa kikanda Mohamed Fall.
Ni nchi sita tu za Afrika ambazo zimefungua kikamilifu shule, kwa mujibu wa utafiti uliofanywa katika nchi 39 na WHO na Unicef.
Baadhi ya nchi zilifunguliwa na baadae kufungwa kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.
Nyingine zinafungua shule kwa wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa masomo yao kwa ajili ya kufanya mitihani muhimu.
Nchi kama Kenya zimefuta mwaka wa masomo wa 2020.
Maharamia wa Somalia waiteka meli yenye bendera ya Panama
Maharamia wa Somalia wameiteka meli yenye bendera ya Panama-iliyokua ikisafiri kutoka Muungano wa Kiarabu ikielekea kwenye bandari mjini Mogadishu.
Meli hiyo ilishambuliwa usiku wakati wahudumu wake walipokua wamelala. Shirika la habari la Anadolu limewanukuu maafisa wa jimbo lililojitenga na Somalia la Puntland.
Maharamia sita walihusika katika shambulio hilo kwa mujibu wa gavana wa eneo la Gardafu katika jimbo la Puntland, Musse Salah, ambaye alinukuliwa na Shirika la habari la Reuters.
Maafisa wa eneo la Bari ambako tukio hilo lilitokea wanasema kuwa meli hiyo ilipatwa na matatizo ya kiufundi.
Viongozi wa mapinduzi nchini Mali waamuru mipaka ifunguliwe tena
Maafisa wa jeshi waliochukua udhibiti nchini Mali wametangaza kwamba mipaka ya ardhini na anga itafunguliwa tena Ijumaa.
Mipaka nchi hiyo ilifungwa baada ya mapinduzi wiki hii.
Viongozi wa mapinduzi wamesema kuwa wanawasiliana na makundi ya upinzani juu ya kuanza kwa mchakato wa kumteua rais wa mpito.
Viongozi wa Afrika Magharibi wameendelea kumuomba rais aliyeng’olewa madarakani, Ibrahim Boubacar Keïta, kurejeshwa madarakani mara moja.
Jumuiya ya kikanda Ecowas inasema inautuma msafara wa wajumbe wake nchini Mali kuhakikisha wanarudisha utawala wa kikatiba.
Upinzani umetoa wito wa kufanyika kwa mkutano mkubwa wa kuunga mkono mapinduzi.
Karibu kwa matangazo yetu ya mubashara leo Ijumaa tarehe 21.08.2020