Wasafiri kutoka nchi 130 wataingia Kenya bila kuwekwa karantini, Tanzania haimo
Kenya imetoa orodha ya nchi 130 ambazo raia wake wataruhusiwa kuingia nchini humo bila masharti ya raia hao kukaa karantini ndani ya taifa hilo
Moja kwa moja
Dinah Gahamanyi
Na huo ndio mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena kesho...
Nakuacha na habari ya mvulana huyu mchezaji wa Ballet kutoka Ghana Athony Mmesoma...unamkumbuka?
Baada ya video yake akicheza Ballet kusambaa mtandaoni, sasa amepata ufadhili wa Masomo nchini Marekani.
Maelezo ya video, Anthony Mmesoma Madu, mchezadensi wa miaka 11 aliyeikonga mioya ya watu mtandaoni
ECOWAS yaangalia uwezekano wa kuwawekea vikwazo waliopanga mapinduzi Mali
Chanzo cha picha, @BASHIRAHMAADTWITTER
Viongozi wa Mataifa yaliyoko magharibi wa
Afrika watafanya kikao cha video leo juu ya mzozo unaoendelea nchini Mali.
Kikao
hicho kitakachofanyika mjini Niamey kinakuja
siku moja baada yaJumuiya ya kiuchumi
ya Mataifa yaliyoko maghraribi mwa Africa ECOWAS kuchukua hatua ya kusitisha
shughuli zake za kiuchumi na Mali.
Nchi 15 wanachama wa ECOWAS zimetangaza
kufunga mipaka yake na Mali, kusitisha shughuli zote zinazohusiana na masuala
ya kifedha na kuiondolea uanachama .
Umoja
wa Mataifa umelaani mapinduzi ya kijeshi ya Mali yaliyomlazimisha RaisBoubacar Keïta aondoke madarakani.
Walinzi sita wa Makamu wa rais wa Sudan Kusini wauawa
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Makamu wa rais James Wani Igga ni mshirika wa Rais Salva Kiir
Walinzi sita wa Makamu wa rais wa Sudan KusiniJames
Wani Igga wamepigwa risasi hadi kufa na
wengine wawili kujeruhiwa baada ya msafara wao wa magarikuvamiwa na waasi , msemaji
wake ameiambia BBC
Bwana Wani hakuwa katika msafara huo wakati
uliposhambuliwa kwa risasi katika kijiji alikozaliwa cha Lobonok,Kusini mwa mji mkuu, Juba, Jumatano jioni,
amesema Bwana Lado .
Gari la walinzi waMakamu wa rais lilikua likisafiri na
liliharibiwa na kuchomwa na waasi kutoka kundi la National Salvation Front
(NAS), aliongeza.
Kundi hilo halijatoa taarifa yoyote juu ya shambulio hilo.
Bwana Igga ni mmoja wa Makamu wa rais
watano nchini Sudan. Anahusika masuala
uchumi.
Sudan Kusini ilipata uhuru wake kutoka kwa Sudan Kaskazini mwaka 2011,
lakini imekuwa katika migogoro ya mara kwa mara.
Mwana FA, Gwajima wapitishwa kugombea Ubunge CCM
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima nchini Tanzania Josephat Gwajima pamoja na mwanamuziki wa Bongo Flava Hamisi Mwinyi marufu Mwana FA wamepitishwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Gwajima na Mwana FA walishindwa katika kura za maoni katika majimbo ya Kawe na Muheza mtawalia mwezi uliopita.
Hata hivyo vikao vya juu vya chama hicho vimewapitisha wao badala ya walioshinda katika ngazi ya jimbo ili kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi wa ubunge mnamo Oktoba 28.
Wawili hao ni baadhi ya wanasiasa ambao majimbo yao yamefanyiwa mabadiliko ya washindi.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Mwandishi wa habari wa Kenya aachiliwa Ethiopia
Chanzo cha picha, Wizara ya Mambo ya nje ya Kenya
Maelezo ya picha, Kitendo cha kukamatwa kwa Yassin Juma kililaaniwa duniani
Mwandishi wabari wa Kenya Yassin Juma ameachiliwa huru kutoka
mahabusu nchini Ethiopia – takriban wiki
moja baada ya wakili wake kusema kuwa alipatwa na maambukizi ya virusi vya
corona gerezani.
Amehamishiwa kwenye
hospitali ya serikali kwa ajili ya
matibabu, na ataruhusiwa kusafiri kurejea nyumbani Kenya baada ya kupona.
Bwana Juma,ambaye ni
mwandishi huru wa habari, alikamatwa katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, mwezi wa Julai, kufuatia ghasia
zilizoibuka baada ya kuuawa kwa mwanamuziki maarufu wa jamii ya Oromo Hachalu Hundessa .
Maafisa nchini
Ethiopia wiki hii waliamuru kuachiliwa kwake, wakisema “alikamatwa kimakosa”.
Wizara ya Mambo ya
nje ya Kenya ilisema kuwa aliachiliwa baada ya ubalozi wake nchini Ethiopia
kuingilia kati na ambao ulipinga kushikiliwa kwake.
Zimbabwe yataka kujua msimamo wa Vatican juu ya ukosoaji wa Maaskofu
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Serikali ilizima kwa ghasia maandamano ya upinzani mwezi Julai
Serikali ya Zimbabwe
imewasiliana na muwakilishi wa Vatican Askofu Mkuu Marek Zalewski kupata maelezo juu ya ukosoaji wa maaskofu
waKikatoliki dhidi yake.
Hivi karibuni maaskofu
hao walitoa barua ya kitume wakielezea ufisadi, umasikini na ukiukaji wa haki
za binadamu vilivyokithiri nchini humo. Walitoa wito wa kutatuliwa haraka wa
matatizo ya kiuchumi na kisiasa nchini humo.
Waziri wa sheria Ziyambi Ziyambi anasema
serikali inataka kujua iwapo maaskofu hao walizungumza kwa niaba ya serikali ya
Vatican.
" Serikali inataka kuzungumza na Vatican kuelewa iwapo taarifa ya aina
hiyo inaonyesha msimamo rasmi wa mkuu wa
Vatican kuelekea utawala wa Zimbabwe au haya ni maoni ya watu ," alisema.
Bwana Ziyambi amesema kuwa Waziri wa Mambo ya nje Sibusiso Moyo atakutana
na muwakili wa Vatican nchini humo.
Magufuli awataka wajumbe wa CCM Tanzania kuweka maslahi ya nchi mbele
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Aboubakar Famau
Nafasi, BBC Swahili, Dar es Salaam
Chanzo cha picha, Reuters
Rais John Pombe Magufuli amewataka wajumbe kufanya uteuzi kwa
kuweka maslahi ya nchi mbele bila kutumia kigezo cha ukanda, udini, udugu na
kuendelea.
Rais huyo wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa Chama Tawala CCM alikuwa akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya
Chama hicho kitakachofanya uteuzi wa wabunge na wawakilishi watakaopeperusha
bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Katika ufunguzi huo, rais Magufuli amesema kazi kubwa tayari imefanywa siku mbili zilizopita
ambapo mafaili 1367 yaliangaliwa na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM.
Huenda Kenya ikaanza kujaribu tiba ya corona
Maelezo kuhusu taarifa
Author, Rhoda Odhiambo
Nafasi, BBC Africa,Nairobi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Kenya ina zaidi ya watu 31,000 wenye virusi vya corona
Huenda Kenya
ikaanza kujaribu kuwatibu wagonjwa wa Covid-19 kwa kutumia plasma. Plasma ni sehemu ya maji maji ya damu ambayo inabakia
wakati seli zote nyeupe na nyekundu za damu pamoja na ute mweupe vinapoondolewa.
Dokta Mercy Mwangangi kutoka
Wizara ya Afya anasema kuwa watalaam wanandaa miongozo ambayo itawaruhusu madakatari
kutumia sehemu hii ya damu kama tiba ya corona.
'Katika uchunguzi huu,
watalaam, watakuwa wanachunguza uwezekano wa kuchukua damu ya mtu ambaye
amepona baada ya kuambukizwa corona na kuitumia damu hiyo kumtibu yeyote ambaye
amepatikana na maambukizi hayo,” Dokta Mwangagi aliwaelezea wanahabari.
Mbinu hiyo ya kutumia damu
kumtibu mtu mwingine ni matibabu ya kale.
Dawa hii inapunguza uvimbe wa mwili kulingana na homoni
inayotengenezwa ndani ya mwili. Katika janga hili, dawa hili hutumika kwa wale ambao wako
katika hali mahututi na hawawezi kupuma vizuri.
Plasma inatumiwa kwasababu ina kinga ya mwili. Lakini, kwa
sasa wataalam hawajui kinga hiyo inadumu kwa muda ngapi au siku ngapi.
Kuna zaidi ya majaribio 80
ambayo yanalenga kuwasajili wagonjwa kushiriki katika uchunguzi huu kote
duniani.
Viongozi wa mapinduzi Mali wazungumza na upinzani
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Viongozi wa mapinduzi Mali
Viongozi wa mapinduzi ya kijeshi nchini Mali wamefanya mazungumzo na viongozi wa
upinzani ambao wamepongeza kung’olewa madarakani kwa Ibrahim Boubacar Keïta.
Wamemlaumu kwa kushindwa kukomesha
mashambulio ya jihad na kuporomoka kwa uchumi wa nchi.
Muungano wa upinzani umesema
unatambua utashi wa jeshi wa kuundwa kwa
serikali ya mpito ya kiraia.
Kanali wa jeshi , Assimi Goita, amejitokeza
kama kiongozi mpya wa jeshi la nchi hiyo. .
Amewataka wafanyakazi wa umma kurejea kazini.
Baraza la usalama la Umoja wa
Maraifa limelaani mapinduzi nchini Mali.
Viongozi wa Afrika Magharibi wametangaza kufunga mipaka yao na Mali na
wanatarajia kufanya mkutano kwa njia ya video kujadili hatua zaidi dhidi ya
Mali.
Raia wa nchi 130 kuingia Kenya bila Karantini
Mamlaka nchini Kenya zimetoa orodha mpya ya raia wa nchi 130 ambao wataruhusiwa kuingia nchini humo bila kukaa karantini.
Kenya ilifungua anga lake Agosti Mosi na Tanzania pia haikuwemo kwenye orodha ya awali. Hali hiyo ilisababisha mamlaka za Tanzania kuzuia ndege za Shirika la Ndege la Kenya kutua nchini humo.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Licha ya viongozi wa pande zote mbili kusema wanafanya mazungumzo, bado undani ama matokeo ya mazungumzo hayo havijawekwa wazi.