Misururu mirefu yashuhudiwa kwenye maduka ya pombe Afrika Kusini
Afrika Kusini imelegeza sheria za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona na kuweka kiwango cha piliJumanne, na kuruhusu mauzo ya pombe na sigara.
Chini ya sheria mpya, mauzo ya pombe yanaruhusiwa kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi kati ya saa tatu za aubuhi hadi saa kumi na moja jioni.
Misururu imekuwa ikionekana nje ya maduka ya pombe katika miji mikubwa nchini humo.
Watu pia wanaruhusiwa kusafiri baina ya mikoa. Imeruhusiwa Kuwatembelea watu wa familia na marafiki lakini kwa makundi mawili.
Mbuga za wanyama na fukwe zimeefunguliwa ili kuwaruhusu watu kujivinjari na matukio yamichezo ili kuruhusu watu kuyatembelea
Uvaaji wa barakoa kwenye maeneo ya umma ni lazima.