Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Marekani yatoa tahadhari ya usafiri Kenya,Tanzania, Rwanda na Uganda, kulikoni?
Marekani imetoa tahadhari dhidi ya usafiri katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda kufuatia ongezeko la virusi vya corona.
Moja kwa moja
Esther Namuhisa
Leo tarehe 10 Agosti katika Dira ya Dunia....
Vilabu vya pombe na makanisa vyafungwa Malawi
Mamlaka ya Malawi imetoa amri ya kufunga vilabu vyote vya pombe na makanisa.
Agizo hilo limekuja baada ya idadi ya maambukizi ya virusi vya corona kuongezeka mara mbili ndani ya mwezi uliopita.
Mpaka sasa taifa hilo lina maambukizi 4,624 ya virusi vya corona kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins
Maafisa wapya wameajiriwa ili kuhakikisha kuwa watu wanafuata muongozo mpya.
Muongozo huo ni pamoja na kupiga marufuku mkusanyiko wa watu zaidi ya 10 na lazima watu kuvaa barakoa.
Taifa hilo lilionekana kupuuzia tishio la maambukizi ya virusi vya corona kwa miezi kadhaa wakati wa marudio ya uchaguzi wa rais ambapo upande wa upinzani ulishinda na Lazarus Chakwera kuwa rais mwezi Juni.
Mahakama ilisitisha marufuku kutoka nje mwezi Aprili, wakihofia watu maskini kuwa na wakati mgumu.
Jadon Sancho atajwa kwenye kikosi cha Borussia Dortmund
Borussia Dortmund imemtaja mshambuliaji Jadon Sancho katika kikosi cha watakaokuwa kwenye kambi ya mazoezi huko Switzerland.
Taarifa hiyo imekuja siku ya mwisho ya makubaliano ambayo iliwekwa na Dortmund ambayo yamekubaliwa kimataifa England, lakini nani ambaye anawaniwa katika kipindi hiki cha kiangazi.
Kwa upande wa Dortmund ya Bundesliga wanataka usajili wa Sancho kuwa £100m , ambaye alisainiwa kutoka Manchester City kwa £10m mwaka 2017.
Sancho mwenye miaka 20,na kiungo wa kati wa England na Jude Bellingham mwenye miaka 17 ni miongoni ya wachezaji 31 watakaosafiri kwenda Bad Ragaz.
Bellingham, alijiunga na Dortmund akitokea klabu ya Birmingham mwezi Julai.
Dortmund itakuwa na mechi mbili katika kambi yao, moja ni dhidi ya Austria SCR siku ya Jumatano na Austria Vienna siku ya Jumapili.
Kuwekwa kwa siku ya mwisho kwa Sancho, ambaye yuko kwenye mkataba mpaka 2022, ni kutaka kuwa na uhakika wa kikosi kamili kwa ajili ya msimu wa 2020-21 wa Bundesliga .
Msimu mpya utaanza Septemba, 18, huku siku ya mwisho ya uhamisho wa wachezaji wa mikataba ya kimataifa ukiwa ni Oktoba 5.
Tanzania yatangaza viwango vya wachezaji kutoka nje
Waziri mwenye dhamana ya michezo nchini Tanzania, Dkt. Harison Mwakyembe ametangaza uamuzi wa Serikali kuendelea kuruhusu idadi ya wachezaji 10 wa kigeni. Ingawa idadi ya wachezaji wanaotakiwa kuanza kucheza itabaki chini ya baraza la michezo nchini humo.
Dkt Mwakyembe amesema Serikali imezingatia maoni ya wadau wa soka na kushirikiana na baraza la michezo.
Aidha wadau hao wa soka watakaa kujadili aina ama viwango vya wachezaji wanaopaswa kusajiliwa na kuingia nchini humo. Angalau nchi zilizopo katika nafasi ya 50 kwa FIFA ndio wasajiliwe hata wa daraja la kwanza ingawa bado hii si sheria ni maoni tu.
"Ni vyema aina ya wachezaji watakaosajiliwa kutoka nje wawe na weledi wawe na uwezo mkubwa," Waziri Mwakyembe ameeleza.
Kando na hivyo wizara imeagiza watu wanaoajiriwa nchini wawe na ulazima wa kujifunza Kiswahili.
DRC kufungua shule baada ya kudhibiti corona
Baadhi ya wanafunzi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameruhusiwa kurejea shule leo baada ya miezi mitano ya tishio la mlipuko wa virusi vya corona.
Wanafunzi wanaojiandaa kufanya mitihani yao ya mwisho ndio watarejelea shule .
Kwa mujibu wa wizara ya elimu, waziri wa elimu bwana Willy Bakongo amesema “Baada ya miezi tano ya kukabiliana na corona, serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeamua kufungua shule".
Wizara ya elimu ilianza wiki iliyopita kutangaza na kutoa barakoa na vifaa vingine vya kinga dhidi yya corona katika shule ambazo zinafunguliwa leo.
Hata hivyo baadhi ya wazazi wanaonekana kutamani wanafunzi wote waruhusiwe kurejea shuleni.
Hatua hii imekuja baada ya rais Felix Tshikedi kutangaza mwisho wa hali ya dharura nchini humo na kusema kuwa maambukizi ya corona yamepungua kutoka asilimia kumi na mbili mpaka asilimia mbili na nusu.
Hifadhi kubwa ya wanyamapori Kenya yateketea kwa moto
Mamlaka ya Kenya imetuma jeshi kusaidia zima moto katika kupambana na moto mkubwa ulioibuka katika hifadhi kubwa ya wanyama pori ya Tsavo ambayo ni kivutio kikubwa cha utalii nchini humo.
Mamlaka ya huduma za hifadhi za wanyama pori imekilaumu kikosi cha zima moto kwa kushindwa kuzima moto huo ambao umekuwa ukiendelea kwa siku kadhaa.
Kwa sasa wanajeshi wanatumia helkopta kumwaga maji kuzima moto huo, wakati mamia ya watu wamejitolewa kutoa usaidizi pia.
Moto huo mkubwa umeharibu sehemu kubwa ya ya hifadhi ya Tsavo, ambayo iko Kusini Mashariki mwa Kenya.
Moto huo umehatarisha maisha ya wanyama pori na mimea.
Hifadhi hiyo ambayo ina mamia ya simba, tembo na vifaru, Imekuwa ikiwavutia watalii wengi wa kimataifa kila mwaka lakini sasa pameathirika na moto wakati ambao Kenya inakabiliana na janga la corona ambalo limesababisha taifa hilo kupoteza mabilioni ya dola katika pato la taifa.
Baadhi ya picha zikionyesha jinsi hifadhi hiyo ilivyoathirika;
Marekani yatoa tahadhari ya usafiri Kenya,Tanzania, Rwanda na Uganda, kulikoni?
Marekani imetoa tahadhari dhidi ya usafiri katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania na Rwanda kufuatia ongezeko la virusi vya corona.
Taarifa katika tovuti ya ubalozi wa Marekani nchini Kenya imesema serikali ya Kenya imeondoa marufuku ya kukaa nyumbani na kurejesha usafiri na baadhi ya shughuli za kibiashara.
"Zingatia upya uamuzi wa kusafiri Kenya kutokana Covid 19" ilisema tahadhari ya kiwango cha tatu iliyotolewa na CDC ikiangazia usafiri ambao sio wa dhararu.
Tahadhari hiyo inawaarifu wasafiri kwamba mlipuko wa virusi vya corona umeongezeka na kwamba watakua hatarini kupata maambukizo ikiwa hawatakua waangalifu
Mataifa mengine ya Afrika ambayo Sudan Kusini, Ethiopia, Djibouti, Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe na nyinginezo.
Huku hayo yakijiri Kenya imemteua mwanariadha bingwa wa Olimpiki mbio za marathon Eliud kuwa balozi wa utalii Kenya wakati taifa hilo likiangalia mianya ya kurejesha utalii wa kimataifa.
Zaidi ya watu milioni mbili wamepoteza ajira zao katika sekta hiyo nchini Kenya na mamlaka inakadiria kuwa hali inaweza kurudi kama awali mwanzoni mwa mwaka 2023.
Karibu katika matangazo yetu mubashara leo Jumatatu 10.08.2020