TB Joshua anasubiri 'sauti kutoka kwa Mungu'

Mchungaji maarufu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua anasema anasubiri kusikia 'sauti ya Mungu' kabla hajafungua huduma za ibada katika jiji la biashara la Lagos.

Moja kwa moja

Esther Namuhisa

  1. Huo ndio mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo tutaonana tena hapo kesho.

  2. Mahakama ya China yamuachia huru mhalifu wa mauaji baada ya miaka 27

    Zhang Yuhuan: Chinese court clears man of murder after 27 years in prison

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanaume moja Mashariki mwa China ambaye alikuwa ameshitakiwa kwa madai ya mauaji ameachiwa huru baada ya kukaa gerezani miaka 27.

    Zhang Yuhuan alikuwa aKIteswa na polisi na kulazimishwa kukiri madai ya mauaji ya vijana wawili mwaka 1993.

    Yuhan alikuwa ni raia wa China aliyekaa gerezani kwa muda mrefu zaidi baada ya kuhukumiwa kimakosa .

    Alikaa gerezani huko Jiangxi kwa siku 9,778 .

    Waendesha mashtaka walifungua tena kesi yake wakisema mtuhumiwa huyo alikiri uhalifu mwingine tofauti na ule uliomueka gerezani.

    Hivyo mahakama ikaamua kumuachia huru na kueleza kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha uhalifu huo.

    Baadhi ya watu wanasema China iko radhi kuwaachia huru wahalifu lakini sio wanasiasa.

    Vyombo vya habari vya China vilionesha video ya bwana Zhang akilakiwa na familia yake, mama yake mwenye umri wa miaka 83 na aliyekuwa mke wake, wakati akitoka gerezani.

  3. TB Joshua anasubiri 'sauti kutoka kwa Mungu'

    Josha

    Chanzo cha picha, AFP

    Mchungaji maarufu wa Nigeria, Temitope Balogun Joshua maarufu kama TB Joshua anasema anasubiri kusikia 'sauti ya Mungu' kabla hajafungua huduma za ibada katika jiji la biashara la Lagos.

    Mamlaka mjini Lagos imeruhusu huduma ibada kuanza siku ya Jumapili kuanza,waumini wakiwa nusu yake baada ya kufungwa kwa huduma hizo kwa miezi kadhaa ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

    Katika video aliyoiweka kwenye kurasa yake ya Twitter, TB Joshua alisema amesikia kutoka kwa mamlaka lakini bado anasubiri kusikia kutoka kwa Mungu.

    "Muwe na uhakika kuwa punde tu nitakaposikia sauti ya Mungu , nitawajulisha huduma za ibada zitaanza lini," aliongeza.

    Mapema mwaka huu nabii huyo alisababisha mkanganyiko baada ya kudai kuwa mlipuko wa virusi vya corona utaisha tarehe 27,Machi.siku chache kabla ya marufuku ya kutoka nje haijaanzishwa katika jimbo la Lagos, Ogun na mji mkuu Abuja.

    "Mwishoni mwa mwezi huu, tupende au tusipende, haijalishi kama dawa gani itatengenezwa kwa ajili ya kutibu, virusi hivi vitaondoka kama jinsi vilivyokuja," alisema hayo katika mahubiri yake.

    Tarehe 27 Machi ilipopita alijikuta anadhihakiwa kwa maono ya uongo.

    Lakini alijitetea kwa kusema kuwa alimaanisha virusi vitaanza kuisha kule vilipoanzia mjini Wuhan nchini China,na tayari vimeondoka."

  4. Waganda waishtaki Marie Stopes baada ya kondomu walizotumia kupasuka

      • Author, Patience Atuhaire
      • Nafasi, BBC News, Kampala
    kondomu

    Chanzo cha picha, MARIE STOPES UGANDA

    Raia watatu wa Uganda wameishtaki mamlaka ya dawa nchini humo pamoja na shirika la kimataifa la Marie Stoppes kwa kupata magonjwa ya zinaa na ujauzito baada ya kutumia kondomu ambazo hazikuwa na ubora.

    Taasisi hiyo isiyokuwa ya kiserikali ilisambaza kondom ambazo baadae mamlaka ya dawa ilisitisha matumizi yake mwaka 2019.

    Mwanaume mmoja alidai kuwa alitumia kondomu ya 'Life Guard' lakini wakati wa kujamiiana ilipasuka na hivyo kumsababishia kupata virusi vya Ukimwi huku mwingine alidai kuwa alipata ugonjwa wa zinaa wa gonorea.

    Na mwanamke mmoja alisema kuwa alipata ujauzito baada ya kutumia kondomu hiyo.

    Madai dhidi ya kondomu hizo yalidai kuwa hazikupimwa na kuthibitishwa ubora wake kabla ya kusambazwa kwa Umma.

    Marie Stoppes ilisambaza kondomu milioni mbili kwa mwezi katika nchi nzima.

    Inaonekana kuwa uingizwaji na usambazaji wa kondomu hizo ulisitishwa.

    Mamlaka ya dawa ya taifa na wahusika wote wa kuthibitisha ubora wa bidhaa za afya wanalalamikiwa kwa kushindwa kutimiza majukumu yao kabla ya kusambazwa kwa kondomu hizo sokoni

    Awamu mbili za ugawaji wa kondomu zipatazo milioni moja, zilisitishwa sokoni na serikali mwezi Novemba 2019, kufuatia malalamiko kutoka kwa Umma.

    Lakini wengi wameuziwa kondomu hizo na asilimia 70 tu ndio ziliweza kuondolewa sokoni.

    Aidha, wanaume wawili waliishtaki Marie Stoppes kwa madai mengine mwezi Februari mwaka huu, wakitaka fidia.

  5. Tanzania yahofiwa jinsi inavyoshughulikia janga la corona

    corona

    Chanzo cha picha, Reuters

    Mkurugenzi wa kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika ameelezea wasiwasi wake kuhusu namna Tanzania inavyokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona.

    Dkt John Nkengasong aliiambia BBC hakuwa na data za kutosha za kufahamu hali ilivyo nchini Tanzania.

    Alisema kituo cha kudhibiti magonjwa kimeanzisha jitihada za pamoja za kupambana na virusi hivyo.

    "Tunaendelea kutumaini na kuiomba Tanzania kuripoti hali ilivyo ili tuweze kufanya kazi kwa pamoja na kuondoa virusi hivi katika bara hili," alisema.

    Alisisitiza kuwa kuna uhitaji wa mataifa yote ya Afrika kushirikiana katika hili.

    "Tunaendelea kuwasiliana na Tanzania lakini bado hatujapata majibu ambayo tunayatarajia," alisema.

    Rais wa Tanzania John Magufuli amesisitiza kusema kuwa taifa lake liko salama.

    Tanzania inajiandaa kufanya uchaguzi mwezi Oktoba na shamrashamra za uchaguzi zimeanza.

    Wananchi wengi wa taifa hilo wamekuwa wakiendelea na shughuli zao bila kuvaa barakoa na wala kuzingatia kukaa mbali.

  6. 'Mama Theresa wa Somalia' akumbukwa kwa huduma za jamii

    bbc

    Daktari na mwanaharakati maarufu nchini Somalia Hawa Abdi amefariki akiwa na umri wa miaka 70.

    Dkt Abdi aliweza kuwahudumia maelfu ya watu kwa kujenga hospitali, shule na vituo vya kulelea watoto karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.

    Wagonjwa wake wengi walikuwa wahanga wa mapigano na aliwatibu bure.

    Dkt Abdi, alijulikana kama Mama Theresa wa Somalia, ambaye alibaki nchini humo kwa miongo mitatu ya mgogoro.

    Mwaka 2011, hospitali yake ilishambuliwa na kundi la wapiganaji wa kiislamu.Alisimama na kuunga mkono mamia ya waandamanaji wanawake.

  7. Magufuli akichukua fomu kwa picha

    Tume ya taifa ya uchaguzi

    Chanzo cha picha, Tume ya taifa ya uchaguzi

    Maelezo ya picha, Rais Mgufuli pamoja na mgombea mwenza wake Bi.Samia Suluhu wakiwa wamepokea fomu za kugombea urais kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)
    Tume ya taifa ya uchaguzi

    Chanzo cha picha, Tume ya taifa ya uchaguzi

    Tume ya taifa ya uchaguzi

    Chanzo cha picha, Tume ya taifa ya uchaguzi

    Maelezo ya picha, Rais Magufuli kuwania muhula wa pili wa urais kupitia chama tawala CCM.
  8. Botswana yapiga marufuku uuzwaji wa pombe

    botswana

    Chanzo cha picha, af

    Serikali ya Botswana imepiga marufuku uuzwaji wa pombe na kusimamisha leseni za wauzaji wote wa vinywaji.

    Marufuku hiyo itaendelea mpaka muongozo mwingine utakapotolewa.

    Maduka yote ya pombe yatasalia kuwa yamefugwa.

    Hatua hiyo imekuja ili kuzuia kasi ya maambukizi ya corona.

    Wiki iliyopita serikali ya Botswana iliweka amri ya kutotoka nje katika mji wa Gaborone kwa muda wa wiki mbili ili kupunguza maambukizi ambayo yalikuwa yanaogngezeka kwa kasi.

    Taifa hilo limethibitisha kuwa na maambukizi 804 ya virusi vya corona na vifo viwili.

  9. Msumbiji yatangaza hali ya dharura kwa mara ya pili

    MSUMBIJI

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharura

    Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ametangaza siku nyingine 30 za dharura kujaribu kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona.

    Hii ni mara ya pili kwa taifa hilo kutangaza dharura ya hali ya afya tangu mwezi Machi wakati walipothibitisha mtu wa kwanza mwenye virusi vya corona nchini humo.

    Rais Nyusi alihutubia taifa kupitia matangazo ya televisheni na kuainisha hatua ambazo zitasaidia kupambana na virusi hivyo kwa urahisi .

    Awamu ya kwanza kuanzia Agosti 18, taasisi za elimu ya juu zitafunguliwa , mafunzo ya jeshi na ufundi. Mikusanyiko ya dini itaruhusiwa kwa watu wasiozidi 50 . Idadi ya watu 20 mpaka 50 wataruhusiwa kuhudhuria katika msiba au mazishi lakini kwa mtu yeyote aliyekufa kutokana na virusi vya corona watu watakaomzika wasizidi 10.

    Awamu ya pili itaanza Septemba; maeneo ya burudani kama sinema, ‘casino’ na sehemu za kufanyia mazoezi zitafuguliwa.

    Awamu ya tatu itaanza Oktoba, wanafunzi wa sekondari ambao wako mwaka wa mwisho wa masomo watarejea shuleni.

    Vilabu vya pombe vitabaki kuwa vimefungwa. Msumbiji imethibitika kuwa na maambukizi 2,079 na vifo 15.

  10. Magufuli achukua fomu kuwania muhula wa pili

    Magufuli

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais John Magufuli amechukua fomu kuwania muhula wa pili wa Urais wa Tanzania katika makao makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dodoma.

    Magufuli anawakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) na alifika katika ofisi za NEC akiwa pamoja na mgombea mwenza wake Bi Samia Suluhu na kupewa muongozo wote wa kufata kisheria.

    Baada ya hapo atakutana na wanachama wa CCM katika makao makuu ya chama hicho jijini Dodoma.

    Uchaguzi wa rais nchini Tanzania unatarajiwa kufanyika tarehe 28.10.2020.

  11. Karibu katika matangazo yetu mubashara leo Alhamisi 06.08.2020