Magufuli: Mkapa ni shujaa wangu, alinilea kama mtoto wake
Rais John Magufuli kuongoza viongozi wengine katika kumuaga rais mstaafu Benjamin Mkapa
Moja kwa moja
Mwili wa Mkapa umewasili kijijini
Mwili wa rais mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa umewasili kijijini Lupaso mkoa wa Mtwara kutokea Dar es Salaam. Shughuli za mazishi zinatarajiwa kuanza kesho saa mbili asubuhi.
Ruka Instagram ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
Idadi ya wagonjwa wa corona Kenya yavuka 18,000
Wizara ya Afya nchini Kenya imetangaza vifo 14 na ongezeko la watu 606 wapya wenye virusi vya corona baada ya watu 4,888 kupimwa ndani ya saa 24.
Kufikia sasa Kenya ina jumla ya watu 18,581 walioambukizwa virusi vya corona.
Kati ya maambukizi hayo mapya watu 583 ni raia wa Kenya, huku wageni ni 23.
Wanaume ni 409 na 197 ni wanawake.
Kati ya maambukizi hayo kuna mtoto wa miezi minne na mzee kuliko wote ana miaka 85.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Wimbo wa Jerusalema waangaliwa na watu milioni 50
Wimbo maarufu wa Jerusalema ulioimbwa na msanii kutoka Afrika Kusini, Master KG,umepata watazamaji milioni 50 katika mtandao wa kijamii wa Youtube.
Muimbaji huyo alisheherekea mafanikio hayo kwa kuhamasisha kwenye mtandao wa kijamii wa Tweeter kwa kuweka kauli mbiu ya mashindano ya Jerusalem #Jerusalemachallenge –kampeni ambayo ilishirikishwa na watu wengi duniani.
Katika mahojiano kadhaa Master KG alisema anafurahia sana anapoona watu kutoka maeneo mbalimbali Afrika au hata duniani wakicheza wimbo wake ambao aliutoa mwishoni mwa mwaka jana.
Ruka YouTube ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje Mitandao ya kijamii inaweza beba matangazoMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa YouTube ujumbe
Viatu virefu, kucha ndefu marufuku ofisi za umma Tanzania
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Munira Noor
- Nafasi, BBC Swahili

Mamlaka nchini Tanzania imetoa muongozo mpya wa mavazi na unadhifu wa wafanyakazi wa umma.
Muongozo huo umepiga marufuku uvaaji wa viatu virefu katika ofisi za umma au shughuli zozote za kiserikali kwa wafanyakazi wa umma, hususani viatu vinavyozidi inchi tano zaidi.
Kwa upande wa kucha wafanyakazi wote wa umma nchini humo sasa hawaruhusiwi kuwa na kucha ndefu , kwa wanaume na wanawake. Lakini pia wanawake wanaopenda kupaka rangi kucha zao basi hawaruhusiwi kuchanganya rangi kama baadhi ya wanawake wanavyofanya.
Suala la nywele pia limegusiwa kwa wanawake na wanaume wafakazi wa wa serikali , zinatakiwa kutokuwekwa rangi au mitindo ambayo sio sahihi.
Kwa mujibu wa waraka wa muongozo kwa watumishi wa umma wa mwaka 2020, na Gazeti la serikali la Habari leo ,mabadiliko hayo yameanza rasmi mwezi huu wa Julai.
'Hali mbaya ya hewa yaufanya ujumbe wa Kenya kugeuza'
Mtandao wa Twitter wa Gazeti la kila siku nchini Kenya la Daily Nation unaripoti kuwa ndege iliyombeba mwakilishi wa rais Uhuru Kenyatta, Samuel Poghisio ilibidi igeuze kabla ya kufika Dar es Salam kutokana na hali mbaya ya hewa.
Katika hafla kumuaga aliyekuwa rais wa Tanzania Benjamin Mkapa, Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania Profesa Palamagamba Kabudi alieleza kuwa ndege hiyo ilibidi igeuke katika anga ya Tanzania eneo la Monduli mkoani Arusha.
Hata hivyo hakueleza sababu ya ndege hiyo kugeuza kabla ya kuwasili Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Daily Nation, "maafisa jijini Dar es Salaam wameeleza kuwa ndege hiyo iligeuza kutokana na hali mbaya ya hewa."
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
NRM yamuidhinisha rasmi Museveni kuwa mgombea wa urais 2021
Maelezo kuhusu taarifa - Author, Isaac Mumema
- Nafasi, BBC Swahili

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ameidhinishwa rasmi kuwa mgombea wa kiti cha urais kupitia chama cha NRM na pia kuwa mwenyekiti wa chama hicho.
Katika zoezi lilofanyika leo asubuhi makao makau ya chama Kyadondo mjini Kampala.
Rais Museveni alipendekezwa na ndugu Rukana Rugunda ambaye pia ni waziri mkuu wa Uganda na kuhidhinishwa na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa chama tawala NRM bwanaTanga Odoi.
Wengine waliongozana na rais Museveni ni mkewe bi.Janet Museveni, makamu wa chama tawala Alhaji Mosese Kigongo na makamu wa pili mwanamuke ambaye pia ni Spika wa bunge la Uganda bi. Rebecca Kadaga.
Baada ya kuidhinishwa rais Museveni amehutubia baadhi ya viongozi na wanachama waliokuwepo hapo na kusisitiza wananchi kujikinga na virusi vya covid19.
Hatua inayofuata ni mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya chama cha NRM utakaofanyika mwezi ujao wa Agosti na kumuidhinisha kuwa mgombea wa chama cha NRM katika uchaguzi mkuu wa urais mwaka 2021.
Mwili wa Mkapa wasafirishwa Mtwara
Helikopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania iliyobeba mwili wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa imeondoka jijini Dar es Salaam kuelekea Masasi Mtwara ambapo kiongozi huyo atazikwa kesho kijini kwake Lupaso.
Ruka Instagram ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa Instagram ujumbe
'Hatutawaona tena wakiwa pamoja'

Rais wa Tanzania John Magufuli amesema kuwa ni majonzi kuwa picha iliyokuwa ikiwapendeza wengi ya marais wa nchi hiyo wakiwa pamoja haitapigwa tena.
Picha hiyo ni ya marais wastaafu watatu wa taifa hilo, Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete. Rais Magufuli pia amekuwa akijumuika nao.
"Mtakumbuka hivi karibuni tuliwaona viongozi hawa watatu katika uzinduzi wa kitabu cha historia cha Mkapa, tuliwaona wakiwa pamoja katika uzinduzi wa mfuko wa jamii wa Tasaf, walikuwa pamoja katika uzinduzi wa Ikulu Chamweno Dodoma, na tuliwaona pamoja Julai 11 katika mkutano mkuu wa CCM," Magufuli alisema.
"Kwa hakika ilikuwa inapendeza sana kufurahisha sana. Lakini sasa hatutawaona wote kwa pamoja, Mzee Mkapa hatunaye tena. Ilikuwa inapendeza sana kuwaona marais wote wastaa lakini sasa hatutamuona mmoja kamwe. Kazi yake ameikamilisha".
Uwanja wa Taifa wapewa jina la Mkapa

Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam umebadilishwa jina rasmi na kutoka leo utaitwa uwanja wa Mkapa.
Hilo limetangazwa na Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya kitaifa ya kumuaga marehemu Benjamin Mkapa ambaye alifariki wiki ilopita.
Mkapa alikuwa rais wa awamu ya tatu wa Tanzania kutoka mwaka 1995 mpaka 2005. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ulijengwa wakati wa kipindi chake.
Magufuli ameeleza kuwa anafahamu Mkapa mwenyewe hakupenda vitu viitwe jina lake "ila leo kwa sababu amelala na hawezi kuniadhibu kwa namna yoyote ile, nauita rasmi uwanja ule kwa jina lake."
Japo hakujipambanua kama shabiki wa michezo, Magufuli amesema Mkapa alikuwa shabiki klabu ya Yanga.
Magufuli: Mzee Mkapa ni shujaa wangu, alinilea kama mtoto wake

Rais John Magufuli amesema kifo cha rais mstaafu Benjamin Mkapa ni pigo kwake binafsi na kumuita kiongozi huyo kuwa ni "shujaa wangu."
Mzee Mkapa ndiye aliemuibua Magufuli katika ulimwengu wa siasa kwa kumteua kuwa naibu waziri mwaka 1995 na baadaye kumpa uwaziri kamili mwaka 2000.
"Bila Mzee Mkapa huenda nisingekuwa hapa nilipo. Mzee Mkapa ni shujaa wangu, hata nilipopatwa na shida na changamoto mbalimbali, mzee Mkapa hakuniacha. Alinilea kama mtoto wake," alieleza Magufuli ambaye alikuwa akizuia machozi.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Magufuli pia amemueleza Mkapa kama kiongozi ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kuibua viongozi wengine.
"...unaweza kusema alikuwa na maono makubwa, ni yeye ndiye aliniibua mimi. Alimteua rais mstaafu Jakaya Kikwete kuwa waziri wake wa Mambo ya Nje kwa miaka 10, unaweza kusema alikuwa anamuandaa kumrithi. Pia amemuibua rais Shein wa Zanzibar na hata mgombea wa CCM Zanzibar Dkt Mwinyi amemuibua yeye."
Magufuli pia amesema kuwa hakuna mtu anayeweza kumulezea Mkapa zaidi ya kitabu chake mwenyewe ambacho alikizindua miezi minane iliyopita.
Waziri Mkuu wa Burundi atoa salamu za rambirambi

Waziri mkuu wa Burundi Jenerali Alain Guillaume ameongozana na spika wa bunge la taifa hilo kuwakilisha salamu za rambirambi kutoka Burundi.
Amesema rais wa Burundi na taifa zima linatoa pole kwa Tanzania na wao wamefika kuwafariji kipindi kigumu, "muhimu ni tueendelea kumuombea hayati Mkapa."
Ujumbe wa Burundi ndio pekee uliofika katika hafla hiyo kutoka nje ya Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania ameeleza kuwa wanatarajia kupokea uwakilishi kutoka Zimbabwe, na kuwa ndege iliyombeba muwakilishi wa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Samuel Poghisio ilibidi irejee Kenya kabla kuwasili Tanzania. Hata hivyo hakueleza sababu ya ndege hiyo angani.
Kutoka uwanja wa Uhuru kwa picha








Hafla ya kitaifa ya kumuaga Mkapa yaanza
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli anaongoza mamia ya watu katika hafla ya kitaifa ya kumuaga rais mstaafu wa taifa hilo Benjamin Mkapa ambaye aliaga dunia usiku wa kuamkia Ijumaa.
Toka Jumapili mwili wa Marehemu Mkapa umekuwa ukiagwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Hii leo, ni zamu ya viongozi wakuu wa taifa hilo pamoja na wageni kutoka nje kuaga.
Mzee Mkapa anatarajiwa kuzikwa kesho Kijijini kwake Lupaso, mkoni Mtwara kusini mwa Tanzania.

Karibu katika matangazo yetu ya moja kwa moja leo 28.07.2020
