Tundu Lissu awasili Tanzania
Lissu awasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Moja kwa moja
Habari za hivi punde, Rais Uhuru Kenyatta apiga marufuku uuzaji wa pombe Kenya kwa siku 30
Hakutakuwa na uuzaji wa pombe katika mikahawa na maeneo ya kuuza vyakula kwa kipindi cha siku 30 zijazo, amesema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
Rais Kenyatta amesema kwamba baa zote zitafungwa mara moja akiongezea kwamba zile ambazo zitakiuka agizo hilo jipya zitapokonywa leseni zao.
Masharti ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku hadi alfajiri kuendelea kwa siku 30 nyengine.
Masharti yaliotolewa na Uhuru kenya
- Hakuna uuzaji wa pombe katika mikahawa
- Baa zote zimefungwa mara moja .
- Baa yoyote itakayopuuza agizo hilo na kufungua itapokonywa leseni kabisa
- Inspekta jenerali wa polisi atamkamata mtu yeyote atakayepuuza masharti ya kutotoka nje usiku .
- Masharti ya kukabiliana na corona yataendelea kuheshimiwa katika maeneo yote ya umma na mazishi.
- Wizara ya Afya kuwarudisha kazini kwa muda wafanyakazi wa vyumba vya wagonjwa mahututi waliostaafu ili kusaidia katika kukabiliana na corona..
- Vituo vyote vya afya vilivyotajwa na serikali kutumika kwa lengo la kuwatenga wagonjwa

Chanzo cha picha, Ikulu ya rais
Maelezo ya picha, Rais Uhuru kenyatta wa Kenya Mbunge aliyeathirika na virusi vya Ukimwi akutwa na covid-19

Maelezo ya picha, Mbunge wa Zambia,bi. Princess Kasune Zulu Mbunge wa Zambia,bi. Princess Kasune Zulu, ambaye anashi na virusi vya Ukimwi na anafahamika zaidi kwa harakati zake za kupambana na virusi vya Ukimwi, ametangaza kuwa na virusi vya corona.
Bi.Zulu,mbunge wa chama cha upinzani United Party for National Development, alipima corona Alhamisi iliyopita.
Wabunge 15 wa Zambia walikutwa na virusi vya corona, kwa mujibu wa wizara ya afya Chitalu Chilufya.
Bunge limeahirishwa kwa muda.
Bi.Zulu aliiambia BBC kuwa hajashtushwa na matokeo kuwa ana virusi kwa sababu bunge la Zambia lilikuwa linaendelea licha ya ongezeko la virusi vya corona.
“Nadhani kuna mtu aliona jambo hili linakuja kutokana na tabia ya watu kutofuata muongozo wa afya nchini Zambia, na bunge liliendelea na shughuli zake badala ya kugeuza mfumo wa ufanyaji kazi kwa kufanyia kazi nyumbani na kuwasiliana kwa video,” alisema.
“Muongozo wa kiafya kutozingatiwa, masuala ya kisiasa na uongozi mbaya umesababisha maambukizi ya Covid-19 kuongezeka Zambia.”
Aliwahamasisha watu kutafuta tiba.
Bi. Zulu alisema imekuwa inakabiliana na mlipuko huo polepole.
Zambia imeripotiwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona 4,481 na vifo 139 vilivyotokana na corona.
Lissu awasili Dar es Salaam

Mwanasiasa wa upinzani Tanzania, Tundu Lissu amerejea nyumbani na kulakiwa na mamia ya wafuasi wake katika jiji la kibiashara la Dar es Salaam, karibu miaka mitatu tangu anusurike na jaribio la mauaji.


Maelezo ya picha, Wanachama wa Chadema wakimpokea Tundu Lissu Majira ya saa nane mchana, saa za Afrika mashariki katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere. Akiwa na tabasamu kubwa usoni, Tundu Lissu alikuwa akiwapungia wafuasi wake.
Lissu aliondoka Tanzania mwezi Septemba 2017 baada ya kupigwa risasi 16.
Leo mwanasiasa huyo, alishangiliwa kwa shangwe rais, rais, rais.
Maelezo ya video, Mamia ya watu wamlaki Tundu Lissu 
Maelezo ya picha, Mapokezi ya Lissu Mapokezi hayo yalionekana kuwa ya amani na shangwe ingawa siku ya Jumamosi,Jeshi la polisi nchini Tanzania lilitoa tamko la kuzuia mikusanyiko ya watu siku ya Jumatatu ya Julai 27, hatua ambayo ilikuja baada ya viongozi mbalimbali wa chama cha siasa cha Chadema kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenda kumpokea mwanasiasa wa chama hicho Tundu Lissu.

Jeshi la polisi lilisema taifa lipo katika kipindi cha maombolezo ya kitaifa hivyo vyombo vya dola vinapaswa kuhakikisha kuwa hali ya amani na utulivu inakuepo katika kipindi chote cha maombolezo.
Viongozi na wanachama wa Chadema wafurika uwanja wa ndege kumpokea Tundu Lissu

Maelezo ya picha, Mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe akiwasili kumpokea Tundu Lissu Viongozi na wanachama wa Chadema wafurika kumpokea Tundu Lissu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Joseph Mbilinyi ,mbunge amesema "Unaachaje kuja kumpokea mtu aliyepigwa risasi 16 na bado yuko hai, huyo ni mbeba maono lazima tumpokee".

Maelezo ya picha, Mbunge Joseph Mbilinyi akiwa na wanasiasa wengine wa upinzani 
Maelezo ya picha, Joseph Haule, Mbunge wa chama cha Chadema "Nimekuja kushuhudia miujiza ya kupona kwa Lissu, sisi tuliokuwa Dodoma tuliona jinsi alivyokuwa ndio maana tumekuja kumshuhudia shujaa", Joseph Haule mbunge wa chama hicho.


Mabango mengi yakiwa yameandikwa karibu kiongozi yalikuwa yamebebwa na wanachama huku wakiwa wamevalia sare.
Mapokezi ya Tundu Lissu yanavyoendelea
Msichana akatwa mkono baada ya kukataa posa
Polisi nchini Uganda wanachunguza tukio la binti wa miaka 16 aliyekatwa mikono kwa kukataa posa, kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor Uganda.
Inadaiwa kuwa mtuhumiwa aliwasili nyumbani kwa binti huyo mwenye umri wa miaka 16 majira ya saa tatu usiku wiki iliyopita na kumkata mkono wake wa kulia.
Binti huyo wa kidato cha pili alijeruhiwa pia katika maeneo mengine ya mwili.
“Alitaka kunioa lakini nilikataa kwa sababu ninapenda masomo yangu.Hakufurahia jibu langu na akanikasirikia sana,”aliliambia gazeti la Daily Monitor.
Alisema baada ya kukatwa mkono, aliondoka na kumuacha akimiminika na damu.
"Rafiki yangu aliwapigia ndugu zangu na kunipeleka hospitali ya Bududa na baadae nikapelekwa hospitali ya rufaa ya Mbale,” alisema.
Zambia kusajili mikokoteni
Mamlaka ya Zambia imepanga kusajili mikokoteni yote ambayo inatumika kwa matumizi ya kibiashara baada ongezeko la vitendo vya wizi.
Wasukuma mikokoteni husaidia kubeba mizigo mjini kwa gharama nafuu.Wafanyabiashara hupenda kutumia wachuuzi hao kwa sababu gharama ya usafirishaji wao ni nafuu.
Meya wa Lusaka bwana Miles Sampa alisema kumekuwa na ongezeko la malalamiko ya wizi kutoka kwa wafanyabiashara ambao hutafuta huduma hiyo .
Kutokana na malalamiko hayo ,meya ameamua kuanzisha malipo ya kodi ya mikokoteni hiyo.
“Baraza litasajili mikokoteni yote inayotumika kwa ajili ya biashara kwa sababu za kiusalama kutokana na ongezeko la malalamiko ya wizi katika masoko yetu.“Usajili wake utamaanisha kuwa watawajibika waziwazi kwa wale ambao wanafanya biashara sokoni na katika vituo vya daladala maeneo ya mjini,”alisema bwana Sampa na hakutakuwa na ushuru ambao wasukuma mikokoteni watatakiwa kulipa.
Wasukuma mikokoteni wameshauriwa kusajili mikokoteni yao katika shirikisho la wasukuma mikokoteni Zambia.
Yanga yamtimua kocha wake kwa madai ya ubaguzi
Klabu kongwe ya mpira wa miguu nchini Tanzania Yanga imeamua kumfukuza kazi Kocha wake, Luc Eymael kwa madai ya 'kutoa kauli za kibaguzi na zisizo za kiungwana'.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji anadaiwa kutoa matamshi ya kibaguzi hapo jana.
Uongozi wa Yanga umeomba radhi kwa mashabiki wa Yanga viongozi wa shirikisho la mpira nchini Tanzania pamoja na wadau wote wa soka.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Kwa taarifa zaidi soma: https://bbc.com.im/swahili/michezo-53549823%3C/a%3E%3C/p%3E%3C/div%3E%3C/div%3E%3C/article%3E%3C/li%3E%3Cli class="css-xxlek1">
Tundu Lissu njiani kurejea Tanzania
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Karibu kwenye matangazo mubashara
Idhaa ya Kiswahili ya BBC ina furaha kukukaribisha msomaji wetu katika ukurasa huu wa habari mubashara. Kupitia ukurasa huu maalum tutakuwa tunakuletea habari kemkem na za moja kwa moja kutoka Afrika Mashariki, Afrika na kila pembe ya dunia.
Ukurasa huu, utaletwa kwako kila siku kutoka Jumatatu mpaka Ijumaa, saa tatu asubuhi mpaka saa 11 jioni.
