Mo Dewji apatikana baada ya siku tisa

Mo Dewji, bilionea Mtanzania aliyetekwa na watu wasiojulikana Alhamisi wiki iliyopita, amerejea nyumbani salama

Moja kwa moja

  1. Habari za hivi punde, Polisi waapa kuwanasa waliomteka Mo Dewji

    Polisi nchini Tanzania wamesema watafanya kila wawezalo kuwatia nguvuni watu waliomteka na kumshikilia bilionea Mohammed Deji, Mo, kwa siku tisa.

    Mkuu wa jeshi hilo, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Sirro amewaambia waandishi wa habari hii leo Oktoba 20 kuwa kuachiwa kwa Mo ni mwanzo wa kuwanasa wahalifu hao na kjuahidi kuwapata wakiwa wazima au wamekufa.

    "Mbio ukizianza sharti uzimalize. Huu ni mwanzo tu. Hao wahalifu wanaotaka kuchafua jina la nchi yetu lazima tuwatie nguvuni."

    Sirro amesema upelelezi umeimarishwa kwa kushirikiana na mtandao wa polisi wa kimataifa Interpol.

    "Nataka niwaambie (wahalifu) yawezekana wananisikiliza hivi sasa kuwa, popote watakapoenda tutawanasa. Wakienda Afrika Kusini tunao, Kenya tunao, Uganda tunao hata Msumbiji, popote pale tutawakamata maana tayari tunaushirikiano na wenzetu."

  2. Sirro: Wahalifu walijaribu kuchoma moto gari

  3. Gari lililotumika kumteka Mo Dewji lapatikana

  4. Godbless Lema aahirisha mkutano na wanahabari

  5. Mo Dewji: Ninawashukuru Watanzania kwa kuniombea

    Afisa mkuu wa polisi wa kanda ya Dar es salaam Lazaro Mombasa aliyetembelea nyumbani kwao Dewji kuthibitisha kurejea kwake nyumbani, watu waliomkamata walikuwa na lafudhi ya mojawapo ya lugha za mataifa ya Afrika Kusini. Aliongezea kwamba hatua hiyo imethibitisha wazi kwamba waliomteka sio watanzania.

    ''Nataka kuuthibitishia umma wa Tanzania kwamba nimefika nyumbani kwa akina Mo Dewji nimeongea naye niko na kikosi cha makachero hapa na ndugu yetu ni mzima kama IGP alivyozungumza na umma kwamba jeshi la polisi litaendelea na uchunguzi ili kuhakikisha kwamba tunampata muhusika akiwa mzima.

    Mo Dewji ambaye alionekana mchovu alimshukuru mwenyezi mungu na serikali ya rais Pombe Magufuli pamoja na Watanzania kwa kumuombea.

    ''Namshkuru mwenyezi mungu , serikali ya magufuli na IGP , ahsanteni mimi ni mzima nawashukuru Watanzania wote kwa kuniombea.

    Babake Mo alivimbia vyombo vya habari kwamba mwendo wa saa nane alifajiri walipokea simu ya Mo kwamba yuko salama na moja kwa moja wakaelekea katika eneo la Gymkhana ambako alikuwa amewachwa na watekaji wake.

    '' Tumshukuru mwenyezi Mungu kwamba tumempata salama na anaendelea vizuri. Walikuwa wamemuacha pale na kuondoka. Lakini alikuwa hajafungwa na yuko sawasawa. Tunawashukuru Watanzania wote na rais''.

    Mo Dewji
    Afisa mkuu wa polisi wa kanda ya Dar es salaam Lazaro Mombasasa
  6. Mo Dewji akithibitisha kurudi nyumbai katika ujumbe wake wa Twitter kupitia kampuni yake

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

  7. Mo Dewji atangazwa kupatikana

    Mkuu wa Jeshi la Polisi kanda ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa akitangaza kupatikana kwa Mo Dewji aliyerejea nyumbani kwao akiwa salama

    Maelezo ya video, Mo Dewji aliporudi nyumbani
  8. Waziri nchini Tanzania January Makamba alikutana na kuzungumza na Mo Dewji

    Ruka X ujumbe, 1
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 1

    Ruka X ujumbe, 2
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe, 2

  9. Habari za hivi punde, Mo Dewji hatimaye apatikana

    Mo Dewji, bilionea Mtanzania aliyetekwa na watu wasiojulikana Alhamisi wiki iliyopita, amerejea nyumbani salama.

    Katika ujumbe ulioandikwa kwenye ukurasa wa Twitter wa kampuni yake, amesema: "Namshukuru Mwenyezi Mungu nimerudi salama nyumbani. Nawashukuru Watanzania wenzangu na watu wote kote duniani kwa dua na sala zao. Nashukuru mamlaka zote, ikiwemo Jeshi la Polisi, zilizofanya kazi ya kuhakikisha narudi salama."

    Ujumbe huo umeandikwa saa tisa na robo alfajiri, na umeelekezwa kwamba umeandikwa kutoka Dar es Salaam.

    • Gari alilotekewa Mo Dewji limesajiliwa Msumbiji
    • Wasifu wa Mo Dewji, Mtanzania bilionea wa umri mdogo zaidi Afrika
    • Visa 10 vya utekaji nyara vilivyoishangaza dunia

    Waziri wa Muungano na Mazingira Tanzania Januari Makamba naye ameandika kwenye Twitter kwamba: "Mohammed Dewji amerudi salama. Nimezungumza naye kwa simu dakika 20 zilizopita. Sauti yake inaonyesha yu mzima bukheri wa afya. Shukrani kwa wote kwa dua na sala. Naenda nyumbani kwake kumuona muda huu."

    Bilionea Mtanzania Mo Dewji hatimaye amerejea nyumbani kwao huko Dar es Salaam

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Bilionea Mtanzania Mo Dewji hatimaye amerejea nyumbani kwao huko Dar es Salaam