Pape Gueye asusa kuichezea Senegal hadi benchi la ufundi litakapobadilishwa

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa Senegal, Pape Gueye, amesema kuwa atasitisha kwa muda kuichezea timu ya taifa kwa muda wote ambao benchi la ufundi la sasa litaendelea kuiongoza timu hiyo.
Uamuzi wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 unafuatia kuondolewa kwa Senegal katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Dunia, baada ya kupoteza kwa kufungwa na Ubelgiji kwa mabao 3-2 chini ya kocha Pape Thiaw.
Habib Diarra na Ismaïla Sarr waliifungia Senegal mabao mawili yaliyoiweka mbele, lakini mabao ya dakika za mwisho kutoka kwa Romelu Lukaku na Youri Tielemans yalipeleka mchezo huo katika muda wa nyongeza.
Belgium ilipewa penalti yenye utata katika dakika ya 125, na Tielemans akafunga mkwaju huo wa penalti na kuitupa Senegal nje ya mashindano.
Gueye, anayekipiga katika klabu ya Villarreal CF nchini Hispania, alianza mchezo huo lakini alitolewa dakika ya 66 na nafasi yake kuchukuliwa na Lamine Camara.
Kupitia mitandao ya kijamii, Gueye alisema:
"Nitarejea baadaye kuzungumzia kuondolewa kwetu... lakini leo natangaza kwamba mradi tu benchi hili la ufundi litaendelea kuwepo, nitakuwa napumzika kuichezea timu ya taifa."
Gueye ameichezea Senegal mechi 45 na amefunga mabao mawili, yakiwemo yale aliyofunga katika ushindi wa hatua ya makundi dhidi ya Iraq.
Unaweza kusoma;


























